Thursday, November 28, 2013

MAAJABU NA MATENDO MAKUU YA MUNGU KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI KUTOKA TANGA, NA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwasili katika viwanja vya Tangamano, ikiwa ni siku ya Tatu ya mkutano mkubwa na wa kihistoria kufanyika katika Jiji la Tanga, Pichani ameongongozana na moja ya watenda kazi wa Ufufuo na Uzima, aliyekuwa sheihk na mkuu wa chuo cha uganga kilichopo mbagala,jijini Dar es Salaam, lakini alishaokoka na kummpokea Yesu Kristo takriban miaka zaidi ya minne imepita na sasa anamtumikia Mungu kwa jinsi ya ajabu.

Mchungaji Josephat Gwajima (Kulia) akiwa madhabahuni uwanjani Tangamano na Mchungaji Kiongozi Dr. Issa Zacharia Godson wa Tawi la Ufufuo na Uzima la mjini Morogoro,(kwanza kushoto) akifuatiwa na Mchungaji Mwandamizi wa Ufufuo na Uzima Bryson Lema na Shepherd Oumary.

Mchungaji Mwandamizi Mkuu Grace Gwajima, akiwa na Flora na Emmanuel Mbasha.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kutoka Morogoro Dr. Issa Zacharia Godson akimkaribisha Mchungaji Kiongozi Mkuu Josephat M. Gwajima.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima,akiwa anawahubiria maelfu ya wakazi wa Tanga.

Mchungaji Gwajima akiwa anamtambulisha Oumary kwa maelfu ya wakazi wa Tanga, ambapo hapa Tanga ni mahala alipozaliwa na kulelewa.


Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea na kuwafungua kwa Jina la Yesu maelfu ya watu wa Tanga waliofika uwanjani.Maombezi yanaendelea
Watu wengi sana walifunguliwa na Nguvu za Mungu, na kwa haraka haraka unaweza kushuhudia ni jinsi gani watu wengi walivyokuwa katika vifungo vya shetani, lakini saa ya ukombozi imewafikia na Mungu ameileta ufufuo na uzima Jijini Tanga na mchungaji Josephat Gwajima anendelea kutumika kwa kazi ya Mungu


Maelfu ya wakazi wakiwa wamenyoosha, mikono kupokea uponyaji.

Mchungaji Mwandamizi Mkuu Grace Gwajima akiwa anaombea na kuwafungua watoto ambao walikuwa katika vifungo vya sheatani.Mvua ilianza kunyesha lakini watu bado walikuwa hawana mpango wa kuanza kuondoka uwanjani hapo,ni imani ya hali ya juu sana imeoneshwa na wakazi wa Jiji la Tanga.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anawapa baraka za mwisho maelfu ya wakazi wa Tanga huku mvua ikiwa inanyesha uwanjani hapo, lakini watu waliendelea kumuomba andelee pamoja na mvua kuwepo.. 

.   

No comments:

Post a Comment