Sunday, July 6, 2014

TWAENI SILAHA ZOTE ZA MUNGU MPATE KUWEZA KUSHINDA SIKU YA UOVU.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 06/07/2014
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: SIKU YA UOVU
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima
  • I.                    Utangulizi
Waefeso 6:13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.Mtume Paulo anazungumza na kanisa la waefeso hii sura iko kama sura ya kijeshi vile anaelezea silaha za kuvaa wakati wa uovu. Kuna siku ya uovu ambayo huwa inakuja kwenye maisha ya mtu na mtume Paulo amesisitiza tuvae silaha zote kwaajili ya siku ya uovu na siku hii inaitwa siku ya ubaya kwenye “Zaburi27:5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba”. Kuna siku ya ubaya inakuja ambayo wewe hujui ni lini inakuja inaitwa ni siku ya mabaya na huwezi kujua ni lini inakuja.
 “Mhuburi7: 14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.”
 Unapaswa kuelewa siku hii ipo ndio maana mtume Paulo amesema tuvae silaha zote kwaajili ya siku ya uovu.
Imeitwa siku ya uovu au siku ya ubaya au siku ya mabaya
“Mithali 16: 4 Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. “
Maisha yana siku ambayo imekuwa imepangwa kwa namna fulani lakini watu wengi hawajui siku hiyo inakuwa imepangwa.
“Yefania1: 15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, “
Maisha yalianzia rohoni kabla hayajaja mwilini na unapo mwona mtu ameshinda mwilini alishinda kwanza rohoni, mabaya matatizo dhiki tabu magonjwa na mabaya mengine yanakuwa yamepangwa kuanzia rohoni kambla hayajatokea mwilini, kawaida kuna ulimwengu wa rohoni na ulimwengu wa mwilini na mambo mengi yameanzia rohoni mfano Yesu alikuwepo rohoni na akaja mwilini lakini alikuwa Mungu neno rohoni “hapo mwanzo kulikuweko….” Kwahiyo Yesu kabla hajamwaga damu alikuwepo rohoni kwanza. Ukimwona mtu amepata ajali; ajali hiyo imeanzia rohoni kwanza ukimwona mtu amefukuzwa kazi; alifukuzwa rohoni kwanza na uwezo wako wa kushinda mwilini huanzia rohoni kwanza na kushindwa kwako mwilini huanzia rohoni kwanza, ukimwona mtu ameshindwa kitu mwilini jua alishindwa rohoni kwanza “Ufunuo9: 15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.”  hawa malaika wameandaliwa kwa wakati Fulani saa, siku, mwezi na mwaka wameandaliwa kwenye siku ambayo imepangwa Mungu ni mungu wa wakati na majira wakati wa kupanda nawa wakati wa kuvuna, wakati wa kupanga mawe na wakati wa kutupa mawe, wakati wa kuua na wakati wa kuhuisha. Wewe unaweza kudhani ni bahati mbaya, hapana ni siku imepangwa kuanzia rohoni kwaajili ya saa siku mwezi na mwaka fulani na wala sio bahati mbaya.


            II. SOMO
Mungu ana majira ana wakati ana mwezi ana saa na ukisoma hapo unaona malaika wamefungwa kwaajili ya saa na siku Fulani. Ajali inaanzia rohoni baadae inakuja mwilini ukiliona taifa limeanza kumtegemea mganga wa kienyeji ujue limefika mahali fulani rohoni, ukiona kanisa limekuwa jua limefikia mahali Fulani rohoni kawahiyo siku ya uovu ni siku iliyoandaliwa tokea rohoni.
“Matendo ya mitume 13: 6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; 

