Sunday, July 27, 2014

MAELFU YA WATU WAVUNJA NGUVU YA CHAKULA CHA KICHAWI KWENYE MAISHA YAO, NDANI YA BONDE LA KUKATA MANENO KAWE.
IBADA YA JUMAPILI TAREHE27/07/2014
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: CHAKULA CHA KICHAWI
                                                            I.                    UTANGULIZI.
Mchungaji kiongozi  Josephat Gwajima
Danieli 1:1-21
Kweye biblia neno chakula limeandikwa mara 185  na neno usile limeandikwa mara 15 na shetani hana nguvu juu  ya watu wa Mungu mpaka anapopata nafasi na shetani amepata nafasi kubwa sana kwenye chakula kwa kuwaangamiza watu na kuna aina mbili za chakula chakula cha kiroho na chakula cha kimwili  1wakorintho10: 1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10 Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 14 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Biblia ukisema chakula cha kiroho unaweza kutafasiri mambo mawili yani chakula cha rohoni yani chakula cha kiroho. Lakini ni chakula gani kimeitwa chakula cha kiroho kulikuwa na vipande vya mikate vidogovidogo walikula chakula hichohicho tangu waanze safari mpaka mwisho wa safari kwamaana kwamba kulikuwa na nguvu kwenye chakula hicho kunakuwa na nguvu ndani ya chakula hichi kinaonekana cha kimwili ni cha kawaida lakini ndaniyake kuna nguvu za Mungu na anayekula anaonekana ana kula chakula chenye virutubisho.

Hata ukiwa Japani ufufuo na uzima pia inapatikana.
II.                  SOMO.
Ndani ya chakula kunaweza kuwa na mauti na uzima. Baada ya Israeli kuvamiwa wana wa Israeli walipelekwa mpaka nchi ya Babeli (Iraq) utumwani. Walipofika babeli walilazimishwa kula chakula ambacho kimetolewa sadaka kwa  miungu na akinadanieli wakaambiwa wabadilishe majina yao na kabla mfalme hajala kile chakula cha mfalme kinachukuliwa alafu kinaombewa kitu Fulani kwamba mtu atakapokula awe mtu wa aina Fulani, Yesu alisema yeye alayee chakula changu anauzima alafu akasema Baba zenu walikula chakula wakafa lakini mimi ninachakula cha uzima sasa wewe unapokaribishwa kwenye chakula ambacho kimenuiziwa mambo ya kichawi mambo ya kishetani unapatwa na kansa, magonjwa na matatizo na leo ni mwisho.
Yohana6: 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? 49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? 52 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.
Hata alipokuwa na wanafunzi wake aliwaonyesha kwa kuchukua mkate na kuwaambia yeye aulaye mwili wangu atakuwa na uzima wa milele na kwasababu hiyo ule mkate uliingia nguvu ya Yesu kristo unaingia ndani yake. Shetani ni malaika wa ngazi ya kerubi.
Yuda1: 6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu., Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;   malaika wanasifa mojawapo ya kugeuza maumbo. Ndiomaana Ibrahumu aliwapokea malaika wenye maumbo ya watu na mavumbi na akawaandalia chakula wale mabwana wakakaa na kusubiria chakula wakala, sio kila mwenye mavumbi miguuni ni mtu, sio kila anayepiga stori ni mtu, ndiomaana kwenye chakula unaweza kula chakula kilicho nuiziwa unakula balaa, magonjwa, ajali, mauti, bila ya kujua.

Hesabu25: 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori.
Chakula mtu anakitoa sadaka kwa mashetani kinanuiziwa mfano kwenye mila wanachukua pombe na mtama wanakunywa wanaongea maneno maanayake wanatoa sadaka na mashetani, majini, mapepo ugali, pilao, au chakula chochote na unapokula wanaingia mwilini na kufanya kazi ya uharibifu na wewe na hayo mashetani mnakuwa kitu kimoja.
Kuna watu wengi wagonjwa kwasababu ya chakula na Matendo ya mitume15:20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
1Wakorintho10: 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye? 23 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
1Wafalme19:1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. 3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. 4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. 5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6 Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Kumbe unaweza ukapewa chakula cha kishetani ukatembea kwenye balaa kwa chakula hicho mpaka ukaingia mautini na unatakiwa uangalie pale unapokaribishwa chakula kunauzima humo. Lazima ujue mitego ya mwindaji kwingine umefanikiwa lakini anaweza kukukamata kwenye chakula na unatakiwa useme “Baba Mungu ninaweka Baraka kwenye chakula hiki kwa jina la Yesu”.
Kunaweza kuwa na mauti na mauti sio tukio mauti ni roho ni jini kumbuka wana wa manabii waliona roho ya mauti kwenye sufuria.  Mtu anaweza akanuizia jambo Fulani kwenye chakula. Kama Mungu alivyo na watu wake na shetani naye ana watumishi wake. Wakiona imeshindikana kukuletea chakula wanaanza kukuletea ndotoni, ndiomaana unakuta mtu anatafuna akiwa amelala. Tulipookolewa tunalindwa na Mungu kwa njia ya Imani na ndio maana unapotaka kulala lazima uombe na sio useme Bwana Yesu shuka utulinde hapa! Tunaotenda kazi ni sisi tena kwa ujasiri unawaamuru malaika wakulinde.
“Kwa jina la Yesu ikiwa tatizo langu lilianza kwenye chakula nilichopewa kuanzia leo ninakataa kwa jina la Yesu” ndoto ni bayana hakuna aliyeota hakikutokea kina Ebimeleki,yusufu utawala, farao njaa, nebkandneza, askari wa jeshi la midiani kwa mikate iliyoanguka toka mbinguni, hakuna aliyeota ndoto haikutokea. Kama uko imara ndotoni unaota umekaribishwa lakini wewe huli maana yakee uko imara. Wanaolishwa chakula ndotoni kama uko juu unashushwa chini, kama unakazi unaipoteza kazi hiyo, kushindwa kuomba.
Kunawatu wengi wamelishwa chakula nyumbani kwa mtu na wameharibikiwa maisha yao ”kwa jina la Yesu  kuanzia leo magonjwa niliyoyapata kwa kulishwa chakula ndoton ninayakataa kwa jina la Yesu mahala popote nilipokula chakula cha kichawi kuanzia leo enyi mashetani mlioniwekea kutokuolewa kutokufanikiwa kuanzia leo ninawafyeka kwa jina la Yesu navunja maagano yaliyokuwa ndani ya chakula ninayavunja kwa jina la Yesu maagano ya mauti, maagano ya kifo ninayavunja kwa jina Yesu ninaagiza kuanzia sasa majini, majoka , mizimu walionuiziwa kwenyee chakula cha ndotoni, kwenye chakula cha mwilini kuazia leo ninakataaa kwa jina la Yesu”.( ukitaka kutatua tatizo unatakiwa ujue chanzo cha tatizo”)
Wengine  kwa njia ya chakula wanaweza kuchukua nyota yako wananuizia kabisa na hakuna kinachotokea chenyewe vitu vinatengenezwa ndio maana duniani
                                Kuna watu wa aina tatu.
1.       Wale wanaoona matukio yanatokea tu lakini hawajuwi kinachoendelea.
2.       Wale wanaojua kinachoendelea; wakiona nchi wanajua kinachoendelea wakiona mtu kafa wanajua kinachoendelea
3.       Watu wanaotengeneza mambo yatokee wakitaka upatwe ugonjwa unapatwa na ugonjwa.
Tukidili na chanzo cha tatizo tunalimaliza tatizo, kuna mamlaka ya rohoni inayotegemewa kusimamisha mambo Fulani. Maisha ya mtu hujulikana kabla hayajaanza; Yeremia anasema  Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Inawezekana wamekupotezea miaka mingi lakini Mungu anaweza kukurudishia vyote vilivyopotea, Mungu ni Mungu wa nafasi ya pili na usiangalie vile ulivyo Biblia inasema amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu kwa jambo lolote.
Baraka ndani ya chakula na laana ndani ya chakula, kabla hujazaliwa Baraka zako zinaonekana ukiwa tumboni mwa mama yako. Kuna wakati mwingine mtu huwa hapendi lakini hubalansi kwasababu ya urafiki, kuna mambo unakula leo halafu madhara yanaanza mwaka kesho. Haung’ai kwasababu unavyoonekana kwa nje hapana bali kuna kitu kimewekwa ndani yako na Mungu na wachawi hukiona na kukichukua na wewe unadhani unafanyiwa fitina kumbe ulipewa chakula kilichonuiziwa.
