Sunday, May 9, 2010

Ushuhuda mkubwa:Mtoto afufuka


Mchungaji Mwangasa(Mchungaji Msaidizi-Resident Pastor) wa kanisa la Glory of Christ Tanzania Church(Nyumba ya Ufufuo na Uzima) akiulezea ushuhuda mkubwa wa kufufuka kwa mtoto aitwaye Praygod.

Mtoto aliyefufuka katika Picha


wachungaji wakimuombea mtoto aloyefufuka kuwa na maisha marefu na kumtumikia Mungu akishakuwa mkubwa.


Mama mzazi wa mtoto aliyefufuka(Isabela) kulia, akishuhudia namna mtoto wake alivyokufa na hatimaye kukufuka baada ya kuliitia Jina la BWANA.

Mtoto afufuka siku ya Jumapili ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima


Usiku wa Jumapili ya tarehe 2 mwezi Mei mwaka 2010 majira ya saa kumi alfajiri kuamkia jumatatu, BWANA YESU ambaye jina lake ni “Ufufuo na Uzima” alifanya jambo la ajaabu na la kutisha ndani ya Nyumba yake ya “Ufufuo na Uzima” baada ya kumfufua kutoka kwa wafu mtoto Praygod (Kitoto kichanga). Jumapili ya leo tarehe 8 mwezi Mei mwaka 2010. Mama wa mtoto huyo akiwa na mumewe hawakusita kumshushua na kumuabisha shetani huku wakimtukuza Mungu YEHOVA kwa muujiza huu mkubwa. Mama wa mtoto Praygod (Isabela) akishuhudia jinsi ambavyo mtoto wake alivyokufa na baadaye kuutafuta msaada wa BWANA ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima ambapo sasa kwa ushuhuda huu hakika yake linalotimia sasa ni neno la unabii wa Nabii Yoeli (Yoeli 3: 14) “makutano makubwa wamo katika bonde la kukata maneno” Katika ibada yenye makutano ya watu wengi leo hii ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima mama wa mtoto Praygod aliposhuhudia alikuwa na haya ya kuelezea “Mimi naitwa Isabela na mume wangu anaitwa Odani, na mtoto wangu anaitwa Praygod. Siku ya jumapili saa nane kasoro(usiku), mimi nilitoka nje kujisaidia na watoto wangu wawili twins(mapacha) nilimuacha Praygod ni mzima kabisa hana tatizo na nimemaliza kumnyonyesha. Nilivyorudi ndani nikawa ninambadilisha, kumuangalia mtoto ghafla amebadilika ni kwamba amelegea na hawezi kunyonya tena, amenyoosha miguu anapiga kwikwi za haraka haraka. Kwa hivyo simu yangu haikuwa na chaji, lakini najua ulikuwa ni mpango wa Mungu; kwa sababu ningehangaika kumtafuta baba yake kwenye simu na kuhangaika kutafuta watu ina maana natafuta msaada kwa wanadamu. Basi, mimi nilichokifanya niliwaamsha watoto wangu kwa haraka sana ni wadogo pia, amkeni amkeni tusaidiane kuomba Praygod hali yake imebadilika. Kwa kweli tulisaidiana kwa maombi, lakini hata hivyo Mungu alinifunga kinywa sikumwamsha jirani yangu yoyote. Niliamka mimi na watoto wangu nikafunga kanga moja tu nikawaambia wanangu twendeni Ufufuo na Uzima. Kwa kweli nilimwona Mungu, kila mtoto wangu aliwajibika kwa mtoto huyu kwa nafasi yake; mimi nilisimama na kumwambia Mungu ninakataa kifo juu ya mtoto wangu, Praygod ni mzima na atamtumikia Mungu. Hakika nilimwona Mungu! Wakati naendelea kukata hatua za kuja hapa(ufufuo na uzima), tumefika katikati ya bonde hili , mtoto alizimika na akanyooka na hakuwa na pumzi tena. Lakini hata hivyo sikukata tamaa nilimwambia Mungu naamini Praygod ni mzima na ataishi hatakufa! Nilifika hapa niliwakuta watu wapo kwenye mkesha, niliangalia nimpe nani mtoto nilichotamka ni Bwana Yesu! Ndipo walikuja watumishi wa Mungu akiwepo Pastor (Mchungaji) huyu hapa, wakanipokea mtoto na kaniambia tulia umefika Ufufuo na Uzima. Mungu atamfufua mtoto wako. Wakati huo mtoto wangu wa pili kwa kuona hofu ya mdogo wao kukata roho akapoteza fahamu; lakini basi, Mungu hakuniacha aliwajibika kwa nafasi yake juu ya Praygod, Oh Haleluya! Walimfanyia maombi mwanangu tangu ile saa nane ilipofika saa kumi kasoro Mumgu alimrudishia ‘pumzi’. Na sasa Prayod ni mzima na ninaahidi kwamba kusudi la Mungu juu ya mtoto wangu litimilike. Praygod amtumikie Mungu katika maisha yake”

