Wednesday, June 30, 2010

KOREA 2010 CONFERENCES WITH PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA

MKUTANO WA KOREA MWEZI JULY 2010

Conference with Josephat Gwajima

July 13 - July 19, 2010 (Seoul - Great Faith Church)
July 21 - July 24, 2010 (Cheonan Sinbu-dong Church)

MKUTANO WA KOREA MWEZI JULY 2010

KOREA 2010 CONFERENCES WITH PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA:

Conference with Josephat Gwajima

July 13 - July 19, 2010 (Seoul - Great Faith Church)
July 21 - July 24, 2010 (Cheonan Sinbu-dong Church


Tuesday, June 8, 2010

Ibada ya Jumapili tarehe 6 June 2010 Watu wengi wampa Yesu Maisha yao

Makutano makubwa ya watu walikata shauri na kumpa Yesu maisha yao katika ibada ya Jumapili tarehe 6 June 2010.
Siku mbili baada ya kutoka Japan, Makutano makubwa ya watu "wamekata shauri" na "kumpa Yesu maisha yao" Kama wanavyoonekana hapa pamoja na Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akiwaongoza "sala ya toba".

Mchungaji Maximilian Machumu, RP (mwenye suti nyekundu) akiwa na kundi la waimbaji wake(wenye nguo nyeusi kulia) akiimba kibao cha wimbo wake mpya wa "ufufuo na Uzima" huku akisindikizwa kwa kushangilia na kumuimbia Sifa Mungu wetu YEHOVA. Pembeni yake ni Mchungaji Mwangasa, RP (Kushoto kwa mchungaji Max), Mchungaji Bryson,RP(kushoto kwa Mchungaji Mwangasa).

Monday, June 7, 2010

Sherehe ya Mapokezi katika Picha Mbalimbali

Waandhishi wa habari kutoka kituo cha Mlimani Television wakimhoji Mchungaji Josephat Gwajima, mara baada ya sherehe fupi ya kumkaribisha ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima katika bonde la kukata maneno

Baada ya kumchakaza shetani Japan sasa ni katika Bonde la ukata maneno

Mama Mchungaji, Mchungaji Grace Gwajima(RP) akiwa kanisani Ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima(Bonde la Kukata maneno, Kawe Tanganyika Packers, jijini Dar es salaam) katika Ibada ya Jumapili 6 June 2010, siku mbili baada ya kurejea kutoka Japan ambapo Mchungaji Josephat Gwajima alikuwa akiwasambaratisha miungu wa Kijapani(mashetani,majoka) kwa Jina lenye nguvu, uweza na Mamlaka, jina lipitalo majina yote, Jina la Yesu.

Sunday, June 6, 2010

Mama Mchungaji RP Grace Gwajima Akilisalimia Kanisa katika Sherehe ya Mapokezi


Mama Mchungaji, Mchungaji Grace Gwajima(RP) akilisalimia kanisa mara baada ya kurejea kutoka Japan ambapo alikwenda pamoja na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.

Mapokezi ya Mchungaji Gwajima katika Picha

Karibu Baba Gwajima...mmoja wa watoto wa kiroho wa Mchungaji Gwajima akionesha Bango kuanshiria yupo tayari kumpokea Mzazi wake katika BWANA.

Waandishi wa Habari wakimhoji Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima huku akiwapungia mkono watu waliojitokeza kumkaribisha nchini Tanzania.

Mchungaji msaidizi RP Yekonia Bihagaze na RP Maximilliam Machumu wakisindikizwa na maelfu ya watu wakimpokea Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kwa furaha ya ajabu mara baada ya Kutua na ndege ya Quater Airways kutokea nchini Japan.


Mapokezi Makubwa ya Mchungaji Gwajima yaifunika Dar na Utukufu wa Mungu

Mchungaji Josephat Gwajima, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa lenye maelfu ya watu (zaidi ya 30,000) “Nyumba ya Ufufuo na Uzima” akipokelewa kwa shangwe na nderemo na maelfu ya watu katika uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Mwl. J.K Nyerere, aliporejea tarehe 4 June 2010 majira ya saa 7 mchana kutoka nchini Japan ambapo alihubiri Mkutano wa Ulimwengu “ushahidi 12 wa Kibiblia kwa nini lazima wafu wafufuliwe” na kufundisha neno la Mungu Jijini Tokyo, Okinawa, Nagoya, Hiroshima, Nagasaki, Osaka na Kobe ambapo Mungu alitenda mambo makubwa katika uponjaji, ishara na maajabu ambayo hayaelezeki kwa kuwa utukufu wa Mungu uliijaza Japan yote kwa mkono wa mpakwa mafuta wake Mchungaji Gwajima.