Monday, June 29, 2015

RATIBA ZA VIPINDI VYA RUDISHA RADIO & RUDISHA TV

RUDISHA RADIO & TV SCHEDULE


10:00-1400 Gospel Music


14:00-17:30 Mahubiri (Bishop Gwajima)


17:30-20:00 Ibada (midweeks)


20:30-21:00 Vijana na Ukristo


21:00-21:30 Shuhuda 


21:30-22:30 Maombi na Maombezi


22:30-23:00 Sifa na Kuabudu


23:00-00:00 Wimbaji wetu


Friday, January 2, 2015

SIKU YA KWANZA:
Bishop Josephat Gwajima

MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ALIAHIRISHE LILE JAMBO BAYA ALILOLIPANGA ATALILETA KWENYE MAISHA YAKO

Maombi haya yana uwezo wa kuleta matokeo makubwa Kwenye maisha ya mtu. Kwa kawaida mtu anapotenda uovu, Mungu huwa anapanga kuleta uovu juu ya mtu huyo, hata Kama Mungu alikuwa anakupenda, au amekutumia kwa kiasi gani, unapotenda uovu Mungu anakawaida ya kuruhusu mabaya yaje juu yako pale unapotenda uovu.

Imeandikwa: Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. (UFU. 3:19 SUV).

Mungu anaonyesha asili yake, wale anaowapenda huwa anawakemea na kuwarudi, ukiona Mungu hakukemei unapofanya maovu ujue Mungu hakupendi.
Mungu huwa anakemea watu, na kwenye kukemea kule ndio unaweza kuona mtu amepata jambo baya, kama ajali, magonjwa,shida na taabu mbalimbali.

Imeandikwa : tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? (EBR. 12:5-9 SUV)

Mungu anapokupenda, akiona unaanza kwenda Kwenye njia iliyoopo toka , Mungu anaruhusu jambo baya linakupata ili kukurudishia katika njia iliyonyooka.

Biblia inasema mabaya hayatakupata wewe, kwahiyo unapoona mabaya yanaanza kukupata unakua ni lugha ya Kimungu ya kukuonya uache hiyo njia unayoiendea,

Mungu anakurudi kwa kutumia tukio, anaruhusu tukio likupate ili kukurudishia katika njia unayoiendea, na Mungu anaweza kulirudi taifa, mchungaji au mtu yeyote kwa kuruhusu tukio limpate.

Ndio sababu Mungu anawaruhusu hata watumishi wake kukemea

Imeandikwa : lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. (2 TIM. 4:2 SUV)

Imeandikwa :Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote. (TIT. 2:15 SUV)

Imeandikwa :, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. (UFU. 2:5 SUV)

"Kukiondoa kinara chako"maana yake ni kuruhusu mabaya yakupate, au nitaongea na wewe kwa njia ya matatizo.

Ni kama ambavyo sisi ni wazazi, wakati mwingine tuna wachapa watoto wetu, yamkini inaweza kana ukawa inauma, lakini tunakua tukijua kwamba ni kwa faida ya mtoto, ndivyo alivyo na Mungu pia

Mtu anaweza kufanya maovu tena na tena mpaka malaika wa huruma anaondoka, na malaika wa huruma anapoondoka Mungu anaruhusu mabaya .

Inaweza kana kuna mambo umetenda 2014 na Mungu amepanga kukupigania 2015, yawezekana hakuna mtu anayefahamu kuhusiana na mambo unayoyatenda, na Mungu amekua akiuonya Mara nyingi bila wewe kusikia,  Leo tutamuomba Mungu ili kuahirisha lile jambo alilolipanga baya juu ya Yale uliyoyatenda.

Wana wa Israel Mungu aliwatoa kutoka katika nchi ya utumwa kwa gharama kubwa, na walipoingia katika nchi ya Ahadi walianza kufanya yaliyo  mbele za Bwana, Mungu akaanza kuwaambia mabaya yatawapata, mtachukuliwa utumwani, mtachinjwa na mambo Kama hayo.

