Sunday, March 16, 2014

MAELFU WASAMBARITISHA MAZAO YA NDOA ZA KISHETANI NA MCH. JOSEPHAT GWAJIMAKUHARIBU MAZAO YA KISHETANI/KICHAWI


PASTOR: JOSEPHAT GWAJIMA
16/03/2014

1samweli3:4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.
5 Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.
6 Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.
7 Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
8 Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto.
9 Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
10 Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.

Mungu anamwita samweli mara tatu na sauti ya Mungu inafanana kabisa na Baba yake wa kiroho Eli na anamwendea mara tatu ndipo Eli alimfundisha jinsi ya kuitika na akamwambia aseme 'sema Bwana mtumishi wako anakusikia ' na Mungu anatufundisha kuwa anaweza kututokea na katufundisha jinsi ya mfanop wa Baba wa kiroho.
Ukiona mtu anafanya vizuri jua kuna nguvu ya kiroho na ukiona anasuasua jua pia kuna nguvu za kiroho zinazofanya kazi na kukusababisha mambo yakutokee kimwili.
Mungu tunaye mwabudu anatuponya magonjwa na tabu zote za maisha yetu.na watu wengi wanapenda kudharau ndoto.
yuda1:1 Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.
2 Mwongezewe rehema na amani na upendano.
3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
8 Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

 ufunuo12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.


