Saturday, November 2, 2013

MAAJABU MAKUBWA YATOKEA BAADA MCHAWI KUKAMATWA LIVE, NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA MJINI MOSHI.

Ilikuwa ni siku ya Tarehe 27,October 2013 katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi, siku ya mwisho ya mkutano mkubwa wa Injili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, Kulikuwa na nguvu nyingi sana za Mungu na palikuwa  na maajabu na uponyaji wa hali ya juu. Kama ilivyokuwa desturi ya shetani kujishtukia kuingia sehemu asiyotakiwa na kujikuta akiambulia kichapo kikali kwa jina la Yesu.

Wakati wa kufunga mkutano mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alikuwa akiwaaga na kuwaomba makutano makubwa uwanjani hapo kwa kuwaomba akisema, "Nawaombeni watu wa Mungu muda wetu kuwepo uwanjani hapa umeisha, turejee majumbani kwetu, ili tutii amri na taratibu za serikali" Lakini ghafla pakatokea hali ya taharuki kupita kiasi na watu wote walisikika wakipiga kelele kubwa sana wakisema...Mchawi!!,,,Mchawi!! kumbe kuna mwanamke mmoja katika kundi lile kubwa alikuwa anajaribu kufanya uchawi lakini akanaswa na nguvu za Mungu.

Alishuhudiwa akitaka kumvamia Mama mmoja na mwanae kwa njia za kujigeuza kuwa jitu kubwa jeusi, hii ni kutokana na taarifa za aliyevamiwa(pichani chini amevaalia gauni jekundu akilalamika na kujitetea yeye na mwanae)
i
Gaudensia akijitetea.
  Angela Msafiri (Mwenye Blausi yenye mistari ya pundamilia)  akidaiwa  kufanya matendo ya kichawi mbele ya umati  wa watu waliokuwa wamehudhuri mkutano katika viwanja vya mashujaa.Mwana mama huyu  alishutumiwa kuwa alionekena kutaka kuiba mtoto wa mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Gaudensia.Pichani ni dada mchawi aliyejitambulisa kwa jina la Angela aliyenaswa na nguvu za Mungu, akijaribu kufanya uchawi na watu wakimmpisha kwa hofu.


Hatimaye Mchungaji Kiongozi, akaamuru dada huyu apandishwe madhabahuni na punde baada ya kupandishwa madhabahuni, ukafika wakati wake wa kuanza kujitetea dhidi ya nguvu za Mungu alionekana akigala gala chini kwa uchungu.
Alikuwa akijitahidi sana kujitetea lakini aliambulia patupu aliishia kushindwa kwa Jina la YesuBaada ya kupandishwa madhabahuni Angela alihojiwa na  Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima (kulia) akiwa na Wachungaji waandamini RP Mwangasa (kushoto) na Machumu (katikati)
Angela alihojiwa na alikuwa akikataa kabisa kwamba yeye ni mchawi. Baada ya kukataa, ghafla kitu cha maajabu kikaanza kutokea, madhabahuni, Juu ya madhabahu palikuwa na kundi la akina dada wakitoa shuhuda zao ambao waliokuwa wamerudishwa kutoka msukuleni, wengine walikuwa wameponywa magonjwa yao, wengine walikuwa wametoka punde tu kuwekwa huru toka katika vifungo vya kumtumikia shetani yaani walikuwa mawakala kabisa wa shetani.

Kina dada hao baada ya kutoka kuombewa na kurudishwa walikuwa na macho ya rohoni kwa lugha nyingine walikuwa na uwezo wa kuuona kabisa ulimwengu wa roho... ulimwengu wa asili ambao umegawanyika katika ulimwengu wa roho wa nuru (MUNGU) na ulimwengu wa roho wa giza (wa shetani), hatimaye wakawa na uweza wa kuona hali ya kichawi aliyokuwa nayo dada huyu Angela ambaye alikamatwa uchawi ila yeye akawa anakana.
Dada hapa juu aliyejitambulisha kwa jina la Sarah aliyekuwa amerudishwa kutoka msukuleni alikasirika baada ya Angela kuukana uchawi wake,akanyanyuka kwa ghadhabu... akimshutumu kwa uchungu na kwa ghadhabu kuwa dada huyu (Angela) kuwa ni mchawi, Pichani anaonekana akimuhakikishia kwa asilimia mia moja Mchungaji Mwandamizi (RP) Mwangasa kuwa huyo dada aliyemshika ni mchawi na amemuona alikuwa akijaribu kufanya matendo ya kishirikina lakini nguvu za Mungu zilizokuwepo zilimshinda akashtukia amekamatwa.

Waliendelea kuongezeka kwa idadi ya waliokuwa wanamshutumu kuwa yeye ni mchawi, pichani anaoneka dada mwingine aitwaye Asha Mohamed ambaye alikuwa ameokolewa siku hiyo hiyo kutoka katika utumishi wa shetani, na yeye pia alikuwa akimshutumu kwa uchungu kuwa ni mchawi.

