Friday, December 31, 2010

SHANGWE ZA MWAKA MPYA 2011 ZINAENDELEA

Mch. Yekonia Bihagaze-RP, akisisitiza jambo wakati akimkaribisha Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima katika Ibada ya Mkesha wa Kuukaribisha Mwaka Mpaya leo tarehe 1, Januari 2011.

SHANGWE ZA MWAKA MPYA 2011 ZINAENDELEA

Shangwe na nderemo katika Nyumba ya BWANA, maelfu ya watu wakisherehekea ujio wa Mwaka wa Mavuno .........
Taswira ya Candle Lighty Party ya mwaka Mpya inavyoonekana katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Kawe-Tanganyika Packers. shamrashamra za mwaka mpya bado zinaendelea...

SHANGWE ZA MWAKA MPYAA

Na hili ndilo Box kubwaaaaa ambalo ndani yake tumeweka maombi 10 ya kila mmoja wetu na tunamuomba Mungu ajibu mamobi hayo ndani ya Mwaka Mpyaa 2011
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa live katika Madhabahu akiukaribisha MWAKA MPYA kwa Shangwe kubwaa akifurahia kwa kucheza pembeni yake mwenye suti nyekundu ni Mchungaji Maximillian Machumu-RP, na kulia kwake ni Mchungaji Winner Mbasyula-RP

Mch. David-RP, Mch. Bryson Lema-RP na Mch. Maximillian Machumu-RP wakishangilia kwa shangwe kubwa sanaa kuukaribisha Mwaka Mpya 2011

CANDLE PARTY YA MWAKA MPYA

Hivi ndivyo ilivyokuwa mara tu baada ya kufikia saa 6:00 usiku wa leo, na Nyumba ya Ufufuo na Uzima ilifurika MOTO wa mishumaa uliwashwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wakati wa Ibada ya Kuukaribisha MWAKA MPYA 2011. Kwa niaba ya Mchungaji Kionongozi, Josephat Gwajima, information ministry inawatakieni nyote HERI YA MWAKA MPYA 2011. TIA MUNDU WAKO UKAVUNE SASA!

Video ya Baranaba Cassian katika ibada ya sifa

WAIMBAJI KATIKA IBADA YA SIFA

Barnaba Mwana wa Faraja
Barnaba Cassian a.k.a Mwana wa Faraja
Platform Kwaya wakimsindikiza Odilia katika sifa......
Anna
Anna
Saraphina Urio
Muimbaji Odilia akimsifu BWANA katika ibada ya Sifa........

IBADA YA MKESHA LIVE: MWAKA MPYA 2011

Mwanamuziki Brandina akimsifu Bwana katika ibad ya kuukaribisha mwaka Mpya katika bonde la kukata maneno kawe, Tanganyika Packers...
Ibada ya sifa bado inaendelea na hapa Watanzania mbalimbali wako tayari kabisa kuupokea mwaka mpya wakiwa Nyumbani mwa BWANA, Ufufuo na Uzima......
Maelfu ya watu wakiwa katika ibada ya Mkesha ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima wakati ibada ya Sifa ikiendelea....

IBADA YA MKESHA LIVE: MWAKA MPYA


Ibada ya Mkesha inarushwa live hivi sasa kwa hisani kubwa ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Information Ministry inakuletea matukio yote ya kukaribisha Mwaka Mpya. Hivi sasa ni ibada ya Sifa na kijana unayemuona katika picha ni Muimbaji wa Muziki wa Injili anayejulikana kwa jina la Eliyona(kulia) akiimba muda mfupi uliopita. Tafadhali endela kufautilia matukio katika Blogu hii ya ufufuo na Uzima kutokea Kawe, Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Thursday, December 30, 2010

IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA

SWAHILI

Information Ministry kwa niaba ya Mchungji Kiongozi, Josephat Gwajima inapenda kuwaletea ratiba nzima ya Ibada katika Mkesha wa Mwaka Mpya. Ibada ya leo katika Kuukaribisha Mwaka Mpya inatarajiwa kuanza saa 3:00 Usiku mpaka saa 12:30 Usiku.

