Sunday, March 30, 2014

 SOMO: KUWAFUATILIA

PASTOR: ADRIANO 
TAREHE: 30-03-2014
Mchungaji Baraka Thomas (RP) akimkaribisha mch Adriano
Utangulizi: Leo tutawafuatilia adui zetu mahali popote walipo na tutarudisha nyara walizochukua kutoka kwetu kwa jina la YESU, tunaamua kuwafuata kupigana nao na kurudisha kila walichokichukua kwetu kwa jina la YESU
Mchungaji Ngazi ya RP ADRIANO MAKAZI akianza kufundisha Neno la Bwana 
Isaya 42:22 “Lakini watu hawa ni watu walioibiwa, wamekuwa mawindo wala hapana okoaye, wamekuwa mawindo wala hapana asemaye rudisha”
 Isaya alikuwa anaona maono ya Bwana na katika maono aliona kuna watu walioibiwa na kutekwa na katika majira hayo wachawi walikuwa wanaweza kufanya lolote na hakuna aliyewakataza, nyakati zile watu walikuwa hawana jinsi maana hakuna aliyesema RUDISHA.
Biblia inasema watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa,  maana yake kuna watu walioibiwa nyota zao , akilia zao , ndugu zao , mali zao na nyuso zao,  watu wengine wameibiwa vichwa. Kuna mtu anaweza kutekwa kama anafanya biashara akili na nyota yake ikaanza kutumiwa na mtu mwingine na yeye hawezi kufanya jambo lolote kwa uwezo wake binafsi, unashangaa mtu anafanyiwa mambo ya ajabu lakini anakua hana uwezo hata wa kuhoji kwasababu nyota yake imeibiwa.  .Leo tunawafuata adui zetu maana tunaye kiongozi YESU KRISTO na nguvu tunazo na hakuna anayeweza kutuzuia tukiwa na kamanada Yesu .  Kwa nyakati hizi tunazoziendea lazima wachawi waaibishe na hawatakuwa na la kusema kwa jina la Yesu kwa maana tunawafuata kwa uwezo wa jina la Yesu.
Leo tunafanya maandamano ya rohoni na kuwafuatilia maana sisi ni majeshi ya Bwana na tunajua kila mahali na kila kitu, kwa kuwa shetani hana kitu kwa maana alipoasi mbinguni alinyang’anywa vyote hivyo naye anachofanya ni kuiba vya wengine ili avitumie , lakini leo tunamfuata na kumnyang’anya vyote , katika jina la YESU.
Neno rudisha ni silaha hatari  linapotamkwa lazima kuzimu nzima itaharuki na kuwaka moto, kwa hiyo tunapowaendea lazima tuwanyang’anye vyote. Shetani anawateka na kuwaweka watu gerezni na ndo maana mtu anapokuwa ibadani anaanza kusinzia kumbe shetani katangaza kuwa wafungwa wake wote lazima walale. Unapokuwa gereza la rohoni unakua unapanga mipango yako lakini haiwezi kutekelezeka kwa sababu uko gerezani unapopanga nifunge na kuomba inashindikana kwa maana tangazo linatoka kuzimu wafungwa wangu wawe na hamu sana ya chakula. Kwa hiyo huwezi kutoka gerezani mpaka atokee wa kusema rudisha. Na mchana wa leo utaona tunaposema njoo magereza ya kuzimu yanapsasuka na kuvunjika vipande vipande na watu wa Mungu  wanaachiliwa.
Wanajua kuna milango mingine inayofunguka kumbe ni mitego ya shetani anakutega ukiingia anafunga. Kwa hiyo kuna uwezekano kabisa mtu kuwa gerezani ndiyo maana unaweza akapanga kuomba lakini ukashindwa kumbe mkuu wa gereza(shetani) ametangaza wafungwa wote walale. Mahali kama hapo unatakiwa kutumia neon njoo na sio toka. Unapoita njoo inakuwa hatari kwa shetani kwa maana anajua mwenyewe amekuja lakini  neno toka halimsumbui kwa maana hawezi kuuacha mwili peke yake yeye ndo ameumiliki, kwahiyo neno njoo linasababisha yule mfungwa aliyefungwa kwenye gereza la kishateni kuchomoka na kuwa huru kabisa.
IBRAHIMU ALIRUDISHA BAADA YA KUFUATA
