Sunday, February 26, 2012

Ushuhuda wa Ibrahim ambaye mke wake alikufa kwenye mazingira tata.

Ibada ya Jumapili 26 Februari 2012

Ushuhuda wa Ibrahim athumani ambaye mke wake alikufa kwenye mazingira tata.

Mimi nilikaa na kukulia Arusha, na nilipata kazi na nikapata hela nyingi, maana niliajiliwa mgodini, basi nikaenda kwetu same na kujenga nyumba kwaajili ya wazazi wangu ili baba na mama yangu wakae. lakini cha ajabu baba akaniambia kuwa mama yako siwezi kuishi naye tena, na sitakaa kwenye hiyo nyumba labda unijengee nyingine. basi nikamwambia nitamjengea...

Basi baada ya muda baba akawa anasema mtaani, kuwa eti najidai na hela. Na kuwa mama yangu ananipa kiburi. Na Huo ulikuwa mwaka 2004 na baada ya muda nilipigiwa simu kuwa baba mkwe anaumwa. Kwa hiyo mke wangu akaamua kwenda lakini alipofika akaanza kuwashwa sana na akaanza kuumwa. Basi nikamwambia mke wangu arudi nyumbani, kwa kipindi kile nilikuwa mwislamu safi. Basi kumbe kule nje baba yangu akawa akasema mke wangu ndio ananiletea kiburi ili nisimsaidie. Na atanionyesha Mimi na huyo mke wangu.

Kwa kuogopa nikaamua kuhamia dar es salaam, basi mke wangu akazidi kuumwa nikampeleka hospitali nyingi , Kama muhimbili, Kenya, bugando na kcmc na hapo nikamwacha hospitali ya kcmc bila kuwa na matumaini kwa kuwa madaktari walikuwa hawajui ni aina gani ya ugonjwa unaomsumbua. Basi nikarudi dar. Kuangalia watoto.. Maana ilikuwa miezi minne nazunguka hospitalini. Basi kulikuwa na daktari mmoja mkongo akasema mke wako ni msukule mpelekeni kwenye maombi, na kwasababu kwa kipindi hicho nilikuwa mwislamu swala tano, sikukubali aende hospitali.. Basi baba aliendelea na maneno kuwa mke wangu lazima afe hata nimpeleke wapi. Akasema kuwa hata nimpeleke nje ya nchi atakufa tu.

Baada ya siku mbili baadaye mke wangu akafa, basi baba yangu akaja msibani , cha ajabu nilipomaliza kuzika tu, baba sikumwona tena. . Basi baada ya kumzika mke wangu , siku nne tu wakaja mashehe wengi sana nyumbani karibu kumi na kitu hivi. wakanishawishi nioe tena, nikawambia yaani siku nne tu mnanishauri nioe tena. Nikakataa kuwa sitaoa tena.

Ghafla siku moja nikiwa nimelala nyumbani nikasikia mlango ukigongwa, na mlangoni nikasikia sauti ya mke wangu ikinisalimia, nikakimbia kufungua mlango na cha kushangaza sikumuona mtu, hapohapo nikaanguka na kuzimia ,sikuamka mpaka kesho yake.. Na nilipoamka nikakuta mashehe wengi nyumbani, wakaniambia huo ni mzimu wa mkeo, wakaja na madawa mengi wakaniambia nitumie ili nimsahau nikakataa kutumia madawa yao nikasema mke wangu hajafa.

Basi kwa sababu ya uoga nikawaita ndugu zangu karibu 6 , nyumbani kwangu. siku moja nikiwa na ndugu zangu tumelala sebuleni, usiku mke wangu akanitokea tena.. Na hapo alipotokea nikamfinya mdogo wangu ili aamke naye aone lakini hakuamka wala kusikia, mke wangu akaniambia saa ya ukombozi imefika. Na hapo tuliongea karibu dakika 45. Baadaye nikamwambia natakaka nije alipo nilipomfuata akapotea na sikumwona. Nikaangusha friji na meza. Ndipo ndugu zangunwalipoamka. Na asubuhi mkono wa mdogo wangu ulivimba kwa vile nilvyokuwa nikimfinya..

Basi nilikuwa mwislamu mzuri kipindi hicho , nikamwambia mama kiongozi wa kiislamu, naye akaniambia niombe dua ili asipatikane tena. Akaniambia nitumie ubani, ili kumfanya asinitokee tena. Mimi nikamkatalia kwa kumwambia siwezi omba hiyo dua maana mke wangu hajafa.