Tunawakaribisha Watanzania wote na watu kutoka Nchi zote. Unapokuja kanisani Mchungaji Kiongozi angependa uje na Karatasi utakayoandika MAHITAJI 10 ambayo wewe binafsi ungependa an unaomba Mungu akutimizie ndani ya MWAKA MPYA 2011. Makaratasi yatawekwa kwenye boxi moja kubwa kwa ajili ya Maombezi atakayofanya Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima.

Karibuni Nyote tuukaribishe Mwaka Mpya ndani ya Nyumba ya BWANA, Ufufuo na Uzima Katika Bonde la Kukata Maneno. Kumbuka mwaka 2011 ni mwaka wa KUTIA MUNDU WAKO na KUVUNA.

ENGLISH

On behalf of the Senior Pastor, Rev. Josephat Gwajima, information ministry brings to you the schedule for today's overnight service for the NEW YEAR Celebrations. The service is expected to start from 21:00 hours up to 00:30 tonight as we welcome the NEW YEAR.

We welcome all the Tanzanians, and people from every nation. When you come at the church tonight the Senior Pastor would like to see you coming with a piece of Paper in it you write 10 NEEDS of which you pray and wish that God should fulfill them for you. The papers will be put in the box ready for breakthrough prayers from the Senior Pastor, Rev. Josephat Gwajima

Welcome all of yuo once again, so we may concrete our heart before our LORD as we welcome the NEW YEAR 2011 in the house of life and Ressurection. Mind you that the NEW YEAR is the year of CASTING YOUR SICKLE and HARVEST!

Monday, December 27, 2010

FAIDA 11 ZA KUMTUMIKIA MUNGU

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, jumapili ya leo 26 Disemba 2010 ambayo ndiyo jumapili ya mwisho ya Mwaka amefundisha neno la Mungu juu ya faida 11 za kumtumika Mungu. Kwa ufupi kabisa tumekuandika faida hizo. Tunakushauri upate nakala yako ya CD au DVD kwa kupiga simu namba +255 716 369190 au fika Kawe-Tanganyika Packers katika Viwanja vya Nyumba ya Ufufuo na Uzima katika kontena letu linalouza vitabu na utajipatia nakala yako. USIPITWE na Baraka hizi za kumtumikia Mungu chukua nakala yako Sasa.

Faida za Kumtumikia Mungu kwa ufupi:- Kutoka 23: 25-29

1. Atabariki Chakula Chako

2. Atabariki Maji yako

3. Atakuondolea ugonjwa katikati yako

4. Hapatakuwa na Mwenye Kuharibu Mimba

5. Ataondoa Utasa

6. Hesabu za siku zako ataitimiza

7. Atatuma Utiisho wake mbele yako

8. Atawafadhaisha wote wakufikirio

9. Adui zako watakuonyesha maungo yao

10. Atapeleka mavu mbele yako; watakao mfukuza Mhivi, na Mkaanani na Mhiti wote watoke mbele yako

11. Ukimtumikia Mungu, atakuheshimu- soma Yohana 12: 26

Nitakutumika BWANA

Maelfu ya watu waliomua Kumtumikia BWANA baada ya Kujifunza faida 11 za Kumtumika BWANA. Neno la Msingi katika Somo hilo la faida za kumfuata Yesu na lililofundishwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima (Hayupo pichani) linatoka KUTOKA 23: 25 na MATHAYO 27: 55

Sunday, December 19, 2010

Yaliyojiri Leo Katika Ibada 19 Disemba 2010

RP David, Akiongoza Ibada ya Sifa kwa Kulikung'uta gitaa la Solo huku pembeni yake MP Peter akimsindikiza kwa kucheza katika ibada ya leo tarehe 19 Disemba 2010
Omega Mwangella akipiga keyboard wakati wa Ibada ya Sifa na Kuabudu katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima.

