Sunday, June 30, 2013

WATU WALIOCHUKULIWA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA.                                   SUNDAY, 30th June 2013.“Saa inakuja na sasa ipo, ambapo wafu wataisikia  sauti ya mwana wa Adamu”

2Wafalme3:4-27,”Ndipo akamtwaa mwanae wa kwanza…….” hizi ni habari za mfalme wa israeli ambae aliamua kwenda vitani  kumpiga mfalme wa Moabu, na alipoona kuwa vita inakuwa ngumu sana, akaamua kumtoa kafala mwanaye wa kiume. Hii ilikuwa agano la kale lakini hata sasa bado kuna watu ambao wakitaka ushindi huwa anatoa kafara ili apate ushindi, kafara hii inaweza kutolewa na mkuu wa nchi au yeyote atakaye ushindi. Inaweza kuwa ili kupata ushindi wa biashara, uongozi au mali.
1Wafalme 16:29-34, "Ahabu mwana wa Omrai lianza kutawala juu ya Israeli………..34’ Katika siku zake Hieli Mbetheli akajenga Yeriko, akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu sawasawa na neno la BWANA alilonena kwa Yoshua mwana wa Nuni”

Biblia inasema, Ingawa tunaenenda kwa jinsi ya mwili lakini hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, vita vyetu ni vya rohoni. Ndio maana hata tunapoimba sifa kwenye ulimwengu wa mwili ndivyio tunabomoa misingi ya kisheni katika ulimwengu wa roho, Ukiweza kuutawala ulimwengu wa roho unakuwa wumeutawala ulimwengu wa mwili bila kipingamizi.

 
Maombi: Naamuru ngome ya magonjwa, balaa, mikosi na ngome zote za giza amabazo zimeletwa kwenye maisha yako kwasababu ya kafala ziharibiwe katika Jina la Yesu. Na kama Yoshua alivyotangaza kwa atakaye ujenga tena Yeriko name naalaaniwe pepo yeyote atakaye jaribu kukufunga tena.

Huwezi kwenda kwenye utawala bila kuwekwa na  mamlaka ya rohoni, ama  mamalaka ya shetani au mamlaka ya kutoka kwa Mungu. Hivyo kiongozi ambaye hajatoka kwa Mungu ni lazima atakuwa ametoka kwa shetani kwasababu watoa kafara hizi wapo hata sasa.

NINI KINAWAFANYA WATU WANATOA KAFARA WAFANIKIWE.
Biblia iko wazi kabisa kuhusu watu wanaotoa watu kuwa kafala, swali kwanini wanafanikiwa? Ni muhimu kujua kuwa chakula cha mashetani ni damu, hivyo wachawi wanapotoa kafara ya watu wanamwaga damu ambayo kimsingi inawapa uhai na nguvu kwa mashetani, na mtu huyo anayetoa kafara huwa ananuiza damu hiyo kwa ajili ya kushindwa na kupata matatizo kwa mtu aliye mkusudia.

Damu ni uhai, Mwanzo 9:4, Kafara inapotolewa damu humwagika na kwasababu damu ni uhai, Damu hiyo hunena kwa jina lako na kwa ubaya ilikusudiwa kwayo.  Ukisoma Mwanzo 4:10, utagundua kuwa Habili alipouawa na ndugu yake Kaini, damu yake ilikuwa ikinenea katika ulimwengu wa roho. Vivyohivyo, damu inaponena mashetani huja na kuitimiza makusudi iliyonuiwa kwayo. Leo una matatizo kwasababu ya kafara iliyo tolewa na adui yako. Uwezi kuwa huru bila kunyamazisha kafara zote na damu zote zinazonena mabaya juu ya maisha yako.

Pale ambapo damu imemwagika ndipo madhabahu ya kifungo chako na ndipo sauti ya kifungo chako inapotokea na inaweza kuwa sehemu yeyote ama shambani, njia panda kuzimu ama mahali popote, ndio maana ajali inaweza kutokea na mtu mmoja tu ndio akapoteza maisha kwasababu yeye ndio aliyekusudiwa.