Kilichowekwa ndani yako kinakupigisha hatua kwa elimu na kisipokuwepo unakuta unasoma lakini hauwezi kufanikiwa kumbe ni chakula. “Kwa jina la Yesu ninajikinga na chakula au vinywaji au kitu chochotee kilichotolewa sadaka kwa mashetani na mtu yeyote aliyetoa sadaka ninamteketeza kwa jina la Yesu chochote alichonipa mtu ndugu rafiki au mtu yeyote bila kujua nikala au nikanywa kuanzia leo yamrudie yeye mwenyewe kwa jina la Yesu” unamatatizo na haujui matatizo hayo yanatokea wapi na kuwa wa kwanza darasani sio kuwa na maisha mazuri lakini Mungu ameweka kitu ndani ya mtu nyota uwezo karama imewekwa ndani ya mtu na elimu inamsaidia mtu huyo. Kila chakula unachokula lazima kiwe kimetolewa sadaka mahali Fulani na ndio maana watu wa Mungu wanapotaka kula wanakiombea “kwa jina la Yesu  ninawashinda wote walioandaa chakula wiki hii kwenye ndoto, kwenye sherehe nawashinda kwa jina la Yesu”
Unapokaribishwa chakula lazima uangalie unaweza kula kilichonuiziwa na shida watu wamezoea kuombewa, unatakiwa ujifunze kupigana wewe mwenyewe unapiganaje unapigana kwa jina la Yesu”kwa jina la Yesu kila chakula kilichoandaliwa kichukue nyota naamuru roho yangu ikatae kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu kila aliyeandaa chakula cha mauti, kinywaji cha kifo namrudishia yeyee kwa jina la Yesu  aliye andaa kwenye ndoto au mahala popote ninakataa kwa jina la Yesu” kila unachosema kinakuwa.
Kwanini ninasisitiza kuomba mathayo10: 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Kila mtu aliyempokea Yesu anauwezo 1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Marko7:6 luka 10:19  Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Kwahiyo usiseme niombeeni unatakiwa uvunje mwenyewe kama unamjua mchawi unamtaja na jina Mathayo18: 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Vita vya rohoni ni kwamba wewe unaomba ukitaja maneno na utakuwa vile unavyoamini. Sisi mbele za Mungu ni watoto wa Mungu na Mungu hutenda sawa na vile vile unavyoamini, ukiamini nikimfunga shetani anafungika na inakuwa hivyo hivyo ulivyoamini.
III.                UKIRI
Baba wa mbinguni nimeisikia sauti yako na ninaomba nguvu ya uweza kushindana na wakala wote wa shetani na kila mtu aliye nihusisha  kwa jambo lolote la kuweza kunisababishia uharibifu ndani yangu  leo ninaomba asipate nguvu juu yangu na kwasababu hiyo ninapokea nguvu  na kujitakasa.
Maelfu ndani ya bonde la kukata maneno kawe


IV.                MAOMBI
Katika jina la Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai ninavunja mashetani yote yaliyoingizwa kwenye familia  yangu kwa njia ya  chakula kwa jina la Yesu. Ninasambaratisha kuanzia sasa magonjwa yaliyopandwa kwa njia ya chakula ninayaharibu na kuyaangamiza kwa jina la Yesu, kila kufeli, kuanguka kulikosababishwa kwa njia ya chakula ninasimama kinyume nacho kwa damu ya mwana Kondoo, kila kinywaji nilichokinywa   kila kushindwa kulikosababishwa kwasababu ya  chakula ninasambaratisha kwa jina Yesu, ninaharibu wasimamizi wa chakula mlioungamanishwa na chakula kwa damu ya mwanakondoo, ninafungua vingufungo vyote vilivyofungwa na wakala wa shetani kwenyee familia yangu na maisha yangu kwa njia ya chakula ninabomoa kwa damu ya mwanakondo katika jina la Yesu, mauti iliyoingia kwa njia ya chakula ninaiharibu kwa jinala laYesu, ninaharibu udhaifu wowote ulionuiziwa kwenye chakula juu yangu kwa damu ya mwana kondoo, “vita sio vyangu vita ni vya Bwana” ninaharibu kila chanzo cha magonjwa, mikosi, kukataliwa, ninafungua kamba zote katika jina la Yesu. Kwa jina la Yesu kila atakaye niletea zawadi au chakula kwa njia ya siri naiamuru laana ile imrudie yeye kwa jina la Yesu lakini mimi sitalogwa kwa jina la Yesu.
                  AMEN.

Sunday, July 20, 2014

JE WAJUWA KUWA UKOO WAKO UNAWEZA KUWA UKOO TATA?
TAREHE: 20.07.2014
NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: UKOO TATA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima

MANENO YA MSINGI: Mwanzo 50:24, 1 Nyakati 4:9


Baraka au laana ya ukoo inatokana sana na shina la ukoo. Ulivyo ukoo wa mtu,ndivyo alivyo mtu kama hana Mungu. Kuna koo ambazo ni tata sana, hata zikitoa mambo, na mambo hayo nayo huwa ni tata.  Mara nyingi vyanzo vingi vya matatizo aliyo nayo mtu yana uhusiano wa karibu na ukoo alipotokea mtu huyo.
Mwanzo 50:24 “Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo alivyowabariki”. Tunaona jinsi ambavyo Unaweza kukuta ukoo Fulani kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho watoto wote ni tata. Hivyo kabla hujaoa wala kuolewa chunguza ukoo kama ni tata au sio tata. Watu wengine wakishafika mjini wanaanza kujisifu na wanasahau kama huko walikotoka  mfano shangazi hana hata viatu na bibi anapuliza kiko cha ugolo hadi sasa!
Kutokana na neon hili unaweza kuona Yakobo alikuwa na watoto 12, na kabila 12 zilitokana na watoto wale. Hivyo kila tabia ya mtu inatokana na msingi wa  ukoo wake. Hivyo yatupasa tuchimbe na tung’oe msingi ya koo tata. Kumbuka niliwahi kufundisha habari ya majeshi ya wafu, nikasema sio vizuri kabisa kuendekeza na kuwatolea sadaka.
Kitabu cha kwanaza cha maneno matakatifu kinaanza na majina ya ukoo. Mfano katika kitabu cha 1Nyakati 1. Kutokana na majina ya koo hizi, inatufindisha kuwa kila majina ya koo yalitengeneza majina ya sehemu hizo leo. Kila mtu ajue chochote utendacho leo unatengeneza ukoo wenye baraka au laana ya kizazi kijacho. Usifikirie kuwa unaposoma sana ndio kushinda katika maisha, lakini elimu inakupa tu mwanga wa kukuangazia utafute jinsi ya kujikwamua katika maisha yako, ukitumia kipawa alichokupa Mungu.
Unaweza kuona baadhi ya koo mabinti hawezi kuolewa, au kusoma mpaka chuo kikuu, au wanakufa katika umri mdogo. Kwa namna hii unaweza kuona kuwa matatizo hayo ndio chanzo na msingi wa ukoo huo. Hivyo rudia maneno haya “ katika jina la Yesu nayavunja mambo yote mabaya katika ukoo wangu “ Ukoo wa mtu unatabili maisha ya mtu anayoishi leo. Unaweza kukuta kila kinachotokea mfano kifo katika ukoo ni cha namna ileile. Mfano kule Bukoba unaweza kukuta nyumba ya Profesa Fulani , lakini maisha ya familia yake sio sawa na kiwango cha elimu walionayo. Jambo hilo limetokana na msingi wa ukoo wake. Sema maneno haya “ Kwa jina la yesu navunja mahusiano ya taabu yangu na familia yangu katika jina la Yesu
Leo uhame hapo ulipo kwenye ukoo wa laana na mikosi uingie kwenye ukoo wa kushinda kaita jina la Yesu. 1 Nyakati 4:9Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.”
Huyu mtu alizaliwa kwa huzuni na akaitwa jina lake ni huzuni, lakini baada hapo alimtafuta Mungu akaishia kuwa wa furaha na kuheshimiwa na ndugu zake. Walawi 25:47Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni”
 Na wewe ukiamua kumtii na kumtumikia Mungu ataona hata utakao wazaa hawataanzia wewe ulikoanzia bali ulikoishia wewe. Hivyo mtii Mungu na kumuheshimu Mungu utaheshimika na watu wote na viongozi wa nchi hii watokane na wewe katika jina la Yesu. Kama ukoo wako ni ukoo wa kushindwa utabaki kuwa wa kushindwa mpaka uhame katika jina la Yesu. Leo nahama kutoka katika ukoo wa laana, mkosi, kushindwa, kukataliwa, kuachwa, magonjwa, vifo vya mara kwa mara.
Zamani mtu alikuwa anaweza kujiuza kutoka kwenye familia ya umaskini na kuingia katika familia ya kitajiri na anakuwa mali ya familia au ukoo huo na sisi tumeamua kujiuza kwenye familia  ya mwana kondoo.
Mchungaji kiongozi katikati ya makutano

 2 Wakorintho 8:9
Inatwambia kumbe yesu alifanyika kuwa maskini ili tuwe matajiri. Na yesu ametukubali kwa umaskini wetu sisi tupate kuwa matajiri kwa njia ya imani. Na kwa namna hiyo tunapata kibali na kuweza kuendelea mbele. Ndo maana unaweza kuona unaweza kuwa na sifa nzuri za kupata visa, tenda, kazi lakini usipate. Hili kwa sababu ukoo wako umeandikiwa muwe wa kukosa. “Leo natangaza kwa jina la yesu lazima  uhame katika jina la yesu.”Unaweza kukuta familia zinatawaliwa na nguvu za giza? Kabla hatujamjua yesu, wazazi wetu walikuwa wanatumia ulinzi wa kimila. Kuna familia nyingine wewe kabla kuja mjini kuna kitu ulipewa uje nacho kama ulinzi kwako dhidi ya watu wabaya. Anaweza kuletwa na baba wa familia au bibi au babu wa ukoo, akiwa na nia njema ya kuwawekea ulinzi, lakini kumbe ndo chanzo cha nyinyi kuanza kulindwa na mashetani.