Mungu alikuwa anazungumza kwa vinywa vya watumishi wake,

Imeandikwa :  Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. (EZE. 18:24 SUV)


Hapa unaona mtu anaweza akaanza vizuri, lakini baadae akageuka na kuanza kufanya yaliyo maovu, biblia inasema utakufa katika uovu huo.

Kuna watu matatizo that aondoke pale tu utakapomuona kuacha njia ya uovu unayoiendea.

Imeandikwa :Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo. (EZE. 33:13 SUV)

Kufa kuna hatua, kuna matukio yanaweza kukupata Kama magonjwa au ajali ilimuishie kufa, Mungu anayo kawaida ya kutotenda jambo bila kuwajulisha watumishi wake, ndio sababu amekua akikuonya tena na tena ili uache uovu Kabla hujafa

Imeandikwa :Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga. (YER. 20:4 SUV)

Mungu alikuwa akiyazungumza haya Kabla hayajawapata ili waweze kutubu, na Yeremia alikuwa akiwaonya tena na tena lakini hawakusikia.

Hakuna mtu yeyote aliyemuona Mungu wakati wowote, na Mungu huwa anazungumza kwa vinywa vya watumishi wake. Na baadhi ya watu bila kufahamu wanakua na desturi ya kushindana na mtumishi wa Mungu akifikiri anashindana na mtu.

Hii inasababisha maovu yaje katika maisha yako.

Hakuna furaha katika dhambi. Dawa ya dhambi ni kutubu.
Nimeonyeshwa katika Roho Mtakatifu kwamba kutokana na maovu uliyoyatenda Mungu amepanga akukemee, lakini makemeo yake yanaweza Kuwa ya uchungu sana. Ndio sababu unatakiwa umuombe Mungu msamaha ili mabaya yaliyokusudiwa katika maisha yako yasikupate.


Waweza kusikiliza maombi ya siku ya kwanza kupitia link ifuatayo

https://www.youtube.com/watch?v=zoMuYl2a4jI&feature=youtu.be

Monday, December 29, 2014

KWANINI HUKUOGOPA?JUMAPILI YA TAREHE 28/12/2014
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KWANINI HUKUOGOPA?
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
“Ikawa baada ya kufa kwake Sauli, hapo Daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi; hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia. Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli. Daudi akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa. Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa? Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi. Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa. Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu. Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu. Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga. Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki. Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa Bwana.” 2 Samweli 1:1-16


Daudi alikuwa mwenye umri wa miaka 16 tu alipomuua Goliathi, naye Mfalme Sauli akapata hisia kwamba huyu kijana kwa nguvu zake anaweza akawa Mfalme badala yake. Hivyo akaanza kumwinda Daudi ili amuue. Hivyo Daudi akawa mtu wa kutangatanga akimikimbia Sauli. Daudi akiwa porini akijificha Sauli akaenda vitani na Wafilisti. Daudi hakuwa sehemu ya vita hii kwa kuwa alikuwa mafichoni.
Baada ya vita kuwa imeisha, Daudi akamuona huyu kijana Mmaleki ambaye alikuja kumjuza taarifa za yaliyojiri vitani. Kijana huyu anaeleza na kusema kuwa Mfalme Sauli pamoja na mwanae Yonathani wameuawa vitani na anakiri kuwa yeye ndiye aliyemuua na kisha anatoa sababu kuwa alijua asingepona mbele ya Wafilisti. Inaonekana kijana Mmaleki alijua kuwa Daudi na Sauli ni maadui hivyo alitegemea Daudi afurahi. Lakini mambo yalikuwa tofauti kidogo. Daudi aliposikia hayo akararua mavazi yake akayatupa chini pamoja na mashujaa wake wakaacha kula mpaka jioni wakiumwombolezea Sauli masihi wa Bwana.
Masihi wa Bwana ni mtu ambaye amepakwa mafuta na Mungu ili atengwe kwa ajili ya kazi ya Bwana. Katika agano la kale watu waliopakwa mafuta ni mfalme, kuhani na nabii. Vilikuwepo vyombo ambavyo vilipakwa mafuta pia kwa ajili ya kazi ya Bwana. Neno masihi ni sawa na neno Kristo yaani aliyetengwa kwa ajili ya Bwana. Ndio maana biblia katika ufunuo inasema kuwa katika siku za mwisho watatokea makristo wa uongo, haisemi maYesu wa uongo.
Kwa desturi za kiyahudi mtu hawezi kuitwa masihi mpaka amwagiwe mafuta maalum na nabii. Hii ndio sababu iliyowafanya wayahudi wamkatae Yesu kwasababu alijiita Kristo “masihi wa Bwana” bila kuwa amepakwa mafuta na nabii yoyote waliyemfahamu wao. Umasihi ni uungu wa Mungu juu ya mwadamu; mwanadamu anakuwa ana vipande viwili uwanadamu wake na uungu ulioko ndani yake.  Katika agano jipya mtu anakuwa masihi wa Bwana si kwa kumwagiwa mafuta tena bali kwa kujazwa Roho Mtakatifu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu, alipokuwa anabatizwa lilishuka wingu zito kutoka juu nah ii ndio ilikuwa ishara kuwa amemwagiwa Roho Mtakatifu. Lakini Wayahudi hawakuelewa mambo haya.
Biblia inasema;

“Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.” Zaburi 105:15

Daudi aliliifahamu jambo hili vizuri. Sio kwamba hakupata nafasi ya kumuua Sauli; lakini mara zote hakufanya hivyo kwa kuwa alijua kuwa pamoja na uovu wote anaomfanyia bado Sauli ni masihi wa Bwana na hapaswi kuguswa.
“Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu.  Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kuifunika miguu. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia Bwana, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.  Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli. Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neon hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.” 1 Samweli 24:1-6
Daudi akasema, Aishivyo Bwana, Bwana atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea. Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi.”1 Samweli 26:10-11

 Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi. Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia.” 1Samweli 28:11
Hizi zote zilikuwa ni nyakati tofauti ambazo Daudi aliweza kumuua Sauli lakini hakufanya hivyo kwa kuwa alijua ni masihi wa Bwana. Na kwa sababu ya hili, Mungu alimpenda sana Daudi. Katika biblia ni watu wawili tu ambao Mungu alitamka waziwazi kuwa alipendezwa nao na Daudi ni mmoja kati ya watu hao mwingine akiwa ni Yesu.
Baada ya kuomboleza kwa ajili ya Sauli na Yonathani, Daudi alimgeukia yule kijana Mmaleki na kumuuliza, “Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA?”  Kumbe Mungu anategemea tuwe na hofu kunyoosha mikono na midomo yetu kuwaangamiza masihi wake.
Kisha Daudi aliamuru kijana Mmaleki auawe kwa sababu alikiri kwa nafsi yake kuwa alimuua masihi wa Bwana. Lakini ukweli ni kwamba kijana huyu hakumuua Sauli, alikuta amekwishauawa. Naye kwa kutaka sifa mbele ya Daudi akadanganya na kuishia kuuawa.
Ipo laana itokanayo na wewe kuwaongelea vibaya watumishi wa Mungu. Haijalishi ni watumishi wa kanisa lako au lingine. Ubaya wa laana ni kuwa madhara yake  hayataonekana leo au kwa wakati mmoja. Itakutafuna wewe, familia yako, biashara polepole mpaka vyote vimeisha kabisa. Biblia iinayo mifano ya namna watu walivyobeba laana katika maisha yao kwa kuwainukia masihi wa Bwana kwa maneno au matendo.
“Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.  Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.  Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.  Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.  Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.  Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.  Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.  Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena. Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.” Hesabu 12:1-16
Miriamu na Haruni walikuwa ndugu wa damu kabisa wa Musa. Miriamu alikuwa ndiye dada mkubwa wa Musa aliyehusika kumficha Musa Farao alipotoa amri ya watoto wa kiume kuuawa katika Misri. Miriamu na Haruni pia walikuwa watumishi wa Mungu; Miriamu akiwa mwimbaji na Haruni kuhani. Kwa hiyo walikuwa wamemzoea sana Musa na wakashindwa kuuona umasihi wake hata wakaanza kumsema juu ya mke aliyemuoa aliyekuwa mkushi yaani mwafrika. Walichosahau kina Miriamu ni kuwa mtu anapochaguliwa kuwa masihi wa Bwana mara moja anabadilika na kuwa si mtu wa kawaida tena kwa kuwa Mungu anakuwa anafanya kazi kupitia