Monday, September 30, 2013

WATOTO WAZIMIA BAADA YA KUMUONA MAMA YAO ALIYEKUFA MIAKA MINGI KUFUFUKA TOKA KWA WAFU

Ni siku ya nne ya mkutano mkubwa wa ufufuo na uzima na Mchungaji Josephat Gwajima jijini arusha, ambapo miujiza mingi imeendelea kutendeka.

Leo Mch. Kiongozi Josephat Gwajima amefundisha kuhusu "ULIMWENGU WA ROHO" na kufundisha aina za misukule na jinsi wanavyochukuliwa somo ambalo lilifungua watu wengi ambao walikuwa msukuleni.

Umati uliokuwepo mkutanoni siku ya nne...


Watu wengi walirudishwa kutoka msukuleni na kufanya watu kushangazwa sana na matendo makuu ya Mungu, kiasi kufanya hata baada ya kuruhusiwa kuondoka wao wakaamua kubaki ili tu waone maajabbu ya Mungu...Ni makutano makubwa sana katika viwanja vya relini jijini Ariusha; Mungu amedhihirisha uweza wake kwa namna isiyokuwa ya kawaida.

Dada aliyekuwa amechukuliwa msukule akitoa ushuhuda baada ya Kurudishwa.

Siku ya nne kumetokea jambo la ajabu pale wanawake wawili walipoanguka karibu na eneo la mkutano kutoka hewani. Na kuleta taharuki miongoni mwa watu waliokuwepo mkutanoni. picha zifuatazo zinaonyesha tukio zima.

Mmoja wa mwanamke aliyeanguka kutoka hewani muda mfupi baada ya maombi ya Mchungaji Gwajima


   Kulia ni bibi aliyefufuka wakati mkutano ukiendelea na kuzua tafrani ya wanawe kuzimia, na kushoto ni mwanamke mmoja mchawi aliyedondokea katika viwanja vya mkutano wa injili unaoendelea hapa Arusha
  
Mtoto azimia mara baada ya kumwona mamaye aliyekufa miaka mingi.

Watoto wa mwanamke aliyekufa miaka mingi baada ya kuzinduka..tena...Maelfu ya watu wakiwahawataki kiondoka mara baada ya kushuhudia mambo makuu ya Yesu.

Sunday, September 29, 2013

MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI ARUSHA SIKU YA TATU

We are Broadcasting live from Relini Grounds, Arusha City in Tanzania. The Ufufuo na Uzima Mega Crusade with Pastor Josephat Gwajima via This link:

Sikiliza Mkutano wa Injili kutoka Arusha; Mchungaji Josephat Gwajima anafundisha kupitia link hii:


CLICK HERE

BONYEZA HAPA

Siku ya tatu ya mkutano ilianza kwa kipindi cha sifa na kuabudu na watu walimiminika wengi viwanjani hata kabla ya mkutano kuanza. Kama ilivyoada Mchungaji Josephat Gwajima aliwasili viwanjani mapema sana, na kuanza kuhubiri saa kumi kamili.


Sifa na Kuabudu zilimdhihirisha Mungu katika mkutano mapema kabla hata ya maombezi. Ni kweli Mungu huketi katikati ya sifa
Sehemu ya Umati uliokuwepo katika mkutano uliofanyika viwanja vya Relini, jijini Arusha.


Jackson Benty akiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu ilikuwa Baraka sana

Binti Joyce ambaye alikufa na kufufuliwa baada ya maombezi naye alikuwepo kutoa ushuhuda wake.Mchungaji Josephat Gwajima akifundisha neno la Uzima: Vyanzo vya Matatizo.Saturday, September 28, 2013

Ufufuo na Uzima yalitikisa Jiji la Arusha kwa Ishara na Maajabu

Na Mwandishi wetu | 28 Septemba 2013 | Arusha

Ufufuo na Uzima ambaye ni Yesu mwenyewe amelitikisa jiji la Arusha kwa ishara miujiza na maajabu akiwamo kurudishwa toka msukuleni kwa binti mmoja na wengine wengi kufunguliwa toka katika vifungo vya majini. 
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akimfungua binti aliyerudi toka msukuleni dakika chache baada ya maombi.

Haya yote yametokea ndani ya Mkutano Mkubwa wa Injili ulioandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima chini ya uongozi makini wa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima ambaye Mungu amempaka mafuta kuipeleka injili ya Ufufuo wa wafu duniani kote akianzia bara Amerika, Ulaya, Asia na sasa ni zamu ya Afrika ikianzia na jiji la Arusha.

Akiongoza ibada iliyohudhuliwa na zaidi wa watu ishirini elfu (20,000) katika viwanja vya Relini hapa jijini Arusha, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory of Christ Tanzania Church) Josephat Gwajima amerudisha msukule baada ya maombi yaliyojaa nguvu ya Mungu yenye kurudisha watu waliochukuliwa ama kufa katika mazingira yenye utata. 


Binti aliyerudi toka msukuleni akitafakari neno moyoni mwake na kustaajabu ukuu wa Mungu
Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha wakiombewa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima


Ikiwa ni siku ya kwanza tu ya kufundisha, kufungua watu walioonewa, kufufua wafu Mch. Gwajima alifundisha somo liitwalo "Vyanzo vya Matatizo" na mara baada ya hapo maombi yalianza na kufuatiwa na ishara, miujiza na maajabu. Zaidi ya yote viwete wametembea na misukule imerudi toka vifungoni. 

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiishambulia ngome ya mashetani wa Arusha katika mkutano wa maelfu kwa elfu wa wakazi wa jiji hili.
Mkutano huu utaendelea hapa jijini Arusha mpaka tarehe 13 Octoba 2013 na baadaye majeshi ya Ufufuo na Uzima yatang'oa nanga jijini Arusha na kutua Manispaa ya Moshi mkoni Kilimanjaro na kuanza mkutano mwingine tarehe 20 Octoba 2013 katika viwanja vya Mashujaa. 

MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI ARUSHA SIKU YA PILI

We are Broadcasting live from Relini Grounds, Arusha City in Tanzania. The Ufufuo na Uzima Mega Crusade with Pastor Josephat Gwajima via This link:

Sikiliza Mkutano wa Injili kutoka Arusha; Mchungaji Josephat Gwajima anafundisha kupitia link hii:


CLICK HERE

BONYEZA HAPA

Friday, September 27, 2013

ARUSHA MEGA CRUSADE WITH PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA

Kusikiliza mkutano Live kutoka Arusha, Bonyeza link hii 

                              BONYEZA HAPA


Enjoy Live Audio Streaming From Arusha
                              CLICK HEREKupata Picha za Matukio kutoka Arusha leo: CLICK HERE


Tuesday, September 24, 2013

VIDEO: MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA AKIONGEA KUHUSU MKUTANO WA ARUSHA

Katika Video hii, Mchungaji Gwajima ametoa mchanganuo wa maandiko yanayoonyesha uwezekano wa mtu aliyekufa kufufuka na pia, ameeleza nia na madhumuni ya kufanya mikutano mikubwa ya Injili, Tanzania Nzima, akianzia na Arusha. 

Fuatilia Video hii:KARIBU VIWANJA VYA RELINI JIJINI ARUSHA UONE ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA AMBAYO YESU KRISTO ANATENDA.

Sunday, September 22, 2013

UJUMBE: KUISHI SAWASAWA NA NDOTO YAKO (LIVE YOUR DREAM)

Na Mch. Josephat Gwajima

Utangulizi:
Biblia imetaja sana kwa habari ya ndoto, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo pekee, neno “ndoto ” limeandikwa zaidi ya mara 36. Pia, katika kitabu cha Daniel neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 29. Na ndio maana Mungu alipotaka watu wake wajenge ama madhabahu au hekelu aliwaonyesha kwanza katika ndoto; kumbe ujenzi wowote huanzia katika kuona. Vivyo hivyo hata watu wanaomtegemea shetani huingia ulimwengu wa roho na kujenga kile walichokiona kutoka kwa shetani.

TABIA YA MUNGU KATIKA NDOTO:
Kutoka 25:8-9; Mungu akitaka ujenge anaanza kukuonyesha; ndio maana alimwonyesha pia na Musa na kumtaka ajenge sawa sawa na alichomwonyesha “exactly like the pattern I will show you” Kutoka 25:37-40; Hii ni tabia ya Mungu kuwaonyesha watu kupitia ndoto na watu wengi pasipo kujua wamejikuta wakidharau ndoto.

Ukisoma katika kitabu cha Habakuki 2:2-3; Mungu alimwamuru Habakuki aiandike ile ndoto; kwasababu asingeweza kufanya kuona kwanza katika ulimwengu wa roho. Na ndio maana neno ndoto limeandikwa mara nyingi katika kitabu cha Mwanzo kwasababu hicho ndicho kitabu cha asili (origin). Hiyo inatufundisha kuwa mwanzo wa vitu huanzia katika ndoto.
Mambo ambayo Mungu anaweza kuyafanya kupitia ndoto:
i)                    Mungu anaweza kufumbua mafumbo kupitia ndoto:-
Mwanzo 40: 2-19; Hapa tunaona kwa habari ya mwokaji na mwoshaji wa Farao ambao walipata kujua hatari iliyokuwa imejificha kwa njia ya ndoto. Kwa njia hiyo wote wawili wakajua maisha yao siku tatu mbele. Kumbe ndoto yaweza kukufunulia mitego au hatari iliyojificha au kupangwa na watu wabaya.

Farao alikwisha kupanga kuwa siku ya tatu itakuwa hukumu yao lakini bila kuwambia; lakini waliweza kufunuliwa katika ndoto. Ni maombi yangu kuwa Mungu na akuonyeshe hatari zote ulizopangiwa sirini.

ii)                  Mungu anaweza kukurudisha au kukurudishia ulichokipoteza:-
Katika kitabu cha Danieli pekee, neno “ndoto” limeandikwa zaidi ya mara 29; Danieli alikuwa uhamishoni Babeli; akiwa huko Mungu akamwonyesha kwa habari ya kumrudisha mahali pake. Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulikuwa na mafanikio lakini sasa hayapo; au ulikuwa na afya nzuri lakini sasa haipo; katika ndoto Mungu aweza kukurudisha sehemu unayotakiwa kuwapo.

Na ndio maana kila siku huwa nasema Tanzania mpya niliyoiona katika ndoto inakuja; Tanzania yenye maendeleo; yenye hospitali nzuri, yenye gesi, Tanzania yenye madini inakuja na sifi leo ama kesho mpaka ndoto itimie.

Ni maombi yangu Mungu akurudishie ile hatma njema ya maisha yako ambayo shetani aliichukua katika maisha yako.

iii)                Ndoto zinaweza kukuonya:-
Ndoto zaweza kukuonya usichukue maamuzi ambayo sio sahihi, uache tabia mbaya ambayo ina mwisho mbaya. Mathayo  2: 13-16; Baada ya Herode kugundua kuwa amedhihakiwa na mamajusi akaamua kuua watoto ili amwangamize Yesu; lakini Yusufu akapewa onyo na Mungu kuwa ampeleke mtoto Misri. Ni kweli Herode aliangamiza lakini walioangamizwa ni wale ambao baba na mama zao hawakuota ndoto.

Hapa tunaona athari moja ya kutoota ndoto, maana madhara yake yaliwahi kugharimu maisha ya watoto wao. Kupitia ndoto Yesu aliokolewa, Mungu huongea pia kupitia ndoto. Ndio maana ni muhimu kumwomba Mungu akupe ndoto ya kuokoa familia au ukoo wako.

iv)                Mungu anaweza kutufariji katika ndoto:-
Katika maisha unaweza kupitia wakati mgumu, umezungukwa na madeni au kukata tamaa lakini Kupitia ndoto Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye. Kwa njia hii Yusufu alifarijiwa kupitia ndoto; kwa njia hiyo Yusufu alipokea faraja na kuhakikishiwa ushindi.

