Sunday, September 19, 2010

Ni Mwendo wa Viriba Vipya

Saraphina akiimba kibao chake cha Sifa Zivume
Peter akiimba wakati wa ibada ya Sifa

Veraikunda akimwimbia YEHOVA

Hivi karibuni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania almaarufu kama Nyumba ya Ufufuo na Uzima ameanza mkakati mahususi wa kuibua vipaji vya waimbaji wapya wa Muziki wa injili Tanzania. Mkakati huu una lengo la kuibua viriba vipya vyenye divai mpya.

Viriba vipya vilivyoaanza kumshambulia shetani kwa mtindo wa injili ya uimbaji ni Pamoja na Peter, Veraikunda na Saraphina.Waimbaji wengine wengi wanatarajiwa kutambulishwa hivi punde.Ili uweze kuwaona waimbaji hawa wakiwa live usikose kuja kanisani jumapili ijayo ya tarehe 26 Agosti, ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe katika viwanja vya Tanganyika packers.