Sunday, September 19, 2010

Jane Misso Live Katika Bonde la Kukata Maneno

Saa chache kabla ya kufanya uzinduzi wa albamu yake katika ukumbi wa Diamond Jibulee, Muimbaji Maarufu nchini wa muziki wa Injili Jane Misso akipiga kibao chake kinachokwenda kwa Jina la "Oh moyo". Muimbaji huyu alifika ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima (Bonde la kukata maneno) akiambatana na rafiki yake ambaye ni Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya, Bi. Peace Muluu

Jane Misso
Jane Misso akiwa na wachungaji wa Nyumba ya ufufuo na Uzima, kutoka Kushoto ni RP Mwangasa, anayefuta ni RP Maximilian Machumu a.k.a Mwanapinduzi. Kuanzia kulia ni RP Joyce Mvula, RP Jane Brown na RP Kamzee(mwenye shati la bluu)
Wapenzi wa muziki wa injili ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima wakimshangilia BWANA wakati Jane Misso akipiga kibao chake maarufu saa chacke kablya ya Uzinduzi wa albamu yake.
Mwanamapinduzi, RP Maximilian Machumu na RP Kamzee wakimsindikiza Jane Misso alipokuwa akiimba.

Jane Misso
Maelfu ya watu wakimshangilia BWANA pale Jane Misso alipokuwakiimba Live ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe, Tanganyika Packer, Jijini Dar es salaam.