Yusufu alipoota ndoto zilisababisha achukiwe na ndugu zake, na wakamtupa shimoni na baadaye kumuuza Misri lakini ndoto yake ilibaki palepale. Haikutosha hapo, bali alisingiziwa ametaka kumbaka mke wa waziri mkuu wa Misri na akaja kufungwa. Lakini katika mateso yake Mungu alikuja kumfariji kupitia ndoto na kumrudisha katika nafasi yake.

Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulisingiziwa na kupoteza nafasi ambayo Mungu alikupa; leo kila aliyekunyang’anya nafasi naamuru uchukue nafasi yake; nafasi ya ndoa, nafasi ya umeneja, nafasi ya uongozi ninaiamuru irudi kwako katika jina la Yesu Kristo.  Yule Yule aliyekupiga vita mwaka jana mwaka huu utachukua nafasi yake katika jina la Yesu.

Kutoka katika ufungwa gerezeni hadi kuwa mkuu katika nchi ya Misri, yote hii ilianza katika ndoto. Kumbuka ndoto za Yusufu zilianza alipokuwa na miaka 16 lakini alikuja kuimiliki akiwa na miaka 40. Tatizo la watu wengi wanakata tamaa mapema; hutakiwi kufa moyo, hapo katikati wakati unaisubiria ndoto unaweza ukapitia mateso na mabonde lakini ndoto itakuja na itatimia usipozimia moyo.

v)                  Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye katika ndoto:-
Mungu hutenda kazi tofauti na sisi tunavyowaza; Yule mtu unayemuona mdhaifu ndiye ambaye Mungu anamuona shujaa; vivyo hivyo kwa habari ya Yesu, yeye alizaliwa katika hema ya ng’ombe; Samweli alizaliwa na Hana ambaye alikuwa hazai hapo mwanzo; Musa naye alitupwa kwenye mto akakulia kwa baba wa kambo; Samson alizaliwa na mama ambaye alikuwa tasa hapo mwanzo; na ndio maana hata siku moja usidharau mambo madogo kwasababu ndiyo ambayo Mungu huyatumia.

vi)                Mungu anaweza kutuonyesha ushindi juu ya adui zetu katika ndoto:-
Kila mtu ana adui wa maisha wake; awe rais, waziri, mchungaji, au askofu lazima utakuwa na adui wa maisha yako. Yaani kwa kila hatua unayopiga unatengeneza marafiki na adui wengi kwasababu hiyo kila mtu ana adui zake. Lakini Mungu anaweza kukuonyesha ushindi wako katika ndoto. Ukisoma katika kitabu cha Waamuzi utaona kwa habari za Gideoni ambaye alitakiwa kupigana na Wamidiani; lakini kabla ya kwenda vitani Mungu akatumia ndoto kumwonyesha ushindi unaokuja mbele.

Ni maombi yangu Mungu akuonyeshe ushindi juu ya adui zako katika jina la Yesu Kristo. Kumbe kupitia ndoto unaweza kuonyeshwa adui ambaye hapendi mafanikio yako yaani Mungu akupe ushindi dhidi ya hila zake mbaya katika Jina la Yesu.

NDOTO:
Sikumoja nilikuwa nasafari kutoka nchi moja kwenda nyingine, nikakata tiketi ya kusafiri kesho yake; usiku wake nikiwa nimelala nikaota ndoto nipo ndani ya lile basi ghafla nikajiona nipo ndani ya basi na likawa linakwenda; gari likiwa linaendelea kwenda kulikuwa na mzigo juu ya siti niliyokuwa nimekaa ghafla mzigo ule ukaniangukia na kila nilipojaribu kuinuka nikashindwa ghafla gari likaanguka alafu nikashtuka kutoka ndoto.

Nilipoamka nikaanza kuomba kwa bidii na kwa muda mrefu kufika kituoni nikakuta gari limeshaniacha; basi nikaomba kusafiri na gari linalofuata la kampuni hiyo. Cha ajabu tukawa tunafuatana na hilo gari ambalo nilitakiwa nipande mimi; mbele ya macho yangu nikaona gari lile limepata ajali mbaya na moyoni nikasikia niende kuangalia katika ile siti niliyotakiwa kukakaa; ndipo nikakuta Yule mtu amepondwa na jeki iliyokuwa ndani ya begi.

vii)             Mungu anawezakukuonyesha jinsi ya kumtendea mtu katika ndoto:-
Kupitia ndoto Mungu anaweza kukuonya juu ya uamuzi mbaya unaotaka kuuchukua juu ya mtu fulani katika ndoto; hii tunaiona kwa habari ya Yesu ambapo mkewe pilato alionywa katika ndoto juu ya hatua alizotaka kuchukua Pilato juu ya hukumu ya Yesu. Kumbe Mungu aweza kumuonya mtu juu ya uamuzi mbaya ambao waweza kumgharimu mtu huyo kupitia ndoto.

Mungu anaweza kukuonya juu ya uamuzi unaotaka kuchukua juu ya mtu wakati wa hasira, wakati wa uoga au wakati mgumu. Mungu huonya kupitia ndoto na ndio maana ni muhimu kutokufanya maamuzi yoyote wakati wa hasira; hofu; wakati mgumu kwasababu unaweza kujikuta unafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Watu wengi wamevunja mahusiano mazuri na watu kwasababu ya maamuzi mabaya lakini kupitia ndoto Mungu aweza kukuonya na kukuonyesha njia ya kufanya.

NINI CHA KUFANYA UNAPOOTA NDOTO:
-          Baada ya kuota ndoto ambayo si nzuri unatakiwa usimame kinyume katika maombi. Sambaratisha ndoto zote na wasimamizi wake wote katika ulimwengu wa roho.

-          Na ikitokea umeota ndoto nzuri unatakiwa uiteke na kuimiliki ndoto hiyo; kushindwa kuchukua hatua kutakufanya usiimiliki hiyo ndoto. Ukiota umefanikiwa katika biashara fulani, unatakiwa uanze kwa kuomba halafu chukua hatua ya kuimiliki ndoto hiyo.