Wakati mwingine mambo hayo yanatengenezwa kama karatasi yenye maandishi ya kutoka kulia kwenda kushoto Fundo hili linaitwa talasim. Kimsingi kupitia zindiko hili familia inaanza kulindwa na masheteni. Kwa mfano pia unaweza kukuta mtua ana namba ya waziri mkuu, mkurugenzi au mtu mkubwa.Lakini pamoja na kuwajua watu hao haikukusaidia kwa kuwa kuna utata wa kishetani unaolinda familia yenu. Unahitaji kuhama ukoo huo wa utata.  kwa jina la yesu nakataa kabisa kung’ang’ania ukoo tata”
Wakati mwingine unaanza kujiuliza mbona nimejitahidi kusoma sana lakini bado mambo
2 Timetheo1:3
“Leo navunja kila laana, balaa namatatizo yaliopandwa ndani ya ukoo wangu katika jina la Yesu”
Maombolezo 3:30-32
Isaya 53:4
Tumeumba kwa neno hivyo unapaswa kutamka  kwa kinywa chako. Na utambue imeandikwa wewe u rungu langu na silaha za bwana za vita. Mtu yeyote kuanzia sasa naamuru achiwe katika jina la Yesu. Unaweza kujiuliza maswali ya kwamba mbona kaka  zangu wananafuu? Tambua kuwa balaa iliyo ndani ya famila au ndani ya ukoo inaweza kijidhihirisha kupitia mtu mmoja. Imeandikwa pi kuwa amelaaniwa mtu Yule amwagaye damu ya mtu asiye na hatia. Inaweza kutokea ajali inatokea anakufa mtu mmoja au unazaa mtoto anaulemavu wa ngozi. Lakini kwanini usijiulize kwanini itokee kwako?  Kimsingi lazima ujue kuwa kunakitu kinapelekea au kimepengwa kikupate kama ilivyofanyika katika ulimwengu waroho.
Mfano katika taifa la Marekani kila raisi aliyekuwa anaingia madarakani alikuwa anauwawa mpaka walipoamua kuingia ikulu na kuomba na kuvunja laana hiyo na haikutokea tena. Unaweza kukuta kunatabia Fulani inatawala kabila Fulani, lakini hakuna kabila bora kuliko nyingine sema tu inategemea kiwango cha kutawaliwa na mashetani hao. Jiulize pia wakati naomba kwa nini watu wanalipuka mapepo? Hii ni kwasababu mtu anayelipuka mapepo kimsingi ameshikiliwa na mashetani wasimamizi wa laani maana wamewekwa kusimamia laana hiyo na kuhakikisha unaangamia na kupotea kabisa. Lakini kwa wanao mwamini Yesu pia kuna damu ya mwanakondoo imewekwa ilikusimamia na kuvunja laana ya ukoo huo au inayokufatilia wewe.
watu wenye shida mbali mbali wakifunguliwa.
Watu wa hospitalini huwa wanasema tutaweza kuicontrol pressure yako au kisukari lakini sisi tumepewa mamlaka ya kung’oa kubomoa na kuharibu. “Lakini leo sema nakataa kusimamiwa na mashetani wa balaa, laana na mikosi na toroka na kuhama kutoka maeneo ya kishetani katika jina la Yesu.” Kuna namna mbili shetani anazoweza kutumia kukushambulia.
1.       Anaweza kuwa nje
2.       Anaweza kuwa ndani yako
Zakari3:1
Maelfu ya watu wakiwa ndani ya Bonde la kukata maneno
Kuna mtu analalamika anadegree 2, au 3, lakini hapati kazi.
Pamoja na kushindwa lakini unaweza kuanza tena, kushinda tena, kutengeneza tena. Tumejifunza kuomba wenyewe kwa mamlaka ya jina la Yesu.  Unatakiwa ujue kuwa hatumuombi Mungu atende bali twatumia mamlaka ya Yesu iliyoko ndani mwetu. Hivyo unatakiwa ujue kuomba mwenyewe. Kila mtu anayo  mamlaka shida tu huwezi kutumia usichokijua.  Uwezo  wako wa kuvunja, kushambulia na kuharibu katika ulimwngu wa roho, ndo uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu wa mwili. Utakuwa kama bwana anavyotaka uwe, wala hautakuwa kama watu wanasema nini juu yako. Mungu anajua kesho yako kabla haujaiona, na kesho ya maisha yako iko mikononi mwako. Wanakuita aliyeshindwa lakini mbinguni wanakujua kama shujaa.
Tanzania mpya inakuja, na wewe unayonafasi ya kustawi katika nchi mpya ijayo katika jina la Yesu. Mungu anawatafuta waliodharauliwa na watu, na anakufanya kuwa wa heshima na anaanza kukufanya hatua kwa hatua.” Nina kataa  balaa zilizopangwa kuharibu  kesho yangu, naiona kesho yangu  inang’aa  katika jina la Yesu.”