yeye. Hii haimaanishi kuwa atakuwa mtakatifu asiyetenda dhambi kabisa, hapana. Anaweza akakosea kabisa kwa sababu ile sehemu ya uanadmu bado imo ndani yake pia. Ni kweli haiikuwa sahihi kwa Musa kuoa mwanamke Mkushi kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye aliyeweka sheria hiyo kati ya Waisraeli. Lakini haikuwa sehemu ya kina Miriamu kuhukumu jambo hilo kama ambavyo leo sio nafasi yako kuwahukumu na kuwasema watumishi wa Mungu hata kama wamekosea kweli. Acha Mungu mwenyewe liyewachagua ashughulike nao.  Ni muhimu sana ufahamu kuwa Watu hawawi watumishi wa Mungu kwa sababu wametaka au kwa kuwa wanaweza bali ni kwa sababu wamechaguliwa na Mungu.
Tunaona jinsi laana ya ukoma ilivyompata Miriamu kwa kumsema Musa masihi wa Bwana; Musa hakuwa ameyasikia haya maneno lakini biblia inasema Mungu alisikia. Inawezekana kweli maneno yako unayasemea mbali kabisa na mtumishi husika lakini kumbuka Mungu anasikia. Wakati mwingine unamsema mtumishi wa Mungu vibaya halafu unapofika mbele yake unajifanya kuwa mnyenyekevu naye hutamka baraka juu yako na wewe unaitikia “Amina!”  Zile Baraka hugeuka na kuwa laana katika maisha yako.
Kama ambavyo ilibidi Miriamu atengwe kwa siku saba hata baada ya Musa kumuombea msamaha kwa Bwana; ndivyo inavyokuwa kwenye maisha yetu hata leo. Wakati mwingine safari ya kiroho ya mtu inaweza kukwama kwasababu ya kuwasema watumishi wa Bwana.
“Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;  nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,  Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.  Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? Bwana akasema na Musa, na kumwambia, Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu. Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakaandamana naye.  Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.  Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi.  Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.  Kisha moto ukatoka kwa Bwana, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.” Hesabu 16:1-35
Huu ni mfano mwingine wa watu ambao waliinuka kinyume na mtumishi wa Mungu Musa na laana ya mauti ikawakumba. Si wao tu bali familia zao pia.
Kuna sehemu katika maisha yako sio maombi au kusoma neno au kutoa kwako sadaka kutaweza kukuvusha bali neema tu ya Mungu. Lakini Mungu naye anaweza akakumbuka yale maneno yako mabaya juu ya watumishi wake uliyoyanena naye akanyamaza. Kama ambavyo dhabihu na maombi hukumbukwa mbele za Bwana ndivyo yatakavyokumbukwa maneno yako. Ni kweli Bwana kasema nasi kuwa mwaka 2015 ni mwaka wa kutiisha, kumiliki na kutawala lakini tusipoangalia tutaishia kusema bila kupokea. Kwa nini? Laana ya kuwasema masihi wake.
Kuwasema watumishi wa Mungu au wakuu wa watu wako kunaleta laana iwe ulisema kwa kutokujua au kwa kurubuniwa na watu. Sio lazima itokee leo lakini hakika yake itakupata hata kama ni miaka kumi ijayo. Basi leo kwa kadri ambavyo unahukumiwa ndani yako fanya toba ya kweli. Biblia inasema aziungamaye dhambi zake na kuziacha atasamehewa. Baada ya toba dhamiria kabisa kutoka ndani yako kutokuwasema watumishi wa Mungu wawe wa kanisa lako au lingine. Utakapokutana na mtu au watu ambao wametengeneza kikao cha kuwasema watu wa Mungu hakikisha unawataarifu kuwa si sawa na pia ujitenge nao. Usikubali kuishi ndani ya laana kwa kushindwa kukizuia kinywa chako kusema yasiyostahili.
 