Unapoinyamazisha damu leo,wanaweza kwenda kumwaga tena damu nyingine kwa kutoa kafara na tatizo lako kuanza tena,cha msingi ni kubomoa madhabahu hiyo na kumteka nyara kuhani wa madhabahu hiyo na kumyonga kwa Jina la Yes,ukifanya hivo utakuwa umemkamata farasi na mpanda farasi na kuwatupa baharini.Kuna wengine huwa hawamwagi damu bali hupeleka mashataka kwenye vikao vyao vya kichawi.

Roho yako kulazwa usingizi na Mashetani.
Kama unavyojua mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili, hivyo Shetani anaweza kumwingia mtu na kuikaba roho yake, mtu wa namna hii huanza kusikia kichwa kinamuuma na baadaye anapata kujikuta amekufa au anaishi huku akiwa hawezi kufanya mipango yoyote kwasababu roho imelezwa ndani au anaweza kuonekana amechanganyikiwa ; mtu kama huyo aweza kufunguliwa kwa jina la Yesu.
3.Kuchukuliwa mzima mzima
Watu wa namna hii huitwa mzima mzima usiku,hapo yako ndiyo huitwa na kama huna Yesu lazima utaitika kwasababu roho yako haina ulinzi wa Yesu, Na unapoitwa unafungua mlango mwenyewe na kuifuata sauti na matokeo yake unapotea na unakuwa hauonekani. Ndio utasikia matangazo kwenye kwenye vyombo vya habari kuwa mtu Fulani amepotea kumbe kwasababu ya kuitwa.

Kwa njia hii shetani ametumia roho za watu. Shetani huamua kutumia wanadamu kwasababu roho za pepo ni rahisi kuangamizwa kwa Jina la Yesu, Hivyo huamua kutumia roho ya mwanadamu (superior).

Kutoa roho ndani ya mwili wa mtu na kuweka pepo.
Kwa kawaida mtu wa jinsi hii roho yake hutolewa na huingizwa ndani, na unapokuwa unaomba watu wa namna hii hawawezi kuangamia kwasababu Yesu anawapenda wanadamu, watu wa namna hii ni wengi kwelikweli. Watu wengi unawaona ni wagonjwa sana, wana matatizo sana ndani wanakuwa wamechukuliwa, watu wanamna hii unaweza kuwaombea muda mrefu na pepo lisitoke, ukiona hivyo tambua kuwa mtu huyo ambaye ni roho hayumo ndani hayumo ndani.


Watu hawa ndio ambao huombewa makanisani miaka mingi bila kufunguliwa lakini kumbe siri hii kuwa roho imetekwa haijajulikana kwao. Katika Jina la Yesu Kristo ninaamuru roho yako iwe huru. Na ufunguliwe kutoka katika udhaifu wako.

Friday, June 28, 2013

WIKI YA BARAKA NA MIUJIZA UFUFUO NA UZIMA


Na Mwandishi wetu | Kawe, Dar es Salaam.
Wiki hii imekuwa wiki ya baraka sana kwa kanisa la Ufufuo na Uzima, sio tu kwasababu ya neema za Mungu kwetu bali pia tumeshuhudia matendo makuu ya Mungu aliyotenda katikati yetu. 

Wiki ilianza kwa ujio wa Wachungaji zaidi ya 23 kutoka Japan kuja kushuhudia makuu ambayo Bwana amekuwa akitenda, kiongozi wa msafara huo, Pastor Yoshida alipopewa nafasi ya kuongea na waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima alisema wazi kuwa lengo lao la kuja Tanzania, na zaidi sana Ufufuo na Uzima ni kuja kuchukua nguvu ya Uhamsho iliyo ndani ya Mchungaji Josephat Gwajima na kuipeleka Japan. Kwa mujibu wa Takwimu zinaonyesha ni asilimia 1 tu ya wajapan ndio wanaomjua Kristo wengi wao wanaabudu miungu. Wachungaji hao kutoka Japani walipatanafasi ya kuabudu nasi ibada ya Jumapili wakiishuhudia matendo makuu yale Mungu aliyotenda.

