Sunday, August 29, 2010

Christina Shusho Katika Picha

Mama Mchungaji (Mchungaji Grace Gwajima) akimtukuza BWANA wakati akimsindikiza Christina Shusho alipokuwa akipiga kibao chake.
Christina Shusho akiimba kibao chake kinachokwenda kwa jina la Mtetezi wangu yu Hai (My reedemer lives). Kibao hiki ni moja kati ya kazi nzuri za huduma anazofanya dada huyu ambaye ni mkali katika medani ya muziki wa Injili.

Christina Shusho akiimba ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima katika Tamasha kubwa la Miujiza anayofanya Yesu. Misukule ambao ni watu walichukuliwa na shetani na hatimaye Yesu kuwarudisha wanaoneshwa leo.


Muimbaji Maarufu nchini Tanzania, Christina Shusho akiimba kibao chake cha mtetezi wangu yu hai. Muimbaji huyu anafanya vizuri sana katika medani ya muziki wa injili. Katika picha hii akiimba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Kawe jijini Dar es Salaam.