TUTAKUWA NA MFUNGO WA SIKU 30 KUANZIA 1/1/2015 MPAKA 30/1/2015. MFUNGO HUU UTAAMBATANA NA MAOMBI YATAKAYOFANYIKA KUANZIA SAA TISA ALASIRI KATIKA VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS. PIA, MAOMBI HAYA YATAAMBATANA NA MAFUNDISHO JUU YA SERIKALI YA SHETANI NA MAPEPO YANAYOTAWALA SIKU. KARIBU TUUANZE MWAKA 2015 KWA NGUVU. MFUNGO HUU NI KWA AJILI YA KILA MTU, HIVYO WAKARIBISHE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO. HAKITAKUWA KITU RAHISI LAKINI MUNGU AKUTIE NGUVU UWEZE KUFUNGA NA KUHUDHURIA IBADA HIZI ZA MAOMBI NA HAKIKA BAADA YA TAREHE 30/1/2015 UTAKUWA MTU WA OFAUTI KWA JINA LA YESU. KARIBU TUTIISHE, TUMILIKI NA KUTAWALA!

Thursday, December 25, 2014

SPIRITUAL TRANSFER


The word of Today: Spiritual transfer
By Bishop: Josephat Gwajima
Date: 21/12/2014
 
All the generations, therefore, from Abraham to David were fourteen generations; and from David until the carrying away of Babylon, fourteen generations; and from the carrying away of Babylon unto the Christ, fourteen generations. Matthew 17:1

  “Jehoiachin was eighteen years old when he began to reign; and he reigned three months in Jerusalem; and his mother's name was Nehushta, daughter of Elnathan of Jerusalem. And he did evil in the sight of Jehovah, according to all that his father had done. At that time the servants of Nebuchadnezzar king of Babylon came up against Jerusalem, and the city was besieged. And Nebuchadnezzar king of Babylon came against the city, while his servants were besieging it. And Jehoiachin king of Judah went out to the king of Babylon, he, and his mother, and his servants, and his princes, and his chamberlains; and the king of Babylon took him in the eighth year of his reign. 

And he brought out thence all the treasures of the house of Jehovah, and the treasures of the king's house, and cut in pieces all the vessels of gold that Solomon king of Israel had made in the temple of Jehovah, as Jehovah had said. And he carried away all Jerusalem, and all the princes, and all the mighty men of valour, ten thousand captives, and all the craftsmen and smiths: none remained but the poorest sort of the people of the land. And he carried away Jehoiachin to Babylon, and the king's mother, and the king's wives, and his chamberlains, and the mighty of the land, he led into captivity from Jerusalem to Babylon; and all the men of valour, seven thousand, and the craftsmen and smiths a thousand, all strong men apt for war, and the king of Babylon brought them captive to Babylon. And the king of Babylon made Mattaniah his uncle king in his stead, and changed his name to Zedekiah. Zedekiah was twenty-one years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem; and his mother's name was Hamutal, daughter of Jeremiah of Libnah. 2 KINGS 24:8-18

