Sunday, April 21, 2013

TAWALA KUANZIA ROHONI


RP FRANK ANDREW

Utangulizi
Mungu huongea na watu wanaoona,ndio sababu Mungu kwenye biblia alikua anakawaida ya kuwauliza watu unaona nini.Kutawala kunaanzia kwenye ulimwenguu wa roho na kushindwa pia kunaanzia  katika ulimwengu roho.
Waebrania 11:3-Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri
Kila vinavyoonekana vimetokana na vile visivyoonekana,mafanikio ya mwilini yanatokana na mafanikio yaliyoanzia kwenye ulimwengu usioonekana yaani ulimwengu wa roho.Ndio sababu vile visivyooonekana ni vya kudumu milele na vinavyoonekana ni vya muda tu.

2 Wakorintho 4:16-18 “…tusiviangalie vinavyoonekana,bali visivyoonekana.kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu,bali visivyoonekana ni vya milele
Ukiviangalia vile visivyoonekana tunapata ufumbuzi wa milele na tunapoviangalia vile vinavyoonekana tunapata ufumbuzi wa muda tu.Vitu vinavyoonekana vinakua na ufumbuzi wa muda tu lakini vitu vile visivyoonekana vinakawaida ya kutokua na mipaka.
1Wakorintho 2:9-lakini kama ilivyoandikwa,mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo hayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Mambo ambayo hata hujawahi kuyawaza wala jicho halijawahi kuyaona, mambo hayo Bwana amewaandalia wampendao, Kama vitu vinaanzia kwenye kutokuonekana tunatakiwa kung’ang’ania kwenye vile visivyoonekana ili kupokea majibu yetu yenye kuonekana.
Yeremia 1:11-tena neno la Bwana likanijia kusema, Yeremia, waona nini?. Nikasema ninaona ufito wa mlozi, ndipo Bwana akaniambia umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimize.Bwana anaongea na wale wanaoona vitu,ukiona ushindi,ushindi unatokea kwako,ukiona ufumbuzi ufumbuzi unatokea kwako,ukiona taabu, taabu inatokea kwako.

Hata  vita tunayopigana ni katika ulimwengu usioonekana, mambo yasiyoonekana yanasababisha mambo yanayoonekana.Waefeso 6:12-  “kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama….katika ulimwengu waroho”
Unaposhinda rohoni ushindi unaonekana mwilini na unapopigwa rohoni na mwilini unashindwa, kwa sababu majeshi tunayopambana nayo yako katika ulimwengu wa roho.

Nini maana ya ulimwengu wa roho?
Ulimwengu wa roho maana yake ni ulimwengu usioonekana,au ulimwengu wa asili,Mambo yanaanzia rohoni ndio yanadhihirika mwilini,ushindi unaanzia rohoni na baadae unadhihirika katika ulimwengu wa mwili.

Nafasi yako rohoni
Kila mtu aliyeokoka anayo nafasi yake katika ulimwengu wa roho,Waefeso 1:3-  “…aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu waroho katika Kristo yesu.
Hatuhitaji kumwambia Mungu atubariki kwasababu Mungu ameshatubariki kwa baraka zote katika ulimwengu wa roho, biblia haisemi kwamba Bwana atatubariki!!hapana,  biblia inasema Bwana ameshatubariki kwa  baraka zote katika ulimwengu wa roho.Tunatakiwa kuzibeba baraka zetu kutoka kwenye ulimwengu waroho na kuzilieta kwenye ulimwengu wa mwili
Waefeso 1:18-Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wake katika watakatifu jinsi ulivyo ;kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake

Namna ya kuvileta vitu katika ulimwengu wa mwili
Unatakiwa kufahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umepewa kumiliki vyote,tumepewa kumiliki vyote katika ulimwengu wa roho,tunatakiwa kutumia mamlaka tuliyonayo kuhakikisha tunamiliki kwasababu  tushaandikiwa kushinda katika ulimwengu wa roho
Luka 10:19-Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui wala hakuna kitu kinahoweza kuwadhuru
Ushindi wetu uko katika ulimwengu wa roho na tunatakiwa tusababishe uje mwilini.unatakiwa kupambana katika maombi na kuhakikisha vile ulivyonavyo rohoni vinatokea katika ulimwengu wa roho,Yesu alishalipia kila kitu tunachokihitaji 2Wakorintho 8:9.

Unapogundua vitu vyako viko katika ulimwengu wa roho ni jukumu letu kuvidai mpaka vitokee mwilini,2Wakorintho 4:3-4-Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Silaha kubwa ya shetani kwa mkristo ni kwa kumzuia asione anachotakiwa kuona anavyostahili kupokea.Shetani anao uwezo wa kupofusha fikra na mawazo na kukufanya usiyaone yale Mungu aliyokusudia kwako.

Warumi 12:1-2-  “Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu
Unapookoka unatakiwa kubadilisha namna ya kuwaza,na namna moja ya kuwaza ni kwamba hatushindwi hata siku moja,na baada ya kugeuza namna ya kuwaza ndio utayajua mapenzi ya Mungu yaliyo mema katika maisha yako.Ukigeuzwa upya nia yako ndio utaanza kujua kumbe ni mapenzi ya Mungu wewe usiwe mgonjwa,ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe.


No comments:

Post a Comment