          Amen

Sunday, July 13, 2014

MASHIMO YA KICHAWI YAFUKIWA NA KUSAWAZISHWA KATIKA BONDE LA KUKATA MANENO KAWE.JUMAPILI YA TAREHE 13/07/2014MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MASHIMO YA KIROHO/KICHAWI
I.                    Utangulizi
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima
Kuna ulimwengu wa aina mbili ; ulimwengu unaoonekana kwa macho na ulimwengu usio onekana kwa macho. Kwanini unaitwa ulimwengu wa roho kwasababu unakaa rohoni na pia kila kinachokaa kule ni roho mfano gari, mtu, mti, nyumba ni roho zinazogeuka kuwa vitu na watu wengi wanaupata kupitia ndoto na ukitaka kwenda kule ni mpaka uwe rohoni na vitu vingi vinaanzia rohoni na uwezo wako wa kushindana kwenye ulimwengu waroho ndio uwezekano wako wa kupokea Baraka za mwili. Wakristo wengi hawatambui taifa linaweza kushikiliwa rohoni, uso wa mtu unaweza kushikiliwa rohoni hata nyumba inaweza kushikiliwa rohoni.
II.                  SOMO.
Waefeso1:33 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 
Waefeso2: 2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;   
Waefeso3: 10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;     
Waefeso6: 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 
Akitolewa shimoni
Zamani kwenye agano la kale kulikuwa na  mashimo walikuwa hawana magereza kama ya leo bali yalikuwa ni mashimo marefu sana na ulipokuwa unafanya kosa unatupwa shimoni na kuna aina nyingine ya mashimo ambayo yalikuwa yanawekwa wanyama kama danieli alivyotupiwa kwenye tundu la Simba, na mashimo mengine yalikuwa yana maji na ndio maana ya lile andiko watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa wamefichwa mashimoni wala hapana aokoaye wamekuwa mateka wala hapana  asemaye rudisha. Lakini kwenye agano jipya hakuna mashimo kama hayo bali kuna mashimo ya kiroho ya kichawi ambayo yamejengwa kwenye ulimwengu wa kiroho na wachawi ili kuwaweka watu na ndio maana yesu alipokuja duniani alisema roho wa Bwana yu juu yangu amenitia mafuta niwatangazie wafungwa kufunguliwa kwao.
Ufunuo9: 1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 
2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 
Shimo la kuzimu ndio makao makuu ya shetani ni shimo mama lipo kwenye ulimwengu wa rohoni ni refu lisilo onekana linaitwa kuzimu linaitwa shimo la uharibifu, shimo la kifo na hata mashetani walipoasi walitupwa kwenye shimo hilo 2petro2: 2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 
 na hilo shimo ndilo shimo wenye hekima za utawala wanakwenda kuchukua kule au umaarufu wa utawala au nuru ya utawala na sisi tuliookolewa tunapahali petu tunapata ambapo ni Mbinguni juu.  Ndio maana Yesu alisema amelijenga kanisa juu ya mwamba na milango ya kuzimu haita lishinda.
Luka 8: 26 Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 
27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. 
28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. 
29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 
30 Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. 
31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. 
Miji inaweza kuwa na mashimo ya rohoni na utakaposhughulika na shimo hilo unauteka mji. Mashetani yanamwambia Yesu tunaomba usitupeleke shimoni kwahiyo kila mji kuna mashimo ya kichawi na kuna makao makuu ya utawala wa kishetani matatu nayo ni 1. Shimo la kwanza kubwa la mashetani ni katika nchi “Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. ” 2. Katika maji mnyama anapeenme mbili anatokea baharini [pembe ya kwanza ni utawala wa kidini na utawala wa kishetani mwana kondoo maana yake anaonekana mwema] 3. Angani Belzebuli mama wa makahaba anayerutubisha uovu kwa uasherati.
Kuna vishimo vidogovidogo kwenye nchi na unapoona mtu amefariki unasema ameitwa na Bwana kumbe amewekwa mule ndani. Mashimo haya ya kichawi ni kitu gani hasa?. Tulishawahi kujifunza shetani anaweza kuvaa umbo la mtu, malaika walienda kwa Abrahamu wakala wakaongea.  
 Mashetani ni malaika waovu ndio maana kwenye biblia imeaandikwa kuzimu na mauti itawatoa watu wake na ni shimo lisilo na kina na wasiookolewa wote huenda huko.
Mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili  na wanapouzika mwili wanakuwa wameuzika mwili pekee lakini mwenyewe hayupo pale tena.