Siku moja nikiwa nimepanda kwenye gari, nikazozana sana na konda, na hapo nilikuwa narudi dar . nilikuwa nimepanga nikifika dar. Niende nimpige risasi baba, basi ndani ya gari nilikuwa nimekaa na mzee fulani simjui , akanisii sana nimuelezee matatizo yangu, nikakataa lakini nikajikuta nimemueleza. Na nilipomwambia ,akanielekeza niende kanisani ufufuo na uzima. na nikakutana na Mch Adriano .bakaniombea na nikawa naendelea kuja na mkesha. Ingawa sikuwa na imani kubwaa..
Ijumaa moja nikiwa kwenye mkesha akaletwa mama mmoja aliyekuwa amekufa, tukaenda kumuombea nikapenya kuona kama amekufa kweli, nikamgusa alikuwa amekufa basi baada ya maombi kama saa hii akafufuka, lile jambo likanipa imani kubwa sana.. Na ndipo imani ikaiingia kuwa mke wangu anaweza kurudi.

Sikuchache, baadaye nikapigiwa simu kuwa mke wangu ameonekana anaosha vyombo boko. Na hapo nilienda nikakuta mwenye kibanda kile amefunga kibanda na hayupo tena amekwenda same. Na huyu mama alikuwa rafiki wa familia yetu kwa kuwa alikuwa karibu na baba yangu. Kifamilia nikashangaa kumbe ndiye aliyekuwa amepanga mbinu moja na baba.... Na hili ni tukio lililotokea kama wiki tu imepita.... Naamini Mungu anaweza... Na atamtudisha mke wangu....
Amen... Mungu akubariki.

Ushuhuda wa kijana Eliya ambaye alikuwa akiishi na jini bila kujua..

Ibada ya Jumapili 26 Februari 2012

Shuhuda ya kijana Eliya ambaye alikuwa akiishi na jini bila kujua..
Eliya :-
Nilikuwa zanzibar kibiashara na nilikuwa nafanya biashara ya kuuza computer, ambazo nilikuwa nazifuata huko. Nikiwa katika mapumziko Zanzibar maeneo ya forodhani, na wa dada wawili wakaja wakaniambia tunahitaji kampani, kwakuwa nilikuwa bar. Wakniuliza una mtu, basi nikasema hapana, basi wakaja na tukaanza kunywa, baada ya muda tukiendelea kunywa. Wakaniuliza jina langu na shughuli zangu, nami nikawatajia.

Kesho yake asubuhi wakati nimetoka kutafuta riziki nyuma yangu, nikashangaa imesimama gari, na nikawaona wadada wale wale ambao niliwaona jana yake. Basi waliniomba niende nao nikawambia naenda kazini, wakanisihi ninywe nao supu. Basi baada ya hapo siku ile ikapita tena.

Siku moja nikiwa mwenge, gari aina ya vx lilipaki karibu nami ( namna alitaja ila tunaziifadhi) . Na pale akatoka yule yule binti aliyemuona Zanzibar na safari hii alikuwa mmoja. Nikamwambia naenda ofisini. Akaniambia tuingie kwenye gari na nikapanda. Na Yule binti akanipeleka hotelini, basi yule binti akaniambia Nina kitu cha kunieleza nikamshawishi aniambie. Basi akaniambia kuwa anaomba tuwe marafiki , basi nikamkubalia na nikaanza kumchukulia kama dada yangu. Basi tukaondoka na kuendelea kuwasiliana. basi baada ya siku chache nilienda zanzibar na Yule dada alinisaidia kutafuta mzigo na badala ya kukaa siku tano akakaa siku tatu........

.......ameruka baadhi ya matukio kwaajili ya muda kuwa mdogo.....

Nilikuwa msaada kwake kwa kipindi cha mwanzo, lakini baada ya muda, Mimi ndio nikaonekana ndiye ninaye hitaji msaada, kwa kuwa alikuwa na hela ambazo awali hakujidhihirisha.. Mwanzoni alikuwa Kama mtu asiye na hela.. Akawa ananipa hela siku baada ya siku. Basi nikafanikiwa kujenga nyumba mbili mlandizi, na baada ya hapo nilishangaa alikuwa anaendelea kunipa pesa, mwanzoni alinipa laki 7 lakini ilifikia kipindi ananipa hadi sh. Milioni 40.. Na bila kujua anatoa wapi kwakuwa hakuniambia anafanya kazi gani. Na hapo huyo msichana akanipa gari, alinipa vitu vingi. Na baada ya muda mazoea yakazidi basi nikamshirikisha kuwa kama inawezekana tuwe pamoja kama mtu na mchumba wake. Alikubali na kwa wakati huo nilikuwa sijui anapoishi na hapo nikamuuliza akaniambia baba na mama yake wako Nugwi Zanzibar. Basi tukakubaliana tuanze kwa kwenda kwa wazazi wangu ambao wapo singida,

