Wednesday, November 20, 2013

UTENZI KUTOKA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA - MOYONI MWANGU

Huu ni Utenzi uliotungwa na binti Pepita Samuel ikiwa ni Mpango wa kanisa la Ufufuo na Uzima kukuza vipaji vya vijana katika kumtumikia Mungu. Pepita ametunga utenzi huu na kuuita MOYONI MWANGU ukiwa umejikita katika somo la Mchungaji Gwajima alilofundisha Tar. 10.11.2013 kuhusu kusudi la mtu la milele.
Pepita Samweli akionesha uwezo wake wa hali ya juu sana katika utunzi na uimbaji wa mashairi.
Ukiacha ujasiri alionao, Pepita ameweza kuongea utenzi hili bila kusoma ikiwa ni sehemu ya kipawa ambacho kinamtofautisha na watunzi wengine. Tunaamini utabarikiwa unapokwenda kusoma utenzi huu.

Utenzi wa Pepita

Kuliko vyote ulindavyo, linda moyo wako, Maana ndiko zitokazo, Chemichemi za uzima wako. Mungu alipotuumba sisi, Aliweka kitu ndani yetu, Ndani ya mioyo yetu. 

Ni zile hisia, nia na utashi Ule tulioutoa kule mbinguni kwetu. Kuna thamani ndani yako, Kuna maelekezo ndani yako. Ila shetani anataka yale yakwake ndo yawe yalekwako. 

Kukataa huwezi maana zimechakachuliwa fikra zako. Kuna thamani ndani ya moyo wako. Nilikua nikiona walevi, wezi na mambo mabaya ninajiuliza, Hivi hata haya Mungu amewaagiza? 

Vijana wadogo, watu wazima, wazee wamepotezwa, Kwenye giza nene wameingizwa. Nikafikiri ni mapepo tu, Kumbe ni maelekezo yasiyo mioyoni mwetu. 

Utambishia nini mtu akilini aliyeamua moyoni? Akiwa ameamini ni nia yake hata ukimuangalia machoni. Ukimkemea na kudhani anamapepo, Mtakesha miaka hapo hapo. 

Kuliko vyote ulindavyo, linda moyo wako. Si huu wa nyama, ni ule uliomo ndani yako. Shetani anakupa maelezo ambayo sio, na unayatekeleza, Ukiambiwa useme kwanini, Wasema yametoka moyoni! Kisha anakaa na kusubiri, Anafurahia akiona ukiyatafsiri, Kama ni ya kwako. 

Waweza penda asiye, Waweza mdhania siye ambaye ndiye, Waweza jenga ufamle wa shetani, Waweza fanya vyote ukidhani, Yametoka moyoni mwako.
Shetani atakuongoza ndani ya maelezo yake, Na wala hayataamka mapingamizi. 

Pale tu utakapo amka na kuugundua usingizi, Hadi nyumbani kwako atakuletea wezi! Kuliko vyote ulindavyo, linda moyo wako, Amka sasa usije ukashtuka wakati umekutupa umri wako. 

Amka sasa uujenge ufalme wa wetu Baba, Amka sasa! Nafasi kama hizi ni haba! Amka sasa uelekee katika kusudi lako la milele! Amka sasa mbinguni uziskie hizi shangwe na vigelegele. 

Kabla ya kuamua, Kabla ya kupenda, Kabla ya kuchagua, Kabla ya kutenda, Jiulize, ni moyo wangu huu? Ni moyo wako huo? Above all else guard your heart, Because from it, comes the issues of life! From it, comes a husband's wife, Comes all you decide is wrong or right, Comes the strength to move on and put up a fight! Kuliko vyote ulindavyo linda moyo wako. Ni kisima! Maana ndiko zitokazo chemichemi za uzima!


MUNGU NI MUNGU WA KUSUDI HAKUNA AMBACHO AMEKIUMBA BILA KUSUDI.

1 comment:

  1. What comes from her is pure fruit of the spirit..I'm impressed!
    Glory be to Jesus

    ReplyDelete