Friday, October 25, 2013

MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA MASUJAA MJINI MOSHI, NA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA WA KANISA UFUFUO NA UZIMA


MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA MJINI MOSHI.                           
TAREHE:  25/10/2013.                           
SOMO: LAANA ZA FAMILIA 
Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima
Mch.Kiongozi Josephat Gwajima.

Kuna familia zinaandamwa na matatizo mbalimbali, mfano. matatizo ya kutokuolewa,umasikini au matatizo mengine yanayotokana na laana za familia. Mchungaji Kiongozi alihaidi kuvunja matatizo yote ya kifamilia yanayoletwa na familia,na kusema kuwa leo kuna mambo ambayo anataka kuusemea ukweli.
kuna familia ambazo zinakuwa  zipo chini ya laana fulani na hata mtu akipenya anapenya kwa taabu sana.
Sasa tutaangalia siri iliyopo nyuma yake halafu utafunguliwa katika Jina la yesu.

Tukiangalia maandiko 

Mwanzo 9:18-25..
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
 19 Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.
 20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;     
 21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
 23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
 24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
 25 Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

Tukiangalia kitu hiki cha ajabu, Hamu ndiye aliyeona uchi wa babaye lakini anayelaniwa ni mwanaye Kanaani.Hapa tunaanza kujifunza jambo ya kuwa jambo linapotokea kwa wazazi linakwenda kwa watoto,wajukuu na watoto na watoto.

Lakini Kanaani alikuja kuwa na watoto baadae,hebu tuwaone watoto waliozaliwa na Kanaani aliyelaaniwa walikuwa kina nani na maisha yao walikuwaje;

Mwanzo 10:15-19. 
 15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
 16 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
 17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
 18 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
 19 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.

Ndio haohao watoto ambao wana wa Israeli wakati wanatoka katika nchi ya utumwa, Mungu alimwambia Musa waangamizwe njiani wauawe wote,hii inatupa picha ya ajabu ya kwamba wote waliozaliwa na Kanaani walikuwa na laana na ndio Mungu akamwambia Musa ili wauawe.

Tukiangalia tena maandiko matakaifu

Kitabu cha Kutoka 3:7-8. 
 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

Hapa tunaanza kuona kumbe laana zinaweza kutokea katika familia,hivyo inawezekana leo hii una matatizo siyo kwa sababu umetenda dhambi ila ni kwa sababu kuna mambo yalitendwa kwenye familia yenu yankuandama mchana na usiku, hivyo naomba leo unifatilie kwa makini ili tuvunje hizo laana na Baraka yako itakwenda kutokea katika jina la Yesu.

Kitabu cha Kutoka 3:17
“Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali”
Hapa Mungu alikuwa akiongea na wana wa Israeli.Kwa hiyo utaona mojawapo ya alama ya laana ni kunyang’anywa kile kitu ulichokimiliki kwa nguvu zote.

Kitabu cha Mithali 26:2 
“Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.”

Kwa hiyo kumbe maana yake ni  laana yenye sababu inampiga mtu.
Lakini utaona pia kuwa mambo ya imani nayo yanaweza kwenda familia hata familia.2Timoteo 1:3-5. 
 3 Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
 4 Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha;
 5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.

Maelfu ya wakazi wa mjini Moshi waliofika kwenye mkutano wa Mchungaji Kiongozi Jospehat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima., wakiwa wamenyoosha mikono yao kumkabidhi Yesu maisha yao.
                           No comments:

Post a Comment