Tuesday, June 8, 2010

Ibada ya Jumapili tarehe 6 June 2010 Watu wengi wampa Yesu Maisha yao

Makutano makubwa ya watu walikata shauri na kumpa Yesu maisha yao katika ibada ya Jumapili tarehe 6 June 2010.
Siku mbili baada ya kutoka Japan, Makutano makubwa ya watu "wamekata shauri" na "kumpa Yesu maisha yao" Kama wanavyoonekana hapa pamoja na Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akiwaongoza "sala ya toba".

Mchungaji Maximilian Machumu, RP (mwenye suti nyekundu) akiwa na kundi la waimbaji wake(wenye nguo nyeusi kulia) akiimba kibao cha wimbo wake mpya wa "ufufuo na Uzima" huku akisindikizwa kwa kushangilia na kumuimbia Sifa Mungu wetu YEHOVA. Pembeni yake ni Mchungaji Mwangasa, RP (Kushoto kwa mchungaji Max), Mchungaji Bryson,RP(kushoto kwa Mchungaji Mwangasa).