Thursday, November 7, 2013

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA AKABIDHIWA TUZO NA MAASKOFU

Umoja wa wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Kilimanjaro (PPK)wamempa tuzo ya heshima kanisa la Ufufuo na Uzima kwa mafanikio yao katika kumtangaza Kristo. Tuzo hiyo imekabidhiwa tarehe 30 mwezi uliopita ikiwa ni siku tatu toka kumalizika kwa mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na mchungaji Gwajima chini ya kanisa la Ufufuo na Uzima katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi.

Tuzo hiyo ya heshima yenye picha ya mlima Kilimanjaro ilitolewa na mchungaji kiongozi wa umoja huo Samweli Yohana katika ukumbi wa hosteli za Umoja kanisa la Kilutheri Moshi mjini. Mkutano wa wiki moja uliofanyika viwanja vya mashujaa mjini moshi ulivunja rekudi ya idadi ya wahudhuriaji na watu kutoka dini tofauti.

Picha zifuatazo ni matukio ya kukabidhiwa Tuzo hiyo


No comments:

Post a Comment