-          Ukiota ndoto halafu huilewi ni nzuri au mbaya unatakiwa uamuru katika maombi kuwa kama ndoto hii ni mbaya ninaisambaratisha katika jina la Yesu na kama ndoto hii ni nzuri imiliki katika jina la Yesu. 

Saturday, September 21, 2013

MAANDALIZI MKUTANO WA ARUSHA

Na Mwandishi wetu,

Asubuhi majira ya saa tatu asubuhi majeshi ya Bwana walikutana katika viwanja vya relini,hii ni pamoja na wale waliokua waliofikia sehemu mbali mbali tofauti na kambini.

Baada ya kufika uwanjani watu wote waligawanywa katika makundi kumi yaliyokua chini ya ma MP’s , na makundi yote hayo kumi yalikua chini ya AP.

Baada ya kugawanywa katika makundi imbali mbali majeshi ya Bwana yalipanda mabasi ya ufufuo na uzima kuelekea mahali ambapo walitakiwakwenda kubandika matangazo kwa siku hiyo.

Wakati wakielekea huko walipofika njiani eneo la Mrefu walisimama kwa muda kulisubiri gari la matangazo ambalo lilifika panapo majira ya saa nane mchana.

Wakati gari la matangazo likisubiriwa maeneo ya Mrefu baadhi ya watenda kazi walitumia nafasi hiyo kukaribisha watu wa maeneo hayo katika mkutano unaoanza tarehe 27 /9 /2013.
Baadhi ya mambo yaliyojitokeza wakati huo ni pale baadhi ya watu walionyesha kiu ya kutaka kumpokea Yesu ,ndipo baadhi ya mashepherd wa Ufufuo na uzima walipotumia fulsa hiyo kuongoza watu hao sala ya toba na kuwaombea baadhi yao.
Kati ya mambo yaliyotendeka mahali hapo ni tukio la mamammoja aliyekua miongoni mwa waliompokea Yesu kushuhudia na kusema alikua akisumbuliwa na maumivu ya tumbo muda mrefu na alipokwenda hospitali walisema ana vidonda vya tumbo, lakini baaada ya kuombewa maumivu yaliisha pale pale,

Haikuishia hapo mama mmoja nae aliyekua akisumbuliwa muda mrefu na matatizo ya miguu alipokea ponyaji wake pale pale na kushuhudia kua maumivu yaliyokua yakimsumbua yametoweka mara moja.

Tuliondoka mahali pale majira ya saa nane na nusu mchana na kuwaacha watu wa eneo la mrefu wenye furaha huku wakiahidi kutokukosa katika mkutano baada yakuona Mungu akiwagusa hao wachache waliokua hapo.

Baada ya hapo tuliondoka na kwenda moja kwa moja katika eneo la Tengeru, Eneo hili lilikua na watu wengi kidogo kulingana na shughuli mbali mbali zilizokua zikiendelea mahali hapo.

Majeshi ya ufufuo na uzima yalipofika mahali hapo watu walionekana kuguswa na matangazo hayo na ndipo waliposogea kwenye gari la matangazo kwa wingi ili kusikiliza kilichokua kikiendelea hapo.

Tulipoongea na baadhi ya watu kuwakaribisha kwenye mkutano walionekana kuwa na shauku kubwa yakuhudhuria, huku wengine wakiuliza kanisa lenu liko sehemu gain hapa Arusha ili tuje?

Maeneo ya Tengeru lilibandikwa tangazo kubwa la mkutano lenye picha ya baba (SNP JOSEPHAT GWAJIMA)

Na panapo majira saa 11:45 jioni majeshi ya Bwana yalianza kurudi uwanjani. Wakati tuko njiani kurudi tulifika eneo moja ambapo jina lake halikuweza kupatikana kwa haraka hapo napo liliwekwa tangazo jingine kubwa barabarani.

Majeshi ya Bwana yakarudi uwanjani panapo majira ya saa moja usiku wakafika wote uwanjani,.

Mnamo saa mbili usiku majeshi ya Bwana yaliongozwa na Rp Bryson kufanya maombi na kuzunguka uwanja huku wakipiga majeshi .

Baada ya maombi majeshi ya Bwana walielekea kambini kwaajili ya kupata chakula cha usiku pamoja na kupumzika


IKAWA JIONI IKAWA ASUBUHI, SIKU YA JUMAPILI

Imetayarishwa na Shepherd Frank John Minja.
Na kuhaririwa na Mp Davie M Abson

Wednesday, September 18, 2013

MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI ARUSHA

Kuanzia tarehe 27.09.2013, jiji la Arusha litakuwa chini ya mamlaka nyingine ya Yesu Kristo. Mchungaji Josephat Gwajima na timu ya watendakazi wa kanisa la Ufufuo na Uzima watamiminika katika viwanja vya Relini. 

Mkutano huwa unatarajiwa kumalizika Tarehe 10.10.2013; Walete wafu, wenye matatizo mbalimbali, na wanaoteswa na shetani nao watafunguliwa kwa nguvu za Yesu Kristo. 

From 27.09.2013, Arusha City will be under the authority of Jesus Christ. Pastor Josephat Gwajima with thousands of co-workers at Ufufuo na Uzima will be in the Relini Grounds, Arusha.

This Crusade will be taken up-to 10.10.2013; bring those who are in sufferings, tormented and living in the satanic snares; they will be saved by the blood of Jesus. 

Don't Miss this Crusade

Our God will restore your lusted years

Sunday, September 15, 2013

KESHO ILIYOCHELEWESHWA

Na Mch. Josephat Gwajima.

