Sunday, February 26, 2012

Ushuhuda wa Ibrahim ambaye mke wake alikufa kwenye mazingira tata.

Ibada ya Jumapili 26 Februari 2012

Ushuhuda wa Ibrahim athumani ambaye mke wake alikufa kwenye mazingira tata.

Mimi nilikaa na kukulia Arusha, na nilipata kazi na nikapata hela nyingi, maana niliajiliwa mgodini, basi nikaenda kwetu same na kujenga nyumba kwaajili ya wazazi wangu ili baba na mama yangu wakae. lakini cha ajabu baba akaniambia kuwa mama yako siwezi kuishi naye tena, na sitakaa kwenye hiyo nyumba labda unijengee nyingine. basi nikamwambia nitamjengea...

Basi baada ya muda baba akawa anasema mtaani, kuwa eti najidai na hela. Na kuwa mama yangu ananipa kiburi. Na Huo ulikuwa mwaka 2004 na baada ya muda nilipigiwa simu kuwa baba mkwe anaumwa. Kwa hiyo mke wangu akaamua kwenda lakini alipofika akaanza kuwashwa sana na akaanza kuumwa. Basi nikamwambia mke wangu arudi nyumbani, kwa kipindi kile nilikuwa mwislamu safi. Basi kumbe kule nje baba yangu akawa akasema mke wangu ndio ananiletea kiburi ili nisimsaidie. Na atanionyesha Mimi na huyo mke wangu.

Kwa kuogopa nikaamua kuhamia dar es salaam, basi mke wangu akazidi kuumwa nikampeleka hospitali nyingi , Kama muhimbili, Kenya, bugando na kcmc na hapo nikamwacha hospitali ya kcmc bila kuwa na matumaini kwa kuwa madaktari walikuwa hawajui ni aina gani ya ugonjwa unaomsumbua. Basi nikarudi dar. Kuangalia watoto.. Maana ilikuwa miezi minne nazunguka hospitalini. Basi kulikuwa na daktari mmoja mkongo akasema mke wako ni msukule mpelekeni kwenye maombi, na kwasababu kwa kipindi hicho nilikuwa mwislamu swala tano, sikukubali aende hospitali.. Basi baba aliendelea na maneno kuwa mke wangu lazima afe hata nimpeleke wapi. Akasema kuwa hata nimpeleke nje ya nchi atakufa tu.

Baada ya siku mbili baadaye mke wangu akafa, basi baba yangu akaja msibani , cha ajabu nilipomaliza kuzika tu, baba sikumwona tena. . Basi baada ya kumzika mke wangu , siku nne tu wakaja mashehe wengi sana nyumbani karibu kumi na kitu hivi. wakanishawishi nioe tena, nikawambia yaani siku nne tu mnanishauri nioe tena. Nikakataa kuwa sitaoa tena.

Ghafla siku moja nikiwa nimelala nyumbani nikasikia mlango ukigongwa, na mlangoni nikasikia sauti ya mke wangu ikinisalimia, nikakimbia kufungua mlango na cha kushangaza sikumuona mtu, hapohapo nikaanguka na kuzimia ,sikuamka mpaka kesho yake.. Na nilipoamka nikakuta mashehe wengi nyumbani, wakaniambia huo ni mzimu wa mkeo, wakaja na madawa mengi wakaniambia nitumie ili nimsahau nikakataa kutumia madawa yao nikasema mke wangu hajafa.

Basi kwa sababu ya uoga nikawaita ndugu zangu karibu 6 , nyumbani kwangu. siku moja nikiwa na ndugu zangu tumelala sebuleni, usiku mke wangu akanitokea tena.. Na hapo alipotokea nikamfinya mdogo wangu ili aamke naye aone lakini hakuamka wala kusikia, mke wangu akaniambia saa ya ukombozi imefika. Na hapo tuliongea karibu dakika 45. Baadaye nikamwambia natakaka nije alipo nilipomfuata akapotea na sikumwona. Nikaangusha friji na meza. Ndipo ndugu zangunwalipoamka. Na asubuhi mkono wa mdogo wangu ulivimba kwa vile nilvyokuwa nikimfinya..

Basi nilikuwa mwislamu mzuri kipindi hicho , nikamwambia mama kiongozi wa kiislamu, naye akaniambia niombe dua ili asipatikane tena. Akaniambia nitumie ubani, ili kumfanya asinitokee tena. Mimi nikamkatalia kwa kumwambia siwezi omba hiyo dua maana mke wangu hajafa.

Siku moja nikiwa nimepanda kwenye gari, nikazozana sana na konda, na hapo nilikuwa narudi dar . nilikuwa nimepanga nikifika dar. Niende nimpige risasi baba, basi ndani ya gari nilikuwa nimekaa na mzee fulani simjui , akanisii sana nimuelezee matatizo yangu, nikakataa lakini nikajikuta nimemueleza. Na nilipomwambia ,akanielekeza niende kanisani ufufuo na uzima. na nikakutana na Mch Adriano .bakaniombea na nikawa naendelea kuja na mkesha. Ingawa sikuwa na imani kubwaa..
Ijumaa moja nikiwa kwenye mkesha akaletwa mama mmoja aliyekuwa amekufa, tukaenda kumuombea nikapenya kuona kama amekufa kweli, nikamgusa alikuwa amekufa basi baada ya maombi kama saa hii akafufuka, lile jambo likanipa imani kubwa sana.. Na ndipo imani ikaiingia kuwa mke wangu anaweza kurudi.

Sikuchache, baadaye nikapigiwa simu kuwa mke wangu ameonekana anaosha vyombo boko. Na hapo nilienda nikakuta mwenye kibanda kile amefunga kibanda na hayupo tena amekwenda same. Na huyu mama alikuwa rafiki wa familia yetu kwa kuwa alikuwa karibu na baba yangu. Kifamilia nikashangaa kumbe ndiye aliyekuwa amepanga mbinu moja na baba.... Na hili ni tukio lililotokea kama wiki tu imepita.... Naamini Mungu anaweza... Na atamtudisha mke wangu....
Amen... Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment