Sunday, May 9, 2010

Mtoto afufuka siku ya Jumapili ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima


Usiku wa Jumapili ya tarehe 2 mwezi Mei mwaka 2010 majira ya saa kumi alfajiri kuamkia jumatatu, BWANA YESU ambaye jina lake ni “Ufufuo na Uzima” alifanya jambo la ajaabu na la kutisha ndani ya Nyumba yake ya “Ufufuo na Uzima” baada ya kumfufua kutoka kwa wafu mtoto Praygod (Kitoto kichanga). Jumapili ya leo tarehe 8 mwezi Mei mwaka 2010. Mama wa mtoto huyo akiwa na mumewe hawakusita kumshushua na kumuabisha shetani huku wakimtukuza Mungu YEHOVA kwa muujiza huu mkubwa. Mama wa mtoto Praygod (Isabela) akishuhudia jinsi ambavyo mtoto wake alivyokufa na baadaye kuutafuta msaada wa BWANA ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima ambapo sasa kwa ushuhuda huu hakika yake linalotimia sasa ni neno la unabii wa Nabii Yoeli (Yoeli 3: 14) “makutano makubwa wamo katika bonde la kukata maneno” Katika ibada yenye makutano ya watu wengi leo hii ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima mama wa mtoto Praygod aliposhuhudia alikuwa na haya ya kuelezea “Mimi naitwa Isabela na mume wangu anaitwa Odani, na mtoto wangu anaitwa Praygod. Siku ya jumapili saa nane kasoro(usiku), mimi nilitoka nje kujisaidia na watoto wangu wawili twins(mapacha) nilimuacha Praygod ni mzima kabisa hana tatizo na nimemaliza kumnyonyesha. Nilivyorudi ndani nikawa ninambadilisha, kumuangalia mtoto ghafla amebadilika ni kwamba amelegea na hawezi kunyonya tena, amenyoosha miguu anapiga kwikwi za haraka haraka. Kwa hivyo simu yangu haikuwa na chaji, lakini najua ulikuwa ni mpango wa Mungu; kwa sababu ningehangaika kumtafuta baba yake kwenye simu na kuhangaika kutafuta watu ina maana natafuta msaada kwa wanadamu. Basi, mimi nilichokifanya niliwaamsha watoto wangu kwa haraka sana ni wadogo pia, amkeni amkeni tusaidiane kuomba Praygod hali yake imebadilika. Kwa kweli tulisaidiana kwa maombi, lakini hata hivyo Mungu alinifunga kinywa sikumwamsha jirani yangu yoyote. Niliamka mimi na watoto wangu nikafunga kanga moja tu nikawaambia wanangu twendeni Ufufuo na Uzima. Kwa kweli nilimwona Mungu, kila mtoto wangu aliwajibika kwa mtoto huyu kwa nafasi yake; mimi nilisimama na kumwambia Mungu ninakataa kifo juu ya mtoto wangu, Praygod ni mzima na atamtumikia Mungu. Hakika nilimwona Mungu! Wakati naendelea kukata hatua za kuja hapa(ufufuo na uzima), tumefika katikati ya bonde hili , mtoto alizimika na akanyooka na hakuwa na pumzi tena. Lakini hata hivyo sikukata tamaa nilimwambia Mungu naamini Praygod ni mzima na ataishi hatakufa! Nilifika hapa niliwakuta watu wapo kwenye mkesha, niliangalia nimpe nani mtoto nilichotamka ni Bwana Yesu! Ndipo walikuja watumishi wa Mungu akiwepo Pastor (Mchungaji) huyu hapa, wakanipokea mtoto na kaniambia tulia umefika Ufufuo na Uzima. Mungu atamfufua mtoto wako. Wakati huo mtoto wangu wa pili kwa kuona hofu ya mdogo wao kukata roho akapoteza fahamu; lakini basi, Mungu hakuniacha aliwajibika kwa nafasi yake juu ya Praygod, Oh Haleluya! Walimfanyia maombi mwanangu tangu ile saa nane ilipofika saa kumi kasoro Mumgu alimrudishia ‘pumzi’. Na sasa Prayod ni mzima na ninaahidi kwamba kusudi la Mungu juu ya mtoto wangu litimilike. Praygod amtumikie Mungu katika maisha yake”