Haikuishia hapo, wiki hii tumepata ugeni mkubwa wa Waimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel na Flora Mbasha pamoja Jane Misso. Waimbaji hao walipata wasaa wa kuhudu katika viwanja vya Tanganyika Packers, wote wakishuhudia yale makuu Bwana aliyotenda siku ya Jumapili kupitia mtumishi wake, Mchungaji Josephat Gwajima. Walionekana kustaajabiwa na ule umati walioukuta katika viwanja hivyo.

Kwa upande wa ibada ya Jumapili, ilianza asubuhi ya saa mbili huku kukiwa na wimbi la watu waliokuwa wakimiminika kutoka kila kona ya Dar es Salaam, wengi walikuwa wagonjwa na hawawezi walikuja wakitarajia miujiza yao na uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo. Kikubwa ni wingi wa wagonjwa waliotoka katika hospitali ya Mhimbili na Ocean road pamoja na madaktari wao wakija kumwomba Mungu awaponye kutoka katika matatizo ya moyo, kansa na magonjwa mbalimbali. Ibada ilianza kwa maombi ya saa moja kama kawaida, na baadaye kufuatiwa na watoto wa Children Ministry waliovalia sare zao nyeupe. Hapo ndipo waimbaji binafsi walifuata kama Joshua, Magreth, Rp Salama, n.k wote walimsifu Mungu kufikia kipindi cha neno la matoleo na kufuatiwa na Showers of Glory. 

Platform Choir iliongoza kipindi cha kusifu na kuabudu, ambapo walimwabudu Bwana kwa muda kabla ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kuanza kufundisha, kichwa somo kikiwa "Kwanini mateso haya" akiongea kwa ujasiri mbele ya ma laki ya watu walioudhuria, alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiteseka kwasababu ya vyanzo vya rohoni, matatizo mengi yana vyanzo vya rohoni ambavyo ni shetani na mawakala wake kama wachawi na waganga wa kienyeji. Hapo ndipo Flora Mbasha alipewa nafasi ya kumsifu Mungu kwa muda huku Mch. Gwajima akiendelea na somo alilokuwa akifundisha, wingi wa watu haukumzuia Mch. gwajima kutelemkia makutano na kuwaombea waliokuwa hawawezi na kutoa mapepo wa kila aina. Katikati ya ma laki ya watu alipita na kuwawekea mikono wagonjwa na wenye matatizo. 

Miujiza mikubwa ilianza baada za shuhuda za watu ambao walikuwa wamekufa na wengine kuchukuliwa misukule, wengi walitoa shuhuda zao akiwemo kijana Charles aliyekufa kwenye mashua ziwa Victoria, na msichana aliyerudi na kusema amemwacha Amina Chifupa, akizungumzia sakata hilo Mchungaji Gwajima alisema kuwa mimi sikuongea chochote kuhusu Amina bali huyu binti alirudi kanisani na kusema mwenyewe wazi kuwa amemwacha Amina Chifupa, huku akishangiliwa na ma laki ya waumini Mch. Gwajima aliwasimamisha watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo ambayo binti huyo alirudi, naam walikuwa wengi sana. 

Nafasi muhimu ilikuja pale, Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Mch. Gwajima aliwahita wote waliowagonjwa mbele kwaajili ya uponyaji, walikuja watu wengi sana na wengi wao wakiwa wagonjwa na wasiojiweza. Ndipo mbele ya macho ya wengi ulishuka moto wa uponyaji uliowaweka huru watu wote waliokuwa na mateso ya waliokuwa hawatembei walitembea. Kulishuudiwa wagonjwa waliotoka hospitalini wakisimama kutoka kwenye vitu, na waliokuwa walemavu wakitembea bila kushikwa na mtu. Kipindi kilidumu kwa muda kadhaa na ndipo ambapo Bwana alishuka mzima mzima kuponya.

Awali, Mchungaji Gwajima aliamuruwatu wenye mapepo watoke mbele kwa miguu yao, bila kushikwa na mtu kwa wakati huo waote waliokuwa na mapepo walilipuka na kuja mbele wenyewe na kupitia watendakazi Mungu aliwafungua wote na kuwaweka huru. biblia inasema Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye. mungu amekupa kusikia haya ili imani yako ijengwe na zaidi sana uliamini Jina la Mwokozi Yesu Kristo. 

