Wednesday, November 27, 2013

SHUHUDIA WACHAWI WALIODONDOKA "KAMA MAEMBE MTINI" KWENYE MKUTANO WA INJILI NA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA JIJINI TANGA


Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akiwasili katika uwanja wa Tangamano.


Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima, akipanda madhabahuni katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, akiwa amesindikizana na Mchungaji Mwandamizi, RP Bryson Lema wakifika madhabahuni.

Mchungaji Kiongozi Jospehat Gwajima akifurahia jambo kwa Tabasamu zito.


Mchungaji Kiongozi, Jospehat Gwajima kwa furaha sana wakisalimiana na Mchungaji Kiongozi wa Tawi la Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko Mjini Moshi, Mchungaji Gwandu Mwangasa, ambaye alifika akitokea Moshi kumsindikiza na kumuunga mkono Mchungaji wake mkuu katika Crusade hii Jijini Tanga.Mchungaji Mwandamizi Mkuu wa Kanisa la Glory of Christ (T) ufufuo na Uzima (Kushoto) Grace Gwajima, akisalimiana na Mchungaji Kiongozi wa Tawi la Glory of Christ (T) Church la Mjini Moshi, Mch.Gwandu Mwangasa.

Mchungaji Mwangasa akisalimiana na Mwimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Flora MbashaFlora na Emmanuel Mbasha wakiwa katika mkutano wa Injili katika uwanja wa Tangamano na Mchugaji Kiongozi Josephat Gwajima.

Emmanuel na Flora mbasha wakimsifu Mungu pamoja na maelfu ya watu wa Jijini Tanga waliofika uwanja wa Tangamano.
Mchungaji Kiongozi Mkuu Josephat Gwajima akiwa amekaribishwa na Mchungaji Mwangasa.

Mchungaj Josephat Gwajima akiwahubiria maelfu ya wakazi wa Tanga.


Maelfu ya wakazi kutoka kila pande ya Jiji la Tanga wakiwa wanamfuatilia Mchungaji Josephat Gwajima.Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea maelfu ya wakazi wa Tanga.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea kwa Jina la Yesu, watu wa Tanga na kusambaratisha Kila nguvu za giza, majini na mashetani ambayo yanawatesa watu kwa kuwaletea balaa, laana na mikosi....katika maisha ya watu

Mchungaji Mwangasa


Watu wenye matatizo na kuteswa na shetani kwa kuwekwa kwenye vifungo, walianza kufunguliwa kwa njia za Ajabu, Roho wa Mungu alitenda kazi kupita kawaida.


WACHAWI WADONDOKA KUTOKA ANGANI
Mchungaji msaidizi akimsadia Bibi mchawi aliyedondoka baada ya maombi na Roho wa Mungu kufanya kazi kupitia kwa Mchugaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima akimhakikisha Bibi mchawi aliyedondoka..

Bibi akiwa amesalimu amri baada ya Nguvu za MUNGU kumfurumusha kutoka angani...alikokuwa anaendelea na biashara yake ya uchawi.


Maelfu kwa maelfu wakiwa wanaendelea kuombewa na kufunguliwa...

Watu wa Mungu wa Tanga wakaanza kumsihi Mchungaji Kiongozi, amruhusu yule mchawi ashuke, watu hawa walikuwa na hasira kali sana, na nia yao ikagundulika na Mchungaji, maana zikaanza kuskika kelele kubwa za watu wakimuomba yule mchawi ili kumloweka kwenye mafuta wamchome moto kabisa kabisa...Kwa maana wamekiri kuchoka sana kuteswa na wachawi kila kukicha katika jiji la Tanga

Mchungaji Mwandamizi Mkuu, Grace Gwajima (kushoto) akimhoji Bibi Mchawi

Mchungaji Josephat Gwajima, akimuangalia mchawi aliyedondoshwa na nguvu za Mungu akijitetea,katika madhabahu..


Wachawi wakaendelea kudondoka wingi, Pichani Mchungaji Josephat Gwajima, akiwaamuru watenda kazi wamuokoe mchawi huyo ambaye tayari watu wa Tanga walishaanza kumshughulikia kwa njia za mwilini...wakampandisha juu ya madhabahu mchawi wa pili aliyedondoshwa kwa Nguvu za Mungu.Maelfu ya wakazi wa Tanga kwa kelele na sauti kubwa , pamoja na Mchungaji Josephat Gwajima wakimtukuza Mungu baba wa Mbinguni kwa Neema hii ya Kuwafungua maelfu na kuwadhihirishia wazi wazi mchana kweupe waliokuwa wanawavurugia maisha na kuwaloga watu wa Tanga...
Pichani hapo juu ni mchawi wa pili akiwa anapandishwa madhabahuni.

Bibi Mchawi aliyedondoka mara ya kwanza akiwa ameombewa hapa analetwa ili atambulishwe mbele za watu ili aachiwe...

Akiwa anataka kutambulishwa

Ghafla watu wa Tanga walilipuka kwa kelele za hasira wakimtaka mchawi yule ili wamshughulikie, lakini Mchungaji Josephat Gwajima kwa hekima na Busara Mungu alizomjalia, aliwaasa na kuwaelekeza, maelfu ya watu wa Tanga kuwa """Jamani ndugu zangu..nawaombeni mnielewe kuwa wachawi hawa haipasi kuwapiga kwa mwili, ni vyema tuwe tunawaombea ili waachane na mambo ya kishirikina na Hatimaye wammpokee Yesu"""

Watu wa Tanga wakafurahi pamoja na Mchungaji wakiyaelewa na kusadiki walioyaoswa.

Hatimaye mchawi yule akaambiwa akae kwanza madhabahuni.

Na huyu ni mchawi wa pili aliyedondoshwa na Nguvu za Mungu, akiwa anahojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.

Wachawi wote wawili wakionekana pichani, na huyu mwenye kanga na dera la njano ni mchawi wa pili aliyekutwa na hirizi nyingi kila kona ya mwili.Wachawi waliwashangaza wengi...


Mchungaji Josphat Gwajima akiwaangalia wachawi hao waliodondoka.


Watu wa Tanga waliendelea kuimba YESU..YESU...YESU..Kutokana na matendo makuu yaliyojitokeza, lakini pia waligoma kabisa kuondoka hadi wawaone vizuri wachawi wale maana ni watu wa jamii ya watanga na wangependa kuwatambua.

Watu wa Tanga wakaapa kutokumdhuru mchawi yeyote, jambo ambalo Mchungaji alilifurahia.Akawaombea na kuwabariki kisha wakaletwa mbele yao,wabibi hao wawili waliodondoka..Wachawi wote walikiri makosa na wakahidi kuwa hawatarudia tena uchawi na waliomba msamaha kwa yote waliyoyatenda.


Hatimaye mkutano ukafungwa kwa nderemo za shangwe kubwa...na watu wote wa Tanga wakammpazia sauti Mungu na kumtukuza kwa kuwaletea Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, katika Jiji la Tanga na wengi walikiri kuwa hakika Nguvu hizi za Mungu ndio ambazo wamekuwa na kiu nazo kwa kipindi kirefu sana...na wengi walimmpazia Mungu sauti wakisema hakika Mungu wetu ni Mungu wa miungu...Bwana wa bwana,Mfalme wa wafalme Alfa na Omega....na Hakuna kama Yeye.


No comments:

Post a Comment