King Jehoiachin was taken captive because of his rebellion, he offended God and that is why God allowed the king of Babylon to win over his kingdom and turn him and all his mighty men of valour into captives. King Jehoiachin saw no chances of winning the war because of his disobedience which is why he surrendered and this teaches us when someone is in sin he will never get out of his chains even if he consoles himself the only way is to repent. King Nebuchadnezzar took ten thousands captives including the king’s mother, and only the poorest were left behind.
 The question is why king Nebuchadnezzar only took the mighty and left the poor behind? Why did he took the king’s mother and made her a captive while she didn’t have anything to offer?. This is because even the women who give birth to kings and rulers are blessed because not every womb can deliver kings that is why the king took her he knew she can be give him rulers.
The king of Babylon symbolizes Satan.  The devil usually takes captive all people who are potential and gifted but not the weak because the weak has nothing to offer or challenge him, he can see ones gifts in the spiritual realm even before he’s born, he knows how that person will be in the future that is the reason he takes such people  captives. Same applies in families a child who is highly gifted and expected to save the family from poverty is the one encountering many problems and misfortunes, why? Because the devil has captured him and he is using his gifts and abilities to build his kingdom.
You are going through sufferings and torments in your life it’s because you have something great inside in you that can destroy the devil and that why the he can’t not allow you to prosper, the devil can see your prosperity in the spiritual realm he knows if he leaves free one you will destroy him as a servant of God.
The Word of God says before you are kept in your mother’s womb, you were known from heaven that you are sent to earth to build God’s kingdom through your gifts that God gave you, Satan saw you since the time you were descending as a spirit from heaven to your mother’s womb he also saw how gifted you are and that is why he took you into captivity  
“God is a spirit; and they who worship him must worship him in spirit and truth”. John 4:24

But everyone who is born of spirit wins the world, we are spirits but it pleased God for us to have flesh. We have a flesh father and mother have given us the flesh body and our Spiritual Father is the father of our spirits. Once we die our flesh goes back to the earth because our flesh is dust but our spirits don’t die because they resemble our heavenly father We should rejoice for we carry the labels of Jesus Christ in us ,we rejoice because for our spirits and not flesh, because the flesh will perish, any flesh without Christ has meaningless. Once you accept Jesus he lives in you and you will die but you will live. We are spirits because our heavenly Father is a spirit although it pleased for to us to have flesh and hence we are not of this world we came from heaven.
I have given them thy word, and the world has hated them, because they are not of the world, as I am not of the world”. John 17:14
Satan, witchcrafts, witches and star readers can see you in the spiritual realm, when they look at the spiritual realm they can see your star, your mission and your purpose in this world and that is why they take your abilities and use it to build the devil’s kingdom which in the last days we simply not work.
“And after the carrying away of Babylon, Jechonias begat Salathiel, and Salathiel begat Zorobabel and Zorobabel begat Abiud, and Abiud begat Eliakim, and Eliakim begat Azor, and Azor begat Sadoc, and Sadoc begat Achim, and Achim begat Eliud,and Eliud begat Eliazar, and Eliazar begat Matthan, and  Matthan begat Jacob,and Jacob begat Joseph, the husband of Mary, of whom was  born Jesus, who is called Christ”. Matthew 1:12-16
We have been spiritually transferred and that is why the miracles which happened then are not happening anymore, if you ask the people why such miracles have disappeared they say that was in the past and now we live in the future but this is not true because God is the same yesterday, today and forever, even pastors today are not preaching like how they are supposed to preach in in the kingdom of God because even they are spiritually transferred   and become captive but they are not aware of it! we must return back home.
Now that we know of the spiritual transfer the question is where have we been transferred to?. There are spiritual cities which are built in the spiritual realm and a person can be taken to live there.
“And the wall of the city had twelve foundations, and on them twelve names of the twelve apostles of the Lamb”.  Revelation 21:14
 “And I saw no temple in it; for the Lord God Almighty is its temple, and the Lamb.  And the city has no need of the sun or of the moon that they should shine for it; for the glory of God has enlightened it, and the lamp thereof is the Lamb”. Revelation 21:22-23
“In that day shall there be five cities in the land of Egypt speaking the language of Canaan, and swearing by Jehovah of hosts: one shall be called, the city of Heres”. Isaiah 19:18
“Mine eyes are consumed with tears, my bowels are troubled; my liver is poured upon the earth, because of the ruin of the daughter of my people; because infant and suckling swoon in the streets of the city”. Lamentations 2:11
These scriptures reveal to us that there are cities in the spiritual realm, some of these are cities belong to God and some of them belong to the devil though these cities cannot be seen by our flesh eyes, they do exist, these cities need no sun nor moon for God’s glory is the light of his city and as for the devil darkness is the light his city which is called the city of Heres.  This is the city where the devil has kept people captive; he has transferred them from their native place by taking their abilities and uses them for his kingdom. The devil may not take you whole it may be your eyes, your mind, attitude, confidence or ability which you are blessed with that is taken to the city of Heres to serve the devil like how the king of Babylon took ten thousand people of Judah captive with different abilities to serve him.
When I speak of attitude I mean, a personal interpretation of things, it is how you look at things and give their proper names, it is your personal judgement over matter and Confidence is knowing beyond the shadows of guts. If these things are taken from what remains is arrogance
“And now, why hast thou not reproved Jeremiah of Anathoth, who maketh himself a prophet to you? For as much as he hath sent unto us in Babylon, saying, It will be long; build houses, and dwell in them, and plant  gardens, and eat the fruit of them.  And Zephaniah the priest read this letter in the ears of the prophet Jeremiah. And the word of Jehovah came unto Jeremiah, saying Send to all them of the captivity, saying, Thus saith Jehovah concerning Shemaiah the Nehelamite: Because that  Shemaiah hath prophesied unto you, and I sent him not, and he  hath caused you to trust in falsehood”. Jeremiah 29:27-31

