Sunday, June 2, 2013

Breaking News: Habari zilizotufikia hivi punde: Zaidi ya watu 50 wamerudishwa toka msukuleni

Na Mwandishi wetu. | Dar es Salaam 2 Juni 2013

Zaidi ya watu 50 wamerudishwa toka msukuleni baada ya kufanyika maombi ya kuwarudisa leo mchana hapa Kanisani Ufufuo na Uzima kanisa la maelfu ya Watu ambapo Mchunguji kiongozi Josephat Gwajima alifundisha somo liitwalo ‘Unaishi ingawa umekufa’ na baadaye maombi yakiongozwa na yeye kwa zaidi ya dakika 15 ambapo watu hao walitoa ushuhuda kuwa walikuwa wamewekwa kwenye makabati, kibuyu, kwenye chupa, makaburini na kwa waganga wa kienyeji.

Akishuhudia mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema alisema kuwa alikuwa kwenye chupa alimowekwa na mke mwenzake, baadaye akasikia sauti ya watu wakimwita kwa nguvu njoo njoo na baadaye alijikuta yupo chini kanisani akiombewa na wachungaji.

Akieleza maana ya kuishi lakini umekufa katika somo alilofundisha Mch. Kiongozi Josephat Gwajima alisema kuwa mtu sio mwili bali mtu ni roho, na roho yenyewe ina nafsi  hai na inakaa ndani ya nyumba na nyumba yenyewe inaitwa mwili. Akielezea zaidi Mchungaji alisema kuwa mtu anaweza kuwa anaishi anakula anafanya kila jambo mwilini lakini kwa namna ya rohoni ameibiwa na ametekwana kuhifadhiwa sehemu ama ndani ya chupa,au ndani ya kabati .

Somo hilo lilifundishwa kwa msingi wa neno la Mungu (Biblia) ambapo Mchungaji alisoma vifungu vingi vya neno la Mungu ambavyo msingi wake ni kufichua siri za shetani za kuwaiba watu ambao ni roho zao ingali miili yao inaonekana kuwa hai. Sehemu ya vifungu hivyo ni pamoja na 1 samweli 22:23,

1 falme 17;22 1 falme 19; 14, Ayubu 33;30 roho inaweza kupelekwa shimoni. Maandiko haya huelezea namna roho ya mtu inavyoweza kutekwa na ibilisi shetani joka la zamani na baba wa uongo. Pamoja na hayo Mchungaji alitoa dalili za mtu alikufa angawa anaishi kutoka 1 Tim 5:6 ‘Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa angawa yu hai’.

No comments:

Post a Comment