Sunday, February 16, 2014

MBEGU NJEMA YA USHINDI YAPANDWA KATIKA KONGAMANO LA MAKANISA YOTE YA KIPENTEKOSTE NCHINI TANZANIA

MUNGU WA MBINGUNI AJIDHIHIRISHA KATIKA KONGAMANO LA MAKANISA YOTE YA KIPENTEKOSTE LILILOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA, UKUMBI WA PTA JIJINI DAR ES SALAAM.

Jumamosi ya Tarehe 15.02.2014 palifanyika jambo la baraka na la kihistoria pale ambapo makanisa ya kipentekoste nchini Tanzania,yalipokutana katika Ukumbi wa PTA, Ndani wa Viwanja vya SabaSaba wakiwa wamekutana kwa pamoja, kwa nia moja,Mitume, Manabii, na Wachungaji

Palikuwa na mkusanyiko mkubwa sana wa watu wa Mungu kutoka makanisa mbalimbali ya kipentekoste kama vile Full Gospel Bible Fellowship, TAG, EAGT, EFATHA, Glory of Christ (T) Church-Ufufuo na Uzima, Mito ya Baraka na Mengine mengi.Mchungaji Zakarya Kakobe akiingia ukumbini

Mchungaji Zakarya Kakobe, mchungaji kiongozi wa Kanisa la full Gospel bible fellowship.Mchungaji Josephat Gwajima akiingia ukumbini siku ya Kongamano katika ukumbi wa PTA.
Maelfu ya watu waliokuwepo ukumbini wakimshangilia mchungaji josephat Gwajima

 Mchungaji Kakobe akihubiri

 Mchungaji Zacharya kakobe akimkaribisha na kumtambulisha Mchungaji Josephat
 Mchungaji wa Kanisa la Full gospel  bible fellowship Zakarya kakobe akiwa na Mchungaji kiongozi wa Josphat Gwajima

Ukaribisho wa Furaha    Mchungaji Kakobe akiendelea kuhubiri.

 Mchungaji Kakobe akiongoza maombi ya kutuma mafarakano kwenye kambi ya adui yako
 Mchungaji Josephat Gwajima katika Maombi

 Mchungaji kakobe akihitimisha maombi
 Muda wa Mchungaji Gwajima kuhubiri uliwadia

    


Monday, February 3, 2014

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA AWACHAFULIA USEMI WATESI WA MAISHA YA WATU

KILA MTU ALIGUSWA KWA NAMNA YA KIPEKEE WAKATI MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA ANAFUNDISHA NA KUONGOZA MAOMBI YA KUWACHAFULIA USEMI WANAOWATESA WATU KATIKA MAISHA YAO.

Mchungaji Josephat Gwajima akionesha umahiri mkubwa katika upigaji wa Guitar.
Ni wachungaji wachache wenye vipaya vingi kama alivyonavyo Mchungaji Josephat GwajimaKila aliyekuwepo alimsifu Mungu Baba yetu wa mbinguni kwa hali ya kipekee sana.

Kilikuwa kipindi cha sifa ambacho kilifanyika kuwa baraka sana

Platform Choir wakisifu

Mchungaji Yekonia Bihagaze akimkaribisha Mchungaji Josephat Gwajima

Muimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Flora Mbasha

SOMO:KUWACHAFULIA USEMI ADUI


Na. Mchungaji Josephat Gwajima
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe

Utangulizi ZABURI 18Mungu aliwaumba watu na akawaagiza wazae na kuongezeka juu ya uso wa nchi lakini wakapatikana watu waliokwenda kinyume na amri hiyo ya Mungu na kufanya kinyume, wao wakasema watakaa mahali pamoja ili wasitawanyike usoni pa nchi. Unaanza kujifunza kumbe wanaweza wakapatikana watu wakaenda kinyume na mambo yale ambayo Mungu amesema juu ya maisha yako, Mungu anataka ubarikiwe, uwe na afya njema na ufanikiwe lakini wapo waganga na wachawi na wanadamu ambao wanaweza kuja kinyume na makusudi ya Mungu katika maisha yako.

Leo kwa jina la Yesu tutawachafulia adui wote wa maisha yako usemi wao na utaanza kumuona Mungu kwa namna ya ajabu tena katika maisha yako.

Mwanzo 1:27

Mungu alipomuumba mtu alisema nendeni mkazae mkaongezeke mkaijaze nchi.

Mwanzo 11:1-7

“…Tushuke mpaka huko tukawachafulie usemi…” 

 
Baada ya kuwa wameongezeka sana wakaamua kujenga mnara wa babeli ili wajikusanye mahala pamoja wasije wakatawanyika katika nchi, wakapinganana agizo la Mungu. Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu wakaamua washuke duniani kuja kuwachafulia usemi wasiendelee na makusudi yao ya kujenga mnara mpaka mbinguni.

Mungu alikuwa ametoa amri ya awali kwamba enendeni mkaongezeke mkaijaze nchi, watu wakazaa wakaongezeka kweli kweli, baadae akatokea kiongozi mmoja alietangaza kujenga mnara utakaowakusanya mahali pamoja wasije wakatawanyika katika nchi. Nina wasiwasi huyu bwana ndie aliekuwa mwanzilishi wa umoja wa mataifa wa wakati ule. Mungu amesema tawanyikeni, halafu huyu bwana anasema wakusanyike mahala pamoja, huwezi kupinganana agizo la Mungu na ukabaki salama.Mungu amesema ukaolewe wao wanasema hutaolewa, Mungu amesema muacheni huyu asome, wao wanasema hasomi huyu, Mungu kasema mwacheni huyu akafanye biashara wao wanasema huwezi fanya biashara, akazae huyu wao wanasema hata beba mimba, akafanye kazi huyu wao wanasema hutafanya kazi, akamtumikie Mungu huyu wao wanasema huta mtumikia, wanapingana na agizo la Mungu, leo tunawachafulia usemi wagombane wao kwa wao, wasielewane wao kwa wao kamwe kwa jina la Yesu.

