Saturday, September 28, 2013

Ufufuo na Uzima yalitikisa Jiji la Arusha kwa Ishara na Maajabu

Na Mwandishi wetu | 28 Septemba 2013 | Arusha

Ufufuo na Uzima ambaye ni Yesu mwenyewe amelitikisa jiji la Arusha kwa ishara miujiza na maajabu akiwamo kurudishwa toka msukuleni kwa binti mmoja na wengine wengi kufunguliwa toka katika vifungo vya majini. 
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akimfungua binti aliyerudi toka msukuleni dakika chache baada ya maombi.

Haya yote yametokea ndani ya Mkutano Mkubwa wa Injili ulioandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima chini ya uongozi makini wa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima ambaye Mungu amempaka mafuta kuipeleka injili ya Ufufuo wa wafu duniani kote akianzia bara Amerika, Ulaya, Asia na sasa ni zamu ya Afrika ikianzia na jiji la Arusha.

Akiongoza ibada iliyohudhuliwa na zaidi wa watu ishirini elfu (20,000) katika viwanja vya Relini hapa jijini Arusha, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory of Christ Tanzania Church) Josephat Gwajima amerudisha msukule baada ya maombi yaliyojaa nguvu ya Mungu yenye kurudisha watu waliochukuliwa ama kufa katika mazingira yenye utata. 


Binti aliyerudi toka msukuleni akitafakari neno moyoni mwake na kustaajabu ukuu wa Mungu
Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha wakiombewa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima


Ikiwa ni siku ya kwanza tu ya kufundisha, kufungua watu walioonewa, kufufua wafu Mch. Gwajima alifundisha somo liitwalo "Vyanzo vya Matatizo" na mara baada ya hapo maombi yalianza na kufuatiwa na ishara, miujiza na maajabu. Zaidi ya yote viwete wametembea na misukule imerudi toka vifungoni. 

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiishambulia ngome ya mashetani wa Arusha katika mkutano wa maelfu kwa elfu wa wakazi wa jiji hili.
Mkutano huu utaendelea hapa jijini Arusha mpaka tarehe 13 Octoba 2013 na baadaye majeshi ya Ufufuo na Uzima yatang'oa nanga jijini Arusha na kutua Manispaa ya Moshi mkoni Kilimanjaro na kuanza mkutano mwingine tarehe 20 Octoba 2013 katika viwanja vya Mashujaa. 

No comments:

Post a Comment