Sunday, June 15, 2014

MIMI SIO KAMA WALE.IBADA YA JUMAPILI TAREHE 15-06-2014

SOMO: MIMI SIYO KAMA WALE


mchungaji kiongozi Josephat Gwajima
NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
Utangulizi
Zaburi 118: 1-29 (sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo ya Bwana)
I.                    Somo
Maandiko ya msingi  Luka 4:14- 24, Daniel 5:2 -26
Bwana Yesu siku moja alikwenda kwenye sinagogi mahali alipozaliwa na pale alipewa chuo cha nabii Isaya ili asome na aliposema “ Roho wa bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta,  aliposema maneno haya yametimia leo wayahudi walikasirika sana wakamtoa Yesu ili wamtupe kwenye ukingo wa mlima na kumwua. Wayahudi walikuwa wamewatupa watu wengi kwenye ukingo lakini Yesu alipofika pale ukingoni alipita kataikati yao kwa maana yeye siyo kama wale ambao walikuwa wakitupwa. Hii inatufundisha kuwa hata wewe mtu uliyeokoka huwezi kupata madhara ya maadui zako kwa maana mtu aliyeokoka ni tofauti na wengine, kwa hiyo uchawi, mitego na majungu ya adui zako  hayana nguvu juu yako kwa jina la Yesu.
Leo tunawatangazia adui zetu wote kwamba yale waliyowafanyia wengine hawawezi kutufanyia kwa maana  sisi siyo kama wale kwa hiyo  mambo yao hayawezi kutupata kwa jina la Yesu. Sisi  walokole wa kizazi cha sasa siyo kama wale walokole wa kale walipopigwa shavu moja wakageuza na lingine, waliponyang’anywa kanzu wakatoa na Joho sisi ni watu tofauti tumetumwa kutenda na kutimiza kusudi la Mungu mpaka ulimwengu mzima wajue saa ya Ufufuo na Uzima, kwa hiyo hakuna wa kutuzuia hata kama wamedondosha na kukatisha tamaa wengi lakini sisi siyo kama wale , sisi tunazidi kusonga mbele kwa jina la Yesu.
mchungaji kiongozi kazini
Wayahudi waliposikia Bwana Yesu anasema Roho wa Bwana yu juu yangu walifadhaika sana kwa maana walijua maana ya Roho wa Bwana kuwa juu ya mtu. Roho wa bwana na anapokuwa juu ya mtu , mtu Yule anakuwa na uwezo mkubwa wa kutenda lolote kama ilivyoandikwa Roho wa Bwana akamjia Samson naye akawaua wafilist maelfu, Imeandikwa tena roho wa bwana aliopokuwa juu ya Daud alimwua Goliath kwa hiyo aliposema hivyo walisema huyu naye atapiga mtu . Vile vile aliposema Bwana amenitia mafuta walitafakari kuwa watu wanaotakiwa kutiwa mafuta ni Nabii, Mfalme, Kuhani na Vyombo vya Hekalu. Kwa hiyo waliogopa kwamba mafuta yale labda anataka kuwa mfalme , au nabii kwa hiyo wakaona shaka na kuamua kumtupa ukingoni ili wamwuue na kusudi la mafuta yale lisitimie lakini Yesu alipita katikati yao. Leo nakutangazia mtu uliyeokoka mabaya waliokuandalia adui zako hayatatimia lakini kusudi la Mungu litatimia kwako kwa jina la Yesu.
Vyombo vya hekalu huwa havichezewi kwa maana vimetiwa mafuta, imeandikwa kwenye Daniel 5:2 -26 mfalmwe wa Babeli alipotumia vyombo vya hekalu kwa ajili ya kunywea kwenye sherehe Mungu alikasirika na kumwandikia maneno yafuatayo kwenye ukuta MENE MENE TEKELI NA PERESI, maana yake ufalme wako umepimwa na kuonekana umepungua kwa hiyo amepewa mwenzako.  Kwa hiyo mtu uliyeokoka ni chombo cha hekalu na yeyote anayekuchezea anakatiliwa mbali na wengine wanachukua mahali pao kwa jina la Yesu. Tunawatangazia hata viongozi wa Tanzania wanaowachezea watumishi wa Mungu kuwa ufalme wao umepimwa na kuonekana umepungua kwa hiyo watapewa wenzao.
