Sunday, June 8, 2014

MAKUHANI WA KICHAWI WATEKETEA NA KUNYONGWA KABISA NA MAHALI PAO HAPAJAONEKANA TENA.


IBADA YA TAREHE 08_06_2014
Kuwaangamiza Makuhani wa Kichawi
 Na Mchungaji Josephat Gwajima
Utangulizi
Zaburi 116:1-19

Mambo muhimu yanayoambatana na madhabahu ni
Madhabahu, Kafara ya madhabahu, kuhani wa madhabahu, Mungu wa madhabahu na nguvu ya madhabahu.Utaona kwenye biblia watu wengi wa  Mungu mfano Ibrahimu, Nuhu na Yakobo walitengeneza madhabahu ili wapate kukutana na Mungu. Eliya alipoitengeneza madhabahu ya Yehova iliyokuwa imevunjika , Eliya alikuwa  kuhani wa madhabahu na ng’ombe aliyemchinja alikuwa kafara ya madhabahu na moto uliotoka madhabahuni ndiyo nguvu ya madhabahu na Mungu wa madhabahu alikuwa Yehova.  Hivyo Mungu hawezi kutenda kazi isipokuwa kwa kupitia watumishi wake manabii, wachungaji, wainjilist, mitume.  Shetani naye vile vile hawezi kutenda kazi mwenyewe kwa maana yeye ni roho kwa hiyo lazima atumie watumishi wake wachawi , waganga, wasoma nyota , wafuga majini , watabiri na madarueshi.
Madhabahu ni daraja au kiunganishi kutoka ulimwengu wa roho kwenda ulimwengu wa mwili au kutoka ulimwengu wa mwili kwenda ulimwengu wa  roho. Na kuhani anapokuwa madhabahuni  anabeba vitu kutoka ulimwengu wa roho na kuvileta ulimwengu wa mwili kwa watu. Hata bwana Yesu alipokuwa  msalabani kalvari alifanyika kafara/sadaka na damu yake ilipomwagika pale kalvari inaendelea kunena hata sasa kwa hiyo kalvari ikafanyika madhabahu  ya wokovu. Kwa hiyo kila damu inayomwagwa huwa inanena maana imeandikwa na damu ya Yesu kristo mjumbe wa agano jipya inenayo mema kuliko damu ya Abili ineneayo kisasi. Hii inatudhihirishia kuwa katika dunia hii zipo kafara nyingi za damu  zinazotolewa na wachawi lakini  tunaposema damu ya Yesu inaharibu kafara zote.
Utaona kwenye historia sehemu zote ambazo ukristo ulianzia kwa sasa sehemu hizo ndiyo makao ya shetani, kwa mfano bustani ya Eden Mungu alipokuwa anatembea wakati   wa jua kupunga kwa sasa  mahali pale  ndiyo Iraq ya sasa yaani ni ngome ya Uislam. Dameski mtume Paulo alipokuwa anaenda kuwakamata walokole safi kwa sasa mahali pale kunaitwa Siryia yaani nchi ya kiislam .  Ufunuo 1:2-6, utaona mahalii ambapo kulikuwa na makanisa saba ambayo mtume Paul aliwaandikia waraka kwa sasa mahali pale panaitwa Uturuki yaani nchi ya kiislam. Sasa unaweza kujiuliza kitu gani kilitokea mpaka mahali patakatifu kukageuzwa kuwa ngome za majini na Uislaam. Hii  ni kwa sababu shetani alifanya  ya hila ya kuwainua watawala ambao ni makuhani wake ili watende kazi  na hatimaye watokomeze ukiristo na ushetani (uislaam) Ukaimarika. Uislaam unaendana na ushetani kwa maana imeandikwa  kila Roho isiyokiri kwamba Yesu Kristo ni bwana haitokani na Mungu  kwa hiyo maeneo yote yanayoongozwa na uislaam ni ngome za kishetani. 
Utaona hata mahali pale Yesu alipozaliwa Bethelehem na kupelekwa Misri ili asiuawe na Herode na huo ulikuwa unabii ya kuwa wakati wa mwisho injili ya uamsho ya kuokoa ulimwengu mzima dunia itaanzia Africa, lakini sasa utajiuliza mahali pale ambapo Yesu alillewa na sasa imekuwa nchi ya kishetani (Kiislam). Utaona pia mahali alipozaliwa Yesu Bethelehem kwa sasa mahali pale ni nchi ya Waparestina yaani waislam. Yote haya yalitokea kwa sababu shetani aliyateka maeneo hayo na kuyatawala kwa kujenga madhabahu zake na kuwaweka makuhani wake. Utaona  pia rais  wa Uingereza , King James ndiye alitafsiri kitabu cha King James version , hii ina maana kuwa nchi yote ilikuwa chini ya ukristo lakini sasa shetani anatawala mpaka kuna ndoa za  jinsia moja pale. Misri  pia ilikuwa nchi ya kikristo lakini alipoingia rais mmoja kuhani wa kishetani alitoa amri kuwa hakuna kukarabati wala kujenga kanisa kwa hiyo makanisa mengi yakaharibika na kuisha wakati huo misikiti ikaongezeka kila mahali.
Lakini  tunaamini na kutumaini  kwamba ukristo ni dini ya kurudisha  kama Mungu wetu alivyo Mungu wa kurudisha kwa mfano aliwarudisha wana wa Israel kutoka utumwani Misri , aliwarudisha wayahudi kutoka utumwani Babel na alimrudisha Yesu kutoka Misri  alipofariki mfalme Herode. Kwa hiyo maeneo yote yaliyotekwa na shetani yatarudishwa kwa jina la Yesu na kila kitu kilichotekwa na kuibiwa kwenye maisha yetu leo kinarudishwa kwa jina la Yesu.
