Sunday, March 25, 2012

Ujumbe : VYANZO VIWILI VYA NGUVU YA MUNGU.

Na. Mch. Kiongozi Josephat Gwajima. 25 Machi, 2012

NGUVU ni uweza au mamlaka ya kufanya jambo Fulani, sisi kama wakristo tunahitaji nguvu ya kutuwezesha kutenda mapenzi na kazi za Mungu duniani, na Biblia inasema hatuwezi kutenda , kwa usahihi duniani kama hatuta kuwa na nguvu za Mungu, 2 Wakorintho 2 :4…., Wakorintho 4:20, unapoongelea ukristo unaongelea nguvu kwa maana ukristo ni nguvu. Injili ya Yesu kristo imejengwa katika nguvu za MUNGU. Tofauti kati ya ukristo na dini nyingine ni nguvu iliyo ndani ya jina la Yesu..

Kama tulivyoona ukristo sio maneno matupu tu au tunavyokili bali ukristo umejengwa kwenye nguvu ya Mungu.. nguvu kuponya, kufufua, kufungua na kuokoa.. na ndio maana mtume Paulo anasema kwenye kitabu cha Wathethalonike 1:8.. kuhubiri kwetu hakukuwa katika maneno bali katika Nguvu ya Mungu.. 1 Timotheo 1:7 ´´Mungu hakutupa roho ya hofu bali roho ya nguvu´´ na ndio maana biblia inasema kuwa ´´nanyi mtapokea nguvu akishawajilia juu yenu roho mtakatifu´´

Yesu yu hai, na ana nguvu, Yesu wetu hayupo kaburini, alifufuka ..hayupo ndani ya tumbo la bikira Maria bali yupo hai mbinguni na anatenda kazi duniani.. Waefeso 3:20.. ´´ kulingana na NGUVU itendayo kazi ndani yetu´´ ndani ya kila mtu aliyeokoka kuna nguvu ya Mungu.. Waefeso 6:10 ´´katika uweza..¨ uweza unamaanisha nguvu.. YESU ALITUPA NGUVU HIZO ambazo twazipata kupitia vyanzo viwili..

NGUVU YA MSALABA WA YESU KRISTO..

Unaweza kujiuliza kwanini ukiweka msalaba wa Yesu kwenye nchi kama Iran, au nchi nyingi za kiarabu utapingwa sana na unaweza hata kuuawa, Hii ni kwasababu msalaba wa Yesu kristo una nguvu.. kuna nguvu ipatikanayo kwenye msalaba inaitwa ¨NGUVU YA MSALABA¨ 1 Wakorintho 1:18 ¨ujumbe wa msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi lakini kwetu sisi tunaoamini ni nguvu ya Mungu¨ kumbe kwenye msalaba wa Yesu Kristo kuna uweza uletao wokovu. Msalaba wa Kristo una nguvu.

Kwanini ujumbe wa msalaba unabeba nguvu?,

Unaweza kujiuliza ni kwanini, iwe nguvu ya msalaba na isiwe nguvu ya kitu kingine kama jua, mwezi, dunia au nabii.. mfano : nilisoma (Mch. Gwajima) kitabu kimoja kuhusu ajali ya ndege, ambayo rubani aliwatangazia watu kuwa ndege inaanguka na kila mtu alishauriwa kuandika mambo aua ujumbe kwa ajili ya familia au watu anao waacha duniani.. ukijaribu kuwaza wakati huu utagundua mtu awezi kuandika non-sense pale , maana ni wakati wa mwisho. Kila mtu ataandika jambo la muhimu ambalo angehitaji watuanaowaacha wajue.

Kwa mfano huo, tunaweza kuona kuwa maneno saba ya mwisho ya Yesu Kristo kabla ya kufa ni maneno ya muhimu na nguvu ya msalaba imejengwa kwenye maneno yale.. ni muhimu kujua Yesu alipigwa kwa ajili Yetu.. na magonjwa na matatizo yetu yalipigwa pamoja naye.


MANENO 7 ALIYOYASEMA YESU KABLA YA KUFA..


i.) Mathayo 27:46, Kwa wakati ule alibeba dhambi zetu zote. Na ndio maana Mungu akamwacha pale msalabani tunajua kuwa Mungu alimwacha kwa maneno ambayo Yesu alitamka akisema ´´ baba mbona umeniacha´´ baada ya Yesu kubeba dhambi za ulimwengu, Mungu akamwacha na Yesu akasurubishwa kwa dhambi ambazo hakutenda bali alitenda.. Yesu alisulubiwa kwa makosa YETU..


ii.) Luka 23: 34 -Katikati ya maumivu Yesu alisamehe.. watu wa dunia wanaweza kukwambia nimekusamehe lakini sitasahau lakini Yesu akiwa msalabani na katikati ya maumivu makuu ya msalaba akasema ´´baba wasamehe maana hawajui walitendalo´´ ZABURI 103:3 Nguvu ya msalaba unatupa nguvu ya kusamehe, kuna watu wengi wapo kwenye matatizo kwasababu ya kuto kusamehe.. ni kanuni ya Mungu kusamehe na kuponya . tunajifunza hili kwa wale waliomleta mtu kwa Yesu , mgonjwa akiwa kwenye godolo.. na Yesu kabla ya kumponya alimtangazia msamaha wa dhambi kwanza na baada ya hapo akamponya.. Kumbe msalaba unatuwezesha kusamehewa..


iii.) Luka 23:42-43 - ¨..Leo utakuwa pamoja nami peponi ..¨ hili ni neno ambalo Yesu alimwambia mmoja kati ya wale wanyang´anyi, akimwambia kuwa tutakuwa wote peponi, Yesu alisurubiwa pamoja na wanang´anyi.. kumbe usitishe na mtu anaye vaa msalaba akasema ni mtu wa Mungu, kwasababu wengine wanaweza kuvaa msalaba wa wanyang´anyi.. na kwa andiko hili tunajifunza kuwa nguvu ya msalaba inatupa nguvu ya kukumbukwa kwenye Ufalme wa Yesu.. kumbe msalaba unatupa nguvu ya kukumbukwa .. Mungu anakumbuka maombi yako, kazi yako, maisha yako na hata taifa lako.. Mtu yeyote awezi kukuhakikishia kwenda na kuuona ufalme wa Yesu isipokuwa msalaba wa Yesu ndio unaotupa uwakika wa kuuona Ufalme wa Mungu ´´hakuna jina jingine duniani, litupasalo kuokolewa kwalo isipokuwa jina la Yesu..


iv.)Luka 23:46, Kwa mtu yeyote aliyeokoka ,amekabidhiwa kwenye mikono ya Yesu kristo.. na hutakufa mpaka siku ya Bwana , kwasababu roho yako imekabidhiwa kwenye mikono ya Yesu Kristo.. huu ni ulinzi ambao kila mtu aliyeokoka anakuwa nao.. tupo mikononi mwa Mungu na hakuna mtu awezaye kututoa kutoka katika mikono ya Yesu Kristo..


v.) Yohana 19:29 Yesu akiwa msalabani , alikuwa anajali mahusiano.. hii inaonyesha kuwa msalaba wa Yesu unatupa usalama ndani ya mahusiano na wazazi na watu wengine.. Msalaba wa Yesu unatupa mahusihano bora . ukimwomba Mungu akupe nguvu ya mahusiano.. Kumbe msalaba ulileta Nguvu ya upatanisho.. Nguvu ya msalaba inaleta watu pamoja , watumishi wa Mungu pamoja, familia pamoja.. ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwao wasioamini lakini kwetu sisi ni NGUVU YA UPATANISHO.


vi.) Yohana 19:28 ¨..ninasikia kiu..¨ hapa Yesu alikuwa amekaa msalabani kwa muda , na alisikia kiu.. kwa kuwa hakuwa amekunywa maji.. kumbe msalaba wa Yesu unakupa kiu ya kumtafuta Mungu, kiu ya kuomba, kiu ya kuponya na kuokoa na rahisi kusikia watu wakisema nyinyi watu wa ufufuo na uzima kwanini kila kitu mnataka mtende nyinyi.. ni muhimu kujua kuwa msalaba wa kristo unatupa kiu ya kutenda na kuthibitisha nguvu ya Mungu.. na inawezeka ulipokuwa umeokoka ulipata hamu sana ya kuomba na kumtafuta Mungu..lakini baada ya muda ile kiu imepotea basi kama unatatizo hilo ni wakati wa kwenda mbele ya msalaba wa Yesu kristo.. na kuomba KIU ya kumtafuta Mungu na Mungu atakupa.. unaweza kuniuliza mimi( Mch. Gwajima) kiu yako ni nini? Mi nitakwambia kiu yangu ni kuona watu milioni moja wanakuja ndani ya ufufuo na uzima Dar es salaam.. nah ii ni kiu nilionayo… kuwa dunia iokolewe na waarabu waokolewe.. ninaona njia kuu ya udhihirisho wa nguvu ya Mungu itakayo tikisa mataifa kutoka katika msalaba wa Yesu.. Nguvu ya msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi lakini kwetu sisi ni KIU YA KUMTAFUTA MUNGU.

vii.) Yohana 19:30 ´´.. Yesu alipopokea kile kinywaji akasema IMEKWISHA´´ Kimsingi hakuna aliyemuua Yesu bali aliutoa uhai wake , ili aupokee tena.. na kimsingi Yesu alitenda mambo makubwa ya ufalme wa Mungu, na kwasababu hiyo shetani akakusanya watawala na watu wamuue Yesu na alipokuwa msalabani na kupiga kelele kusema imekwisha.. shetani akafikiri kuwa amemuangamiza na inawezekana kabisa kule kuzimu mashetani walianza kushangilia na inawezekana hata wachawi wa kipindi kile walienda kwenye sherehe .. lakini katikati ya sherehe yao. na Yesu akiwa nanig´inia msalabani Yesu akasema IMEKWISHA..

Baada ya Yesu kusema kuwa IMEKWISHA.. BIBLIA inasema

I. Dunia ikatikisika,.. kumbe Nguvu ya msalaba inaweza kutikisa dunia,
II. Makaburi yakafunguka, miili mingi ya watakatifu wengi ikafufuka. Kumbe Nguvu ya msalaba yaweza kurudisha. Na ndio maana mimi nashangaa watu wanaokataa kuwa wafu hawafufuki..najiuliza ni msalaba gani wanao uhubiri.. labda ni misalaba ya wale wanyang´anyi ..
III. Miamba ikavunjika kumbe msalaba wa Yesu unaweza kuvunja miamba.
IV. Jua likatiwa giza
V. Pazia la hekalu likapasuka.


KWELI KADHAA KUHUSU NGUVU YA MSALABA..


Kipindi cha zamani kulikuwa na aina za usulubishaji.. aina ya kwanza ni ya mti mmoja kama namba moja, ya pili ilikuwa alama ya kuzidisha yaani ´X´ , tatu ni wa alama ya T, na alama ya kujumlisha nah ii inamaanisha msalaba wa Yesu unatupa kujumlisha , kuongezeka, na kukua.. sisi tumesulubishwa pamoja na kristo

Yesu alisurubishwa kwenye mlima, na mahali pale kila mtu aliweza kumuona ,, watu kutoka kila mahali walimuona.. kumbe Yesu alisurubiwa mlimani ili kila mtu aone nakama Yesu alivyoinuliwa mlimani ili kila mtu amuone..´´kama vile Musa alivyomuinua nyoka jangwani mwana wa adamu naye aliinuliwa..

Na unagundua watu walimuona Yesu akisurubiwa mbele ya watu, njiani, mlimani na alipo taka kupaa akaenda mlimani pia..ili watu wote wamuone,, kumbe kama ulikuwa chini na watu walikuona chini Msalaba wa Yesu utakuinua mbele ya watu wote walikuona ukiahibika..

Yesu akashuka kuzimu katika zile siku tatu alipokuwa amekufa, akamnyang´anya funguo za mamlaka.. na hapo akamkanyaga kichwa shetani .. kutimiza andiko ´´uzao wa mwanamke utamkanyaga nyoka kichwa´´NGUVU YA KABURI LA KRISTO LILILO WAZI..

Hii ni nguvu tunayoipata kutoka katika nguvu ya kaburi la kristo.. kwa maana malaika alikuja kaburini na kukuta .. walinzi pale na baada kutetemesha lile eneo .. wakalisukuma jiwe la kaburi na kulikalia na hapo Yesu akafufuka na kutoka kaburini.. nah ii ni nguvu ya ufufuo na baada ya siku chache kabla ya kupaa akatangaza ´´mamlaka yote nimewapa ninyi ..´´ tuna mamlaka ya kuitawala dunia.. Nguvu ya kaburi lililowazi imetupa mamlaka.. sisi tuko ndani ya Yesu na Yesu yupo ndani yetu.. ´´tunalindwa na NGUVU za Mungu kwa njia ya imani..

Baba Josephat Gwajima atakuwepo katikati ya wiki kwa ufafanuzi zaidi wa somo hili.. Mungu akubariki sana..

Sunday, March 11, 2012

SOMO: Viti vya Enzi

Jumapili, Machi 11, 2012.

Na. Mch. Kingozi : Josephat Gwajima

Enzi ni utawala ambao mtu anakuwa nao.. mfano Mfalme akishika madaraka anaitwa mfalme ameingia kwenye enzi yake, pia Rais naye ni hivyo hivyo.. kwenye somo hili tutaangalia kwa undani zaidi kuhusu viti vya Enzi..