Pichani juu, Asha Mohamed akimnyooshea kidole na akiendelea kumuhakikishia Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima,kuwa dada huyu Angela ni mchawi na hawezi kukana kuwa sio mchawi, na aliendelea kulia kwa uchungu akisikika akisema " kumbe ndiyo wabaya wangu!!, kumbe ndio wabaya wangu!! kumbe ndio waliokuwa wananitesa!! kumbe ndio walioniharibia maisha yangu",Asha alilia kwa uchungu mkubwa sana akionesha kuwa ameteswa na wachawi kwa kipindi kirefu.
Mama huyu hapa juu aitwaye Gaudensia(aliyepiga magoti mwenye blausi nyekundu) ambaye ndio tunamuona juu kabisa kule kwenye picha ya kwanza aliyezungushiwa dura jeusi ambaye ndiye alikuwa kwenye kundi kubwa la watu akijitetea, anakiri kwa uchugu kuwa aliona jitu kubwa sana jeusi likimkamata yeye na mtoto wake na yeye akajiskia kama anaishiwa pumzi lakini akawa anajitetea kwa kupiga makelele na kuliitia jina la Yesu,kwa tafsiri hapa Gaudensia anasema wakati sisi tunaona ni msichana aitwaaye Angela alikuwa akimkamata, kumbe alikuwa amejibadilisha kwa njia za kishirikina na kuwa jitu kubwa.
Walizidi kunyanyuka wengi zaidi kumshutumu walioweza kumuona kuwa ni mchawi, wakiwa na ghadhabu na wakitaka kumuadhibu kwa adhabu za mwilini.
Hatimaye Busara za Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima na Wachungaji Waandamizi (RP) Mwangasa (Kushoto) na Maximillian Machumu (Kulia) wakaona wamuokoe na kumsogeza pembeni kidogo na wakaanza kumuhoji tena.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima aliamua kutumia mamlaka aliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristo
na akaanza kumuhoji tena kwa mara ya pili tena akimuamuru Angela aseme ukweli huku akimuuliza,"iweje kundi loote hili la watu wakushutumu wewe tu kuwa ni mchawi kama hakuna ukweli wowote?"lakini angela akawa mkimya kwa muda kidogo


Mmoja kati ya wanawake ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kumgundua Angela kuwa ni mchawi tena kwa haraka ni Dada huyu aitwaye Asha Mohamed mwenye umri wa miaka 19, aliyekiri kuwa amekuwa mjumbe wa shetani kwa kufanyishwa mambo mazito na ya kutisha tangu akiwa na umri wa miaka 8.

 Asha ameweza kueleza mambo aliyoyatenda japo ilikuwa ni ngumu sana kuongea kutokan na ukweli kwamba alikuwa anasikia uchungu sana kwa kuwa alijiona kuwa mambo hayo yote hakuna wa kumsamehe makosa yake na watu wange mtenga.Lakini Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima alimshauri kuwa Mungu anasamehe kila dhambi hata iwe na ukubwa kiasi gani, cha msingi ni ukiri kuwa umekosa ujinyenyekeshe mbele zake na usiyarudie tena.


Hatimaye Asha akaelewa na akaanza kueleza, kuwa wakati anasoma darasa la nane nchini Kenya, ulikuwa usiku wa manane walimjia kundi la watu wengi wakamzunguka alikokuwa amelala na kumwambia unahitajika kijijini kwenu. Kulipokucha mchana wa saa sita, walikuja wasichana 3, wakiwa uchi walimfunika machoni na gafla alijikuta yuko kijijini kwao katikati ya kundi la wachawi wa kijijini.
Baada ya kuchukuliwa, alianza kufunzwa jinsi ya kuroga, na mwalimu wake alimtaja kwa jina la Hamis. Asha liendelea kupewa kazi na majukumu  kama kubadilishwa maumbile na kuwa mwanaume nakuanza kuwaingiia wanawake usiku jambo lililokuwa likisababisha wanawake kuvunja ndoa zao. Na wakati mwingine alikuwa akiwaingilia wanawake kwa kugeuzwa maumbile alikuwa nasababisha saratani na kupooza. Jambo la kusikitisha sana Asha amekuwa mateka kwa muda wa miaka 11 huku chakula chake kikiwa ni kunywa maji ya chooni

Matendo haya yaliyotokea katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi yalishangaza kweli kweli,  maajabu na miujiza yalimfanya kila mmoja wetu tuliokuwa katika uwanja huu kuungana na Baba yetu Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, kukaa kwa muda kuyatafakari matendo makuu ya Mungu kwa tabasamu huku roho mtakatifu akiendlea kutoa uponyaji na kutenda kazi ya kuwamalizia mawakala wote wa shetani.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajiam akiwa na Binti Aisha Mohamed, hapa Aisha alikuwa katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Moshi akiwa anakiri mbele ya Maefu ya watu walifika kanisani hapo siku ya Ibada ya Jumatatu jioni, kuwa alikuwa akimtumikia shetani lakini kwa sasa amempokea Yesu Kristo na anamtumikia Bwana Mungu wetu aliyezifanya mbingu na nchi.
Pichani ni Muimbaji wa kimataifa Flora Mbasha wakiwa na Binti Asha mohamed (Kulia) ambaye alimkiri kuwa Yesu Kristo ni Mungu na kwa sasa amempokea Yesu Kristo  na ameokoka.
Hapa wakiwa katika Kanisa la Ufufuo na Uzima mjini Moshi.

"Na ndio maana kama kuna wakuchukia Duniani.... ambaye anatakiwa abezwe na watu wote.... ni mchawi ambaye ndiye anaye "m-host"  shetani - -Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima

No comments:

Post a Comment