Sunday, November 10, 2013

IBADA YA JUMAPILI KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA MJINI MOSHI,KILIMANJAROKUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA-MOSHI.   
            
Tarehe;10.11.2013
                
Na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima-Moshi; Gwandu  Mwangasa

SOMO:MUNGU ATAKURUDISHIA NGUVU ZAKO.
Mchungaji Kiongozi Gwandu Mwangasa


Waamuzi 13:2-5.
 2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
 3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
 4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
 5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
Kushoto ni Mchungaji Mwandamizi Maxmillian Machumu, akiwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la ufufuo na Uzima Moshi, Katika Ibada ya Jumapili.

Waamuzi 16:21-28
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
 22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
 23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
 25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.
 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
 

Habari hii ni ndefu sana lakini tumesoma vipande hivi viwili lakini ninaomba nikusimulie ujue jinsi ilivyokuwa; kuna wakati wana wa Israel walifanya makosa mbele za Bwana na hivyo Mungu akawaacha wakawa mateka kwa Wafilisti na wafilisti wakawatawala,sasa wakati wakiwa wametawaliwa na Wafilisti,Mungu akaona anastahili kutafuta njia ya namna ya kuwatoa watu wake katika utumwa wa wafilisti,sasa katika Israel kulikuwa kuna mwanamke ambaye ni mke wa mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Manoa.Mama huyu alikuwa hajapata mtoto kwa muda mrefu sana,mimi nataka nikwambie ndugu yangu usimcheke wala kumdhihaki mtu ambaye hajapata mtoto maana hujui kwenye tumbo lake amebeba nini.Sasa watu wakawa wanamwita Yule mama kuwa tasa,mana kama  ilivyo kawaida ya wanadamu huwa wanamwita mtu kwa tatizo lake hivyo tatizo linakuzwa na kuwa kubwa na baadae linachukua jina lako na badala hilo tatizo ndio linakuwa jina lakeKwa kawaida huwa wanadamu tatizo likionekana kwa Macho huwa linakuzwa na kuwa utambulisho wako,ila mimi nataka nikwambie usiogope wanadamu wamekuitaje Mungu aweza kukuita kwa jina lingine tofauti na wanadamu wanavyokuita hivyo wewe hutakuwa kama wanadamu wanavyokuita bali utakuwa kama Mungu anavyokuita .
 
Kwa hiyo wakati Yule mama pale mtaani wanamwita tasa,Mungu alikuwa na mpango na Yule mama.Mungu akamtuma malaika akamwambie Yule mama kuwa atapata mimba na atazaaa mtoto wa kiume ambaye ni mnadhiri wa bwana hivyo asinywe kileo chochote wala asile chochote kilicho najisi na mtoto atakayezaliwa wembe usipite kichwani mwake.Baadae Yule mtoto akazaliwa na akakuwa akiwa hajawahi kunyolewa nywele,Biblia inasema kijana Yule aliua samba,habari hii ni ndefu sana lakini hapa namuongelea Samson.Samson baadae akamuoa Delila ambaye ndiye huyu mwanamke aliyemsaliti Samson.
Nataka nikwambie maisha waliyoishi wana wa Israel ni sura ya kanisa ya leo lakini nina habari njema leo ya kwamba “nywele” za kanisa zimeanza kuota tena maana kanisa lilinyolewa nywele likaondolewa nguvu lakini sasa nywele zimeanza kuota tena.

No comments:

Post a Comment