Unajua watu wakishakuwa na lugha moja ni hatari sana, yaani wakiamua kunuia jambo ni lazima watalifanikisha, kama wakiafikiana kwa lugha ya pamoja huyu bwana apate ajali, yaani kikundi cha wachawi chote kikakubaliana apate ajali, kumbe tumegundua wakiwa wanaongea lugha moja hawawezi kuzuiliwa neno, leo lazima tuwatengeneze, tuwachafulie usemi wasielewane kabisa kwenye vikao vyao.

Kila maeneo kuna vikundi vya wachawi na huwa wanakuwa na maeneo yao ambayo wanakusanyika usiku, kwenye vikao vyao kuna mwenyekiti na wakikaa wanaanza kuleta hoja zao, tunataka fulani avimbe tumbo, wakishakubaliana wanaongea lugha moja avimbe tumbo, mmoja akisema avimbe mguu hapo lugha ishachafuka, hawatafanikiwa. Ila wakikubaliana wote wataondoka kwa lugha moja kwenda kutekeleza adhma yao, kuwashinda hapo mpaka mtu uwe unaishi sawasawa na sharia ya Mungu inavyotuagiza.

Joshua 8:12 “…akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai…”

Wachawi huwa wanaweza wakamuotea mtu hata kwa miaka mingi ili wafanye yale waliyoyakusudia katika maisha ya mtu huyo, wakikubaliana kwa lugha moja ufe, watakufuatilia mpaka wakushinde, wakifika wakikuta mtu huyu ameokoka yupo vizuri na Mungu, wanaanza kukufuatilia ili siku ukamkosea Mungu ulinzi wa Mungu ukatoka kwako waweze kufanikisha adhma yao. Namna ya kuwashinda hawa ni kuishi sawasawa na neno la Bwana.

Hata ukija serikalini kikundi cha viongozi wanao ongea lugha moja wakikubaliana jambo, hawatazuiliwa na mtu. Kama CCM saivi wameanza kuongea lugha tofauti, hapo chama ndio kinavyo meguka, maana Hawa wanasema Lowasa fisadi wengine wanasema huyu msafi ndie mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Kinachowaumiza CCM sasa ni lugha tofauti, mnaemwita mwizi kwa wengine ni mzee wao, yule mnaemwita dhaifu kwa wengine ni baba yao, na chama kilipo saivi kipo pabaya kweli kweli.

 Hakuna kitu imara ambacho kikipewa lugha tofauti kitaendelea kusimama. Mungu alivyoona wale watu wanaongea lugha moja na wana mshikamano kweli kweli Mungu akaona awachafulie lugha na hawakufanikiwa kuendelea na ujenzi wa mnara wao.

Ufufuo na uzima pia tuna lugha yetu, na hakuna wakutuzuia, na ndio tunasambaa duniani hivyo kwa lugha yetu hiyo moja. Tumeijaza Tanzania na sasa tunaelekea kuijaza dunia. Ili jambo lifanikiwe lazima wawepo watu wanaoongea lugha moja, ukitaka kuwatawanya wagawie lugha tofauti.
 
Mama Mchungaji Grace Gwajima akiwa katika Ibada ya Jumapili

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anafundisha maelfu ya watu katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima

Mchungaji Josephat Gwajima,Akihubiri nyuma yake wanaonekana na nyuso za furaha ni Mchungaji Bryson Lema(kushoto) na Mchungaji Baraka Tegge (kulia)

Maelfu ya watu wa Mungu walikuwa wakiwekwa huru dhidi ya maadui zao wa kiroho

Mtoto akiombewa na Mchungaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima akipita katikati ya kundi la watu huku maombi yenye nguvu yakiendelea na watu wakiendelea kuwachafulia lugha maadaui zao.Kila jambo gumu unalopitia usifikiri imekuja hivi hivi, kuna watu wanaongea lugha moja huko, leo lazima tuwachafulie usemi. Leo walionitesa nakwenda kuwavisha kila mtu na lugha yake. Kila aliefanya vita na wewe  nasema lugha tofauti zitaendelea kwenye vienge vyao kwa jina la Yesu. Na adhma yao haitafanikiwa kwa jina la Yesu.

Makamanda watatu wakishetani ni mpinga kristo,nabii wa uongo na Lucifer/shetani, leo nikuwachafulia usemi hawa makamanda, muujiza wa kuwachafulia usemi unafanywa na Mungu mwana, Mungu baba na Roho mtakatifu huwa wanashuka wenyewe kuchafua usemi. Wanachafuliwa usemi wasielewane wao kwa wao, na wewe unasonga mbele na Mungu na maisha yako

Hata mtu na mkewe mkiongea lugha moja familia itajengeka, ila mkiongea lugha tofauti mtatawanyika. Wawili hawawezi kwenda pamoja isipokuwa wamepatana, nami leo nawachafulia usemi wawili waliopatana kukuangamiza hawatapatana kwa jina la Yesu.

Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima