Sunday, July 22, 2012

Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima Tarehe 22-07-2012. Ujumbe: Kerubi Afunikaye

UTANGULIZI:
Huu ni mwendelezo wa somo la KERUBI AFUNIKAYE, EZEKIELI 28:13-18..     Kerubi ni aina malaika wanaobeba uwepo wa BWANA, Ni malaika wa ngazi ya juu.. mbele za BWANA.  Maana malaika wapo katika ngazi tofauti ndiyo maana katika kitabua cha ISAYA wametajwa malaika aina ya MASERAFI, na pia YUDA 1:  Kitabu hiki kimetaja Mikaeli kama malaika mkuu kumbe kama kuna malaika mkuu basi chini yake kuna malaika wengine.KWELI KUHUSU MALAIKA:

Kuna malaika wa ngazi tofauti, kama tulivyosoma kwenye YUDA 1:9 na DANIELI 12:7  Ttunaona wamemtaja malaika Mikaeli kama malaika mkuu, na katika ISAYA 6:1—BIBLIA inasema kuna malaika wanaitwa maserafi ambao wao ni malaika wanaokaa karibu na BWANA ambao Isaya aliwaona kwenye maono, na pia kuna Makerubi AMBAPO shetani alikuwa katika ngazi hii ya malaika.  UFUNUO 12:7 Mikaeli kama malaika mkuuwa vita, chini yake ana malaika wa ngazi mbalimbali. Na ndio maana katika kitabu hiki cha UFUNUO 12 tunaona jeshi la malaika waliochini ya mikaeli.UNAPOOKOKA MALAIKA WANAKUWA UPANDE WAKO:

Kama tulivyoona malaika Mikaeli ni malaika mkuu wa vita, na chini yake kuna malaika mbalimbali, yaani baada ya kuokoka kuna malaika wanaokulinda yaani kuna mambo unapitia unajihisi kama duniani uko mwenyewe lakini ni kukosa maarifa tu ya rohoni lakini kimsingi mtu wa Mungu yoyote ana malaika wanaotenda kazi kwa ajili yako. Na ndio maana kwenye Biblia ilitokea kipindi Elisha na mtumishi wake walizungukwa na majeshi ya maadui, kwasababu Mtumishi Yule hakujua ulinzi wa malaika akaanza kuogopa, ndipo malaika alipo mfungua macho ya rohoni ili aone jeshi la malaika lililo pamoja nao.Malaika wanatenda kazi kwaajili yetu na ni watumishi wetu. Kuna malaika mwingine mkuu wa taarifa anaitwa Gabrieli huyu ni malaika mkuu wa taarifa naye ameonekana kwenye biblia sehemu nyingi akileta taarifa mbalimbali, yaani unaweza ukapitia kwenye kipindi kigumu ukiwa hujui la kufanya basi huyu hutumika kuleta taarifa za kimungu kwetu. HATA Danieli alipofunga siku 21 akiwa haoni matokeo yoyote Malaika aliyekuja kuleta taarifa kwa Danieli. Mikaeli ni malaika anayetupa taarifa za kutoka mbinguni. Ndio maana hata kama watu wanakupiga vita kwa siri usiogope maana tuna malaika Mikaeli.KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE:

Tumeona aina za malaika mbalimbali na kazi zao, lakini kuna huyu malaika wa Tatu ambaye ndio kerubi afunikaye, ambaye ni shetani . shetani kabla ya kuasi alikuwa malaika wa mkuu kwenye ngazi ya kerubi, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufunika na ilikuwa kama eneo lina uharibifu akifika yeye aliweza kufunika na kulifanya liwe takatifu mbele za Mungu.Lakini baada ya kuasi shetani bado anaouwezo ule na anautumia kuharibu maisha ya watu. kimsingi maisha ya mtu yanaweza kutafsiriwa kirahisi kwa kutumia nyota. Kwahiyo kwakuwa shetani yupo rohoni anaweza kuona viashiria hivi vya rohoni na kwa njia hiyo anatumia uweza wake wa kufunika kufunika viashiria hivi na kufanya matokeo yake yanakuja kuonekana katika mwili.Nyota ni nini basi? Nyota ni kile kiashiria cha rohoni kinachoonyesha eneo ambalo Mungu amekubarikia katika ulimwengu waroho. Kimsingi kila mtu aliye duniani amepewa kitu na MUNGU  ambacho kwa hicho anaweza kukitumia ili afanikiwe kwenye maisha.mfano nyota ya mtu yaweza kuwa ni akili au macho au mikono n.k.Wachawi kwa kuwa ni watumishi wa shetani wanauwezo wa kusoma nyota na kujua nini ambacho nyota inamaanisha. Hivyo kwa njia hii wanatumia kuiba au kiufunika . akichukua nyota anaenda kumpandia mtu mwingine. Kwahiyo shetani anaweza kufunika, na ndio maana wasoma nyota na wasafisha nyota wanachofanya ni kuiba au kufunika nyota na kumpa mwingine anayehitaji kwa wakati huo. Kuna watu wanaotumia nyota za watu kuendesha maisha ya watu..RUDISHA NYOTA ILIYOIBIWA AU KUFUNIKWA:

Kuna watu wanaishi kwa kutumia nyota za watu, na kwa mamlaka tuliyopewa tunaweza kurudisha kwa Jina La Yesu. Tumia mamlaka hiyo kurudisha vyote LUKA 10:19 Tuna mamlaka ya kurudisha. Unaamuru kwa Jina la Yesu nyota yako irudi kabisa. Mtu aliyechukua nyota yako anaweza kuwa wa karibu sana. Maana adui wa mtu ni wa karibu ya huyo mtu ndugu au jirani.. lakini tuna mamlaka dhidi yao wote amuru warudishe, nyota haiombwi bali unaamuru irudishwe. Hatumwombi shetani bali tuna mwamuru.

1 comment:

  1. Hakika mafundisho haya huwezi kuyapata mahali popote pale duniani na wala sio akili za mwanadamu ziwezikiri na kuyasema haya wazi wazi....

    ReplyDelete