Tukapanaga safari , tukiwa safarini kuelekea singida, Dodoma. Akapotea ndani ya gari tulilokuwa tumepanda. Maana yeye alikuwa amekaa siti ya dirishani hapo , nikawauliza abilia wengine nao walikuwa hawajui, . Na mara wakati tunajadili yule binti aliyekuwa akiitwa Hawa, akarudi . basi kukawa kimnya kila mtu alikuwa anaogopa. tuliposhuka kwa mapunziko mzee mmoja amabaye alikuwa abiria akaniambia nishuke.. Maana nitawaletea matatizo. Nikashuka naye baada ya kunisisitiza abiria kunisisitiza.

Tukiwa dodoma, nikatamani nimuone mguu wake, maana niliambiwa awali kuwa jini anakuwa na kwato. Kwa kuwa kwa wakati huo nilikuwa sijawahi kuona miguu yake, tokachukua chumba pale Kilimanjaro hotel Dodoma, akatoka kidogo, lakini nilimvizia akirudi nione miguu yake, cha ajabubbaada ya kurudi Yule binti akakataa kupumzika na alikataa kuvua viatu pia. Basi kwakuwa alikuwa na nguvu kunizidi basi nikapanga kumkimbia, kwa kuwa nilianza kuingiwa na hofu, nikamwambia kwa kumdanganya kuwa naenda kununua vocha. Lakini nilipotaka kukimbia kufika getini nikakutana naye anatokea ninakoelekea. Basi ikabidi nirudi ili nimuangalie miguu asubuhi wakati wa kuamka, Asubuhi nilipoamka yeye akaniwekea mkono kichwani hapo nikalala hadi akaoga akamaliza. Nakuja kuamka baada ya masaa bila kujua usingizi niliupatia wapi..

Basi kesho yake tukapanda gari lingine la kuelekea singida. Tukiwa njiani, manyoni polini, ghafla akaanza kupiga kelele akisema sitaki kwenda kwenu siwezi kwenda, na sitaki kwenda.. Basi gari likasimama manyoni singida na kwa kuwa sikuwa na jinsi ikabidi nishuke na tulipofika tu akatoweka tena. hapo nikasema sina jinsi zaidi ya kukimbia nikakimbia umbali kama wa kutoka Kawe hadi ubungo kufika tu nataka nipumzike nikamuona kutokea mbele, na akawa ananihoji unaenda wapi.. Nikamuomba msamaha nikataka kwenda polisi nikakutana naye anatoka polisi. Nikawa sina jinsi zaidi ya kumtii tu. basi tukarudi dodoma, na hapo akainua mikono yake ikamwagika kitu Kama maji, akanimwagia mguu akiniambia tutaona nani baba Kati yako na Mimi. Baada ya hapo .. Yeye aka toweka

Nikiwa Dodoma nikaamua kutafuta kanisa.. Kwakuwa alikuwa amechukua hela zote, Na nikapata kanisa nikamwelezea Mch. Na akaniombea na akaniambia nipumzike na ghafla yule binti akatokea hofisini nilipomuelezea Mch. , mchungaji akakimbia kutoka ofisi na Mimi nikakimbia kumfuata mchungaji basi Yule Mch. Akaniambia kamtafute pastor Max. Wa ufufuo na uzima ndiye atanisaidia kwa kudai Mimi nitamletea matatizo.

Basi walinipa nauli kidogo na nikaja dar. nilipofika dar. Nikaenda kwenye nyumba yangu mikocheni nikaenda lakini sikuikuta tena eneo amabalo ilikuwepo awali. Na nikaamua kuja kumtafuta Mch. Max. Basi nikaja kanisani na nikaombewa japo nilikuwa sina imani kabisa ndani.

