Sunday, April 6, 2014

JINA LA YESU LAWARUDISHIA VYOTE VILIVYOIBWA NA SHETANI KATIKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA

ROHO WA BWANA ATENDA MIUJIZA ISIYOKUWA YA KAWAIDA

KURUDISHA KILICHOIBIWA
 06th April, 2014 
Jumapili
Resident Pastor Mwongela akimkaribisha Pastor Adriano


Resident Pastor 
ADRIANO MAKAZI


Kuna vitu vimeibiwa vingi sana, ni muhimu ugundue shetani anaweza kuiba.  Na unapogundua lazma ujiulize aliibajeibaje na wakati wewe upo, ukishagundua unatakiwa uanze mikakati ya kurudisha na sio kulalamika tu.  Unachotakiwa ni kujitia nguvu katika Bwana na kuanza kufatilia.

Isaya 42:22‘Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.’ 
Kwa hiyo kilichokosekana ni wa kusema rudisha, kwa hiyo kurudisha inawezekana ila ni hadi atokee wa kusema rudisha.

Isaya 22:18-19, 18 Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. 
19 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana? 

Hapa wanaongelewa wote waliookoka, si lazma uwe mchungaji ili kuwa mtumishi wa Bwana, hapana kuna majukumu tofauti tofauti.  Mfano imeandikwa aliwaita wengine kuwa manabii, mitume nk.  hivyo kila mtu ameitwa katika eneo lake.  Wengine wameitwa kuwa kinywa cha Bwana, kwamba kila anachotamka kinakuwa! Wengine ni mkono wa BWANA duniani akigusa kimeeleweka.  Na hakuna huduma kubwa kuliko nyingine, kama wewe umeitwa kwenye maombi, kazana hapohapo na BWANA atakutokelezea hapohapo. Kila mtu ana enzi yake(wito), kumbuka  malaika walioshindwa kuilinda enzi yao waliadhibiwa, Kwa hiyo jitahidi kulinda enzi yako.  Kuna wengine watasema mimi mbona sina enzi, ndugu unayo ila umeibiwa na leo tunakwenda kurudisha.  Kutokujifahamu kwako hakubadilishi chochote.

Resident Pastor Adriano Makazi

Kuna watu leo hii ni vyombo vya BWANA, lakini hawajijui na shetani amewateka na kuwatumia kwa kazi zake, mfano wachawi.  Shetani hashughuliki na watu wasio na kitu, anawachukua watu walioandaliwa na Mungu kwa jambo la maana kwa ajili ya ufalme wake (Mungu) na  kuwatumia katika kujenga ufalme wake(shetani).  Lakini tazama hekima ya Mungu ilivyo kubwa, anamruhusu shetani awatumie watu atakavyo halafu baadae anawaokoa na shetani anageukwa. Kupitia hao watu mbinu za shetani zinafahamika.  Na vita inakuwa rahisi mana majeshi ya BWANA yanakuwa yanajua mbinu zake ibilisi.

Mfano Paulo kwa asili alikuwa mtumishi wa Mungu, lakini shetani alimteka akawa anamtumia kuwaua  watakatifu wa BWANA, hadi BWANA alipomtokea na kumbadilisha Matendo 9:1-6 ‘1 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 
2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia … awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 
3 Hata alipokuwa akisafiri, ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. 
4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? 
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. 
6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda….

Sauli alivyokutana na BWANA, Yesu akamrudisha kwenye kusudi lake.  Na leo kila mmoja atakwenda kurudisha kusudi la BWANA katika maisha yake katika jina la Yesu.  Lakini linarudi kwa kupigana, yaani kupigana ni lazma.  Ni kwamba hujapigana hujamiliki!

Isaya 42:18, tutoke kwenye upofu, tumebaki kuridhika na hali mbaya tuliyonayo tukiona amani tu! Kumbe tuko vipofu! Hatuoni uhalisia.