Neno la Mungu katika Ibada ya leo kwa Ufupi: Jumapili tarehe 8 Mei, 2010


Mchungaji Mwangasa(Mchungaji msaidizi-Resident Pastor) wa kanisa la Glory of Christ Tanzania almarufu kama Nyumba ya Ufufuo na Uzima, akihubiri neno la Mungu.


Ujumbe wa Leo: Wakati wa Kuliitia jina la BWANA


Na Mchungaji Mwangasa, Resident Pastor (RP)


Neno la Msingi: Mwanzo 4: 25-26


“Adamu akamjua mkewe tena;akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi;maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua, Sethi naye akazaa mwana, akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia jina la BWANA”

Tuesday, May 4, 2010

Meet Pastor Gwajima in 2010 Japan World Conference


Pastor Gwajima(Right) teaches the word of God with boldness and without compromise which is the greatest weapon to set people free from all kinds of Satan’s oppression. Through the power of the the name of Jesus Christ, Pastor Gwajima has been used by God to bring many who have been afflicted by forces of darkness to a complete freedom.


Here he teaches the word of God recently in Kagoshima, Japan


"Is not My word like a fire?" says the LORD, "And like a hammer that breaks the rock in pieces?( Yer 23:29)

Pastor Gwajima ministering in one of the Conferences in Kogoshima, Japan.

Trip of the Senior Pastor in Japan: Safari ya Mchungaji Kiongozi JapaniEnglish Caption
The Senior Pastor of Glory of Christ Tanzania famously known as “Nyumba ya Ufufuo na Uzima”, Rev. Josephat Gwajima has started to preach the mighty word of God in Japan since last week. Pastor Gwajima has been invited to minister in the Japan 2010 World Conference. During this trip Pastor Gwajima will teach the word of God, pull down, and destroy the kingdom of the Satan, wrestle in the spiritual welfare and set the captives free through the power of Holy Spirit throughout Japan for the word of God says “For we do not wrestle against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this age, against spiritual hosts of wickedness in the heavenly places.”(Ephesians 6:12). Pastor Gwajima will preach in more than 6 big cities of Japan each with not less than 3 conferences. The cities includes Tokyo, Nagoya, Aichi, Okinawa, Osaka and Kagoshima

Click links below for details Kagoshima, Nagoya, Osaka, Okinawa, Aichi

Swahili Caption

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania maarufu kama “ Nyumba ya Ufufuo na Uzima”, Mch. Josephat Gwajima ameanza kuhuribi neno la Mungu lenye nguvu na uweza wa ajabu nchini Japan tangu wiki iliyopita. Mchungaji Gwajima amealikwa kuhudumu katika Mkutano wa Ulimwengu Nchini Japan (Japan 2010 World Conference). Katika ziara hii Mchungaji Gwajima atafundhisha neno la Uzima na kuharibu, kubomoa, kuuponda ponda ufalme wa shetani na wakala wake na kushindana katika vita vya kiroho, na kuwaweka huru watu walionewa na ibilisi nchini Japan kwa kuwa neno la Mungu linasema “ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka na wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika Ulimwengu wa roho” (Waefeso 6:12). Mchungaji Gwajima atahubiri neno la Mungu ndani ya majiji 6 na zaidi nchini Japan. Kila jiji linakadiriwa kuwa na mikutano zaidi ya 2. Majiji hayo ni pamoja na Tokyo, Nagoya, Aichi, Okinawa, Osaka and Kagoshima.

Kuona mikutano hiyo kama upo Japan bofya hapa kwa maelezo zaidi Kagoshima, Nagoya, Osaka, Okinawa, Aichi.