Basi jioni yake nikatoka naelekea kutafuta chochote hapo kufika getini akanigusa na akanilazimisha turudi nyumbani.. Cha ajabu tulipokuwa na yeye ile nyumba nikaikuta Basi akaniambia anataka kwenda kwao Nugwi Zanzibar. Basi alipoondoka. Mimi nikaamua kuja kanisani kuonana na pastor max. Basi nikaamua kuondoka na nguo chache nikaja kanisani. Na hapo akaniombea na baada ya kuniombea akaniambia kuwa twende tukaione hiyo nyumba. Na tulipofika hatukukuta nyumba tena ambapo ndio palepale aliponipeleka awali na ndipo nilipokuwa asubuhi lakini si kuona nyumba tena. Tukakuta uwanja uko wazi.. Basi ndio nikaamua kumpokea Yesu. Amen

Wednesday, February 22, 2012

Matukio katika picha - Uzinduzi wa Hekima ya kiongozi


Poster inayoelezea lengo kuu la kipindi cha 'Hekima ya Kiongozi'


Mh. Samuel Sitta akionyesha cheti alichokabidhiwa na Mch. kiongozi Josephat Gwajima (kushoto) kama shukurani na kumbukumbu ya mahudhurio ya kipindi hicho.

Mh. Harison Mwakyembe akisalimia maelfu ya waumini wa Kanisa la 'Ufufuo na Uzima'
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika ibada ya Ufufuo na Uzima kama sehemu ya kipindi cha 'Hekima ya Kiongozi'.


Mh. Anne Kilango Malecela
Mh. James Lembeli katika madhabahu ya kanisa la Ufufuo na Uzima.


Mhe. Aloyce Kimaro akisalimiaMhe. Sitta akimkaribisha mpiganaji mwenzake kama alivyomtumbulisha Mhe. Hilda Ngoye


Mh. Samuel Sitta


Viongozi waliohudhuria kipindi cha Hekima cha Kiongozi
Viongozi pamoja na Wachungaji waandamizi wa kanisa la Ufufuo na Uzima katika hitimisho la kipindi cha 'Hekima ya Kiongozi'.

Sunday, February 19, 2012

Ushuhuda wa Kijana aliyechukuliwa msukule akiuza vizazi Kariakoo

Leo Jumapili 19 Februari 2012

Ushuhuda wa kijana aliyepotea na kupatikana., usiku wa kuamkia tarehe 18
Hassan William shelukindo

Kaka wa aliyepotea alianza kushuhudia....
Anasema huyu ni mdogo wake aliyetokea Tanga, na kuja Dar asubuhi ya tarehe 30, na alipanda gari la somoe kuja dar. Kaka mtu aliendelea kwa kusema, shemeji yake ndiye aliyemsindikiza mpaka kituoni na kumpandisha gari, tayari kwa safari ya kwenda Masasi shuleni.

Baada ya siku chache taarifa zilikuja kwa njia ya simu kuwa begi lake limekutwa karibu na feri, jijini dar es salaam, kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa begi hilo lilikaa wiki nzima. Ndipo kwa ruhusa ya polisi wakalifungua begi hilo, na ndani ya begi walikuta uniform za shule, na namba kadhaa za simu. Ndipo polisi wakamua kupiga ile simu na ilikuwa ya ndugu yake aliyekuwa tanga. Ndipo walipochukua hatua ya kupiga simu shuleni ili kujua Kama amefika huko. Cha kushangaza ni kuwa walipopiga simu shuleni wakaambiwa kuwa hajafika na anahitajika afike haraka.

Basi Mimi ( kaka wa Hassan ) nikaamua kuja kituoni feri ili kuhakikisha Hilo begi kama ni lake ( Hassan) ndugu zake waaenda kituoni kuhakikisha lile begi. Kaka wa aliyepotea anaendelea kwa kusema, walifika polisi, na akamkuta afande aliyejulikana kwa Jina la Afande Mshindo. Na baada ya kuhakikisha wakagundua kuwa ni begi la Hassan, na kaka wa Hassan anasema, yeye akawaza moyoni nitapata wapi kanisa ili lifanye maombi kwa ajili ya Hassan , basi akaamua kumuuliza yule afande, na Afande Mshindo akamwambia kuna kanisa la ufufuo na uzima, lipo tanganyika packers, Kawe.