Pastor David akimtumikia Bwana wa Majeshi kwa kinanda


 Luka 19:41,‘ Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 
42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 
43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 
44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.’
 Mambo yanaweza kufichwa machoni pako usiyaone, na inakuwa hasara kubwa sana lakini kama ungeona, ungetengeneza. Tunatakiwa tutambue majira ya kujiliwa kwetu.  Haya ndio yale majira Yesu anataka kurudisha heshima ya jina lake, majira ambayo  Yesu anataka kufanya falme za dunia ziwe zake. 
Isaya  anasema unaona mambo mengi lakini huyatii moyoni,  kwanini inakuwa hivyo ndo linapokuja swala la Isaya 42:22 kwamba huyu mtu anakuwa ameibiwa moyo, macho ndo mana anaona lakini hatii moyoni nk.

Kumbuka Samson, alikuwa na nguvu sana za rohoni na mwilini, ndo mana wafilisti walivyomkamata cha kwanza walimtoboa macho kabla ya kumfunga na kumtesa.  Hivyo cha kwanza shetani anapokuteka anakutia upofu ili anapokushughulikia wewe unaona amani tu mwisho unadumbukia shimoni.

 
Akina Daudi walivyorudi na kukuta mji wao umechomwa moto na kila kitu kimeibiwa hadi wakeze.  Wanaume wakaanza kulia hadi wakaishiwa nguvu lakini haikuwa suluhisho! Daudi akaona hili jambo suluhisho si kulia bali ni kuingia mbele za BWANA, kutafuta suluhisho, hata wewe ndugu yangu haijalishi una tatizo kiasi gani, wazazi , ndugu , marafiki , bunge na vyote hapa duniani haviwezi kukusaidia, muige Daudi kwa kumwangalia Yesu maana yeye ndiye mwenye funguo za mauti na kuzimu.   Daudi akaruhusiwa na BWANA aende na atarudisha vyote ndipo Daudi alipowaongoza wenzie na kwenda na hakika walirudisha vyote.

1Sam 30:1  ‘Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. ……………….  Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka………  Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.  Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye…….  Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 
18 Daudi akawapokonya wote waliokuwa wamechukuliwa na Waamaleki; naye Daudi akawaokoa wakeze wawili. 
19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote. ….’ 


Leo tunaenda kulifuatilia jeshi la shetani na kurudisha vyote, kwa msaada wa BWANA itawezekana.2 Samw 22:30  ‘Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi; Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. 
31 Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia..’.

Yoh 5:28 ‘..msistaajabie maneno haya kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 
29 Nao watatoka; ..   
yaani haijalishi shetani aliwapataje pataje, iwe kiuhalali au vinginevyo, mimi najua neno moja tu ‘NAO WATATOKA’

Isaya 49:24 ‘ Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? 25 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka;……’

Isaya 14:17  Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? 17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ’

Efeso 6:10 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 
Pastor Adriano akimuabudu Bwana.

unapoenda kupigana lazima uvae silaha.  Si kila silaha unaweza kuitumia kwa adui yako, lazima ujue yeye ana nini! Sio unaenda na kisu wakati mwenzio ana machine gun, atakushinda tu!  Lakini kumbuka vita yetu ni katika ulimwengu wa roho.Saturday, April 5, 2014

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA KUTUMIWA NA MUNGU KUIKOMBOA NCHI YA JAPAN KUTOKA MIKONONI MWA SHETANI

NI MUENDELEZO WA ZIARA KUBWA YA KUHUBIRI INJILI  DUNIANI KOTE NA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA ANAENDELEA KUTUMIWA NA MUNGU BABA WA MBINGUNI KATIKA VIWANGO VYA JUU SANA

Mchungaji Josephat Gwajima ameshafanya mikutano mikubwa ya Injili katika miji mbali mbali nchini Japani, miji hiyo ni Osaka, Nagawa, Hiroshima,na sasa ni Nagoya na bado Yesu Kristo aliyeishinda mauti anaendelea kutenda miujiza ya kupita fahamu za wanadamu nchi humo.

Yafuatayo ni matendo na miujiza mikubwa ambayo Mungu ameyatenda kupitia kwa Mchungaji Josephat Gwajima katika mwezi huu wa April,2014 nchini Japan


Mchungaji wa nchini Japan akimkaribisha Mchungaji Josephat Gwajima katika mkutano uliokuwa na Nguvu za Mungu za kupita kawaida, Jijini Nagoya nchini Japan

Mchungaji Josephat Gwajima akianza kuhubiri na kushoto kwake ni mkalimani ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Japan


Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na mkalimani atafsirie kiingereza kwenda kijapani...