Luka16: 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 
Mtu anapo kufa anachukuliwa na malaika na anatoka ndani ya mwili anapelekwa kwenye shimo la umilele anasubiri siku ya mwisho atupwe kwenye moto ”na walio kuzimu wanatoka” ila jehanum ndio hawatoki. Sasa unapokuwa umelala unakuwa umechukuliwa na wachawi na kupelekwa shimoni na hata mikono inaweza ikachukuliwa, na ndio maana mtu anapokuwa rohoni analishwa chakula cha kiroho mfano Elia alilishwa mkate na malaika akala akaenda.
Kuna chakula cha rohoni na Neno la Mungu nalo ni chakula cha roho na wachawi nao wanachakula chao Danieli1:7- chakula kimenuiziwa mpaka kimejaa nguvu za rohoni upande wa shetani ndio maana watu wanaota wanakula chakula usiku kimenuiziwa magonjwa, balaa, mikosi, utasa nk. Pia kuna namna ya rohoni uso wako unaondolewa, akili inaondolewa inafichwa kwenye mashimo lakini ukiwa duniani unaanza kuona mara magonjwa ya moyo mara kukataliwa “katika jina la Yesu leo nina amuru ikiwa mimi mwenyewe nimewekwa kwenye shimo ninaamuru leo ninahama kwa jina la Yesu.”
Kwanini wachawi wanamchukua mtu na kumweka kwenye mashimo ni kwasababu unakuta mtu mafanikio yake yamewekwa kwenye uso wake na wachawi wanaweza wakauchukua uso wakaenda kuutumia na mwingine.  wanaweza wakaichukua akili nayo na kuitumia.
Mhubiri9: 11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote. 
Kila mtu ana eneo lake la baraka mwingine amewekewa kwenye kinywa wengine kwenye matumbo yao wengine kwenye muonekano na ndio maana wale wenye Baraka zao kwenye uzazi unakuta wanapatwa na shida kwenye kuolewa na hiyo ni kazi ya wachawi wanachukua nyota za biashara na shetani ni mwizi na kazi yake ndio hiyo ya kuiba “sema kwa damu ya Yesu mahala popote walipoweka tumbo la uzazi, macho yangu, kinywa changu, akili yangu au chochoto kwenye mashimo kwa damu ya Yesu mashimo yote yaliyowekwa na familia yangu mashimo yaliyowekwa akili yangu napiga mashimo kwa jina la Yesu naamuru kuanzia sasa akili yangu njoo kwa jina la Yesu.
Ukimwona mtu anamatatizo sana na umekaa naye unazungumza nae kumbe ameshachukuliwa ama amechukuliwa kitu ndani yake uso, mikono, miguu Isaya42:22
Luka4:1-
Hakika Mungu ni mwema
Shetani anamwambia Yesu atampa mali ila masharti yake amsujudu lakini zaburi24 vitu vyote viijazavyo nchi ni mali ya Bwana. Sasa shetani na wachawi wanauwezo wa kuona Baraka na kusudi watu walilowekewa na Mungu ili watumie kufanikiwa na wachawi wanachukua akili za watu na kwenda kumpa mtu mwingine. Mungu anawapa watu vitu mbali mbali na tangu ukiwa mtoto mdogo wanakuja wanakuibia na kuviweka shimoni na kumpa mtu mwingine, unakuta mtu anatabia mbaya lakini anaolewa lakini wewe unatabia nzuri hauolewi kumbe umeibiwa uso wako Mungu ni Mungu wa kurudisha aliwarudisha waisraeli toka utumwani misri na ndiomaana anasema nitakurudishia afya yako, na anaweza kukurudishia afya yako tena, familia yako, bihashara yako. Mungu ni muumbaji na shetan ni mwizi.
Watu wanaofanikiwa wanasiasa, wenye magari hawana Mungu wana mganga wake wa kienyeji. Na kuna watu wanaenda kwa mganga na kumwambia wanataka uongozi na mganga anamwambia njoo kesho na mganga huyu anatoka usiku anakwenda anazunguka anamkuta mtu haombi ana nyota ya uongozi anaichukua nyota hiyo, anatoka anaenda kwa mwingine kuchukua nyota ya kupendwa, anatoka anakwenda kwa mwingine anachukua nyota ya kuongea. Sasa wale waliochukuliwa nyota zao wanaamka hawajui chochote. Unakuta mtu anamatatizo anatamani kufanya biashara lakini hawezi kuisimamia akafanikiwa kumbe wamechukua akili ya bihashara wameficha kwenye mashimo na unamwona mwingine anafanikiwa na hamtumikii Mungu kumbe amepata toka shimoni. sema kwa jina la Yesu kuanzia sasa shimo lolote lenye nyota yangu rudisha kwa jina la yesu.
