Saturday, November 30, 2013

MAELFU YA WATU WALIOKUWA WAMECHUKULIWA NYOTA ZAO, WARUDISHIWA NYOTA ZAO KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA NA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ (T) Church maarufu kama kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwasili madhabahuni katika uwanja wa Tangamano ikiwa ni siku ya Sita ya Mkutano mkubwa wa Injili na wa Kihistoria kufanyika Jijini Tanga.

Askofu Swai wa Kanisa la TAG Mwanza, akiwa amekuja Tanga kushuhudia na  kumsindikiza Mchungaji Josephat Gwajima, Askofu Swai ndiye baba wa kiroho wa Mchungaji Jospehat Gwajima ambaye ndiye alimlea na kumkuza katika misingi ya Kiroho.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na Mchungaji Swai na Mchungaji Mwandamizi mkuu Grace Gwajima (kwanza kulia) na wachungaji waandamizi RP. Bryson Lema (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na RP. Eng. Yekonia Bihagaze.


 

Mwimbaji wa kimataifa John Lisu akiwa anamsifu Mungu kwa nyimbo na live band....ilikuwa ni Baraka sana..Add caption


Ilikuwa ni vigumu kwa Mchungaji Gwajima kuacha kwenda kumpongeza mpiga saxaphone wa bendi ta John Lisu, maana alikuwa akilipiga kwa umahiri wa hali ya juu kiasi kwamba Mkutano mzima uliingia kwenye uwepo kwa kumsifu Mungu hali ya juu sana.

Ilikuwa ni hali ya Baraka sana wakati John Lisu akimsifu Mungu.Mchungaji Mwandamizi Mkuu Grace Gwajima (Kushoto) akiwa na Emmanuel na Flora Mbasha.


Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wakimuimbia Bwana, kwa Wimbo mzuri uitwao, "Nipe nguvu ya Kushinda" Uwanja mzima ulibarikiwa na wimbo huu.


Mchungaji Mwandamizi RP. Eng. Yekonia Bihagaze akimkaribisha Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anawahubiria maelfu ya wakazi wa Tanga waliofika uwanjani Tangamano.Maelfu kwa Maelfu ya wakazi wa Tanga wakiwa katika kumsikiliza Mchungaji Josephat Gwajima kwa utulivu wa Hali ya Juu.

Mahubiri yakiwa yamekolea...Maelfu ya waliofika uwanjani Tangamano wakiwa wanapokea uponyaji na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya shetani.


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Mch.Josephat Gwajima akiendlea kuwafungua maelfu...
Mchungaji Gwajima akiwa anawaombea watu, pichani tunaona pia Baba yake wa kiroho akimsindikiza..

Mchungaji Gwajima akiendelea kuachia moto kutoka Mbinguni na kuteketeza uharibifu wote ambao shetani na malaika zake wamewatandea watu...waliokuwa wamefika katika uwanja wa Tangamano.


Mchungaji J.Gwajima akifanya maombi ya kushindana ya vita... Imeandika, "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho"

Ni maombi makuu ya kumlazimisha shetani na malaika zake wachukue nafasi zao kuzimu na kuwaachia watu wa Mungu na kuwaweka huru kabisa, Dhidi ya Laan, balaa, mikosi, kulogwa, utasa, kuchanganyikiwa na matambiko mabaya ya ukoo..amayo yanaletwa na shetani.Mchungaji Gwajima akiwa amefungua maelfu ya watu na akiwa anawaandikia ushindi..
Mchungaji Kiongozi Mkuu Josephat Gwajima akiwa na Mchungaji Kiongzi Frank Andrea wa Tawi la Ufufuo na Uzima lililoko Jiji Arusha..wakiwaombea watu..


Ulikuwa na Muda ambao palikuwa na nguvu za Mungu nyingi sana uwanjani Tangamano...


Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea Baraka za Mwisho wakazi wa Tanga waliokuwa wamfurika uwanjani Tangamano.


Mchungaji Kiongozi Gwandu Mwangasa wa Tawi la ufufuo na uzima Mjini Moshi,akiwa anasalimiana na Askofu Swai

Mchungaji Kiongozi Frank Andrea (Kushoto) wa Tawi la Ufufuo naUzima Arusha,  akisalimiana na Askofu Swai

Mchungaji Kiongozi Mkuu Josephat Gwajima, akiwatambulisha Wachungaji viongozi a Moshi na Arusha, SNP Mwangasa na SNP Frank

Mchungaji Kiongozi Mkuu Jospehat Gwajima, akiwa anafurahia jambo na wachungaji viongzoi wa Moshi na Arusha...Mchungaji Gwajima akifurahi na kuimba wakati John Lisu akiwa anaimba katika kufunga siku ya sita ya Mkutano


Mchungaji Josephat Gwajima na Mchugaji Mwangasa.

Mwimbaji John Lisu alikonga nyoyo kweliweli

Mchungaji Josephat Gwajima na Mchungaji Gwandu Mwangasa wakiwaaga maelfu ya wakazi wa Tanga.

Ilikuwa ni siku ya Sita ambayo ilikuwa na furaha sana, na hapa mchungaji Josophat Gwajima,,akiwa na wachungaji wake...SNP Mwangasa (Kushoto) kutoka kulia ni Eng. Yekonia Bihagaze (kulia) akifuatiwa na RP BRyson Lema.

No comments:

Post a Comment