During the 1st century Christianity totally disappeared, only the Catholics remained and many Pentecostal Christians were searched and killed by the roman dollar, for example Peter and others were hanged on the cross and some were smashed by the roman chariots, the remaining Christians ran and hid themselves in the dungeons of the country. Later these Christians received news about the death roman king the one who used to kill them and the rise of the new king , king Constantine  who was a Christian, this king unlike the previous one he summoned all the Christians who were hiding he united them and from  there roman catholic began because the king was catholic and so the Pentecostal Christians had no option than to turn into romans, later Martin Luther arose and turned against catholic and he started he own group called the Lutherans, king James also came up his view of allowing bishops to marry and from him arose Anglicans the word Anglican came from the word ‘Anglo’ which  means English which meaning  the congregation established by the British, later others who protested against some of the things followed by the Catholics, formed their congregation which is today called “protestants”. Till then no one was speaking in tongues until in the 18th century God caused a problem in the city of Azusa which assembled people to pray and that is when they started speaking in tongues again, Americans thought these people have gone mad and from there miracles started happening and the flames of fire which is the Holy Spirit was back again.
I have given this history for you to realize that we are captives and the devil tried to take away our Christianity, our fire and our gifts that why we have to return back home to our nature and refuse to be captives in the name of Jesus.
King Koresh was raised by the LORD to allow the children of Israel to return back home, although they met enemies on their way who were stopping them from moving forward but in the end they overcame. This was the transfer started by God himself so his people could return to their homes and get out their captivity.  That is what happened in life whenever you want to prosper the devil blocks your way to stop from going after your success.
 
PRAYERS
In the name of Jesus I return back home, I return back to my nature and attitude in the name of Jesus, I return back from my transfer in the name of Jesus, whoever is holding me from going back I slay you in the name of Jesus,   today I destroy all those who have planted evil thoughts and attitude in me by the fire of God. In the name of Jesus I pull down all mountains that have stood in front me, I destroy all the witches who are withholding my transfer by the fire of God, I pull you down by the blood of Jesus. I open the passage of my freedom from captivity and return back home in the name of Jesus, I am shifting from where I was kept captive in the spiritual realm, I return back to life in the name of Jesus. I return from death to life in the name of Jesus, I return from failure to victory in the name of Jesus. I return from sadness, fear to my nature of confidence, power, ability, stability, wealthy and success by the blood of Jesus. I diminish anyone who is blocking me in the name of Jesus. I destroy anyone who is preventing me from getting out of my captive the name of Jesus. I return back to my nature of multidisciplinary, ownership and control in the name of Jesus. Amen