Mch Kiongozi Josephat Gwajima
Utangulizi:
Hii ni sehemu ya pili ya somo la hatua iliyocheleweshwa. Ni muhimu kujua kuwa Mungu ni Mungu wa makusudi na hakuna kitu anachofanya pasipo kusudi. Mbele za Mungu; Maisha ya mtu hayaanzi tumboni mwa mama yake bali yanaanza kabla ya mtu kuwa tumboni yaani Mungu huyaona maisha ya mtu kabla ya kuwa tumboni. Kimsingi, Mungu anajua kesho ya mtu kabla haijafika; katika ulimwengu wa roho kusudi la maisha ya mtu laweza kuonekana.

Kwa kuwa shetani ni roho anaweza kuona kesho ya mtu na pia aweza kuichelewesha; leo tunaangalia watu waliowahi kucheleweshwa katika Biblia.

Mchungaji aliyecheleweshwa katika Biblia:
Luka 8:26-39; “…akihubiri katika mji wote” tuangalie pia, habari hiyo katika kitabu cha Marko 5:18-20 “…akaenda kuhubiri katika Dekapoli” maana ya neno Dekapoli, ni “miji kumi” yaani tafsiri ya deka ni kumi, polis ni mji. Kumbe huyu aliyekuwa ameponywa akawa mhubiri katika miji kumi. Na ndio maana baadaye Yesu naye alienda kuhubiri Dekapili kwasababu alishamtanguliza mtu huyo kule, Marko 7:31.  Inawezekana kabisa kuwa Yesu alikuwa anaenda Dekapoli kumtembelea huyo Mchungaji wa huko.

Mambo yote ambayo Mchungaji huyu aliyafanya yalikuwa yamecheleweshwa kwa zaidi ya miaka kumi. Ukisoma katika Marko 5:1-8; tunaona Mchungaji huyu alihamishwa na shetani kutoka sehemu alipokuwa anaishi na kuishi makaburini. Pia tunaona kuwa mtu huyu ambaye alikuwa na huduma ya uchungaji na uwezo wa kuhubiri ndani yake alitupiwa mashetani ili asiweze kumtumikia BWANA. Katika hili tunapata picha hii kuwa kuna uwezekano wa mtu ambaye Mungu alimpangia kuwa ama mchungaji, mfanyabiashara maarufu, mwimbaji au kiongozi; kucheleweshwa na shetani ili asiifikie hatma yake kwa wakati sahihi. Pepo wabaya wanaweza kumchelewesha mtu asifikie kusudi ambalo Mungu amemwekea mtu. Ndio maana ukifuatilia maisha ya watumishi wa Mungu wengi walianza tangu wakiwa na umri mdogo.

Kesho Iliyocheweshwa:
Kama tulivyomuona huyo mhubiri alivyocheleweshwa; vivyohivyo maisha ya watu wengi yamecheleweshwa ili wasiishi maisha ambayo BWANA aliwawekea wayaishi. Mashetani wanaweza kuchelewesha hatma njema ya maisha ya mtu. Unaweza kucheleweshewa utajiri, watoto, ndoa au kazi; na ndio maana Yesu baada ya kumfungua yule aliyekuwa na pepo wachafu hakutaka ajiunge naye bali akamwambia aende akahubiri injili Dekapoli. Kumbe tangu mwanzo Mungu alimwekea kusudi la kuwa mhubiri ndani yake.

Unaweza ukajiuliza; kwanini shetani anaendelea kukufuatilia ingawa umeshaokoka? Jibu ni kuwa, una kitu kikubwa cha Mungu ndani yako; hivyo anachoweza kufanya ni kukuchelewesha usikifikie na kwa njia hii shetani ameteka maisha ya watu wengi.

Mwanamke tajiri aliyecheleweshwa:
Jina Mariamu Magdalene limetajwa mara nyingi katika Biblia, na huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kukutana na Yesu baada ya kukufuka. Mwanamke huyu ndiye aliyekwenda kuwapasha habari mitume kuwa Yesu Kristo amefufuka. Tunafahamu kuwa alikuwa tajiri kwenye kitabu cha Luka 8:1-3 “…waliokuwa wakimhudumia Yesu kwa mali zao” inawezekana mtu, alishapewa neema ya kupata utajiri tangu alipoumbwa; lakini pepo wabaya ambao mtu huyo umetumiwa wanaweza kuchelewesha utajiri huo. Marko 15:40-41, Mariamu Magdalene alipotolewa pepo wabaya akapata utajiri na kwa utajiri huo akamtumikia Mungu.

Marko 16:1-8; Mariamu Magdalene ndiye aliyeendelea kumhudumia Yesu kwa fedha baada ya kutolewa pepo saba. Kumbe inawezekana ulipangiwa uwe tajiri wa kuwezesha kazi ya Mungu au wa kuwasaidia watu lakini shetani amekuchelesha na kukufanya uwe maskini.

Yesu aweza kukuokoa:
Ni kweli kuwa kuna watu wamecheleweshwa kimasomo, kimaendeleo, kiajira au kimahusiano. Na wengine wanaishi kwenye matatizo kwasababu ya kucheleweshewa kesho yao lakini ni muhimu kujua kuwa Yesu Kristo aweza kukuokoa kutoka katika kesho iliyocheleweshwa na kukuweka huru. Kama vile alivyomwokoa Mariamu Magdalene ndivyo atakavyokuokoa nawe. Uwe huru katika Jina la Yesu.

Kwa matukio zaidi na Picha bonyeza hapa: Facebook Page

Wednesday, September 4, 2013

MESSAGE: DELAYED PROGRESS (OR STEPS)


With Senior Pastor Josephat Gwajima | GCTC. Dar es Salaam, Tanzania 

Senior Pastor Josephat Gwajima
PROLOGUE:
By nature, Jehovah is a step by step God, he gives people one step after another. Also, like always, life is lived step by step, day by day; which is why a person's success is not achieved by just picking up a pice of diamond or just by getting lucky, but is by moving step by step heading towards richness.

Genesis 15:13; Here we can see God talking to Abraham telling him that his descendants (Israelites), will be enslaved for four hundred years. But surprisingly, they were enslaved in Egypt for four hundred and thirty years. (Exodus 12:40-41), we get to see here that one's spiritual or physical success can be delayed and other matters not taken action upon or even thought of.