Ndipo nikaamua kuja anasema kaka wa Hassan., nilipofika kanisani nikamkuta mchungaji anayeitwa Mch. Esther na Mch. Evetha. Kaka wa Hassan anaendelea kwa kusema siku hiyo waliomba kwa muda wa masaa 2, na alikuwa hajawahi kumlilia Mungu, lakini siku hiyo alilia. Baada ya maombi niliacha picha kanisani, na baada ya kwenda nyumbani niliota ndoto mbalimbali kuhusiana na mdogo wangu, basi kesho yake tukakuta karatasi za kusajili line ndani ya lile begi. Na wakaamua kupiga ile simu, na kumbe ilikuwa namba ya baba yake hassan , ambaye alimuomba amsajilie. Basi zikaja taarifa kuwa kuna mtu kakutana naye kariakoo, mtu huyo alidai kuwa alimkuta akiuza viazi. Basi Mimi (kaka wa Hassan ) nikaamua kwenda kufuatilia huko kariakoo, hapo wakawakuta watu wanaouza viazi wakawauliza, mmoja wao akasema wamemuona huyo kama nusu saa iliyopita. Na wakamtafuta kariakoo nzima siku hiyo ila hawakumuona.

Basi kaka mtu anasema akaamua kurudi central, akiwa kituoni akapokea simu ya shemeji yake walioachana naye muda mrefu kuwa amemuona, maeneo ya posta, alisema baada ya kumuona kupitia dirisha la daladala akaamua kushuka na kumfuata, alipotea gafla lakini baada ya muda mfupi akaonekana tena. Alipomuona yeye (Hassan ) akaishiwa nguvu. Na hapo polisi wakaja kumchukua kwa mahojiano na haya ndiyo aliyosema hassan.

Hassan anasema, yeye alijisikia kushuka kwenye gari ikwiriri wakati alipokuwa anaelekea masasi, na hapo alitembea kwa miguu kutoka ikwiriri mpaka hapa dar. Na alipofika hapa akaanza kumfanyia kazi mzee ambaye hamjui kwa sura.

Hassan alipokuwa kanisani amesema"..
Anasema anachokumbuka ni kuwa , Alipanda gari na anakumbuka namba ya siti aliyopanda, na anakumbuka alishuka njiani ikwiri, na akatembea kwa miguu hadi dar. Na alipofika akakutana na babu alikuwa amevaa kofia ya cherehani yaani barakashia, hakumbuki Jina la huyo babu kwa kuwa hakumtajia.
Mahojiano kadhaa ya baba Mch. Gwajima na Hassan na ndugu zake j2 hii.
Baba Mch..: Amepotea kwa siku ngapi?
Kaka.: Toka tarehe 30 mwezi wa pili na Jana ( 18.2.2012) ndio amepatikana na yeye amesema hajala kabisa siku zote hizo.

Baba Mch.: kitu gani kinakufanya husisikie njaa?
Hassan : mi sijui ila nakumbuka sikuwahi kula siku zote hizo.
Baba mch : Ulikuwa unauza na wakina nani viazi, na ulikuwa unalipwa, saa ngapi mpaka saa ngapi?
Hassan : . Nilikuwa nauza mwenyewe, nilikuwa silipwi, na tulikuwa tu nauza kuanzia saa 11 jioni hadi 12 hasubuhi

Baba Mch. : ulikuwa unalipwa na ulipookotewa ulikuwa unaenda wapi
Hassan. : Nilikuwa silipwi, na nilikuwa sijui nilikokuwa naelekea maana ufahamu haukuwa vizuri.

Baba mch. : Wewe mama ulikuwa unawaza nini?
Mama. Wa Hassan : Mi nilikuwa sielewi ila nilikuwa naomba hapo niletewe angalau mifupa ya mwanangu, uchungu wa mwana aujuaye mzazi.

Baba Mch : Dada unawaza nini?
Dada : Mimi namshukuru Yesu anaweza. Nawashukuru wachungaji waliomuombea kaka yangu, Mungu awabariki.

Baba Mch : Mjomba wewe unawaza nini, na unahisi alishuka kwenye gari kwasababu gani au ujeuri?
Mjomba :, mi namshukuru Mungu na hapo nadhani si ujeuri kwa kuwa hakuwa hivyo ila nadhani ni uchawi na nguvu za Giza.

Baba Mch : Kaka unadhani alikuwa hapendi shule?
Kaka. :. Hapana maana nilimpeleka mwenyewe shuleni na nikamuuliza Kama anapenda shule, na alijibu kuwa anapenda na asingeweza kushuka kwa sababu alikuwa anapenda shule. Na hii ndio ilinifanya nifanya nitafute kanisa kwaajili ya maombi.

Hili ni moja ya mambo makubwa ambayo Bwana Yesu Kristo anatenda, kupitia Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. Katika nyumba ya ufufuo na uzima.. Barikiwa...

