Monday, April 19, 2010

Matukio ya Jumapili, 18 Aprili 2010 Katika Picha


Kijana Barnaba aliyekuwa msukuleni na baadaye kuokolewa na BWANA Yesu, akimsifu BWANA Yesu kupitia kibao cha wimbo wake unaokwenda kwa jina la “niliteswa”. Pamoja naye katika picha wakimtukuza BWANA Yesu ni Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima. Nyuma katika picha ni watu wanaume,wanawake na watoto waliokuwa msukuleni nao pia wakiungana na Kijana Barnaba Kumsifu na Kumtukuza BWANAYesu katika anga la uweza wake.


Makutano makubwa wakimwabudu YEHOVA katika ibada ya jumapili ya leo 18 Aprili 2010, katika viwanja vya Tanganyika packers ambapo ndipo lilipo kanisa la Ufufuo na Uzima, kawe jijini Dar es Salaam.

: Binti, aliyefufuka kutoka kwa wafu akishuhudia uweza na nguvu za BWANA Yesu. Binti huyu mara baada ya kufa tu kaka yake alianza kuomba maombi ya kumrudisha akilitaja jina la Yesu akisema rudisha katika Jina la Yesu na kupambana katika maombi ya nguvu kwa muda wa masaa sita(6) na hatimaye dada yake alifufuka.Kaka wa binti aliyekufa na baada ya maombi kufufuka, akieleza namna alivyokuwa akiomba maombi ya kumrudisha dada yake mara tu alipokufa.


Kijana kutoka Tanzania, nyumba ya Ufufuo na Uzima, Daniel akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Bi Akali kutoka japani. Pamoja nao katika picha ni Wazazi wa Akali waliotoka Japani kuja kushuhudia mtoto wao akifunga ndoa katika nyumba ya Ufufuo na Uzima. Katika picha pia ni Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima wakiwa na wachungaji wengine kwa pomoja wakimtukuza BWANA Yesu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa hapa kanisani.
Shetani akiaibishwa......

Familia ya Happiness Kahabi katika picha. Wa kwanza ni mama yake mzazi, anayefuata ni kaka yake ambaye ni Daktari wa meno, Happiness mwenyewe wapili kutoka kulia na wa kwanza kulia ni mume wake.


Kijana Emmanuel aliyekufa kwa kujinyonga huko Moshi mkoani Kilimanjaro na hatimaye kufufuka akishuhudia jinsi hali ya mambo ilivyokuwa mara baada ya kujinyonga, kufa na baadaye kufufuka.
Mbongo Akijitwalia jiko la Kijapani.....
Kijana Daniel akimvisha pete ya ndoa mkewe Bi Akali ndani ya Nyumba ya ufufuo na Uzima.

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa na wachungaji wengine wakiwaombea Daniel na Akali mara baaya ya ndoa yao kufungwa katika nyumba ya Ufufuo na Uzima, ndani ya viwanja vya Tanganyika packers vilivyopo kawe, Jijini Dar es Salaam.

Yalioyojiri katika Ibada Jumapili ya leo 18 Aprili 2010


Msukule aliyerudishwa kutoka msukuleni akipitishwa na wachungaji katikati wa watu ili waweze kumuona vizuri ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima katika viwanja vya Tanganyika Packers, kawe jijini Dar es Salaam.Familia ya Happiness Kahabi wakimwaibisha shetani ambaye ni muongo na ni baba wa huo(uongo). Happiness kahabi(wa pili kutoka kulia) alichukuliwa msukule na kupelekwa chini ya ziwa Victoria na baadaye BWANA Yesu alimrudisha kutoka msukuleni.Pamoja nao wakishuhudia na kumpa BWANA Yesu utukufu ni mume wake Happiness (mwenye shati jeupe -wa kwanza kulia), mama yake mzazi(wa pili kushoto) na kaka yake. Katika picha pamoja nao ni Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (GCTC) almaarufu kama “Ufufuo na Uzima”

Wednesday, April 7, 2010

Semina Ya Pasaka: Moto wa Ufufuo na Uzima

Ujumbe wa Leo Kwa Ufupi: 6 April 2010

Na Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima
Somo: Roho aliyemfufua Yesu katika wafu
Neno la Msingi: Warumi 8: 11