Maelfu ya Watu Kubatizwa Siku ya Mwaka Mpya

Maelfu ya watu wakiwa ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Jumapili ya leo tarehe 18 Disemba 2010 ambao wanatarajiwa kubatizwa UBATIZO WA KIBIBLIA katika siku ya Mwaka Mpya. Kwa wale wote waliompokea Yesu (Kuokoka) lakini hawakuwahi kubatizwa Ubatizo wa Kibiblia Mnakaribishwa kufika Kawe Tanganyika Packers Alhamisi tarehe 23 Disemba 2010 katika Semina Maalumu ya Ubatizo wa Kibiblia itakayotolewa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima

Thursday, December 16, 2010

Matukio katika Picha Jumapili tarehe 12 Disemba 2010"Pepo mchafu nakuamuru mtoke huyu na usimwingie tena kwa Jina la Yesu"....... Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akitoa pepo mchafu (unclean sprit)

Pastor Christian casting out demons in the house of life and resurrection (Nyumba ya Ufufuo na Uzima)


Mchungaji kiongozi akihudumia maelfu ya watu katika viwanja vya ufufuo na uzima (Kawe Tanganyika Packers)... BONDE LA KUKATA MANENO

Aliyefufuliwa kupitia maombi ndani ya simu ya Mkononi katika Picha

Agnes Mrema akiwa katika pozi baada ya Kutoa Ushuhuda wa kufufuka kwake ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima-Kawe jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers jumapili ya tarehe 12 Disemba 2010
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akimhoji mtoto wa Agnes Mrema aliyefufuka baada ya kuombewa alipokuwa maiti kupita simu ya mkononi.


Mtoto wa Agnes Mrema akielezea namna miujiza mikuu ya kufufuka kwa mama yake ilivyotendeka.Familia ya Agnes Mrema katika picha ya Pamoja ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima.

MIUJIZA: Maiti yafufuka kupitia maombi ndani ya simu ya mkononi

Agnes Mrema kutoka kushoto mwenye nguo ya damu ya mzee akiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wakati akitoa ushuhuda kanisani ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima


Na Information Ministry

Miujiza mikubwa yatokea ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima baada ya mmoja wa Wachungaji wasaidizi (MP-Ministry Pastor) kupiga majeshi (maombi) kupitia simu ya mkononi na kumfufua Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Agnes Mrema.

Mama huyo alijitokeza jumapili hii kutoa ushuhuda wa jinsi alivyokufa na hatimaye kufufuka kutoka kwa wafu. Mama huyo aliyekuwa na watoto wake wote wakati akitoa ushuhuda huo aliulezea umati mkubwa wa watu zaidi ya 30,000 juu ya namna alivyochukuliwa kwa nguvu na kutaka kuingizwa shimoni.

Katika ushuhuda wake mama huyo aliyekuwa akihojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alikuwa na haya ya kusema “nilianza kuumwa kichwa na kuwashwa mwili mzima muda wa siku 21. Siku ya ijumaa tarehe kumi mwezi Disemba mwaka 2010 nikaona wanakuja watu wenye maumbo ya ajabu na wanatisha sana wakanifunga miguu na kumpeleka kijijini ambako shimo lilikuwa limeshaandaliwa kwa ajili yangu. Baada ya hapo nikaona kuna mtu ananisukuma nisiingie shimoni, ghafla nikafufuka”

Wakati hayo yote yakiendelea katika ulimwengu wa roho, mchungaji msaidi ngaza ya MP (Ministry Pastor) alikuwa akiiombea maiti ya mama huyo ambayo aliagiza iwekewe simu masikioni naye akaanza kuporomosha maombi ya nguvu ya kurudisha. Baada ya muda mfupi maiti hiyo iliinuka kwa nguvu na na pumzi ikamrejea akawa mzima.