Sunday, February 19, 2012

Ushuhuda wa Kijana aliyechukuliwa msukule akiuza vizazi Kariakoo

Leo Jumapili 19 Februari 2012

Ushuhuda wa kijana aliyepotea na kupatikana., usiku wa kuamkia tarehe 18
Hassan William shelukindo

Kaka wa aliyepotea alianza kushuhudia....
Anasema huyu ni mdogo wake aliyetokea Tanga, na kuja Dar asubuhi ya tarehe 30, na alipanda gari la somoe kuja dar. Kaka mtu aliendelea kwa kusema, shemeji yake ndiye aliyemsindikiza mpaka kituoni na kumpandisha gari, tayari kwa safari ya kwenda Masasi shuleni.

Baada ya siku chache taarifa zilikuja kwa njia ya simu kuwa begi lake limekutwa karibu na feri, jijini dar es salaam, kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa begi hilo lilikaa wiki nzima. Ndipo kwa ruhusa ya polisi wakalifungua begi hilo, na ndani ya begi walikuta uniform za shule, na namba kadhaa za simu. Ndipo polisi wakamua kupiga ile simu na ilikuwa ya ndugu yake aliyekuwa tanga. Ndipo walipochukua hatua ya kupiga simu shuleni ili kujua Kama amefika huko. Cha kushangaza ni kuwa walipopiga simu shuleni wakaambiwa kuwa hajafika na anahitajika afike haraka.

Basi Mimi ( kaka wa Hassan ) nikaamua kuja kituoni feri ili kuhakikisha Hilo begi kama ni lake ( Hassan) ndugu zake waaenda kituoni kuhakikisha lile begi. Kaka wa aliyepotea anaendelea kwa kusema, walifika polisi, na akamkuta afande aliyejulikana kwa Jina la Afande Mshindo. Na baada ya kuhakikisha wakagundua kuwa ni begi la Hassan, na kaka wa Hassan anasema, yeye akawaza moyoni nitapata wapi kanisa ili lifanye maombi kwa ajili ya Hassan , basi akaamua kumuuliza yule afande, na Afande Mshindo akamwambia kuna kanisa la ufufuo na uzima, lipo tanganyika packers, Kawe.

Ndipo nikaamua kuja anasema kaka wa Hassan., nilipofika kanisani nikamkuta mchungaji anayeitwa Mch. Esther na Mch. Evetha. Kaka wa Hassan anaendelea kwa kusema siku hiyo waliomba kwa muda wa masaa 2, na alikuwa hajawahi kumlilia Mungu, lakini siku hiyo alilia. Baada ya maombi niliacha picha kanisani, na baada ya kwenda nyumbani niliota ndoto mbalimbali kuhusiana na mdogo wangu, basi kesho yake tukakuta karatasi za kusajili line ndani ya lile begi. Na wakaamua kupiga ile simu, na kumbe ilikuwa namba ya baba yake hassan , ambaye alimuomba amsajilie. Basi zikaja taarifa kuwa kuna mtu kakutana naye kariakoo, mtu huyo alidai kuwa alimkuta akiuza viazi. Basi Mimi (kaka wa Hassan ) nikaamua kwenda kufuatilia huko kariakoo, hapo wakawakuta watu wanaouza viazi wakawauliza, mmoja wao akasema wamemuona huyo kama nusu saa iliyopita. Na wakamtafuta kariakoo nzima siku hiyo ila hawakumuona.

Basi kaka mtu anasema akaamua kurudi central, akiwa kituoni akapokea simu ya shemeji yake walioachana naye muda mrefu kuwa amemuona, maeneo ya posta, alisema baada ya kumuona kupitia dirisha la daladala akaamua kushuka na kumfuata, alipotea gafla lakini baada ya muda mfupi akaonekana tena. Alipomuona yeye (Hassan ) akaishiwa nguvu. Na hapo polisi wakaja kumchukua kwa mahojiano na haya ndiyo aliyosema hassan.

Hassan anasema, yeye alijisikia kushuka kwenye gari ikwiriri wakati alipokuwa anaelekea masasi, na hapo alitembea kwa miguu kutoka ikwiriri mpaka hapa dar. Na alipofika hapa akaanza kumfanyia kazi mzee ambaye hamjui kwa sura.

Hassan alipokuwa kanisani amesema"..
Anasema anachokumbuka ni kuwa , Alipanda gari na anakumbuka namba ya siti aliyopanda, na anakumbuka alishuka njiani ikwiri, na akatembea kwa miguu hadi dar. Na alipofika akakutana na babu alikuwa amevaa kofia ya cherehani yaani barakashia, hakumbuki Jina la huyo babu kwa kuwa hakumtajia.
Mahojiano kadhaa ya baba Mch. Gwajima na Hassan na ndugu zake j2 hii.
Baba Mch..: Amepotea kwa siku ngapi?
Kaka.: Toka tarehe 30 mwezi wa pili na Jana ( 18.2.2012) ndio amepatikana na yeye amesema hajala kabisa siku zote hizo.

Baba Mch.: kitu gani kinakufanya husisikie njaa?
Hassan : mi sijui ila nakumbuka sikuwahi kula siku zote hizo.
Baba mch : Ulikuwa unauza na wakina nani viazi, na ulikuwa unalipwa, saa ngapi mpaka saa ngapi?
Hassan : . Nilikuwa nauza mwenyewe, nilikuwa silipwi, na tulikuwa tu nauza kuanzia saa 11 jioni hadi 12 hasubuhi

Baba Mch. : ulikuwa unalipwa na ulipookotewa ulikuwa unaenda wapi
Hassan. : Nilikuwa silipwi, na nilikuwa sijui nilikokuwa naelekea maana ufahamu haukuwa vizuri.

Baba mch. : Wewe mama ulikuwa unawaza nini?
Mama. Wa Hassan : Mi nilikuwa sielewi ila nilikuwa naomba hapo niletewe angalau mifupa ya mwanangu, uchungu wa mwana aujuaye mzazi.

Baba Mch : Dada unawaza nini?
Dada : Mimi namshukuru Yesu anaweza. Nawashukuru wachungaji waliomuombea kaka yangu, Mungu awabariki.

Baba Mch : Mjomba wewe unawaza nini, na unahisi alishuka kwenye gari kwasababu gani au ujeuri?
Mjomba :, mi namshukuru Mungu na hapo nadhani si ujeuri kwa kuwa hakuwa hivyo ila nadhani ni uchawi na nguvu za Giza.

Baba Mch : Kaka unadhani alikuwa hapendi shule?
Kaka. :. Hapana maana nilimpeleka mwenyewe shuleni na nikamuuliza Kama anapenda shule, na alijibu kuwa anapenda na asingeweza kushuka kwa sababu alikuwa anapenda shule. Na hii ndio ilinifanya nifanya nitafute kanisa kwaajili ya maombi.

Hili ni moja ya mambo makubwa ambayo Bwana Yesu Kristo anatenda, kupitia Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. Katika nyumba ya ufufuo na uzima.. Barikiwa...

No comments:

Post a Comment