Sunday, June 1, 2014

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA AONGOZA MAELFU YA MAJESHI YA BWANA KUWATEKETEZA WACHAWI, KATIKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA


WALIOKUWA WACHAWI WAFICHULIWA NA KUITUPA MIKOBA YA UCHAWI KATIKA IBADA YA LEO JUMAPILI, KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
 
Somo: Kuwaangamiza Makuhani wa Kichawi


            1Falme 18:15-30,1Falme 19:15-22,2 Falme 10:1-15

Kwenye biblia Mungu  anawachukia sana wachawi, imeandikwa usimwache mwanamke mchawi kuishi, makuhani wa kichawi ndiyo hao unaweza kuwaita wataabishaji.  Mungu ni roho kwa hiyo hawezi kutenda Kazi kwa wanadamu hivyo huwatumia watu ili kutenda kazi ambao ni makuhani wa Yehova, Shetani naye ni roho naye anatenda kazi kwa kutumia watu ambao ni wachawi, waganga, madarueshi na wanajimu  ambao tunawaita makuhani wa shetani.

Utaona hata Mungu alipotaka kuja duniani alivaa mwili  akazaliwa kama mwanadamu Yesu Kristo. Kwa hiyo hata shetani anakuwa na nguvu pale anapokuwa amevaa mwili. Mungu aliagiza wachawi wapigwe kwa mawe lakini leo tunayo njia ambayo tunaweza kuwaangamiza wataabishaji wa watu (makuhani wa shetani) na mawe hayo ni neno la Mungu kwa maana imeandikwa neno la Mungu ni nyundo ivunjayo mawe vipande vipande.

 

        II.            SOMO

1Falme 18:15-30 , Eliya aliwakusanya makuhani wa baali mia nne na makuhani wa ashera mia nne hamsini akawapeleka mlima karmeli ili watoe sadaka kwa Mungu wao baali  naye atoe sadaka kwa Mungu wake Yehova ili Mungu atakayejibu kwa moto ndiye awe Mungu  wa Israel kwa maana nyakati zile watu walikuwa hawawezi kumjua Mungu wa kweli. Lakini makuhani wa baali walimwita mungu wao wala hakujibi, ilipofika jioni ikawa zamu ya Eliya, ndipo Eliya alipoitengeneza madhabahu ya Yehova iliyokuwa imevunjika na akaweka mawe kumi na mbili kulingana na kabila kumi na mbili za Israel. Baada ya hapo alichinja ng’ombe  awe kafara na akaimwagia maji mapipa manne halafu akaomba baba Yehova leo ujulikane kuwa ni Mungu, ndipo moto uliposhuka ukairamba sadaka na watu wote wakasema Yehova ndiye Mungu.  Baada ya hapo Eliya akawachinja makuhani wote wa baali na ashera na jumla yao ni mia nane na hamsini kwa maana alijua wakibaki hai wanaweza kujenga madhabahu ya baali na kuendeleza uchawi wao.  Na leo kwa jina la Yesu tunawakusanya wachawi wa pande zote waliotesa maisha yetu na kuwapiga wote.

      III.            ILI MUNGU ATENDE KAZI ANAHITAJI MAMBO YAFUATAYO:

·         Madhabahu (Isaya 19:14-15) Eliya alitengeneza madhabahu kwa maana Mungu hawezi kushuka bila kuwepo madhabahu yake kwa maan nyakati zile madhabahu ya Yehova ilikuwa imevunjwa na madhabahu ya baali ilikuwa imeimarishwa.

·         Kuhani  wa madhabahu,ni mtu anayesimama kama wakili wa Mungu ,Eliya alikuwa kuhani wa Yehova.

·          Kafara ya madhabahu , Eliya alichinja ng,ombe kama kafara ya madhabahu.

·         Mungu wa Madhabahu, Eliya alikuwa anamwabudu Mungu Yehova kwa hiyo Yehova ndiye aliyekuwa Mungu wa madhabahu ya Eliya aliyoitengeneza.

·         Nguvu ya madhabahu,  Eliya alipoomba moto ulishuka, moto ulioshuka ndiyo nguvu ya madhabahu     IV.            ELIYA KABLA YA KUPAA ALIWATIA MAFUTA WATU WATATU ILI WATENDE KAZI PAHALA PAKE

1Falme 19:15-22, Mungu alimwambia Eliya kabla hajapaa awatie mafuta  watu watatu ambao  watasimama badala yake, alimtia mafuta Yehu awe mfalme wa Israel, alimtia mafuta   Elisha awe nabii badala yake na  alimtia mafuta Hezael awe mfalme wa Yuda ili mchawi yeyote atakayepona kwa upanga wa Hezael upanga waYehu au Elisha hautamkosa. Hii inatufundisha kuwa Mungu ni Mungu wa mipango madhubuti kwa ajili ya kazi na watu wake hivyo huwainua manabii na watumishi wake kizazi hata kizazi ili ufalme wa giza ubomolewe kabisa.