SOMO: Mwachie aliyetumwa

Na Mchungaji Kiongozi, Rev. Josephat Gwajima
Jumapili-19 Februari 2012


Kutuma- ni hali ya kupewa ujumbe kwa ajili ya kupeleka palipo kusudiwa. Unaweza ukawa ujumbe wa familia au nchi. Mungu naye Ana kawaida ya kuwafumba watu duniani na Jumbe mbalimbali...

Maandiko yanayotaja uweza wa Mungu wa kutumia watu.

Kama hutaki matatizo mwachie aliyetumwa, kwa desturi Mungu huwa anatuma watu duniani na hii ni desturi ya Mungu. Yeremia 49:14 . Na hawa watu hutumwa kwa makusudi mbalimbali Kutoka 23:20 malaki 3: 1, mathayo 11:10 , watu wa dunia hii kwa kumuonea mtu anakupa pamoja nao, au anaishi katikati Yao huisikia kuwa hajatumwa, lakini hata kwenye biblia watu waliotumwa walikuwa wanaishi na kula kama watu wengine.

mifano ya watu waliotumwa kwenye biblia.
Marko 1:2 huyu ni Yohana mbatizaji, alitumwa kuandaa njia kwa ajili ya Yesu .
Hata Yesu mwenyewe alikuwa ametumwa Kutoka mbinguni lakini alitungwa mimba, akazaliwa, na Akaishi Kama watu wengine, Hesabu 20:16 Mungu anatabia ya kutumia. 2Samweli 12:1 zaburi 105:26. Mathayo 21:37 waamuzi 6:28 Mungu anatabia ya kutuma watu.
Mfano wa wanasayansi.
Wanasayansi wengi wa zamani amabao walikuwa wakristo na ni wavumbuzi wa zamani wa sayansi, mfano 1. isaack newton, 2. Boyle, na watu Kama wakina 3. kelvin waliogundua umeme hawa watu walikuwa wameokoka na hawa waligundua vitu mbalimbali. 4. Michael faraday Kama tulivyoona wagunduzi wa zamani wengi wanakubali kuwa Mungu yupo. 5. John Rey, 6. Creg Maxwell 7. Caros Linus, 8. Kepler. waliokuwa wameokoka.
Lakini ukiangalia maisha yao binafsi, utagundua maisha yao yakipita mambo magumu,
Mfano: isaack newton mama yake akiwa mjamzito, baba yake akafariki ... Hivyo mama yake akaenda kuolewa na mume mwingine, Na hapo newto akaenda kuishi kwa mjomba yake na katika maisha magumu na kutokana na maisha magumu yale , yakamfanya newton akazane kusoma kumbe mtu aliyetumwa kuibadili dunia na hapa lazima dunia imshikilie na kumzuia, lakini mwisho wa siku alikwenda na kumaliza wito wake.
Mfano mwingine ni Robert Boyle naye alizaliwa kwenye shida pia, Faraday pia Alipitia wakati mgumu kwenye maisha yake.

Maisha halisi ya sasa.

Tunapozungumzia kutumwa ni neno pana sana na hapa inaweza ikawa mtu katumwa kubadili nchi, familia, nyumba na Hali ya jamii nzima. Lakini dunia hii tuliopo ina system mbalimbali mfano. Dini, serikari, jeshi ambavyo vinazuia ujumbe wa aliyetumwa. Marko 1:2 , "palitokea mtu ametumwa....." unajikuta unakiu ya jambo fulani kufanikiwa, una kiu ya kufanikisha kitu fulani kinaweza kuwa cha familia au cha taifa na hapo hali ya maisha na umaskini ina kuzuia, na hii ni kawaida ya dunia kujaribu kuwashikilia watu waliotumwa..

Kumbe inawezekana kuwa Mungu amekutuma duniani, na hujijui na kwa vile dunia ilivyokushikilia inakufanya hata usahau kuwa umetumwa. Mfano: inawezekana umetumwa kuwa waziri wa mambo ya nje na hapo inakubidi upate elimu angalau, lakini dunia inakuzuia kwa kukuletea umaskini ili ukose elimu na mwisho wa siku ushindwe kufikia kwenye kule ulipotumwa.

Msaada kutoka kwa Mungu kwa Yule aliyemtuma.

