Monday, September 20, 2010

Tunakwabudu YEHOVA


Tunakwabudu maana wewe ndiwe Mungu wetu, "Nitayainua macho yangu niitazame milima, msaada wangu utatoka wapi?Msaada wangu uu katika BWANA aliyezifanya mbingu na nchi" Zaburi 121:1-2
.

Wafu lazima wafufuke na Watu waje kwa Yesu


Resident Pastor-RP Bryson ambaye ni mchungaji msaidizi katika nyumba ya Ufufuo na Uzima, akihubiri neno la uzima katika ibada ya leo jumapili, 19 September 2010 ambapo mamia ya watu waliamua kukata shauri na kumpa Bwana Yesu maisha yao.

Jackson Benty Ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima

Jackson Benty muimbaji mkongwe wa nyimbo za injili akiwa ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima katika ibada ya leo tarehe 19 Septemba 2010. Jackson aliimba jumla ya vibao vyake vinne ikiwemo na kile kinachosema “Wewe ndiwe Mungu”.
Jackson Benty akimwabudu BWANA ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe Tanganyika Packers.


Sunday, September 19, 2010

Jane Misso Live Katika Bonde la Kukata Maneno

Saa chache kabla ya kufanya uzinduzi wa albamu yake katika ukumbi wa Diamond Jibulee, Muimbaji Maarufu nchini wa muziki wa Injili Jane Misso akipiga kibao chake kinachokwenda kwa Jina la "Oh moyo". Muimbaji huyu alifika ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima (Bonde la kukata maneno) akiambatana na rafiki yake ambaye ni Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya, Bi. Peace Muluu

Jane Misso
Jane Misso akiwa na wachungaji wa Nyumba ya ufufuo na Uzima, kutoka Kushoto ni RP Mwangasa, anayefuta ni RP Maximilian Machumu a.k.a Mwanapinduzi. Kuanzia kulia ni RP Joyce Mvula, RP Jane Brown na RP Kamzee(mwenye shati la bluu)
Wapenzi wa muziki wa injili ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima wakimshangilia BWANA wakati Jane Misso akipiga kibao chake maarufu saa chacke kablya ya Uzinduzi wa albamu yake.
Mwanamapinduzi, RP Maximilian Machumu na RP Kamzee wakimsindikiza Jane Misso alipokuwa akiimba.

Jane Misso
Maelfu ya watu wakimshangilia BWANA pale Jane Misso alipokuwakiimba Live ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe, Tanganyika Packer, Jijini Dar es salaam.

Ni Mwendo wa Viriba Vipya

Saraphina akiimba kibao chake cha Sifa Zivume
Peter akiimba wakati wa ibada ya Sifa

Veraikunda akimwimbia YEHOVA

Hivi karibuni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania almaarufu kama Nyumba ya Ufufuo na Uzima ameanza mkakati mahususi wa kuibua vipaji vya waimbaji wapya wa Muziki wa injili Tanzania. Mkakati huu una lengo la kuibua viriba vipya vyenye divai mpya.

Viriba vipya vilivyoaanza kumshambulia shetani kwa mtindo wa injili ya uimbaji ni Pamoja na Peter, Veraikunda na Saraphina.Waimbaji wengine wengi wanatarajiwa kutambulishwa hivi punde.Ili uweze kuwaona waimbaji hawa wakiwa live usikose kuja kanisani jumapili ijayo ya tarehe 26 Agosti, ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe katika viwanja vya Tanganyika packers.