Kiti cha enzi cha Mungu….

Ufunuo 2:13 .. “….kiti cha enzi cha shetani…hapo akaapo shetani.” Maneno haya yaliandikwa katika karne ya kwanza , kipindi hiki wanafunzi wa Yesu walitawanyika kwa kuwa walikuwa wanauawa na Yohana alikuwa katika kisiwa cha patmo.. hapo Yesu alimtokea na kuumpa ufunuo juu ya makanisa mbalimbali.. ndipo kwenye kanisa mojawapo Yesu akamwambia hayo maneno kwa “ najua ukaapo ndipo kwenye kiti cha enzi cha shetani..”

Maana ya neno kiti cha enzi cha shetani..

Kiti cha enzi ni makao makuu ya utawala au utendaji kazi wa utawala ( center of operation) , tunaweza kuona pia katika ufunuo 16:10 “ kiti cha enzi cha mnyama” lakini ukirudi nyuma ufunuo 13:2 huyu mnyama alipewa uwezo na Yule joka.. “kutoka kwenye kiti cha enzi cha Yule joka” huyu joka kimsingi ni shetani yuleyule. Aliyetajwa kwenye ufunuo 12:7.. kumbe tunagundua kuwa shetani ana kiti cha enzi na hivi vinamaanisha makao makuu ya utendaji kazi wake..

Anaposema kiti cha enzi cha shetani hapa (mwanzo 2:12) ana maanisha ni mji kabisa ambao shetani kaamua kuufanya kuwa makao yake makuu ya utendaji kazi wake.. kumbe shetani anaweza kuweka kiti cha enzi ndania ya mji.. na mji ukakamatwa kwa kiti kile cha enzi..

Shetani anaweza kuweka kiti cha enzi ndani ya mtu.. kumbe shetani anaweza jenga mamlaka yake ndani ya mtu.. huyu anakuwa anatoa msaada wa kishetani. Ili wle wanaotaka kupata msaada wa kishetani wanamfuata na wanakutana na shetani moja kwa moja.. hii inatokea pale shetani anapo amua kuishi na kufanya utawala ndani ya mtu.. na ndio maana mapepo ukitaka kuyatoa yatajibu kwa kusema “mwacheni kiti wangu” hii ikionyesha kuwa Yule pepo amejenga utawala wake au kiti cha enzi ndani ya huyo mtu..

Uthibitisho wa viti vya enzi kwenye biblia..

Matendo ya mitume 16:16-34 tunamuona huyu kijakazi, ambaye shetani ameweka makao yake ndani yake, na kwa kiti hicho alikuwa anatenda kazi zake kwa watu.. ndio maana biblia inasema “aliwapatia faida nyingi sana bwana zake”.. unaweza kujiuliza kidogo kwanini watu wa mji wote waliwageukia wakina Paulo , na wakawaweka katika gereza maalum jiulize shida hapa ilikuwa kutoa pepo kwa huyu binti , kwanini wafanya biashara waliingilia? Utagundua kuwa shetani alikuwa ameweka kiti chake cha enzi ndani ya Yule binti, ambapo wafanya biashara walikuwa wanamfuata kwa ajili ya kuwaagua.. mfano kujua mambo yajayo..

Ni muhimu kujua , haijalishi una umri gani kumfanya shetani aweke kiti chake cha enzi.. na unaweza usijijue kuwa wewe ni kiti cha enzi maana huyu kijakazi alihisi ni sehemu yake ya maisha kumbe , ni shetani anatenda kazi ndani yake.. ni muhimu kupindua kiti cha enzi ndani ya watu kwa Jina la Yesu Kristo..

Kila mji unaouona una kiti cha enzi cha shetani.. na ndio maana ukiangalia miji mbalimbali hata hapa Tanzania kuna viti vyake vya enzi.. hawa ni watu wanaosimamia utawala wa kishetani.. na hawa ndio wanaojenga tawala za kishetani. Ukiangalia nchi nyingi za duniani utajiri unashuka kuzimu kwa shetani kupitia viti hivi vya enzi.. na nchi yaweza kushuka kiuchumi kwasababu ya viti hivi vya enzi..