Kama tulivyoona Mungu anadesturi ya kutuma malaika, binadamu ili kuitengeneza dunia kuishape dunia kuileta mahala pake... Na Mungu ili kuwasaidia aliowatuma huitikisa dunia kwa jambo fulani ili kufanya wale aliowatuma waingie kwenye system, na hapa ndio maana unaona hata nchi Kama Tanzania inapitia kwenye mtikisiko ikionyesha kuwa kuna watu waliotumwa na wanakusudiwa kuingia kwenye nafasi zao.

Mfano mwingine ni wa Ibrahim , ambaye ni baba wa Imani, na huyu aliahidiwa kuwa baba wa mataifa na ili kuwa baba wa mataifa lazima azae awe na watoto, lakini dunia( shetani) akaanza kupinga hiyo, kwa kumwekea utasa, na hapa tunajifunza kuwa kwa kila mtu aliyetumwa lazima atakutana na upinzani.
Mfano mwingine ni Musa , na Musa alipozaliwa tu , shetani akajua na alitumwa na Mungu kuunda taifa imara, la Israel na ndio maana alipozaliwa tu, Farao akaamuru watoto wote waangamizwe, na hapa tunajifunza kumbe ukiwa na kitu kikubwa cha Mungu , lazima utapingwa na kuzuiwa. Lakini Musa kimuujiza alienda kula mezani mwa Farao. Bila Farao kujua hadi wakati wake hutimie.
Kumbe aliyetumwa hawezi kuangamizwa hadi atimize hatma yake.
Kwahiyo Mungu anakwaida ya kuwasaidia wale aliowtuma, tunaona katika habari ya Musa alipokuwa mdogo, na hata yale mapigo aliowaandalia wamisri,

Mfano mwingine wa taifa la Israel, kipindi Sauli alipofanya machukizo... Mungu akamtuma nabii Samuel kwenda kumpaka Mafuta mfalme Daud . Mungu anakawaida ya kutuma watu. kwa hiyo samweli akamchagua na kumtia Mafuta daudi.
Vitu ambavyo vilimshikilia Daud Kama mpakwa mafuta.
1. Kudharuliwa na ndugu zake.
2. Yuko machungoni polini.
3. Alidharauliwa na watu wa taifa lake.
Lakini pamoja na yote daudi aliishia kuwa mfalme sawasawa na alivyoitwa.

Jambo la kufanya:
Ni muhimu kupambana vita vya kiroho ili kuondoa vizuizi vya dunia, ambavyo vinazuia watu waliotumwa... Kwa hiyo ni muhimu kusambaratisha nguvu ya shetani ili kutuachia watu tuliotumwa.

Sunday, February 12, 2012

Somo PART TWO: Kulishwa Chakula Ndotoni

Na Mchungaji Kiongozi-Rev. Josephat Gwajima
12 Februari 2012


Nini maana ya kulishwa Chakula ndotoni

Wachawi wapo an wanapenda kazi duniani, mfano kwenye vikao vyao usiku wanajadili mambo ya kuwafanyia watu baada ya mashaka kutumwa.. Duniani wachawi hata kuvaa vizuri ni sababu tosha kukuangamiza na hapo Jina lako linakuwa limes hakuwa kwenye vikao vya kichawi.
Kwenye biblia kuna vyakula vya aina mbili 1 kor 10: 1-3. chakula cha kutoka mbinguni chakula cha roho , Yohana 6 Yesu anasema " Mimi ni chakula kitokacho mbinguni" na chakula cha Kutoka chini, majini. Limetoka kuzimu. Ni muhimu kujua kuna chakula cha kiroho na chakula cha kimwili, chakula cha kutoka mbinguni na chakula cha Kutoka kuzimu.

Kwahiyo wachawi wanapokuwekea shetani wa balaa au wa mikosi ndani yako, Zakaria 3:1 shetani anaweza kukaa ndani ya mtu au karibu na mtu kutokea nje au anaweza ingia ndani... Yaani kupagawa yaani kuwa ( possessed ) na hapo wachawi watakuwa ili kumlisha Yule pepo aliye ndani yako Matendo 13:6-11 kwahiyo utamwona mtu anatafuna usiku ikionyesha kuwa lile pepo liliko ndani linalishwa chakula, ili likue na kupata nguvu zaidi.

Mshetani wapo aina mbalimbali

Majoka - yaliyo Shushwa pamoja na shetani Kutoka mbinguni.
Majini - wanaofuta mila za kiarabu.
Mizimu - mashetani ya ukoo.
Miungu - mfano sehemu nyingi za Asia nk.

