Sunday, June 23, 2013

Zaidi ya watu 1000 leo wameipa dhambi kisogo na kumpa Yesu Maisha yao katika viwanja vya Tanganyika Packers

Na Mwandishi wetu. Dar es Salaam. Jumapili 23th Juni 2013.

Katika jambo ambalo linampatia Mungu utukufu ni mtu mmoja kuamua kuipa dhambi kisogo na kuamua kuyaachia maisha yake kwa Yesu, kuacha dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu.Vivyo hivyo kuna furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, Luka 15:7.

Hali leo ni tofauti sana katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima kwani shangwe na nderemo mbinguni na duniani ni nyingi zaidi ambapo watu zaidi ya laki mbili (200,000) wamehudhuria ibada ya Uponyaji.
Katika Ibada ya Uponyaji iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, watu zaidi ya 1000  
kama wanavyoonekana Pichani) ambao wanatokea katika vitongoji mbali mbali vya kata na mitaa ya Dar es Salaam wamempa Yesu Maisha yao.

Jambo hili linampatia Mungu utukufu kwa kundi kubwa kama hili kuamua kuipa dhambi kisogo na kuamua kumpa Yesu maisha yao ili awe BWANA na mwokozi wa maisha yao na kuungana na familia ya watu waendao mbinguni.

Jambo hili la kuwaongoza watu wengi kwenda kwa Yesu ni mpango mahususi wa Yesu kumpokonya shetani watu aliokuwa akiwamiliki muda mrefu kwa kuwa ukiwa chini ya dhambi unakuwa mateka wa shetani.

Mchungaji kiongozi amesema kuwa hakuna dini “itakayompeleka mtu Mbinguni isipokuwa Yesu ndiye aliyekufa msalabani kwa ajili ya watu wote, na kuwa Yesu ndiye njia kweli na Uzima, hakuna aendaye Mbinguni isipokuwa kwa njia ya Yesu.”

1 comment:

  1. Hakika tunajivunia mungu wa ufufuo na uzima.hakika mungu wa mchungaji Josephat Gwajima yuko hai na anaishi..

    ReplyDelete