2 Falme 10:1-15, mfalme Yehu alipoanza kutawala akawaagiza watumishi wake wamletee vichwa sabini vya wana wa Ahabu (mchawi) kwenye kikapu. Hii inatufundisha kuwa Mungu hapendi kabisa wachawi na leo kwa jina la Yesu katika ulimwengu wa roho tunaamuru vichwa vya wachawi vifyekwe mahali popote na kuletwa hapa na baadaye tunaviteketeza kwa moto kwa jina la Yesu.

2Falme 10:18-28 ,Baada ya hapo mfalme Yehu aliamua kuwaangamiza makuhani wote wa baali akapanga hila na kusema , mimi nimeamua kumtumikia baali hivyo nawaomba makuhani wate wa baali mkusanyike pamoja ili tumfanyie baali ibada na kafara, walipokusanyika ndipo alipoamuru wachinjwe wote na hivyo akawakomesha makuhani wa baali katika utawala wake.  Na baada ya kuwaangamiza makuhani wa baali akaivunja madhabahu ya baali na mahali pale akapafanya kuwa choo mpaka leo. Hii inatufundisha kuwa Mungu hapendi kabisa wachawi waishi katika maisha ya watu wake, na leo kwa jina la Yesu katika ulimwengu wa roho tunawakusanya wachawi wote, waganga, madarueshi, wafuga majini na wanajimu na tunawachinja wote na kuwaangamiza wote kwa jina la Yesu, na madhabahu zao tunazibomoa na  viwanja vyote wanapokusanyika wachawi  tunavigeuza kuwa jalala kwa jina la Yesu.

Namna ya kumwangamiza mtu anayetaabisha maisha yako  kwa mfano mtu unayemwota sana kwenye ndoto anakufanyia vimbwanga au ambaye moyo wako unakushuhudia kuwa Fulani ndiye anayekutesa basi  ili umwangamize lazima umtaje kwa jina  lake ukisema Fulani leo nakuangamiza kwa jina la Yesu.

       V.            MAOMBI

Kwa jina la Yesu waliofunga biashara yangu, promosheni yangu, ndoa yangu, fedha zangu leo nawakusanya kama Eliya alivyowakusanya makuhani wa baali na kuwachinja nami leo nawakusanya na kuwaangamiza kabisa. Leo napenya na kupita katikati ya wachawi wote kwa maana katika ulimwengu wa  roho  nimebeba silaha za  Mungu.

Leo napambana na kazi za kishetani, Mtu yeyote aliyetesa maisha yangu namwangamiza kabisa kwa jina la Yesu. Leo nafanya vita na mwanadanu yeyote anayetumiwa na shetani kuharibu maisha yangu kwa jina la yesu. Kila mapango, vibanda na ngome vya kichawi leo navibomoa na nyota yangu iliyofichwa humo itoke kwa jina la Yesu.  

Kwa damu ya Yesu naamurisha kila aliyenifunga mimi ajulikane sasa, ninawakusanya wanawake , wanaume, watoto na vijana wachawi na leo ndiyo mwisho wao nawafyeka wote kwa jina la Yesu. Nawakusanya kwenye ulimwengu wa roho walionizuia nisiolewe, walionizuia nistajirike, walionizuia nisisafiri nawakusanya kutoka bahari, angani na kwemye mapango yao na leo nawaangamiza wote kwa jina la Yesu. Nawakusanya wote waliofanya vita na familia yangu, nawakusanya wote walionifanya nikataliwe wote nawaleta hapa na kuwaangamiza kwa jina la Yesu.
Maelfu wakiwa katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima


Namkusanya mjomba, shangazi , dada mkubwa,kaka mkubwa, mama wa kufikia, jirani yangu,boss wangu kutoka kijijini na mahali popote walipo na leo nawateketeza kwa jina la Yesu. Nawakusanya walionifanya nisifanikiwe, walionipaka matope usoni ili nikataliwe, nawakusanya wachawi wote kwenye mikoa yote ya Tanzania na kuwaleta hapa na nawakata nguvu zao, nawafyeka wote kwa damu ya Mwanakondoo.

Kwa jina la Yesu ikiwa ndani yangu imewekwa roho ya uchawi bila mimi kujua naamuru vunjika ewe roho ya uchawi kwa jina la Yesu. Alama zozote za kichawi zilizowekwa kwangu leo nazifuta kwa damu ya Yesu. Leo nakuteka nyara ewe mchawi mkuu wa Tanzania na silaha zake zote nakufyeka kwa jina la Yesu. Nawakusanya wachawi wote waliowekwa kusimama kinyume na kanisa na kazi ya Mungu  nawafyeka wote kwa jina la Yesu.

AMENI

Taswira ya Ibada ya leo Jumapili 1 Juni 2014 ndani ya nyumba ya Ufufuo na Uzima Kawe Tanganyika Packers

No comments:

Post a Comment