MEANING OF PROGRESS:
So that you can understand the meaning of progress, let me use this example: In the life that we live, it is possible for someone to start with a low income, one that is enough for him alone. But after some time, that person may get another job with a higher income and then later on, get a promotion. He then gets to build his first house, and then the second, and then travel far, and build more houses. Those are steps that God has given people to go through as they continue living. By this example, now we see that PROGRESS is someone's ongoing life that God has put for us on Earth.
It is important to know that God has put in everyone's life, steps or divine purpose that will progress a person to success. Which is why King David said "Direct my footsteps according to your word; let no sin rule over me."  Psalms 119:133; King David knew that God gives one step after another to everyone and it is possible for this progress to be hindered.

POSIBILITY OF BEING DELAYED:
If you read Jeremiah 25:11-12; "... and these nations will serve the king of Babylon seventy years..." , from there we will see that God told the Israelites that the time they will be enslaved for is seventy years but the question is, did they stay enslaved for seventy years? We have the answer in Daniel 9:2, the Bible says that from the readings Daniel did, he discovered that the time for being enslaved was up. After finding out so, he decided to fast and pray. Like so, someone's life can be delayed not to reach their destiny; which is why one can be successful in twenty years, and the other in seventy years. Basically, they are both successful, but one, much later than the other.
Someone's progress can be delayed by someone else, certain behavior, or the devil himself. Which is why even when the Israelites were leaving Israel, they had an option between the short way or the long one. But they were taken through the long route for forty years through the desert to avoid a battle. The life of the Israelites is a shadow for our spiritual life; meaning that you can become successful after a long period of time just because you don't want to fight. Which is why someone may get married but at the age of sixty, or one might build a house but at the age of seventy with very little time left to live in that house just because you have been delayed.

HOW THE DEVIL DELAYS PROGRESS:
There are many reasons as to why someone’s progress can be delayed. Those can be a close relative or someone’s behavior (Eg: laziness, jealousy, sin etc.) Today we are going to see just how the devil can delay someone’s progress. In the book of Daniel 10:1-14; Here we can see that Daniel had decided to fast and pray but without any answer, and only on the 21st day did the angel Gabriel appear to Daniel and said, “Do not be afraid Daniel. Since the first day you set your mind to gain understanding and to humble yourself before God, your words were heard…” If you keep reading, you will discover the angel telling Daniel that his answers were being opposed by the prince of the Persian kingdom.

So there are people that pray to God without knowing that the devil is there somewhere trying to block them from getting that which God has promised them in their time. Proverbs 19:9; God is the one that establishes someone’s steps and without the devil delaying them. Basically, God brought you down to Earth and gave you steps that you were supposed to go through but because of the devil, you find that the life you are living is not according to the steps that God had set for you. When you read Psalm 73:2 “… my feet had almost slipped…” The bible shows that there is a possibility that it is possible for someone to slip in their steps. These are not normal physical footsteps, but someone’s spiritual or physical life heading towards success.

AN EXAMPLE OF SOMEONE IN THE BIBLE THAT HAD BEEN DELAYED BY THE DEVIL:
In the bible there is a servant of the Lord that had been delayed, Mark 5:6-20; This person with an evil spirit inside him had a calling to serve the Lord by preaching the gospel; which is why after being saved, he went on to preach the gospel in Decapolis but he did stay in the graveyard for many years which he could have spent serving the Lord. That is why today you can find many people with the calling to serve the God but the devil gives them thoughts opposite of that and they come to realization in the end that they have wasted so many years being delayed.

This is how the devil can delay someone in their studies, business, success, progress, relationships etc. This can happen when unclean spirits enter someone and block their steps in success, and if that person has no knowledge that it is the devil that is doing so, they will end up blaming and giving up hope completely.

MAKE THE RIGHT CHOICES:
To have control over your steps you have to make a decision to fight in the spiritual realm. Which is why there are some people who are born again and others who are not who have been prophesied for by many servants of God but none have come true until this day; this is because they chose not to fight in the spiritual realm. That is why when Daniel realized that the time for being enslaved were long over,  he decided to fast and pray so to take control over the steps that God had planned.

It is important to know that when God promises you something, it is not set that you will receive it at that time because there is someone on its opposition. Daniel prayed for 21 days without answers and it is possible that he started to blame God for not answering but in fact the problem was with the kings of the skies. All the same, if you do not decide to fight with the kings of the skies and the devil, you can find yourself in life battles without any victory. It is important to use the authority that Jesus Christ had lef us at the cross to destroy the devil that is trying to delay your success in the name of Jesus Christ.

Information Ministry, GCTC. (Translation Ministry)

Monday, September 2, 2013

NI KWELI MUSA AMEKUFA LAKINI TUSIOGOPE

Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.( Yoshua 1:1-2)

Ni huzuni na masikitiko. Hivi ni kweli amefariki? Watu wana majonzi na masikitiko. Rafiki yangu kipenzi aliyehudhuria msiba ananiandikia ujumbe kwa kutumia wasapu. Ananiambia mjukuu wa Musa na mwimbaji wa nyimbo za injili leo hajazimia. Nami namuuliza: “kwani lini alizimia?”. Ananijibu: "Juzi alizimia". Ni kweli kuna huzuni. Watu wanamlilia Musa. Wanakumbuka alivyokuwa shupavu kuongea na Farao ili awape watu wa Mungu ruhusa waende. Wanakumbuka alivyoigawa bahari ya shamu wakavuka. Wanakumbuka alivyowatolea maji kwenye mwamba wakanywa. Ni huzuni na masikitiko kuwa Musa mtenda maajabu amekufa kabla watu hawajarithi nchi waliyoahidiwa. Ni huzuni na masikitiko.

