Sunday, November 10, 2013

IBADA YA JUMAPILI NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA KUTOKA KAWE,DSM TAREHE 10.11.2013

BAADA YA MCHUNGAJI KIONGOZI, JOSEPHAT GWAJIMA,ALIYEKUWA AMEONGOZANA NA MAELFU YA WATENDA KAZI WALIOKUWA KATIKA MIKOA YA ARUSHA NA MOSHI HATIMAYE AREJEA KATIKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA KAWE, DSM.
Maelfu ya watu wa Mungu waliokusanyika katika viwanja vya Ufufuo na Uzima, kawe, wakifurahia na kumsifu Mungu kwa Kumtumia vyema  Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima katika mikoa ya Arusha na Moshi na kuikomboa mikoa hiyo Kwa jina la Yesu.Nyuso zilizojaa furaha na kumtukuza Mungu kwa kuwa ametenda mambo Makuu, kupitia kwa Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima.

Waimbaji  wakiwa na nyuso za furaha ambayo ni kubwa sana kiasi wakawa wameshindwa kuielezea baada ya kummpokea Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima.


SOMO: KUSUDI LAKO LA MILELE
Na Mch.Kiongozi, Josephat GwajimaKila mtu alie hai Mungu amepanda ndani yake (moyoni mwake) ambalo ni kusudi lake la milele.
Waefeso 3:11
“…Kwa kadri la kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu…” Inatufundisha hapa kwamba kila mtu alie hai ana kusudi la milele limeandikishwa ndani ya moyo (maelekezo yako ndani ya moyo yameandikishwa ili utakapo kuwa mkubwa, ndio yanatengeneza uwewe na mambo kadha wa kadha), hatma ya maisha yako inauhusiano mkubwa sana na moyo wako.

Nini maana ya moyo?
Kazi ya moyo ni kupeleka minerals (madini), ndani ya mwili kupump (kusukuma) oksijeni, mwili mzima na kusukuma uchafu nje ya mwili. Mara moyo wa mtu utakapo acha kufanya kazi mtu anakufa hapo hapo, sababu moyo ndiyo centre inayofanya mtu aishi.
Kuna utu wa ndani ya mtu ambao ni roho, na nje ya mtu ambao ni mwili, na mtu wa ndani (ambaye ni roho) naye ana moyo pia, ndio maana Mungu ni Roho lakini ana moyo Mwanzo 8:21 “Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni sitailaani nchi tena”.

Mwanzo 17:17 “Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni…” Mwanzo 18:12 “Sara Moyo wake ukacheka Mwanzo 24:45.
Mungu anapotaka kupanda kusudi la maisha ndani ya mtu hupanda moyoni, ndio maana moyo wa mtu ukiwa mzito mambo yake hayawezi kufanikiwa, atakuwa anaona uzito katika kila jambo analolifanya.
Mwanzo 27:41, “…Esau akasema moyoni mwake...” Kutoka 4:14 “… naye atakapokuona atafurahi moyoni mwake…”
Kumbukumbu la torati 2:30 “..akamtia ukaidi moyoni mwake..” tunajifunza unapotiwa ukaidi moyoni mwako, ukaidi huo unajidhihilisha mwilini, unakuta mtu hupendi kuwa mkaidi, lakini ndio unakuwa ushatiwa ukaidi. Ndio maana mtu utamsikia anasema nakupenda kutoka moyoni mwangu, hapo cha kujiuliza je huo moyo anaouzungumzia ni wa kwake, maana watu hutiwa mioyo tofauti na kusudi la Bwana.
Mithali 4:23 “..linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima..” Biblia ya kiingereza inasema “Keep thy heart with all diligence; for out of it are the issues of life” Tunajifunza hapa mambo yote za maisha ya mtu huanzia moyoni, matatizo yanayowakumba watu au mafanikio ya mtu huanzia moyoni mwa mtu, “ISSUES OF LIFE”

Kutoka 35:35 “…Amewajaza watu hao akili za moyoni ili atumike katika kazi ya kila aina...”  
kutoka 35:34 “…nimemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha..”
Siku hii ya leo, ninaomba Mungu apande jambo moyoni mwako, ili kutimiza kusudi la nchi yetu Tanzania. “Utamkuta mtu mwingine anatenda jambo kwa ufanisi ulio wa juu mpaka watu wanashangaa wanamuuliza hivi ulisoma wapi, kumbe hata hajasoma lakini ndio kusudi la moyo wake.

Mungu amepanda kitu ndani ya moyo wako ili kupitia kile uwe na mafanikio, shule haiwezi kukuletea mafanikio, kile kilichopandwa ndani ya moyo wa mtu ndio mafanikio yake. Ufufuo na Uzima imepandwa ndani ya moyo wa Yesu, ndio maana hatuhitaji mtu atuelekeze njia ya namna ya kwenenda.

Kumbukumbu 4:9 “..mambo uliyoyaona yakaondoka moyoni mwako…”, Kumbukumbu 8:2 “…kuyajua yaliyo moyoni mwako…” Hata Mungu kuwapitisha wana wa Israel jangwani ni ili Mungu ajue yaliyo mioyoni mwao, kama watashika amri zake ama sivyo. 


“Issues za maisha zipo mioyoni mwa mtu” Nataka nianze biashara, nataka nisome shule, nataka niache kazi vyote hivyo huanzia moyoni. Moyoni mwangu nikimtumikia Mungu najisikia vizuri, nikimuimbia Mungu njisikia vizuri, nikimtolea Bwana moyoni mwangu najisikia vizuri sana, ndio maana mtu anasema nasema kutoka moyoni Mwangu. Na ukisimamia kusudi hilo utafika pale Mungu alipokukusudia.