Mwanzo 14:8-16 Utaona wafalme wa Sodoma na Gomora  walitegewa mashimo na kunaswa kwa maana hawakujua mbinu za adui zao kuwaita mahali pale, ndo maana kuna watu wameanza vizuri kumtumikia Mungu na baadae  wakanaswa kwenye mashimo ya uharibifu na sasa ni watumishi wa joka(shetani) na wanaona aibu kusema lazima watu walio nje wanajua yeye ni mtumishi wa Mungu lakini wameshamuacha Mungu siku nyingi.  Heri wewe uliyeamua kukimbilia ufufuo na uzima kwa maana  utapewa maarifa ambayo ni Roho Mtakatifu  na utawafuata ndugu zako  na vyote vilivyoibiwa kwa Jina la Yesu.
MGANGA WA KIENYEJI ALIPOFUATWA NA KUHAMISHWA NA MAJESHI YA BWANA
Mchungaji ADRIANO MAKAZI (RP) akiwa anasoma Neno la Bwana 
Wakati tulipokuwa Ubungo  mwaka 2004 kuna mganga mmoja wa kienyeji anaitwa Lamba lamba hapo jirani  sasa siku moja tukaamua kwenda kumuhamisha mahali pale na tulikwenda kama wateja wake.Tulipofika tukamwambia sisi watatu tunakaa pomoja ila tumepotelewa na hela na kila mtu anakataa  sasa tunaomba utuambie nani amechukua  akasema sawa, akaanza kupiga manyanga yake na baada ya muda akasema tokeni kwangu kwa maana mmekuja kwa shari na akasema kama mkiamka asubuhi hai siyo mimi sio mganga lazima mtakufa , na sisi tukamwambia kama ni watumishi wa Mungu ikifika kesho bado uko mahali hapa unakufa. Kesho yake asubuhi na mapema akaamka na kufungasha kila kilicho chake akaondoka. kuna watu wanaoharibu kazi za watu , hii inatufundisha wakati mwingine lazima tuwafuate sio kuomba pakee.
Usidhani Tanzania tulipata Uhuru bila kupigana vita siyo,kwa kuwa baba wa Taifa alikuwa mtu wa rohoni upande wa giza kwa hiyo kuna vitu alivyofanya rohoni na kuwaondoa wakoloni ndiyo maana vitu vile alivyofanya vinatupeleka pabaya utaona tuna rasilimali nyingi lakini hatuwezi kuzitumia wenyewe na tunabaki masikini na omba omba kwa mataifa mengine kwasababu ya msingi wa giza uliowekwa na waanzilishi wa taifa.
SHETANI ALIONDOKA MBINGUNI BAADA YA VITA KUPIGANWA
Ufunuo 12:7-16 , Vita ilipiganwa mbinguni na Lusifa(Shetani) akatupwa chini. Hii inatufundisha kwamba hakuna kumiliki bila kupigana, huwezi kuolewa bila kupigana, huwezi kujenga bila kupigana, huwezi kusoma bila kupigana, huwezi kupata hehima bila kupigana, leo katika ulimwengu wa roho unadharauliwa kwa sababu unapigwa, hata Rebeca alikuwa na mapacha tumboni walioanza kupigana tumboni wakishindana nani amtumikie mwingine. Hata wewe lazima upigane ndo maana wenzako wanaenda kwa waganga wa kienyeji wanapigana na kupata vyeo ndio maana wanapopita barabarani wanapigiwa ving’ora kwa maana wamepigana na kushinda rohoni.
Katika mapigano kuna kujeruhiwa  au kufa lakini sisi katika mapigano haya hatuwezi kufa kwa maana YESU alishakufa kwa ajili yetu ila adui zetu lazima wafe.
Maombi ya kuwafuata adui na kurudisha ulichoibiwa
Mchungaji Ngazi ya RP ADRIANO MAKAZI anasisitiza jambo wakati akifundisha Neno la Bwana 
Kwa mamlaka ya jina la Yesu ninawafuata adui zangu wote walioiba nyota yangu, fedha zangu, ustawi wangu, heshima yangu, kibali change na vyote nilivyoibiwa kwa jina la Yesu. Ninawateketeza adui wote wa rohoni, adui majini, majoka, mizimu na wengine wote ninawateketeza kwa jina la Yesu na ninaangamiza uweza wenu wote.
Ninaamuru kila ambacho mmeniibia anza kurudisha kwa jina la Yesu, ninaamuru vyote vilivyoibiwa njooo kwa jina la Yesu( anza kuita vitu vyote ambavyo unahisi shetani ameviiba katika maisha yako kwa jina la Yesu)

Watu mbali mbali wenye pepo na walikuwa wamechukuliwa Msukule wakiombewa na Wachungaji

Moja wa Wachungaji akimwombea kijana akiyekuwa amepagawa na Mapepo

Wachungaji mbali mbali wakiwaombea walikuwa wamepagawa na mapepo

Mchungaji MAX na Mchungaji YEKONIA BIHAGAZE wakiwa wanamfungua dada ambaye alikuwa amefungwa na ibilisi

Wachungaji wa Ufufuo na Uzima wakiwafungua washirika waliyokuwa na mapepo
No comments:

Post a Comment