Friday, October 25, 2013

SHUHUDA ZA WAKAZI WA MJI WA MOSHI WALIOFIKA KATIKA MKUTANO NA WAKAPONYWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA SHETANI


     Matendo makuu ya Mungu aliyoyafanya Arusha, imemfanya leo MIRRIUM mkazi wa Arusha kufika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi kushuhudia Mungu alivyo mponya.Mirium alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kuvimba, na uvimbe tumboni. Alishuhudia kuwa mara baada ya kuhudhuria mkutano huko Arusha uliokuwa katika viwanja vya relini, alipokea uponyaji wake papo hapo. Binti huyu hakuishia hapo aliamua kwenda katika hospitali ya MOI kuhakikisha muujiza Mungu aliomtendea. Huku akiwa na uso wa furaha, alishuhudia mbele ya madhabahu  kuwa mara baada ya kwenda kufanya uchunguzi hospitalini madaktari walithibitisha muujiza wake maana amekuta moyo wake umepona na uko vizuri na uvimbe umetoweka kabisa.

   Hakika sauti ya "njoo kwa jina la Yesu" inarudisha watu kutoka mateka,Isaya 42:22... Huyu anaitwa DORIS ana umri wa miaka 13, alichukuliwa mateka na kuwekwa uvunguni mwa kitanda.  Leo binti huyu kaisikia sauti ya njoo  kaifuatana nakujikuta yuko katika kundi la watu wengi.Yesu ni yuleyule jana na leo na hata milele.

Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akihoji binti aliyepatwa na muujiza wake katika maombi, Yesu alisema Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake, EUGENIA PHILIPO mkazi wa mjin moshi, mwenye umri wa miaka 22, alichukuliwa na mama yake mdogo na kuwekwa katika zizi la ng’ombe. Huko alikuwa akifanya kazi ya kulisha ng’ombe na kukamua maziwa, huku chakula chake kikiwa ni nyama za watu na kunywa damu. 

kama vile haikutosha mama wa binti  huyu pia alikuwa akimtumikisha kwa njia ya kichawi kwenda  kukamua maziwa ya ng’ombe kwa watu. Aliendelea kushuhudia kuwa ng’ombe wa majirani walikuwa hawatoi maziwa kwa sababu ya kuibiwa kichawi na binti huyu. Yule mtenda miujiza ambaye alikirimiwa Jina lipitalo majina yote YESU KRISTO leo kamtoa katika utumwa wa shetani na kumuweka huru.     NEEMA SELEMAN ni binti wa kiislam aliyeamua kumpa yesu maisha yake mara baada ya kufunguliwa kutoka katika vifungo vya shetani vilivyo mfunga kwa muda wa miaka mingi. Binti huyu alikuwa amefungwa na baba yake mdogo, na akawekwa katika kikapu.

Neema anaendelea kuelezea mbele ya madhabahu matatizo yaliyokuwa yakimuandama ambayo chanzo chake anadai kuwa,aliwahi kutamkiwa na baba yake kuwa ndiye aliye mchukua mateka. Ameendelea kusema kuwa ndoa yake imekuwa na migogoro ya kudumu huku akisema kuwa baba aliyemchukua msukule alimnenea hayo kabla ya kuolewa. Umati wa watu leo wamelithibitisha neno ambalo mchungaji kiongozi JOSEPHAT GWAJIMA amekuwa akilisema kuwa YESU NI WA WATU WOTE!!


   Lazima kila goti lipigwe, na kila ulimi ukiri ya kuwa yesu kristo ni bwana. ZAINA RASHID naye leo kaamua kukiri kuwa Yesu ni bwana mara baada ya kurudishwa toka msukuleni. Zaina alichukuliwa  na babu yake na kuwekwa makaburini  Tanga.

.       HAPPY MACHANGE amerudishwa toka msukuleni alikochukuliwa na kupelekwa kwenye mashamba ya mpunga Singida. Alionekana mwenye kuchoka sana huku akiangua kilio kwa nguvu huku akidai kuwa anajuta kwanini aliokoka na kurudi nyuma, jambo lililomsababishia  kuchukuliwa msukule.Happy amesema mara baada ya watu kuita njoo wachawi waliomchukua wameamua kumrudisha wao wenyewe kwa usafiri wa ungo, jambo lilimfanya aonekane mchovu sana.
Wakazi wa mji wa moshi walipoambiwa wajiwekee mikono na kupokea baraka walipokuwa wanaombewa na mchungaji kiongozi Josphat Gwajima.


No comments:

Post a Comment