Tuesday, December 24, 2013

MAPEPO YAGUNDULIKA KUWA VYANZO VYA MATATIZO MENGI YA WATU

 
Akifundisha katika Mkutano wa maelfu ya watu Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alieleza kuwa mapepo(mashetani au majini) ndio vyanzo vya matatizo yanayowakumba watu wengi leo hii. Baada ya kufundisha kwa dakika chache Mchungaji alianza kufundisha kwa vitendo na alipoanza tu mapepo yaliyokuwa ndani ya watu mbalimbali yalidhirika na baada ya uponyaji watu hao walielezea matatizo yalikuwa yanawasumbua muda mrefu ambayo yalitokana na kupagawa na pepo waliowangia ndani yao.
 
Binti mmoja  aliyefahamika kwa jina la Amina Salum (Chini katika picha) ambaye hapo awali kabla ya kuokoka alikuwa muislamu, alikuja katika mkutano wa Ufufuo na Uzima akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Akieelezea tatizo lake, Amina alisema kuwa alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akisikia kuwa tumbo linachoma choma ndani kiasi cha kushindwa kula. Tatizo ambalo lilimdhoofisha mwili siku hadi siku.

Wakati Mchungaji Gwajima akipita katikati ya makutano alimkuta amekaa na mapepo yaliyokuwa ndani yake walipomuona mchungaji wakadhihirika kutokea ndani yake ambapo na baadaye yalipewa amri yamtoke mtu huyo. Baada ya hapo dada huyo alipona kabisa magonjwa yake papo hapo.


Mchungaji Gwajima akiwa amemshika Amina baada ya kupokea uponyaji wake.

No comments:

Post a Comment