Wayahudi walifadhaika pia Yesu aliposema kuwa nimetiwa mafuta kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao. wayahudi walikasirika sana kwa maana ndani ya hekalu kulikuwa na watu ambao wamewafunga watu kwenye magereza ya kiroho yaani kwemye magonjwa, balaa, mikosi umasikini nakadhalika. Kwa sababu  tabia za shetani ni kuwafunga watu  bila kuwaachia kwenye magereza yake kama ilivyoandikwa  Isaya 14:17-18, Matendo 27:42 .  kwa hiyo shetani na wakala wake walikasirika sana waliposikia Yesu anataka kuwafungua watu kutoka kwenye magereza ya mateso. Mungu naye mpango wake ni kuwaweka huru wafungwa kama ilivyoandikwa kwenye  Yeremia 33 : 7, Zaburi 68:6, Ezekiel 16:53 Hosea 6:11,Nami kama mtumishi wa Mungu leo nawatangazia wafungwa wote kufunguliwa kwao, wafungwa wa magonjwa, wafungwa wa balaa, wafungwa wa madeni, wafungwa wa umasikini, wote nawatangazia uhuru leo kwa jina la Yesu.
Wayahudi walifadhaika pia Yesu aliposema kuwafanya vipovu wapate kuona tena, wayahudi walikuwa wamewatia upofu watu wengi ili wafuate desturi za mafarisayo bila kuona hatima yao.kwa hiyo  Yesu alipotangaza kuwafungua vipofu walikasirika sana kwa maana walijua udhalimu wao utadhihirika mbele za watu . Nami mtumishi wa Mungu nawatangazia vipofu wa kiroho waone tena , naondoa kila utando ulioweka kwenye macho ya watu ili wasione kwa jina la Yesu. Nawatangazia Watanzania wote waliokuwa wametiwa upofu hata wasijue kinachoendelea kwenye nchi yao naamuru waone tena na wajua hatima ya nchi yao kwa jina la Yesu.
Wayahudi walifadhaika pia Yesu aliposema nimekuja kuwaweka huru watu waliosetwa, maana desturi ya mafarisayo ilikuwa kuwaseta (kuwagandamiza) watu na kuwaweka chini ili wao wawe juu.
Nami mtumishi wa Mungu nawatangazia kuinuliwa watu wote waliogandamizwa na magonjwa, umasikini, madeni kwa jina la Yesu.
Wayahudi walikasirika aliposema kuwa amekuja kuutangaza mwaka wa Bwana, kwa maana wayahudi walikuwa na mwaka wa maachilio lakini walikuwa hawaachilie kama ilivyo .kwa hiyo Yesu aliposema kutangaza maachilio ya wale wakosaji walikasirika sana. Nami mtumishi wa Mungu nawatangazia msamaha  watu wote waliofungwa kwa sababu ya shida zao kwa jina la Yesu.
maelfu wakiwa ndani ya bonde la kukata maneno
II.                  Ukiri
Kwa jina la Yesu , Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri masikini habari njema,kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa na kuutangaza mwaka wa bwana uliokubaliwa.
III.                Maombi
Kwa damu ya Yesu najitakasa, Bwana naomba upako wa kufanya vita dhidi ya wale waliotaka nitumbukie kwenye mashimo ya uharibifu kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu nawateka na kuwatumbukiza wao kwenye mashimo waliyoyaandaa kwa ajili yangu kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu naamuru mtu yeyote aliyeandaa shimo la mauti, magonjwa ajali na mikosi  atumbikie mwenyewe kwa jina la Yesu.
 Imeandikwa kila achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe , naamuru mashimo yote waliochimba adui zangu watumbukie wenyewe kwa jina la Yesu. Ninakataa kutumbikia kwenye shimo waliloliandaa kwa ajili yangu au watoto wangu kwa jina la Yesu, nawatangazia adui zangu kuwa  mimi siyo kama wale waliofanikiwa kuwatumbukiza, nakataa kutumbukia kwenye shimo la magonjwa, balaa, mikosi  umasikini na mauti, nakataa kuangamia nakataa kuteketea kwa mitego na mashimo yao kwa jina la Yesu.
Imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa, Katika jina la Yesu nawasukumia nyie kwenye Mashimo ya mauti mliyoyachimba, naamuru silaha zote za maangamizi mlizonitengeneza kwenye ulimwengu wa roho ziwanase wenyewe kwa jina la Yesu. Imeandikwa sitakufa bali nitaishi nami niyasimulie matendo ya Mungu,  nakataa kufa kwa ajali, magonjwa kuvamiwa au kunyweshwa sumu kwa jina la Yesu. Naamuru mashimo yote ya mauti yaliyotengezwa kwa ajili yangu yawameze adui zangu kwa jina la Yesu.
                                           ‘’AMEN’’
No comments:

Post a Comment