Friday, June 28, 2013

WIKI YA BARAKA NA MIUJIZA UFUFUO NA UZIMA


Na Mwandishi wetu | Kawe, Dar es Salaam.
Wiki hii imekuwa wiki ya baraka sana kwa kanisa la Ufufuo na Uzima, sio tu kwasababu ya neema za Mungu kwetu bali pia tumeshuhudia matendo makuu ya Mungu aliyotenda katikati yetu. 

Wiki ilianza kwa ujio wa Wachungaji zaidi ya 23 kutoka Japan kuja kushuhudia makuu ambayo Bwana amekuwa akitenda, kiongozi wa msafara huo, Pastor Yoshida alipopewa nafasi ya kuongea na waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima alisema wazi kuwa lengo lao la kuja Tanzania, na zaidi sana Ufufuo na Uzima ni kuja kuchukua nguvu ya Uhamsho iliyo ndani ya Mchungaji Josephat Gwajima na kuipeleka Japan. Kwa mujibu wa Takwimu zinaonyesha ni asilimia 1 tu ya wajapan ndio wanaomjua Kristo wengi wao wanaabudu miungu. Wachungaji hao kutoka Japani walipatanafasi ya kuabudu nasi ibada ya Jumapili wakiishuhudia matendo makuu yale Mungu aliyotenda.

Haikuishia hapo, wiki hii tumepata ugeni mkubwa wa Waimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel na Flora Mbasha pamoja Jane Misso. Waimbaji hao walipata wasaa wa kuhudu katika viwanja vya Tanganyika Packers, wote wakishuhudia yale makuu Bwana aliyotenda siku ya Jumapili kupitia mtumishi wake, Mchungaji Josephat Gwajima. Walionekana kustaajabiwa na ule umati walioukuta katika viwanja hivyo.

Kwa upande wa ibada ya Jumapili, ilianza asubuhi ya saa mbili huku kukiwa na wimbi la watu waliokuwa wakimiminika kutoka kila kona ya Dar es Salaam, wengi walikuwa wagonjwa na hawawezi walikuja wakitarajia miujiza yao na uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo. Kikubwa ni wingi wa wagonjwa waliotoka katika hospitali ya Mhimbili na Ocean road pamoja na madaktari wao wakija kumwomba Mungu awaponye kutoka katika matatizo ya moyo, kansa na magonjwa mbalimbali. Ibada ilianza kwa maombi ya saa moja kama kawaida, na baadaye kufuatiwa na watoto wa Children Ministry waliovalia sare zao nyeupe. Hapo ndipo waimbaji binafsi walifuata kama Joshua, Magreth, Rp Salama, n.k wote walimsifu Mungu kufikia kipindi cha neno la matoleo na kufuatiwa na Showers of Glory. 

Platform Choir iliongoza kipindi cha kusifu na kuabudu, ambapo walimwabudu Bwana kwa muda kabla ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kuanza kufundisha, kichwa somo kikiwa "Kwanini mateso haya" akiongea kwa ujasiri mbele ya ma laki ya watu walioudhuria, alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiteseka kwasababu ya vyanzo vya rohoni, matatizo mengi yana vyanzo vya rohoni ambavyo ni shetani na mawakala wake kama wachawi na waganga wa kienyeji. Hapo ndipo Flora Mbasha alipewa nafasi ya kumsifu Mungu kwa muda huku Mch. Gwajima akiendelea na somo alilokuwa akifundisha, wingi wa watu haukumzuia Mch. gwajima kutelemkia makutano na kuwaombea waliokuwa hawawezi na kutoa mapepo wa kila aina. Katikati ya ma laki ya watu alipita na kuwawekea mikono wagonjwa na wenye matatizo. 

Miujiza mikubwa ilianza baada za shuhuda za watu ambao walikuwa wamekufa na wengine kuchukuliwa misukule, wengi walitoa shuhuda zao akiwemo kijana Charles aliyekufa kwenye mashua ziwa Victoria, na msichana aliyerudi na kusema amemwacha Amina Chifupa, akizungumzia sakata hilo Mchungaji Gwajima alisema kuwa mimi sikuongea chochote kuhusu Amina bali huyu binti alirudi kanisani na kusema mwenyewe wazi kuwa amemwacha Amina Chifupa, huku akishangiliwa na ma laki ya waumini Mch. Gwajima aliwasimamisha watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo ambayo binti huyo alirudi, naam walikuwa wengi sana. 

Nafasi muhimu ilikuja pale, Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Mch. Gwajima aliwahita wote waliowagonjwa mbele kwaajili ya uponyaji, walikuja watu wengi sana na wengi wao wakiwa wagonjwa na wasiojiweza. Ndipo mbele ya macho ya wengi ulishuka moto wa uponyaji uliowaweka huru watu wote waliokuwa na mateso ya waliokuwa hawatembei walitembea. Kulishuudiwa wagonjwa waliotoka hospitalini wakisimama kutoka kwenye vitu, na waliokuwa walemavu wakitembea bila kushikwa na mtu. Kipindi kilidumu kwa muda kadhaa na ndipo ambapo Bwana alishuka mzima mzima kuponya.

Awali, Mchungaji Gwajima aliamuruwatu wenye mapepo watoke mbele kwa miguu yao, bila kushikwa na mtu kwa wakati huo waote waliokuwa na mapepo walilipuka na kuja mbele wenyewe na kupitia watendakazi Mungu aliwafungua wote na kuwaweka huru. biblia inasema Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye. mungu amekupa kusikia haya ili imani yako ijengwe na zaidi sana uliamini Jina la Mwokozi Yesu Kristo. 

Kanisa la Ufufuo na Uzima liwazi saa 24, na muda wote utawakuta watu wapo watakuhudumia, walete wagonjwa, watu waliokufa katika mazingira tatanishi Yesu Kristo yupo kuwafufua na kuwaweka huru. Kanisa la Ufufuo na Uzima linatoa huduma zake bure kabisa bila malipo ya aina yoyote, na maobezi na ushauri vyote ni bure kabisa hutatakiwa kulipa chochote ili uombewe karibu watu wa dini zote na kabila zote, Yesu anawapenda.

Share this post, like and comment to share blessing with others.

No comments:

Post a Comment