Kanisa la Ufufuo na Uzima liwazi saa 24, na muda wote utawakuta watu wapo watakuhudumia, walete wagonjwa, watu waliokufa katika mazingira tatanishi Yesu Kristo yupo kuwafufua na kuwaweka huru. Kanisa la Ufufuo na Uzima linatoa huduma zake bure kabisa bila malipo ya aina yoyote, na maobezi na ushauri vyote ni bure kabisa hutatakiwa kulipa chochote ili uombewe karibu watu wa dini zote na kabila zote, Yesu anawapenda.

Share this post, like and comment to share blessing with others.

Sunday, June 23, 2013

Zaidi ya watu 1000 leo wameipa dhambi kisogo na kumpa Yesu Maisha yao katika viwanja vya Tanganyika Packers

Na Mwandishi wetu. Dar es Salaam. Jumapili 23th Juni 2013.

Katika jambo ambalo linampatia Mungu utukufu ni mtu mmoja kuamua kuipa dhambi kisogo na kuamua kuyaachia maisha yake kwa Yesu, kuacha dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu.Vivyo hivyo kuna furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, Luka 15:7.

Hali leo ni tofauti sana katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima kwani shangwe na nderemo mbinguni na duniani ni nyingi zaidi ambapo watu zaidi ya laki mbili (200,000) wamehudhuria ibada ya Uponyaji.
Katika Ibada ya Uponyaji iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, watu zaidi ya 1000  
kama wanavyoonekana Pichani) ambao wanatokea katika vitongoji mbali mbali vya kata na mitaa ya Dar es Salaam wamempa Yesu Maisha yao.

Jambo hili linampatia Mungu utukufu kwa kundi kubwa kama hili kuamua kuipa dhambi kisogo na kuamua kumpa Yesu maisha yao ili awe BWANA na mwokozi wa maisha yao na kuungana na familia ya watu waendao mbinguni.

Jambo hili la kuwaongoza watu wengi kwenda kwa Yesu ni mpango mahususi wa Yesu kumpokonya shetani watu aliokuwa akiwamiliki muda mrefu kwa kuwa ukiwa chini ya dhambi unakuwa mateka wa shetani.

Mchungaji kiongozi amesema kuwa hakuna dini “itakayompeleka mtu Mbinguni isipokuwa Yesu ndiye aliyekufa msalabani kwa ajili ya watu wote, na kuwa Yesu ndiye njia kweli na Uzima, hakuna aendaye Mbinguni isipokuwa kwa njia ya Yesu.”

LISTEN LIVE SERVICE: SIKILIZA IBADA YETU LIVE USTREAM

Information Ministry ya Ufufuo na Uzima inakuletea ibada moja kwa moja leo Jumapili 23 Juni 2013 toka kawe Tanganyika Packers kwa njia ya Sauti (Audio). Tupo mbioni kukuletea video pia.

Bofya link hii usikilize: http://www.ustream.tv/channel/jumapili-ya-ufufuo-na-uzima-23-6-2013

Information Ministry of Ufufuo na Uzima brings you the live service today 23 June 2013 from Kawe TanganyikaPackers through audio. We are working out to bring you the Video as well.Flora Mbasha na mumewe wakimtukuza Yehova katikati ya Maelfu ya watu leo katika Ibada hapa Ufufuo na Uzima kawe Tanganyika Packers

Flora Mbasha akisifu kwa wimbo wake mahiri wa Yesu Umwema

Maelfu ya Washirika wa Ufufuo na Uzima wakifuatilia sifa za BWANA wakati Flora Mbasha akimtukuza BWANA (YEHOVA) katika madhabahu wa Ufufuo na Uzima leo Jumapili 23 Juni 2013
Saturday, June 22, 2013

WACHUNGAJI ZAIDI YA 24 KUWASILI LEO TOKA JAPAN KUSHUHUDIA WATU WALIOKUWA MSUKULENI

Jumla ya wachungaji 24 kutoka nchini Japan watakuwepo siku ya kesho, Tanganyika Packers katika nyumba ya Ufufuo na Uzima kushuhudia matendo makuu ambayo Bwana amekuwa akitenda ikiwemo kufufua wafu, kuponya magonjwa yasiyotibika, kurudisha misukule na kuokoa watu wenye shida mbalimbali.

