Sunday, December 9, 2012

MTU WA IMANI 9.12.2012

Na Mch. MWANGASA (Resident Pastor)


Warumi 4:13; Ibrahimu ALiitwa na Mungu kutoka nchi aliyokuwepo (Uru ya wakaldayo), Mungu akamuahidi kuwa atakuwa baba wa mataifa (uzao wake kama mchanga wa bahari). Lakini ikapita miaka bila Ibarahimu kupata mtoto, na kwa hali ya kawaida angeweza kukata tamaa. Kupitia habari hii, tunajifunza mambo matatu:-
1    
  •      Ibrahimu hakuangalia udhaifu wa kutokuzaa bali aliangalia Ahadi ya Mungu.
Kuna wakati wa kuangalia jambo ambalo Mungu amekuahidia. Neno la Mungu ni ahadi za Mungu kwetu. Na ndio maana alipoona uzee na hata tumbo la Sara mkewe. 19-20’ “Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;” 

  •          Pamoja na jambo hilo, Ibrahimu pia aliangalia uweza wa Mungu.

Kuna wakati mwingine majina ya vitu yanaweza kukutisha, aidha kwa kuangalia       desturi au asili. Kama Ibrahimu angeangalia desturi asingetarajia kupata mtoto katika wakati ule. Katika Mstari 21’  huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.Ibrahimu aliangalia uweza wa Mungu anayemwamini. 


Mtu wa Imani huwa anaangalia anapokwenda, na sio anapotoka. Warumi 4:17 “(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”  Mungu anayataja mambo ambayo hayapo, yaani yajayo kama yapo nah ii ndio tafsiri ya Imani. Na ndio maana; ingawa Mungu haonekani kwa macho lakini hilo halimfanyi asiwepo. Mtu mwenye Imani aangalii yanayoonekana bali yasiyoonekana. Mtu mwenye Imani hata kama ameambiwa kuwa ni tasa yeye anakwenda kununua kitanda cha mtoto. Hama kutoka katika kuangalia yaliyopo bali angalia kwa kufuata imani.

  •    Ibarahimu aliamini kwa kutarajia, lisiloweza kutarajiwa.
Warumi 4:18 “Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.”  Usiogope kutarajia makubwa, Mungu anaweza kutenda yaliyo makuu mno. Kuna hazina zipo gizani ambazo imani pekee ndio inaaweza kuzichukua. Ibrahamu kilichomfanaya atarajie yaliyo makubwa Ni kwasababu aliiangalia ahadi ya BWANA. Hata sisi hatujaletwa duniani kwa hasara. Mungu anakusudi la sisi kuwepo hapa duniani.

Yawezekana unapita katika wakati mgumu, lakini unachotakiwa ujue ni kwamba, Mungu anaweza kutenda kwako ambayo watu wengi hawayatarajii. Swali la kujiuliza.. “Unatarajia jambo gani?”  Tafakari na uchague kuwa mtu wa Imani: ili uweze kuwa mtu wa imani jifunze kuangalia kwanza uweza wa Mungu kabla ya uweza wako mwenyewe.

Miliki Milango yote ya Baraka maana sisi ni wa Uzao wa Ibrahimu: Mwanzo 13:14 “Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.”  Miliki ahadi ya Mungu kwetu…Pamoja na Ibada nzuri; kulikuwa na Uzinduzi wa Album mpya ya Mwimbaji Peter (Mp)No comments:

Post a Comment