Hapa tunakuletea matukio katika picha ya ibada hiyo.
Watoto wa Showers wakimwimbia BWANA katika ibada ya leo |
Platform Choir wakimsifu Mungu, mapema asubuhi ibadani leo |
Baba Mchungaji Josephat Gwajima akiwasili ibadani |
Platform Choir wakimsifu Mungu ibadi, Mungu hushuka kupitia sifa |
Madhabahuni kabla ya Mchungaji kiongozi kuanza kufundisha |
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akifundisha madhabahuni |
Sheik Omari akitoa ushuhuda wake alipokuwa akifanya uchawi |
Baba Mchungaji akipita katikati ya watu kuwaombea waliokuwa hawewezi na wagonjwa |
Mama akieleza juu ya mwanaye mwenye matatizo ambaye alizunguka maeneo mengi bila mafanikio yoyote |
Mchungaji Kiongozi akimfungua, aliyekuwa amefungwa na mapepo na nguvu za giza |
Mchungaji Kiongozi akipita katikati ya watu na kuwafungua wote waliokuwa hawawezi na waliokuwa katika tabu na mateso mbalimbali.
wakati huo alikuwa akiruhusu maswali kwa mtu mmoja mmoja, na kupitia maswali hayo wengi walifunguliwa.
Mtoto ambaye alikuwa anatokewa na bibi yake usiku na kumpeleka kula nyama na damu za watu, akifunguliwa katika ibada ya jumapili hii |
dada ambaye katika familia ya watoto tisa yeye pekee ndiye alikuwa hajafanikiwa na shetani alikuwa amemfunga alifunguliwa baada ya maombezi |
Msichana ana aliyezaliwa huku akiwa analilia jina la bibi yake, walipompa jina akaacha kulia jambo ambalo limemletea vifungo vingi katika maisha yake. alifunguliwa baada ya maombezi |
Maelfu wa watu waliojitokeza kumpokea Yesu kwa mara ya kwanza kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yao |
Moto ulishuka wakati baba akiwa anawaombea waliokuja kumpokea Yesu |
Baba Mchungaji akiwaombea watu waliojitokeza kumpokea Yesu Kristo |
0 Comments