Kwenye Marko 5: 1- luka 8:26 hapo tunaona habari nyingine ya kushangaza kidogo, kulikuwa na mji wa wagerasi huu mji ulikuwa wa kibiashara tunalijua hili pale tunapoona nguruwe na kwa wakati ule wayaudi walikuwa hawafugi nguruwe , hii inaonyesha mji huu ulikuwa ni wakibiashara.. na katika njia kuu ya kuelekea katika mji ule kulikuwa na watu wwili wenye pepo mathayo 8:28-… “…..wasiruhusu mtu apite…” utaona hiki ni kiti cha enzi kinachozuia biashara na ndio maana Yesu alipotaka kumtoa walimwambia wasimtoe kutoka kwenye ule mji.. kwasababu walikuwa kiti cha enzi cha mji wa wagerasi.. na hawa walikuwa wanakaa kuchuja wanaoruhusiwa kwenda ndani ya mji huo..

Hata ukoo waweza kuwa na kiti cha enzi cha shetani, kinacho simamia makusudi ya kishetani kufanyika ndani ta ukoo.. na ndio maana unaweza kuona kila ukoo una aina ya magonjwa na aina ya vifo..hiki kiti cha enzi kinawekwa na shetani ndani ya ukoo au familia ili kuutawala ukoo.. na ndio maana hata wale mashetani walimwomba Yesu asiwatoe kutoka kwenye ule mji..

Ili kuhama kutoka kwenye viti hivyo vya enzi, unatakiwa kuomba maombi ya kupindua viti vya enzi vya kishetani kwenye maisha yako.. kwamaana mtu anaweza akazaliwa chini ya kile kiti cha enzi na ikakufanya uwe na matatizo tangu tumboni.. na ndio maana baadhi ya familia zimewekwa chini ya laana na matatizo kwa sababu ya viti hivi vya enzi, yaani bibi aliachwa na babu, naye baba akamwacha mama na sasa wewe umekutana na matatizo ya kuachwaa ni muhimu kujua.. jaribu kuangalia nafasi ya maisha yako na familia yako... na ndio maana Mungu kakuchagua wewe kama kuhani wa familia ili upindue viti hivyo vya enzi.. ni muhimu kujua nafasi yako.. kataa kuishi chini ya kiti kile cha enzi..

Saturday, March 10, 2012

Maelfu wajazwa Roho Mtakatifu katika kilele cha Semina ya Bonde la Baraka

Maelfu wa watu leo katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima iliyopo Kawe, Tanganyika packers wamejazwa Roho Mtakatifu katika semina maalumu ya Kufunga na Kuomba iliyoanza Machi 7 mwaka huu na kuisha Machi 10 ikiongozwa na Mpakwa mafuta wa BWANA Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima. Ibada hiyo ilikuwa kilele cha semina ya maombi maalumu ya kufunga na kuomba yaliyochukua muda wa siku nne, ibada inakadiriwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu 40 kwa mara moja!

Akihubiri na kufundisha neno la uzima, Mch. Josephat Gwajima alisema kuwa baada ya mfungo huo, tutarajie kuingia katika bonde la Baraka (Tekoa) sawa sawa na neno la BWANA alilonena katika kitabu cha mambo ya 2 Nyakati 20: 26 " Hata baada ya siku nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipomkaribia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo"

Hivyo ibada ya kesho asubuhi Jumapili Machi 11, 2012 ni ibada ya Kuchota Baraka katika Bonde la Baraka hapa Tanganyika packers, kawe baada ya kufunga na kumwomba BWANA siku nne mfululizo bila kukoma.

Maelfu ya Watu Wajazwa Roho Mtakatifu katika Semina MaalumuMch. Kiongozi, Josephat Gwajima akiachilia upako wa mafuta ya Roho Mtakatifu kwa mmoja kati ya waliojazwa Roho Mtakatifu leo jioni katika ibada ya kufunga na kuomba iliyomalizika leo, huku ikikadiriwa kuhudhuriwa na zaidi watu wapatao elfu 40 kwa mara moja!


Maelfu ya watu wakiendelea kujaa Roho Mtakatifu leo katika ibada
Mchungaji, RP Maximilian Machumu akibandika mkono tayari kwa kuachilia ujazo wa Roho Mtakatifu!Mch. Kiongozi, Josephat Gwajima akiwaombea maelfu ya watu waliojazwa Roho Mtakatifu muda mfupi baadaye.Mchungaji, RP Yekonia Bihagaze akimwombea mtu ajazwe Roho Mtakatifu leo katika ibada maalumWachungaji wasidizi, APs na MPs wakiomba ujazo wa Roho Mtakatifu leo katika ibada maalumu ya maombi ya kufunga na kuomba iliyodumu kwa siku nne na kuisha leo jioni.