Kwahiyo muda wachawi wanamtia nguvu Yule shetani, napo mtu yule ataota anatafuna au analishwa usiku. Watu wa namna hii unakuta tatizo linakua Kila kukicha kwasababu ya hivyo.
Unaweza hisi ni ndoto tu, kumbe rohoni wanakutia udhafu zaidi, ili ushindwe kuendelea... Na hapo tatizo linazidi kuwa kubwa zaidi.
Ndoto inaweza chelewa lakini itatimia....

Somo PART ONE: Asali ndani ya Mzoga

Na Mchungaji Kiongozi-Rev Josephat Gwajima
12 Februari 2012-Jumapili


Waamuzi 14:1- 8 Samson alimwuua simba na kwa kawaida katikati ya mzoga mtu angetarajia akute pameoza. Na alitarajia akute hata funza , lakini akakuta Asali ambayo si kawaida kukuta nyuki. Na akachua ile asali ili awape baba na mama yake, ni muhimu kujua kuwa kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafunndisho, kwahiyo andiko hili tunaweza kulilinganisha na andiko lingine...... 2wafalme 4:1- Hii ni habari ya mama mane ambaye alikuwa na made ni, na wadai wake walitaka kuchukua watoto wake wawe watumwa. Basi Yule mama alilia mbele ya mtumishi wa Mungu Elisha .

Jambo tunalojifunza kutoka kwenye Maandiko hayo( Asali ndani ya mzoga )

Baba na mama yake wlimkataza Samson kwenda kwa wafilisti lakini alikwenda na akaua simba na ndani ya mzoga wake alipata asali na akawapa baba na mama yake,
Mzoga ni nini?

Ni hile Hali ya kukukatisha tamaa mfano nchi Kama Tanzania ,inaonekana mizoga tabu, matatizo, migomo nk. Na hapa ni muhimu kujua katikati ya mzoga huo na matatizo itatoka asali ...ni muhimu kujua taifa Kama Marekani lilianza vizuri na Mungu, lakini leo ndio taifa linaloshinikiza ndoa za jinsia moja, nchi kama Uingereza nk. Lakini Africa ilianza kwa tabu, vita, kutomjua Mungu lakini wakwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza

Ndio maana hata Yesu walimdharau kwa kusema Nazareth anaweza tokea mwokozi , mji unaopuuzwa lakini alipoanza kuishi maisha yake yakabadilika, na sasa amepewa Jina lipitalo majina yote. Na nchi yetu ni vilevile.

Ni muhimu kujua hata maisha yetu yanaweza kuanza katika shida, matatizo, tupo katika shida lakini tunaye Mungu, na Mungu akiwa upande wetu hakuna aliye juu yetu. Kwa hiyo hakuna haja ya kukata tamaa kwa maana katikati ya mzoga itatoka asali, na pia ni muhimu kujua kuwa Samos kabla ya kupata asali alilazimika kumchanachana mwana simba. Na ili kupata asali nzuri je mwana simba ni nini? Mwana simba ni mafisadi, viongozi wabaya, matatizo yaliyopo. Kwahiyo tunatakiwa tuchanechane wana simba ili kupata asali baadaye kwa kutumia mamlaka tuliyonayo ( authority )

Wednesday, February 8, 2012

Mambo yalivyokuwa katika Ubatizo Mwaka Mpya 2012

Soda ya pamoja kwa ajili ya Afya ya mwaka Mpya 2012
foleni tayari kwa kubatizwa na RP Charles Maganga
foleni tayari kwa kubatizwa na RP Yekonia Bihagaze
foleni tayari kwa kubatizwa na RP Dr. Godson Issa Zacharia
Hapa soda zikiandaliwa kwa ajili ya afya ya mwaka mpya
Hapa RP Bryson Lema akimbatiza mmoja kati ya washirika
foleni tayari kwa kubatizwa na RP Maximilian Machumu
Hapa RP Maximilian Machumu akimbatiza mmoja kati ya washirika
Mchungaji Kiongozi, Rev. Josephat Gwajima akitoa maelekezo kwa ajili ya ubatizo
RP Mwangela akibatiza
Soda zikiandaliwa
Maandalizi ya ubatizo katikati ya Wachungaji waandamizi wa Ufufuo na Uzima wakiwa na
Mchungaji Kiongozi, Rev. Josephat Gwajima
Maelfu ya watu wakishuhudia ibada ya Ubatizo katika bahari ya hindi-kawe beach