Mchungaji Josephat Gwajima anakupenda na anakukaribisha katika mkutano huo, unatarajiwa kuanza majira ya saa mbili asubuhi, katika viwanja vya wazi vya Tanganyika Packers, Kawe. Walete wenye shida mbalimbali, Yesu Kristo atakuwepo kuwafungua wote. Na kwa macho yako utashuhudia wale waliokuwa wamekufa na kufufuliwa. 
Dar es Salaam kwa Yesu na Mchungaji Josephat Gwajima. 

Like, comment and share for AMEN

Thursday, June 13, 2013

KAMA BADO UPO HAI LIPO TUMAINI


Na Mchungaji  Maximillian Machumu (RP)

Ujumbe huu ni ujumbe ambao waweza kubadilisha maisha yako kama utaamua kufungua moyo wako, kwasababu mwenendo wa maisha waweza kukufanya uhisi kuwa hakuna matumaini lakini leo baada ya kusoma somo hili unaenda kuona mwanga mpya kwenye maisha yako.

Ezekieli 37:11 "kisha akaniambia, mwanadamu mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli tazama wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa mbali kabisa" 
Ukiendelea kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi.

Hatua kubwa sana ya kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu, ni ile ambayo mtu mmoja katikati ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu.

Mungu hapendi ukate tamaa, wala umkufuru yeye katikati ya magumu na kwa taarifa yako tu ni kuwa watu wakubwa katika biblia hata walioitwa na Mungu, walipitia magumu lakini katikati ya magumu hayo walitamka maneno ya ushindi. Pia, kutamka maneno ya matumaini katikati ya magumu kunakufanya utoke mapema kwenye hali mtu aliyoko.

Inawezekana unapitia katika hali ngumu kwa sasa, lakini utakalolinena ukiwa katika dhiki hiyo itakufanya ama utoke ukiwa shujaa au aliyeshindwa. Na ndio maana hata Ezekieli alipowekwa mbele ya mifupa mikavu na kuulizwa 'je mifupa hiyonyaweza kuishi?' Naye alijibu kuwa 'wewe Bwana wajua', akionyesha kuwa hakuna jambo la kumshinda Bwana. Na ndio maana hata alipopewa nafasi ya kutamka neno alitamka uzima. Ni muhimu kujua maneno ya kutamka pindi unapopitia katika hali ngumu.

Ni muhimu kujua unachokiongea leo ndicho utakachokiishi kesho; wengine hujikuta wanaongea maneno mabaya juu yao wenyewe, huku wakisahau kuwa ni shetani ambaye anawafanya waongee maneno hayo ili apate nafasi ya kuharibu maisha yao baadaye.

Isaya 57:10 "ulikuwa umechoka kwaajili ya urefu wa njia yako, lakini hukusema hapana matumaini, ulipata kuuhishwa nguvu zako, kwasababu hiyo hukuugua" kumbe watu hawa, hali yao halisi iliwafanya wakate tamaa ya kufika wanapokwenda lakini pamoja na urefu wa njia bado walikiri kuwa matumaini yapo. Na kwasababu ya ukiri huo walipewa nguvu mpya. Usikiri udhaifu, Mungu anayetenda miujiza yupo na ukimkimbilia yeye, ataiondoa aibu yako na kukuvika kicheko.

Ukifuatilia habari ya Yusufu ambaye maisha yake yalianza kwa kuuzwa na ndugu zake kwa wamisri. Na alipouzwa waliigawa kanzu yake maana yake aliuzwa bila mavazi, lakini akiwa Misri na matumaini yakaanza kuja likatokea jambo jingine la kukatisha tamaa. Mke wa potifa akamsingizia kuwa anataka kumbaka, hivyo akatupwa gerezani maisha katiaka hali hiyo ni dhahiri kuwa Yusufu alikata tamaa kabisa. Lakini alipotoka gerezani Yusufu akawa waziri mkuu, jiulize, Mungu aliyemfanya kuwa waziri mkuu alikuwa wapi kipindi anauzwa? Au jiulize alikuwa wapi kipindi anawekwa gerezani? 

