Thursday, April 3, 2014

PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA ANAENDELEA NA MIKUTANO MIKUBWA YA INJILI DUNIANI KOTE,AMEANZIA BARA LA ASIA.

MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA GLORY OF CHRIST (T) CHURCH - UFUFUO NA UZIMA ANAENDELEA NA MIKUTANO MIKUBWA YA INJILI NA YA KIHISTORIA KUFANYIKA KATIKA BARA LA ASIA


Pastor Josephat Gwajima akiwa na Mchungaji Msaidizi Grace Gwajima wakiongozana na baadhi ya watendakazi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wapo katika bara la Asia nchini Japan, ambapo waliondoka Tanzania Tarehe 16 mwezi wa 3 mwana huu 2014 na kuanza kufanya mikutano mikubwa na ya kihistoria ya Injili kufanyika katika nchi ya Japan.

Ikiwa ni mwendelezo wa Mchungaji Josephat Gwajima kupokea mialiko mingi  kila mwaka kutoka nchi mbali mbali na hasa Japan, ila mwaka imekuwa ni bahati kwa watu wa Mungu wa Japan kwa sababu ameanza kuwatembelea wao mwanzo wa mwaka ambapo pia kuna tawi la kanisa la Ufufuo na Uzima na anategemea kuwa na mikuano zaidi ya sehemu ishirini katika nchi ya Japan.
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anahubiri katika Jiji la Hiroshima nchini JapanMandhari ya Jiji la Hiroshima, maarufu kama "wide Island"  ni Jiji kubwa katika maeneo ya Chugoku magharibi mwa Honshu, hili ndilo jiji la kwanza katika historia kupigwa kwa mabomu ya nuclear mnamo Tarehe 6/08/1945 na majeshi ya MarekaniBaadhi ya watu wa Mungu wa nchini Japan ambao ni washirika wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Japan, wakiwa na furaha kubwa kummpokea Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima na Mchungaji Msaidizi Grace Gwajima.

Maombi na uponyaji na watu kufunguliwa kwa Jina la Yesu Kristo

Mchungaji Gwajima akifundishaMchungaji Gwajima akiwa anawaombea watu mbalimbali
Mkazi wa Hiroshima aliyekuwa anasumbuliwa na mapepo yanayosababisha matatizo ya njia ya upumuaji ila akapona baada ya kuombewa kwa Jina la Yesu Kristo na Mchungaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima akimuombea mkazi wa jiji la Hiroshima ambaye alikuwa akisumbuliwa na mapepo yaliyomsababishia maradhi kwa kipindi kirefu.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na mshirika wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Japan

Baadhi ya matangazo yaliyotapakaa katika kila kona ya mji wa Japan.Mchungaji Josephat Gwajima muombea mlemavu wa mguu kwa Jina la Yesu.Mchungaji Josephat Gwajima akiongoza maombi ya ukiri huku akiwaombea watu na kuwafungua kutoka katika vifungo vya Ibilisi.


Mchungaji Josphat Gwajima ameshafanya mikutano mikubwa ya Injili katika miji mbali mbali nchini Japani, toka Tarehe 16.03.2014  hadi sasa miji hiyo ni Osaka, Nagawa, Hiroshima,na sasa ni Nagoya na bado Yesu Kristo aliyeishinda mauti anaendelea kutenda miujiza ya kupita fahamu za wanadamu nchi humo.


Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anahubiri katika jiji la Osaka nchini Japan.Baadhi ya washirika wa Ufufuo na Uzima Japan na watu mbalimbali wakiwa katika maombi makali ya kumlazimisha shetani atoke na watu wa Mungu wawe huru kwa Jina la Yesu.

Shetani amewaachia watu wa Mungu bila kupenda kwa Mchungaji Josephat Gwajim kuliitia jina la Yesu Kristo.

Maombi ya ukiri yanayoongozwwa na Mchungaji Josephat Gwajima


Watenda kazi wa Bwana nchini Japan
Pastor Josephat Gwajima ndani ya Nchi ya Japan.


Pastor Josephat Gwajima

Maelfu waliopita mbele kukabidhi maisha ya kwa Yesu na kuombewa

Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anahubiri kwa Kiingereza na anayeonekana pembeni ni mtafasiri anayetafasiri kwa kijapaniMaelfu ya watu wa Mungu wakiwa wanapita kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima.Mchungaji Jospehat Gwajima akiwa anawabariki na kuwaandikia ushindi kwa Jina la Yesu wakazi wa mji wa Nagawa.


No comments:

Post a Comment