Baadhi ya wachungaji na washirika wakiwa wanamsikiliza Mchungaji Josephat Gwajima kwa umakini....


Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anafundisha mjini Nagoya,Japan

Mungu Baba yetu wa Mbinguni hukaa mahali pa Sifa na hapa kila mmoja aliyekuwa katika ukumbi aliweza kububujika kwa Bwana na kumtukuza Bwana wa Majeshi


Nchi ya Japani imejaliwa watu wa Mungu wenye kusifu sana...
Roho Mtakatifu akiwa anatenda kazi
Ukafika muda ambao Roho Mtakatifu kujidhihirisha kwa nguvu na mamia ya watu waliojazana ukumbini kunena kwa Lugha, wengine kudondoka na vifungo vilikatika kabisa kwa Jina la Yesu.


ROHO WA BWANA ALIKUWA JUU YA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA NA MUNGU ALIMTUMIA KATIKA UPONYAJI KWA KIWANGO CHA JUU SANA 

KARIBU USHUHUDIE MATUKIO HAPA CHINI YA JINSI WATU WALIVYOKUWA WANAFUNGULIWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO MBALI MBALI


Mama huyu hapa juu alikuja kwenye mkutano jijini Nagoya akiwa hawezi kutembea, wakati wa maombezi nguvu za Mungu zilishuka juu yake kwa namna ya kipekee na akaweza kutembea tena
UTUKUFU KWA YESU


Mtu wa Mungu aliyekuwa katika mkutano akimsifu Mungu Baada ya kuweza kunyanyuka na kutembea

Kiti cha matairi alichokuwa anakitumia mama huyu
Akimsifu Mungu Baada ya kuweza kutembea na kuachana na kiti baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima

Mpiga vyombo akiwa anaombewa na Mchungaji Josephat Gwajima.Watu wa Mungu waliokuwa na matatizo mbali mbali na wakisumbuliwa na mapepo, pichani wako katika kuendelea kupokea uponyaji wao.Mchungaji Gwajima akiwaombea watu mbalimbali na hapa mapepo yaliyokuwa ndani ya mtu yakijaribu kuomba msamaha...lakini Moto wa Mungu uliwateketeza bila huruma.
Mapepo yaliyokuwa ndani ya mtu huyu, yalisalimu amrina kumtokaBaada ya Nguvu ya Mungu kushuka wengi walifunguliwa kutoka katika vifungo walivyokuwa navyo na shetani aliwaacha huru kabisa watu wa Mungu.

Mchungaji Josphat Gwajima akimwombea Mchungaji wa nchini Japan.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea mamia ya watu Baraka za Mungu..


Kijana aliyekuwa anasumbuliwa na shetani na hapa alikuwa anaombewa na Mchungaji Jospehat Gwajima
Dada wa kijapani ambae aliacha shughuli alizokuwa anazifanya ili kupata uponyaji,kutoka  kwa Mchungaji Josephat Gwajima na aliwekwa huru kwa Jina la Yesu.


Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, Mkiwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Ufufuo na Uzima tumekuwa tukiendelea na semina za kuwafundisha wachungaji wa mjini Nagoya Japan na mikutano ya watu wote iliyokuwa na mafanikio makubwa. Utukufu wa Mungu ulidhihirika kwa namna isiyokuwa ya kawaida.           

Mchungaji Grace Gwajima akiwa katika mkutano wa Injili nchini Japan.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwaongoza mamia ya waliofika katika mkutano Jijini Nagoya, nchini Japan
Mchungaji Josephat Gwajima akiendelea na mkutano katika Jiji la Nagoya....
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anendelea kufundisha katika mkutano uliofanyika katika Jiji la Nagoya

Mamia ya watu waliofika mkutanoni

Mchungaji Gwajima akimuombea na kumfungua mtu wa Mungu aliyefika mkutanoni
Mchungaji Msaidizi Grace Gwajima
Mchungaji Josephat Gwajima akihitimisha Mkutano wa Injili jijini Nagayo Japan, na tayari kuelekea Katika Jiji la kibiashara la Tokyo ambalo ni kitovu cha nchi ya Japan
Mchungaji Grace Gwajima akiwa na Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa huko Nagayo nchini Japan