Makaburini zimelala hazina nyingi ambazo hazijafanyika hapa duniani na hatari kubwa kuliko yote katika maisha ni kufa kabla hujatumia kipaji ulichopewa na Mungu na elimu ni nzuri na ni ya lazima lakini haikuhakikishii mafanikio bali ni taa inayo kusaidia upate kutumia kipaji ulichopewa na Mungu. Kanisani ni center ya walioteswa ni sehemu ya kuwa huru kwa walioonewa. Kuna namna ambayo Mungu anataka uwe na wachawi nao wanaona vile unavyotakiwa kuwa na wanavichukua na unatakiwa uwe mtu wa kupigana kwamaana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama maana yake kuna mamlaka za kichawi falme za kichawi tunazotakiwa tupigane nazo ndizo zinazotusumbua. Kuna jambo ambalo wewe umezaliwa ili ulitimize na unapolitimiza jambo hilo na ukafa wewe ni mtu uliyefanikiwa kwa hiyo kuna mtu mwingine amefanikiwa nusu na unaweza usifanikiwe kumbe kuna wanaozuia. Katika jina la yesu hakuna atakaye zuia kila nilichokusudiwa nikifanye kabla sijafa kwa jina la Yesu.
Kwenye kitabu cha yeremia Yeremia anaambiwa na Mungu tangu tumboni nalikujua na kuna watu Mungu amewachagua wawe viongozi na unakuta mama tangu mimba ile imeanza inamatatizo tangu tumboni na unakuta umezaliwa na uunamatatizo lakini kuna jambo lilikuja katikati pale ndilo likaleta maisha uliyo nayo na usishukuru kile ulicho nacho ni mapenzi ya wakala wa kishetani ndio wamekufanya uwe hivyo. Ile akili ya bihashara yako inatumiwa na watu mahali fulani ndio maana shetani anamwambia Yesu nikupe mali lakini hana lolote anataka kuwaibia watu ili aje ampe yesu.
Pengine familia yako imeibiwa au kitu chochote utajuaje umeibiwa? Ndoto unazoziota au unakimbizwa maana yake mashetani yanakufuatilia au uko kwenye kichaka maana yake uko kwenye kichaka cha kishetani unapoota unafanya mapenzi na mtu maana yake unaushirika na mashetani unapoota umevunjika miguu maana yake kuna jambo litatokea upatwe na upofu na kila ndoto unayoota ni jinsi ulivyo rohoni unatakiwa uziharibu ndoto zote mbaya.
Mungu anaongea na watu kupitia ndoto na hakuna ndoto ambayo haina maana na kwenye kitabu cha hatari ya ndoto utakuta unatakiwa ufanye nini unapoota.
Na unatakiwa uchukue hatua na biblia inasema adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake na unakuta mtu ameibiwa nyota yake na mjomba lakini hajui unatakiwa uamue kwa jina la Yesu na utashangaa baada ya wiki moja au mbili utajiri wake unaporomoka wote na anabaki mtupu. Pia mwingine ameibiwa akili na inatokea anashindwa kusoma kwasababu wanajua atafanikiwa kupitia masomo. Pia ndoa nyingine zina baraka wale wanaowaonea wivu wanatengeneza jambo na ndoa yake inavurugika.
Maelfu ya watu wakipiga mashimo ya kichawi

III.                 MAOMBI.
Kwa jina la Yesu nayapiga mashimo ambayo yameweka uso wangu, nayateketeza kwa damu ya yesu mashimo ya kuzimu mashimo ya ukoo mashimo ya familia mashimo ya mashetani mashimo ya wachawi nayapiga kwa jina la yesu nayashambulia mashimo ya ukoo kila shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka vutu vya ukoo  kila shimo lililohifadhi familia yangu nayapiga kwa jina la yesu kristo, nafanya vita na walinzi wa mashimo nawateketeza kwa moto wa Mungu. Shimo liloshikilia uso wangu nalipiga kwa jina la Yesu, nayashambulia kila mashimo ya kichawi kwa jina la yesu mashimo yote ya rohoni natetekeza kwa jina la yesu nashambulia shimo la kuzimu lililo meza akili zangu kwa jina la Yesu shimo lililoiba uso wangu naliamuru tapika kwa jina la Yesu shimo lililomeza mvuto wangu naamuru kwa jina la Yesu tapika.
Anza kuita chochote ambacho unaona kimeibiwa ita njooooooooooooo kwa jina la Yesu kila kilichofichwa kwenye mashimo njooooooooooooo kwa jina la Yesu, akili iliyofichwa kwenye mashimo njoooooooooooooo kwa jina la Yesu, elimu iliyofichwa njooooooooooooo kwa jina la Yesu, kinywa kilichoibiwa njooooooooooo kwa jina la Yesu, uso uliofichwa shimoni njooooooooooooooo kwa jina la Yesu, Baraka zilizofichwa kwenye mashimo njooooooooooooo kwa jina la Yesu, nafsi za wanadamu njoooooooooooooooooo kwa jina la Yesu kristo……………………………………………
                                         Amen!