Shetani ana tabia ya kuiba mioyo ya watu yenye kusudi la Mungu, anaandikia maelekezo yake yeye ambayo ni tofauti na maelekezo ya Mungu, anakutole kusudi la Mungu anaandika maelekezo yake ili uelekee upotevuni, utasikia najisikia nikaibe kabisa, najisikia niwe mwana mziki, najisikia nivute bangi, napenda ukahaba, kumbe ndio maelekezo yaliyonakiriwa na shetani ndani ya moyo wako.

Unakuta mtu alivyokuwa mtoto mdogo, alikuwa anampenda Mungu, anasema nataka nimtumikie Mungu, niwe mchungaji, niwe mwimbaji, lakini mtu huyo akishakuwa mtu mzima anakuwa tofauti kabisa “ukiona upo hivyo ujue umebadilishiwa moyo”.

Unakuta mtu ameokoka anaolewa na mganga wa kienyeji, mnamuuliza mnamwambia unawaza nini wewe anakwambia Mchungaji nampenda toka moyoni mwangu, nampenda huyu kaka toka moyoni, ukiangalia kaka mwenyewe ni mvuta bangi, hata haeleweki. Kumbe moyo wako uliibiwa na shetani na huyo kaka mvuta bangi akaandikishwa ndani ya moyo wako, bila wewe kujua.

Mtu umeokoka lakini unakuta unampenda binti/kaka wa kiislamu, kumbe umebadilishiwa moyo, wamenakiri kwenye moyo wako kuwa utaolewa ana kuoa muislam. Leo tunarudisha mioyo yote uliyobadilishiwa, lazima kusudi la Bwana litimie, kusudi la Bwana ulilowekewa ndani ya moyo wako tunalirudisha leo kwa jina la Yesu. “Daudi alisema eeh moyo wangu na vyote vilivyo ndani yangu mche Bwana”.

Shetani anajua issues zako zote za maisha yako zinatokea moyoni, kiu yako ya kuimba, kuhudhulia ibadani, kutoa fungu la kumi, kumtumikia Bwana vyote huanzia moyoni. Shetani ili abadilishe kusudi lako anaiba moyo, anabadilisha kusudi lililonakiriwa na Mungu moyoni mwako, anaweka maelekezo yake, unajikuta uliyokuwa unatenda hutendi tena, unaingiwa na kiu ya kutenda mambo mengine ambayo hujawahi hata kuyawaza. Lakini wewe ukikaa unaona upo sahihi sababu unachokifanya kinatoka moyoni, kumbe umebadilishiwa moyo ili uelekee upotevuni.

Kuna watu huwa wanajuta baada ya kutenda jambo, usiangalie kwamba hili jmbo linatoka moyoni mwangu, cha kufahamu ujue huo moyo ni wa kwako, unayoyatenda ni kusudi la Bwana tangu awali? Huu ni wakati wa kukana maelekezo ya moyoni mwako kama sio kusudi la Mungu. Shetani amepanda jambo ndani ya moyo wako umeanza kulitumikia, kumbe ni kusudi lililopandwa na shetani.

Shetani akitaka kukuandikia maelekezo yake, huwa lazima usumbufu utokee, ulikuwa unajiweza vizuri kifedha, ghafla unakosa hela ya kula, hata hela ya kwenda kanisani huna, kazi unafukuzwa kumbe ni shetani anakuandaa kukuchomoa kwenye lile kusudi la Mungu, ukishaona umechoka hueleweki shetani anakuambia hilo sio kusudi lako, anakubadilishia maelekezo yaliyondani mwako “mara unaalikwa kwenye semina ya “empowerment”, kumbe shetani ndio anakuwa anakutengeneza kwenye kusudi lake.

Leo ninamlazimisha shetani na watenda kazi wake wote kurudisha mioyo yenu ya asili irudi kwenu, na moyo wako unarudi kwa jina la Yesu. Unarudi kwenye kusudi lako la milele.

Namna ya kuomba
Ngo’a maelekezo ya kishetani yaliyopandwa ndani ya moyo wako ili yakuongoze kwenda mbali na kusudi lako la milele, nayaondoa maelekezo hayo kwa jina la Yesu. Ninakataa maelekezo yaliyowekwa ndani ya moyo wangu kugeuza kusudi la Mungu ndani yangu, kama niliandikiwa kuwa muombaji narudisha kusudi hilo kwangu kwa jina la Yesu, ninakataa kiu ya miziki ya kizazi kipya ndani yangu, kiu ya uzinzi, kiu zote za kishetani kunipindisha na kusudi langu la milele nakataa kwa jina la Yesu.
Leo namng’ang’aniza shetani na malaika zake na majini yake na vibwengo vyake warudishe moyo wako kwa jina la Yesu. Maelekezo ya kishetani yalioandikishwa ndani ya moyo wangu ili kunipeleka mbali na Mungu nayakataa kwa Jina la Yesu, maelekezo yaliyonipeleka mbali na baraka zangu naukataa moyo wenye maelekezo hayo kwa jina la Yesu, anza kudai moyo wako, moyo wa kumcha Bwana, moyo wa ubunifu, moyo wa mafanikio, moyo wa safari nautaka moyo wangu kwa jina la Yesu.

Moyo wa kiburi mlioniwekea naukataa kwa jina la Yesu, moyo wa mauti mlioniwekea naukataa kwa jina la yesu, nautaka moyo wangu kwa jina la Yesu. Nataka moyo wangu, moyo wa ushindi, moyo wa kushika fedha, moyo wenye msimamo, moyo unaompenda Yesu, naurudisha moyo wangu katika jina la Yesu Kristo.

No comments:

Post a Comment