Ni muhimu kujua kuwa sio kuwa kwa unayopitia hali ngumu ukahisi Mungu amekuacha, si kweli; Mungu bado yupo pamoja na wewe na matumaini bado yapo. Yesu Kristo ni tumaini la kutosha kwenye maisha yako. Leo sikia sauti yake hii ikisema BADO YAPO MATUMAINI. Pata muda kuingia kwenye maombi na Mungu anakupa tumaini jipya leo. Inawezekana unapitia shida za ndoa, matatizo kazini, vita shuleni, roho ya kukataliwa mpaka umejihisi hakuna kesho ile uliyoiwaza. Leo tambua kuwa hata Ayubu katikati ya dhiki kuu hakuwahi kumkufuru Jehova bali aliweka tumaini lake kwake na kwa saa sahihi matumaini makuu yalionekana.

Hata kama ndoto yako inaonekana inataka kuzimika, inawezekana ulikuwa na ndoto za kusoma katika maisha yako lakini sasa unaona muda umeenda nakwambia bado lipo tumaini. Inawezekana madktari walikwambia kuwa mwisho wa kuzaa ni miaka 45 na wewe sasa unajiona unaelekea huo umri ukiwa hauna mtoto lakini nakwambia neno ambalo Yesu amenituma kwalo kuwa USIKATE TAMAA BADO YAPO MATUMAINI!!!!!

Mchungaji Maximillian Machumu (RP) 12/6/2013

Sunday, June 2, 2013

Breaking News: Habari zilizotufikia hivi punde: Zaidi ya watu 50 wamerudishwa toka msukuleni

Na Mwandishi wetu. | Dar es Salaam 2 Juni 2013

Zaidi ya watu 50 wamerudishwa toka msukuleni baada ya kufanyika maombi ya kuwarudisa leo mchana hapa Kanisani Ufufuo na Uzima kanisa la maelfu ya Watu ambapo Mchunguji kiongozi Josephat Gwajima alifundisha somo liitwalo ‘Unaishi ingawa umekufa’ na baadaye maombi yakiongozwa na yeye kwa zaidi ya dakika 15 ambapo watu hao walitoa ushuhuda kuwa walikuwa wamewekwa kwenye makabati, kibuyu, kwenye chupa, makaburini na kwa waganga wa kienyeji.

Akishuhudia mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema alisema kuwa alikuwa kwenye chupa alimowekwa na mke mwenzake, baadaye akasikia sauti ya watu wakimwita kwa nguvu njoo njoo na baadaye alijikuta yupo chini kanisani akiombewa na wachungaji.

Akieleza maana ya kuishi lakini umekufa katika somo alilofundisha Mch. Kiongozi Josephat Gwajima alisema kuwa mtu sio mwili bali mtu ni roho, na roho yenyewe ina nafsi  hai na inakaa ndani ya nyumba na nyumba yenyewe inaitwa mwili. Akielezea zaidi Mchungaji alisema kuwa mtu anaweza kuwa anaishi anakula anafanya kila jambo mwilini lakini kwa namna ya rohoni ameibiwa na ametekwana kuhifadhiwa sehemu ama ndani ya chupa,au ndani ya kabati .

Somo hilo lilifundishwa kwa msingi wa neno la Mungu (Biblia) ambapo Mchungaji alisoma vifungu vingi vya neno la Mungu ambavyo msingi wake ni kufichua siri za shetani za kuwaiba watu ambao ni roho zao ingali miili yao inaonekana kuwa hai. Sehemu ya vifungu hivyo ni pamoja na 1 samweli 22:23,

1 falme 17;22 1 falme 19; 14, Ayubu 33;30 roho inaweza kupelekwa shimoni. Maandiko haya huelezea namna roho ya mtu inavyoweza kutekwa na ibilisi shetani joka la zamani na baba wa uongo. Pamoja na hayo Mchungaji alitoa dalili za mtu alikufa angawa anaishi kutoka 1 Tim 5:6 ‘Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa angawa yu hai’.