Shetani alifanikiwa kuyateka maeneo matakatifu na kuyageuza kuwa ngome zake kwa kuwatumia makuhani wake yaani wachawi na wasoma nyota. Hata leo kwenye maisha yako inawezekana kuna makuhani wa kishetani waliotumwa kuharibu maisha yako, lakini leo tunaamuru moto kutoka mbinguni na kuwala wote kama Eliya alivyoamuru moto kutoka mbinguni ukawala wale wajumbe hamsini walitumwa na mfalme ili wamkamate.
Ili kazi ya Mungu iende vizuri lazima wawepo makuhani wa Mungu ili wanapozungumza ni kama Mungu amezungumza, wanapobariki ni kama Mungu kabariki. Shetani naye anatenda kazi kupitia makuhani wake yaani wachawi , waganga nakadhalika. Kwa mfano mtu anaweza kuwa anamchukia mtu na akaamua kwenda kwa kuhani wa shetani yaani mganga na kumwambia nitengenezee mambo na mtu Fulani aharibikiwe kwa hiyo kuhani anatuma mashetani na yule mtu matatizo yanampata  Matendo 13:6-8
1krintho 4:20, Ufalme wa Mungu hauwi katika maneno bali unadhihirishwa katika nguvu, kwa hiyo  leo tunatumia nguvu ya jina la damu ya Yesu kuwaharibu makuhani wa kishetani na baada ya hapo maisha yetu yataenda vizuri .Shetani ana namna mbili ya kumshambulia  mtu Anaweza kumshambulia mtu akiwa nje ya mtu Zekaria 3:1-4, 1thesalonike 2:19, Anaweza kutenda kazi akiwa ndani ya  mtu yaani kumpagaa. .
Maombi
 Kwa damu ya Yesu ewe baba Mungu naomba msahaha kwa jambo lolote nililotenda likamfanya shetani anishambulie. Kwa jina la Yesu Nafunga milango yote ambayo shetani alikuwa anatumia kuja kinishambulia , nafunga milango ya hasira ,kiburi, laana za ukoo kwa jina la Yesu. Kwa mamlaka ya jina la Yesu namteketeza kila kuhani wa giza anayefanya vita na maisha yangu, nawafyeka mashetani wote  na wakala wa laana zote kwa jina la Yesu.
Kwa jina la Yesu mtu yeyote katika familia yetu anayejihusisha na uchawi  leo namfyeka kwa jina la Yesu. Mtu yeyote anayefanya uchawi kwenye maisha yangu namfyeka kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu mtu yeyote kwenye familia  yangu anayetumiwa na shetani kunileta magonjwa , balaa au mikosi leo namfyeka kwa jina la Yesu. Imeandikwa mimi ni rungu la bwana kwa hiyo natangaza leo mtu yeyote aliyetuma mashetani  wa ,aibi, umasikini namvunja kwa jina la Yesu .  Naharibu kazi ya kuhani mwanamke, Mtoto, kijana kwa jina la Yesu . Nabomoa madhabahu zote zilizojengwa ili kuharibu biashara yangu, kazi  yangu ,watoto wangu .Imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa, kwa jina la Yesu sila ya mauti, ajali, kukataliwa kushindwa hazitofanikiwa zote kwenye maisha yangu kwa jina Yesu.
Kwa damu ya Yesu leo nawazunguka watu wote wanaonihusu ili wasishambuliwe na nguvu za giza ili  kila jini aliyetumwa kuniharibia mipango yangu  kupitia watu  hao asipate mlango kwa jina la Yesu. Imeandikwa hakika hakuna uchawi juu ya Yakobo wala uganga juu ya Yakobo nami nakataa kufa kwa jina la Yesu Imeandikwa sitakufa bali nitaishi nakataa kufa  kwa magonjwa, ajali au sumu  kwa jina la Yesu.
Kwa jina la Yesu kila mtu aliyepanga vita juu yangu namshinda kwa jina la Yesu, aliyepanga vita ya uchawi au akilia namfyeka kwa damu ya Yesu. Natwaa mamlaka ya kuharibu nguvu na uwezo wa giza kwa jina la Yesu. Imeandikwa hivyo Mungu alimwadhimisha mno akamkirimia jina lipitalo majina yote kwa jina la Yesu nawateka nyara makuhani wote wa giza na majeshi yao nawaponda kwa jionala yesu. Nawateketeza watu wenye nia mbaya na taifa letu la Tanzania naziharibu madhabahu zao na kafara zao naziharibu kwa damu ya Yesu. Kila kuhani wa ibilisi aliyetumwa kusimama kwenye taifa la tanzania leo natumwa moto ikilu, kwenye bunge na baraza la mawazirin na kumteketeza kwa jina la Yesu. Kila nguzo za ufalme wa giza leo tunaziharibu kwa jina la Yesiu. Moyo wa kishetani waliovaa na nia zao leo tunazipurura kwa jina la Yesu. Imeandikwa Mungu wetu na Mungu wa vita kwa jina la Yesu leo natangaza vita katika ulimwengu wa roho na kuwafuata majeshi yote ya giza. Imeandkiwa amelaaniwa kila mtu hauzuiaye upanga wake kumwaga damu kwa jina la Yesu leo nautoa upanga Alani na kuwafyeka wachawi, mapepo mizumu kwa jina la Yesu.
Kila kuhani aliyetumiwa kuharibu maisha yangu namtekeketza  imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, silaha ya balaa, silaha ya magonjwa, ajali, mauti hazitafanikiwa kwa jina la Yesu , leo nimeshindana na nimepenya  na kuingia katika Baraka zangu kwa jina la Yesu.
        AMEEN..

No comments:

Post a Comment