mashetani ni malaika waovu ambao wameshushwa kutoka Mbinguni na kuna malaika wachafu(wa giza) na malaika wazuri na wanapoitwa malaika wanakuwa na uwezo wa kubadilisha maumbo, pia utaona kwenye biblia malaika wakaenda sodoma na gomora na Lutu alikuwa kwenye lindo la mlango siku hiyo na alipo waangalia akaona sio watu wa kawaida akawabeba akawapeleka mpaka nyumbani kwake na Biblia inasema wenyeji wa sodoma na gomora wakawaona wale malaika kuwa ni wazuri kwa maumbo yao wakawataka wawaoe! na hapa tunajifunza kumbe malaika wa aina ya kijini wanaweza kuvaa maumbo ya kibinadamu na wakaolewa.
kwahiyo anavaa umbo ili awe na mahusihano na wewe na baadaye mkiachana mkagombana na yeye anabaki ndani yako ni malaika wa giza lakini si mtu na mnaweza mpaka kuzaa watoto na wanakuwa waluwalu ama ana akili sana ama hana akili; na ukiangalia majini hawa hata akicheka ndita haitoki usoni kwasababu asili yake ni kifo ni motoni kwasababu ni (Jini wakala wa shetani).
Si siku zote majini wanaweza wakavaa miili wakaenda kuoa au kuolewa na mtu lakini wanafanya hivyo kwa mtu aliyeshushwa na Mungu kwasababu ya alicho nacho kinaweza kuwa ni kusudi la kuwa daktari ama mtumishi wa Mungu ama raisi. na jini anatumwa aje kuwaingilia katika maisha yao katika kufunga na huyu mtu wa Mungu ndoa ili ampindishe lile kusudi lake alilowekewa.
Hawa majini ama mashetani wanavaa miili kwasababu wanakuwa wanafahamu watu waliotumwa na Mungu kuja kufanya kazi ya Bwana ili kuwaharibia kusudi lililowekwa na Mungu lisitendeke kupitia maisha mikoni yao.
Mungu amekupa safari ya kuanza na kumaliza na utaimaliza kwa maana imeandikwa "nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."
Ukiona kila kitu kipo vizuri jua kwamba shetani ni rafiki yako na unahatari kubwa, kama gari unalotaka unalo, kazi unayoitaka unayo jua unahatari kubwa kwa maana hakuna mteremko katika wokovu na unatakiwa kupigana. Na shetani hawapendi watu wa Mungu na huwavuruga na kuwa kwamisha. na hatuna matatizo bali tuna changamoto na tunatakiwa tupambane kwa silaha tunazojifunza.
kila aliyetoka Mbinguni ana makusudi ya Mungu na hataenda Mbinguni mpaka kazi aliyotumwa na Mungu ikamilike.kuna vyanzo vya rohonni vinakuzuia usifike katika kusudi lako sio kwamba huna hela Mungu ameacha mambo hayo yatendeke ili ujifunze kupigana vita."we have no failure in chrit but it is just a message that try other way allowed"
Yeremia1:4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.
9 Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
10 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Mungu alikujua tangu tumboni kabla mama na baba yako hawaja fahamiana.aliandaa kazi yako na majukumu yako yaliandaliwa kabla hujazaliwa na unapozaliwa shetani kupitia waganga wa kienyeji na wachawi na malaika wake wanajua amezaliwa Rais ndiyo maana Yesu alipozaliwa mamajusi walitoka mashariki. na mambo yale ambayo hujawahi kuyaona na kuyawaza na kuyamiliki ameyaweka kwetu na ametufunulia kwa uweza wa Roho wake kwamaana siku moja Mungu anaweza kuibadilisha kwa miaka yako 60 uliyo nayo na kubadilishia maisha yako ukafanya kazi ya miaka elfu moja ukawa tajiri kutoka kwenye ufukara.
kwahiyo shetani akiona huyu dada,mama,mchungaji,binti,baba anakitu kule mbele cha ajabu tumejaribu kumzuia imeshindikana basi tumtumie mtu atakaye pindisha kesho yake kutoka kuuzimu na mtu aliyetumwa ayapindishe maisha yako anaweza kufanya kitu chochote.
kama unakitu cha Mungu utajisikia kawaida wala hutajisikia tofauti yeyote na unakuwa unaweza kukosea kama binadamu.
Rada na decoda za kishetani zinaweza kurekodi maisha yako na wanaweza kujua kwenye chuo kikuu cha dar es salaam kuna mtu pale lakini wewe hujijui na unaweza kuitwa lakini wewe hujijui kama yohana mbatizaji alivyokuwa anabatiza na kuwaonyesha watu kuwa mwanakondoo wa Mungu akiwa na miaka 30 na wayaudi wa kawaida wakamwona kijana wa kawaida kutokea nazareti lakini yohana alikuwa anaona ndani yake kuwa ni Mungu aliye umba mbingu na nchi akawaambia nayeye anakuja kubatizwa hapa na yohana akamwambia mimi ndio unibatize wewe na Yesu akawaambia ambatize ili yote yatimie.
Inafika sehemu mtu anapokuwa ana hatima kubwa shetani kuzimu anatumwa kuja kuipindisha hatima yako na anaweza asiwe mume hata bosi anaweza kutumwa na sio lazima awe ni jini anaweza akawa mtu anakuja katika maisha yako ili ushindwe kuifanya hatima yako uliyopewa na Mungu na hata kama amesha kupiga chini simama na uanze
unachotakiwa ukifanye ili usimame tena na kupigana ni mambo haya yafuatayo:
1  Jaribu na ubaini aliye fanya maisha yako yaanze kubadilika anaweza akawa mtu ama jini ulipo kuwa na nani au unafanya nini au kitu ulichokuwa nacho
2  Ubaini yupo wapi huyu mtu na anafanya nini ili asije akarudi tena anaweza kuwa ni shetani anajua hauja mfahamu na ukisha mjua unatakiwa uanze kufyeka katika Jina la Yesu; Na kipindi ambacho unahitaji unatakiwa uwe makini kwasababu unaweza ukaletewa kitu cha kukuharibia maisha yako na ndio maana hayo maisha yako uliyo nayo sasa hukutakiwa kuwa hivyo na Mbinguni wanajua wewe ni mkurugenzi,daktari,waziri ila kuna mashetani ama watu yametumwa kukuzuia.
3 Amua kuacha mara moja na utaachaje unatakiwa  umwambie Mungu naomba uniondolee huyu wakala aliyekuja kwenye maisha yangu"ukisema katika jina la Yesu nakuponda ,nakuvunja,nakufyeka ana fyekwa kwasababu una nguvu ya Jina la Yesu pekee jina lipotalo majina yote tunaweza kushinda mamlaka za giza kwa jina la Yesu na sio dhehebu,sio mtu ni jina la Yesu pekee
mathayo10:Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

Tuna mamlaka ya kumwambia wakala wa shetani yeyote aondoke kwenye maisha yetu kwa jina la Yesu na inawezekana wale majini wanakaa ndani yako kwahiyo warudishe waliko toka kwa jina la Yesu.
Unakuta unaanza dalili za kumalizia vibaya unasema ni kusudi la Mungu ametaka umalizie, si kwamba Mungu ametaka unatakiwa ukatae kwa jina la Yesu na ukifanya hivyo anaondoka awe ni jini,pepo,shetani,mchawi,mganga,mzimu ama binadam ametumwa kwenye maisha yako anaondoka
 waefeso6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

4 Uwe tayari kushindana kwa mamlaka ya Jina la Yesu na vita hizi za mashetani kuwaingilia maisha na kuwa na uhusiano nao yanatokana kwa wale walio na kitu cha ki Mungu  ndani yao na tunashindana kwa jina na Damu ya Yesu kristo wa Nazareti.

No comments:

Post a Comment