Huenda wanawaza kwa nini Musa aondoke wakati huu. Bado tunamwitaji. Musa kweli amekufa lakini safari ya kwenda Kanaani haijafa. Musa ana upako wa kuwatoa wana Israel utumwani na kuwapitisha jangwani. Anao moyo wa kuwavumilia wanaposhindwa kumwelewa na kuanza kumlaumu. Ni mwepesi kuwalilia watu wenye shingo ngumu ili Mungu awarehemu. Sasa Musa huyu amekufa. Ni kweli amekufa na hakuna alithubutu kumfufua. Amerudi kwao alikotoka. Musa alikuwa shujaa. Shujaa karudi nyumbani kupumzika. Imani ameilinda. Mwendo ameumaliza

Katikati ya Majonzi haya, liko tumaini bado. Kuna mtu anaitwa Yoshua amevaa jezi aingie ulingoni. Asingeweza kuingia uwanjani wakati Musa yupo. Lakini alikuwa akiandaliwa. Mazingira ya mchezo yamebadilika na yanamwitaji mchezaji wa akiba. Alikuwa nje anausoma mchezo wakati Musa yuko ulingoni. Ni kweli bado tuko njiani. Mechi inaendelea. Yoshua kavaa jezi ileile yenye jasho ya Musa. Kocha anajua muda wa kumpumzisha Musa ili Yoshua ainngie. Yoshua yeye ana upako wa kuwavusha watu mto Yordani na kuwaingiza Kanani na kuwamilikisha ahadi yao. Yoshua ni mhubiri kijana. Hasubiri mto ugawanyike kama bahari ya shamu ilivyogawanyika ndo avushe watu. Yeye anawaambia watu wakanyage maji waanze safari mto ukiwa unaendelea na shughuli zake na umefurika mpaka kingo zake. Chini ya uongozi wa Yoshua Mnakanyaga kwanza maji ndo yanasimama. Hayasimami na kuwa chuguu ndo mnavuka. Mnayakanyaga kwanza. Hatari ni kubwa lakini hayo ndo maelekezo ya Yoshua

Yoshua si Musa kama ambavyo Musa si Yoshua. Wote wameitwa lakini wanatumiwa kwa staili tofauti kulingana na namna walivyoitwa. Aliyewaita ni mmoja - Mungu wa mbingu na nchi lakini anawatumia kwa namna ya tofauti. Musa amekufa na ametuacha jangwani - Hatujamiliki ahadi. Mbele tunaiona kanani lakini kuna mto Yordani umefurika. Na hata tukivuka kwa mbali kuna ukuta wa Yeriko. Ni vikwazo vizito na vya kweli kabisa. Tusiogope. Mungu ametuinulia Yoshua wetu atuvushe. Tumtii kama tulivyomtii Musa. Staili yake itakuwa tofauti lakini tumsikilize na kumtii kama tulivyomtii Musa. Ana maelekezo muhimu ya kutuvusha na kutumilikisha. Akisema tuukanyage mto ili tuvuke, tumtii. Tusimuulize mbona Mzee Musa alikuwa anayagawa maji ndo anatuamuru tuvuke? Nimeshawaambia Yoshua sio Musa na tusitegemee kuwa atatumia staili za Musa. Akisema tuzunguke ukuta wa Yeriko mara saba tumsikilize. Tusizunguke mara tano halafu tukasema: "mbona hatuoni nyufa kwenye ukuta. Utaanguka kweli?" Inawezekana tusione dalili za nyufa kwenye ukuta wa Yeriko lakini tukifanya kama alivyosema tukazunguka siku 7 na mara 7 siku ya saba, UKUTA utaanguka maana Mungu amesema kama alivyokuwa na Musa ndivyo atakavyokuwa na Yoshua.

NI KWELI MUSA AMEKUFA LAKINI AMEMWACHA YOSHUA. TUTAMILIKI MALANGO YA ADUI ZETU CHINI YA UONGOZI WA YOSHUA

Sunday, September 1, 2013

UJUMBE: UFALME WA MAJINI

Na Mch. Josephat Gwajima | GCTC; Dar es Salaam, Kawe. 01.09.2013

Mchungaji Kiongozi, Ufufuo na Uzima; Josephat Gwajima
UTANGULIZI:
Kwa kichwa cha somo hili, utakuwa umejiuliza maswali kuwa “namaanisha ufalme wa kwenye maji au namaanisha ufalme wa majini au pepo wachafu” lakini vyovyote vile utakavyotafsiri katika maana hizo mbili utakuwa upo sahihi kwa ujumbe huu.

Ufunuo 2:12-13 “..napajua ukaapo ndipo katika kiti cha enzi cha shetani…” ni muhimu kujua kuwa, huwezi kumshinda adui bila kujua mbinu na silaha zake anazozitumia. Maombi ya wakristo wengi yamejikita katika kujilinda dhidi ya shetani (Defensive Prayer) lakini kama unataka kumshinda shetani unatakiwa uwe na maombi ya kumshambilia (Offensive Prayers) na kuwa huwezi kumshinda adui bila kujua mbinu zake, ndio maana tunajifunza kuhusu ufalme wake.

MAANA YA AKAAPO SHETANI:
Kwa kawaida utawala wa shetani duniani, umeweka himaya yake katika maeneo tofauti tofauti, na ndio maana katika kila mkoa au wilaya kuna mtu au eneo ambalo linaogopewa na watu. Katika maeneo mengi utakuta mtu ambaye ama kwa nguvu zake za rohoni au mwilini amekuwa akiogopwa na watu. Mtu huyo au mahali hapo ndipo panaitwa pale akaapo shetani. Maeneo mengi ya vijijini huwa kunakuwa na mtu anayeogopewa na mara nyingi husababishwa na uchawi wake; mtu huyo ndiye anayeitwa kiti cha enzi cha shetani katika kijiji hiko.

Ili kuweza kuitawala dunia, shetani ameweka tawala zake sehemu tofauti; maeneo hayo sio kuzimu yenyewe bali ni ngome ya shetani katika eneo husika. Kimsingi, hata katika maisha, kazi, masomo au biashara za watu kuna maeneo ambayo shetani anakaa; hapo panaitwa kiti cha enzi cha shetani katika biashara, nyumba au katika mwili.

