Sunday, August 29, 2010

Sifa na Kuabudu katika Tamasha

RP David(Mchungaji David) -kushoto akiongoza ibada ya kusifu na kuabudu katika Tamasha la Muziki wa Injili ambapo misukule waliorudishwa kutoka msukuleni walioneshwa tena kwa mara nyingine katika viwanja vya Tanganyika Packers.

Maelfu ya watu katika Tamasha la Maajabu ya watu waliorudishwa kutoka msukuleni
Maelfu ya watu wakiwa katika ibada katika bonde la kukata maneno(Nyumba ya Ufufuo na Uzima) Kawe jijini Dar es Salaam.

Christina Shusho Katika Picha

Mama Mchungaji (Mchungaji Grace Gwajima) akimtukuza BWANA wakati akimsindikiza Christina Shusho alipokuwa akipiga kibao chake.
Christina Shusho akiimba kibao chake kinachokwenda kwa jina la Mtetezi wangu yu Hai (My reedemer lives). Kibao hiki ni moja kati ya kazi nzuri za huduma anazofanya dada huyu ambaye ni mkali katika medani ya muziki wa Injili.

Christina Shusho akiimba ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima katika Tamasha kubwa la Miujiza anayofanya Yesu. Misukule ambao ni watu walichukuliwa na shetani na hatimaye Yesu kuwarudisha wanaoneshwa leo.


Muimbaji Maarufu nchini Tanzania, Christina Shusho akiimba kibao chake cha mtetezi wangu yu hai. Muimbaji huyu anafanya vizuri sana katika medani ya muziki wa injili. Katika picha hii akiimba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Kawe jijini Dar es Salaam.

Mwanamapinduzi Mch. Max akiimba wimbo wakeMchungaji Maximillian Machumu ambaye ni mchungaji msaidizi ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima(Resident Pastor) akiimba kwa hisia zote kibao chake kinachobeba Albamu yake mpya inayokwenda kwa Jina la Saa ya Ufufuo na Uzima. Albamu hii ina kibao maarufu kiitwacho saa ya ufufuo na uzima. Kama unataka kununua Albamu hii, tafadhali fika Kawe katika viwanja vya Tanganyika Packers ulizia Albamu ya Mwanamapinduzi utaipata.

Tamasha la Miujiza Mikubwa-Bonde la kukata maneno

Bendi ya Mwanamapinduzi Mchungaji Maximilliam Machuma, pembeni ni Mkewe na waimbaji wa Bendi ya Mwanapinduzi RP Max.
Rachel Marlon akimtukuza BWANA leo katika Tamasha. Hapa Ilikuwa muda wa Praise and Worship. Yaani Ibada ya Sifa ya Kuabudu

Martha Mwaipaja, akimtukuza BWANA ndani ya Tamasha la Miujiza katika Bonde la kukata maneno ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima iliyopo Kawe jijini Dar es Salaa.


Maelfu na maelfu ya watu waliokuja katika ibada ndani ya nyumba ya ufufuo na Uzima. Leo misukule waliochuliwa wataoneshwa live na kuelezea nani aliyewachukua, chakula chao na mambo mengine mengi ya kushangaza.

Live Live Yanayojiri ndani ya Tamasha-Ufufuo na Uzima

Platform Kwaya wakiimba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Katika Tamasha kubwa la Miujiza ya Yesu Kristo. Misukule zaidi ya 400 kuoneshwa leo live.Na hapa ibada inaendelea.