Tuesday, July 20, 2010

Ushuhuda katika picha : Amina Waziri aliyefufuliwa huko Yombo VitukaBinti Amina Waziri(mwenye kanga za njano kulia) au kwa jina lingine Happy mkazi wa yombo vituka moja kati ya sehemu maarufu hapa jijini Dar aliyefufuka siku ya jumanne tarehe 6 Julai 2010. Anayefuata ni mama mzazi wa binti aliyefufuka, Bi. Halima ambaye aliamua kumpa Yesu maisha yake kwa muujiza mkuu wa kumfufua binti yake. Kushoto kabisa mwenye tai nyekundi ndio shepherd (mtenda kazi) wa nyumba ya ufufuo na uzima aliyeomba maombi ya kurudisha na hatimaye kumfufua binti Amina saa chache baada ya kukata roho. Mwenye suti ya kijivu ni Mpakwa mafuta wa BWANA, Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima. Wote wakimtukuza Yesu kwa Ufufuo na Uzima.