Sunday, February 19, 2012

SOMO: Mwachie aliyetumwa

Na Mchungaji Kiongozi, Rev. Josephat Gwajima
Jumapili-19 Februari 2012


Kutuma- ni hali ya kupewa ujumbe kwa ajili ya kupeleka palipo kusudiwa. Unaweza ukawa ujumbe wa familia au nchi. Mungu naye Ana kawaida ya kuwafumba watu duniani na Jumbe mbalimbali...

Maandiko yanayotaja uweza wa Mungu wa kutumia watu.

Kama hutaki matatizo mwachie aliyetumwa, kwa desturi Mungu huwa anatuma watu duniani na hii ni desturi ya Mungu. Yeremia 49:14 . Na hawa watu hutumwa kwa makusudi mbalimbali Kutoka 23:20 malaki 3: 1, mathayo 11:10 , watu wa dunia hii kwa kumuonea mtu anakupa pamoja nao, au anaishi katikati Yao huisikia kuwa hajatumwa, lakini hata kwenye biblia watu waliotumwa walikuwa wanaishi na kula kama watu wengine.

mifano ya watu waliotumwa kwenye biblia.
Marko 1:2 huyu ni Yohana mbatizaji, alitumwa kuandaa njia kwa ajili ya Yesu .
Hata Yesu mwenyewe alikuwa ametumwa Kutoka mbinguni lakini alitungwa mimba, akazaliwa, na Akaishi Kama watu wengine, Hesabu 20:16 Mungu anatabia ya kutumia. 2Samweli 12:1 zaburi 105:26. Mathayo 21:37 waamuzi 6:28 Mungu anatabia ya kutuma watu.
Mfano wa wanasayansi.
Wanasayansi wengi wa zamani amabao walikuwa wakristo na ni wavumbuzi wa zamani wa sayansi, mfano 1. isaack newton, 2. Boyle, na watu Kama wakina 3. kelvin waliogundua umeme hawa watu walikuwa wameokoka na hawa waligundua vitu mbalimbali. 4. Michael faraday Kama tulivyoona wagunduzi wa zamani wengi wanakubali kuwa Mungu yupo. 5. John Rey, 6. Creg Maxwell 7. Caros Linus, 8. Kepler. waliokuwa wameokoka.
Lakini ukiangalia maisha yao binafsi, utagundua maisha yao yakipita mambo magumu,
Mfano: isaack newton mama yake akiwa mjamzito, baba yake akafariki ... Hivyo mama yake akaenda kuolewa na mume mwingine, Na hapo newto akaenda kuishi kwa mjomba yake na katika maisha magumu na kutokana na maisha magumu yale , yakamfanya newton akazane kusoma kumbe mtu aliyetumwa kuibadili dunia na hapa lazima dunia imshikilie na kumzuia, lakini mwisho wa siku alikwenda na kumaliza wito wake.
Mfano mwingine ni Robert Boyle naye alizaliwa kwenye shida pia, Faraday pia Alipitia wakati mgumu kwenye maisha yake.

Maisha halisi ya sasa.

Tunapozungumzia kutumwa ni neno pana sana na hapa inaweza ikawa mtu katumwa kubadili nchi, familia, nyumba na Hali ya jamii nzima. Lakini dunia hii tuliopo ina system mbalimbali mfano. Dini, serikari, jeshi ambavyo vinazuia ujumbe wa aliyetumwa. Marko 1:2 , "palitokea mtu ametumwa....." unajikuta unakiu ya jambo fulani kufanikiwa, una kiu ya kufanikisha kitu fulani kinaweza kuwa cha familia au cha taifa na hapo hali ya maisha na umaskini ina kuzuia, na hii ni kawaida ya dunia kujaribu kuwashikilia watu waliotumwa..

Kumbe inawezekana kuwa Mungu amekutuma duniani, na hujijui na kwa vile dunia ilivyokushikilia inakufanya hata usahau kuwa umetumwa. Mfano: inawezekana umetumwa kuwa waziri wa mambo ya nje na hapo inakubidi upate elimu angalau, lakini dunia inakuzuia kwa kukuletea umaskini ili ukose elimu na mwisho wa siku ushindwe kufikia kwenye kule ulipotumwa.

Msaada kutoka kwa Mungu kwa Yule aliyemtuma.

Kama tulivyoona Mungu anadesturi ya kutuma malaika, binadamu ili kuitengeneza dunia kuishape dunia kuileta mahala pake... Na Mungu ili kuwasaidia aliowatuma huitikisa dunia kwa jambo fulani ili kufanya wale aliowatuma waingie kwenye system, na hapa ndio maana unaona hata nchi Kama Tanzania inapitia kwenye mtikisiko ikionyesha kuwa kuna watu waliotumwa na wanakusudiwa kuingia kwenye nafasi zao.

Mfano mwingine ni wa Ibrahim , ambaye ni baba wa Imani, na huyu aliahidiwa kuwa baba wa mataifa na ili kuwa baba wa mataifa lazima azae awe na watoto, lakini dunia( shetani) akaanza kupinga hiyo, kwa kumwekea utasa, na hapa tunajifunza kuwa kwa kila mtu aliyetumwa lazima atakutana na upinzani.
Mfano mwingine ni Musa , na Musa alipozaliwa tu , shetani akajua na alitumwa na Mungu kuunda taifa imara, la Israel na ndio maana alipozaliwa tu, Farao akaamuru watoto wote waangamizwe, na hapa tunajifunza kumbe ukiwa na kitu kikubwa cha Mungu , lazima utapingwa na kuzuiwa. Lakini Musa kimuujiza alienda kula mezani mwa Farao. Bila Farao kujua hadi wakati wake hutimie.
Kumbe aliyetumwa hawezi kuangamizwa hadi atimize hatma yake.
Kwahiyo Mungu anakwaida ya kuwasaidia wale aliowtuma, tunaona katika habari ya Musa alipokuwa mdogo, na hata yale mapigo aliowaandalia wamisri,

Mfano mwingine wa taifa la Israel, kipindi Sauli alipofanya machukizo... Mungu akamtuma nabii Samuel kwenda kumpaka Mafuta mfalme Daud . Mungu anakawaida ya kutuma watu. kwa hiyo samweli akamchagua na kumtia Mafuta daudi.
Vitu ambavyo vilimshikilia Daud Kama mpakwa mafuta.
1. Kudharuliwa na ndugu zake.
2. Yuko machungoni polini.
3. Alidharauliwa na watu wa taifa lake.
Lakini pamoja na yote daudi aliishia kuwa mfalme sawasawa na alivyoitwa.

Jambo la kufanya:
Ni muhimu kupambana vita vya kiroho ili kuondoa vizuizi vya dunia, ambavyo vinazuia watu waliotumwa... Kwa hiyo ni muhimu kusambaratisha nguvu ya shetani ili kutuachia watu tuliotumwa.