Warumi 8: 11 imeandikwa “Lakini , ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu”
Katika somo hili Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima anaanza kwa kufundisha akisema……
“……….Tunaanza kusoma mambo kadha wa kadha hapa. Tunajua Yesu alikufa akazikwa, lakini tunaaza kupata picha kwamba kumbe yupo Roho aliyemfufu Yesu katika wafu. Na taarifa zinaendelea kwamba eti, Roho Yule aliyemfufua Yesu katika wafu pia anakaa ndani yetu. Hili ni jambo la ajabu sana kwamba eti Roho aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu………”
“…………………….Tunaanza kupata maswali kadha wa kadha hapa, kwamba kumbe Yesu alipokufa alifufuliwa na Roho wa Mungu. Na huyu Roho aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa pia ndani yetu. Tunapewa majibu kuwa Roho huyu ataifufua na miili yetu iliyo katika hali ya kufa………………..”
Ujumbe huu wa leo tarehe 6 April 2010 unaofundishwa na Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima umewekwa hapa kwa ufupi tu. Na masomo haya yanaendelea katika mfululizo wa Siku zote za semina hii ya Pasaka yenye lengo la kujifunza namna ya kukamata upako au nguvu za Roho Mtakatifu katika Ufufuo na Uzima. Na tunapenda upate nakala yako katika mfumo wa VCD, DVD, AUDIO CD na Kaseti.

Ili kupata ujumbe huu katika VCD, DVD, AUDIO CD, tafadhali wasiliana na Wachungaji wa Media Outreach na Audio Outreach kupitia namba zifuatazo 0713559152 /0716369190 0714117196 /0652033638 /0715808283.

Sunday, April 4, 2010

Semina Ya Pasaka na Mch. Kiongozi, Josephat Gwajima

Kuanzia Jumatatu ya Tarehe 5 April 2010 mpaka tarehe 12 April 2010 kutakuwa na Semina ya Pasaka katika Viwanja vya iliyokuwa Tanganyika packers, Kawe jijini Dar es Salaam. Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima atakuwepo akiongoza Semina hii na kufundisha kwa wiki nzima mpaka Jumapili. Usomapo Tangazo hili Tafadhali mjulishe na mwingine na Mungu akubariki sana. Karibu Katika bonde la kukata maneno ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima.
Muda: Saa 11 jioni.
Mahali: Iliyokuwa Tanganyika packers, Kawe jijini Dar es Salaam

Ujumbe wa leo kwa Ufupi unatoka 2 Samweli 22:38-41

Jumapili, 04 April 2010
Somo: NIMEWAKOMESHA NIMEWAPIGA PIGA WAMESHINDWA KUSIMAMA
Na Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima

2Samweli 22:38-41 “Nimewafuatia adui zangu na kuwaangamiza wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa nami nimewakomesha na kuwapiga piga wasiweze kusimama; naam wameanguka chini ya miguuu yangu maana wamenifunga mshipi wa nguvu kwa vita; umenitiishia chini yangu waliniondokea, naam adui zangu umewafanya wanipe visogo ili niwakatilie mbali wanaonichukia.”

Ili kupata ujumbe huu katika VCD, DVD, AUDIO CD na Kaseti wasiliana na Wachungaji wa Media Outreach na Audio Outreach kupitia namba zifuatazo 0713559152/0716369190/0714117196/0652033638/0715808283
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akiwaombea watu wenye shida mbalimbali katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima ndani ya Viwanja vya Tanganyika packers vilivyopo kawe jijini Dar es Salaam

Yaliyojiri leo katika Ibada ndani ya Ufufuo na Uzima

Sehemu tu kati ya watu 400 waliokuwa misukule katika maeneo mbalimbali kama vile mashambani, mapangoni, kwenye misitu, mashimoni, chini ya uvungu, darini, nyuma ya kabati na milango, chini ya bahari, kuzimu, kwa wasoma nyota na sasa wamerudishwa na Bwana Yesu.Watu hawa katika picha wakishuhudia jinsi wachawi walivyowachukua na kuwatumikisha huko msukuleni. Pamoja nao katika picha ni Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa kanisa la Glory of Christ Tanzania (Maarufu kama Ufufuo na Uzima)

Matukio ya Jumapili ya Leo katika Picha ndani ya Ufufuo na Uzima
“Makutano makubwa, Makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa kuwa siku ya BWANA i karibu (Yoeli 3:14)” Haya ni maneno ya Mungu kupitia nabii Yoeli aliyoyatabiri katika Biblia miaka mingi iliyopita na sasa maneno haya yanatimia machoni petu. Maelfu kwa Maelfu ya watu wakiwa katika ibada ya Jumapili ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima katika “bonde la kukata maneno” sasa sio Ubungo tena bali ni katika Viwanja vya iliyokuwa Tanganyika packers vilivyopo kawe jijini Dar es Salaam!
TANGAZO KWA WATU WOTE

Nyumba ya Ufufuo na Uzima sasa tupo katika
"Bonde la kukata maneno" katika Viwanja vya Tanganyika
Packers, Kawe
Watu wa aina zote,lugha zote, na rangi zote
mnakaribishwa sanaaa!