NENO MAJINI KATIKA BIBLIA:
Mambo ya walawi 17:7, ukiangalia kibiblia neno hili “Jini” kwa lugha ya kingeleza limetajwa kama “goat idols” Kimsingi katika agano la kale kulikuwa na aina nyingi za miungu; na mojawapo alikuwa mungu mbuzi-dume. Na ndio maana katika biblia wakristo hawafananishwi na mbuzi bali kondoo kwasababu mbuzi dume alikuwa moja ya miungu iliyokuwa inaabudiwa kama mashetani. 2Mambo ya Nyakati 11:15, hapa pia wanatajwa aina hiyo ya mashetani waliokuwa wanakaa ndani ya miungu-mbuzi “goat idols” Miungu mbuzi ilikuwa ni mashetani waliokuwa wakiabudiwa na watu katika agano la kale ambao kwasasa ndio walewale wanaofahamika kama majini.

UNDANI KUHUSU MAJINI:
Majini ni mashetani ambao wanafuatana na tamaduni za nchi za kiarabu, lakini pia, majini haya yalikuwa ni mashetani yanayofuatana na maji au mikusanyiko ya maji; kwasababu makao yao makuu yalikuwa majini ukisoma, Ezekieli 29:3-5. Na ndio maana mfalme wa Misri, Farao alikuwa anakwenda kuabudu katika maji, Ukisoma, Ezekieli 32:2-3 inaeleza jinsi Farao alivyotegemea miungu ya katika maji kiasi biblia inamwita joka wa majini.

Kwasababu ya mashetani hao wanaokaa majini, mara nyingi maji katika biblia yamekuwa yakitumika kuonyesha uharibifu, Zaburi 18:16. Ndio maana hata kipindi cha Musa alipokuwa anamfuata Farao ili kuomba ruhusa ya kutoka utumwani, maranyingi, alikuwa akimkuta anatoka au anakwenda majini, Kutoka 7:18; 8:20; Ilikuwa ni desturi ya farao kwenda kuabudu katika mikusanyiko ya maji. Maandiko yameonyesha sana kuhusu mashetani wa baharini, katika Ufunuo 14:31; 20:13, Isaya 27:1, Ayubu 3:8.

Ufunuo 12:1-16; Joka jekundu ni ishara ya shetani. Kama nilivyosema mwanzoni, majini ni mashetani yanayofuatana na desturi za kiarabu, na yanaitwa majini kwasababu yanatokea katika maji. Mashetani haya ndiyo ambayo yalikuwa yakiabudiwa na Mfalme wa Misri, Farao na ndio maana katika maeneo ambayo yametawaliwa sana na waarabu lazima utakuta kuna aina hii ya mashetani. Na mashambulizi mengi ya rohoni huanzia kwa majini hawa.

Hili ni kundi la mashetani, wanaofanya kazi zao ndani ya maji; pia, majini haya yanauwezo wa kukaa nchi kavu na kuishi kama watu, wakaongea na kupanda gari kama watu. Ndio maana matatizo yote ya rohoni katika maeneo ya pwani husababishwa na majini, kuanzia katika tawala za kiserikali mpaka katika nyumba za mtu mmoja mmoja. Asilimia kubwa ya matatizo ya watu yamesababishwa na majini, ambao hutenda kazi kumwakilisha shetani mahali husika. Majini ni aina ya mashetani yanayotumiwa kuvuruga makanisa, kuleta visasi, kufanya watu kuwa wazinzi, kuharibu amani, kuleta kutokuamini (ukiondoa majini kuna baadhi ya dini zinakufa) na magonjwa yote; kazi hizi zote hufanywa na majini.

DALILI ZA UWEPO WA MAJINI KATIKA MAISHA YA WATU:
  • Dalili zifuatazo ni za mtu ambaye ama ana majini au anafuatiliwa na majini:-
  • Unakuwa unaota ndoto upo ndani ya maji; ama unatembea ndani ya maji, unaingia majini au unatembea juu ya maji.
  • kila wakati unajikuta umeona au umeokota pete za dhahabu; mara nyingi majini wanaotaka kukutana kimwili na wanadamu hutegesha mikufu au pete ili kuunganishwa naye.
  • Mara nyingi unapotembea unakuwa unasikia harufu ya udi, ubani au marashi. Si lazima majini hayo yawe ndani yako lakini yanaweza kuwa yanakufuatilia ili kukudhuru.
  • Wakati wa usiku unasikia vitu vimepigwa kwenye bati au darini bila kujua chanzo na mwisho wake.
  • Kudondoka chooni ni dalili nyingine ya mtu anayefuatiliwa na majini.
  • Wewe ni mkristo lakini ukisikia adhana unajisikia kuipenda; na ndio maana watu wengi wakija kuombewa wanalipuka mapepo yanayopiga adhana.
  • Kukonda kupita kiasi.
  • Kupenda kuvaa nguo za nusu uchi.
2 Wathesalonike 2:8, alisema Mtume Paulo alikua amepakwa mafuta na Mungu kutenda mambo makubwa lakini pamoja na hayo shetani aliweza kumzuia kwenda Thesalonike kuifanya kazi ya Bwana. kumbe kupitia majini shetani aweza kutenda kazi ama ndani au nje ya watu ili kufanikisha azma yake ya kutesa maisha ya watu.


USHINDI DHIDI YA MAJINI:
Ili kupashinda na kupaondoa pale akaapo shetani ni lazima kuwashambulia majini ambao ndio wanaotenda kazi katika maisha ya watu. Huwezi kutatua tatizo bila kushughulika na chanzo chake, na kama tulivyoona hapo juu kuwa majini ndio wanaosababisha matatizo ya watu wengi, hivyo ukishambulia majini kwa Jina la Yesu Kristo unajiondoa mwenyewe katika tatizo ambalo limeletwa na shetani katika maisha yako.


Ukiokoka unapokea mamlaka ya kuteketeza kazi za shetani, tumia mamlaka hiyo kuharibu kazi zote za majini katika maisha yako.

For More Information Visit Our Facebook Page