7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 
11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. “
Hapa mtume Paulo ametoka amekwenda kuhubiri ulaya mji wa pafo amekwenda kuhubiri pale amealikwa na mkuu wa mkoa na alipofika pale mkuu wa mkoa alikuwa ana akili nyingi na msomi lakini akasema aende na msaidizi wake bar yesu ambaye ni mchawi, sasa mtume Paulo akaanza kumfundisha injili ya Yesu na mkuu wa mkoa  akawa amsikiliza kwa makini lakini kwenye ulimwengu wa rohoni yule bar yesu(mchawi) akaanza kumtupi vitu ili aiache ile Imani iliyokuwa inamwingia. Biblia inasema akaanza kumpa moyo wa kuiacha ile Imani aanze kuahirisha kumsikiliza mtume Paulo lakini mkuu wa mkoa anafikiri ni akili zake kumbe alikuwa anarushiwa vitu vya kuiacha ile Imani. Sasa Paulo akamwona huyu bwana akaondoa macho wa yule liwali na kumwangalia anayemletea upinzani (bar yesu) akamwambia uwe kipofu wa muda akamwambia ewe mwana wa uovu huachi kuzipotosha njia za Bwana na uwe kipofu kwa muda na biblia inasema viganda vikaingia kwenye yule bar yesu na yule liwali alipoona mabo yale aliyaamini mafundisho ya Bwana.
Kwahiyo wachawi ni wa rohoni wanatenda mambo yao usiku na hawaonekani unakuta mtu anakuja anakuwangia usiku na ukiamka unaanza kujisikia uchovu au humpendi mkeo au hali yeyote ile mbaya na hujui kama umefanyiwa hiyo hali ikutokee kuanzia rohoni. Neno la Bwana linaitwa upanga wa roho maana yake linaweza kukata mabaya yeyote yale yanayopandwa rohoni na wachawi siku ile ya uovu. Kwa kawaida wachawi wakitaka kuua mtu wanapanga siku tarehe na saa ya kumuua mtu. Siku ya uovu ni siku ambayo imepangwa mtu atendewe uovu/ubaya mfano; siku ya kufa mgonjwa unashangaa watu wanashauri mtu mgonjwa asafirishwe hadi hospitali fulani au apelekwe kwa mganga fulani kumbe ni sehemu ya kufanyika tukio lake la uovu katika siku ya uovu na unakuta anaenda kufia huko. Kabla laana haija mpata mtu imepangwa rohoni, kabla ajali haija mpata mtu imepangwa rohoni kwenye ulimwengu wa rohoni kuna matukio yanapangwa kabisa kabla hayajatokea mwilini iwe ni ajali, kufilisika,kufukuzwa kazi,kuachika, kufeli mitihani au mabaya yeyote yale yanapangwa rohoni kwanza kabla hayaja tokea mwilini. Mungu ni roho lakini ana miguu biblia inasema ameweka miguu yake duniani na shetani ni roho lakini anaweza kuandika na kusajili majina kwaajili ya siku ya uovu na wewe uliyeokolewa na Bwana Yesu hatusomeka majina yako au biashara yako haitasomeka katika ulimwengu wa rohoni, ndoa yako haita someka na usiposomeka rohoni, mwilini hakuna baya litakalo kupata “Nailifuta jina langu kwenye madhabahu yeyote iliyotaja jina langu, iliyo andaa ajali kwaajili yangu kwa jina la Yesu”.


“2Thesalonike2:3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
Hapa alizuiwa rohoni na shetani na shetani anaweza kushindana na mtu rohoni na watu wengi wanajua kwamba shetani hawezi kuingia mwilini sababu kuna roho mtakatifu ni kweli na jua shetani anatumia njia mbili kwanza anaweza kushindana na wewe akiwa njie ya mwili “Zakaria3:1- 1 Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. 

2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni? 
3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika. 
4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.
Pia anaweza kukumiliki rohoni ukitaka kwenda kanisani kichwa kinauma, ukija kanisani unataka kuondoka ndiomana Yesu allipokuwa akiondoka aliwaambia mkizubaa shetani atawapepeta kama ngano; japo alisema ametupa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n’ge lakini shetani hachoki na anatumia njia hizo na sio lazima shetani awe ndani anaweza kuwa nje kwa sababu huja kaa vizuri mfano ukienda kuomba kazi hupati japo vigezo unavyo na umeokoka maanake ni kuna mamlaka imejipanga rohoni kukufuatilia kila utendalo na uendako ili kukuzuia.
“Siku ya uovu iliyo pangwa kwa ajili yangu ninaifuta kwa jina la Yesu, ninaifuta siku ya ubaya iliyoandaliwa kwaajili yangu ninaifuta kwa jina la Yesu”
Kuna mashetani maalum kwaajili ya kila siku ya uovu wameandaliwa na hutumika kwaajili ya mambo fulani yanayotaka kutokea kwaajili ya siku ya uharibifu na mashetani ni malaika(walioasi) na sifa mojawapo ya malaika wanaweza kujubadilisha maumbo yao wakawa binadamu au upepo Yuda1:6 ufunuo12:7 Mungu alimwambia shetani kwa habari ya ayubu akamruhusu amguse lakini asiguse roho yake na unaona upepo ulivuma pande zote katika nyumba ile kumbe ni shetani, malaika walijibadilisha wakavaa maumbo ya kibinadamu na kwenda kumtembelea Ibrahimu wakala wakaondoka na tunaposema tukio la siku ya uovu ni kama tukio la kupata ajali ambayo mtu (malaika mwovu) anasababisha ni kwamba yule mtu wa siku ya uovu anaweza kuwa ni shetani amevaa umbo la mwili na tayari tukio lilishapangwa tokea ulimwengu wa mwilini. Na mashetani hawa walishafika eneo la tukio tayari kwaajili ya siku hiyo “katika jina la Yesu naifuta tarehe ya ubaya na uovu kwaajili ya familia yangu tarehe ya uovu tarehe ya ubaya juu yangu ninaifuta kwa jina la Yesu”
Kuna baadhi ya mambo yamepangwa kwenye maisha yako na wewe unasema ni bahati mbaya kumbe yamepangwa na biblia inasema nitakuokoa na mtego wa mwindaji shetani anaitwa ni mwindaji. Na anakuwinda na kama hujaokoka na huna Yesu anakupata kwa urahisi ni lazima siku ya uovu ikupate na huwezi kuiepuka “katika jina la Yesu ninaiharibu siku ya ubaya siku ya uovu iliyopangwa kwenye maisha yangu naiharibu kwa jina la Yesu siku ya ajali, siku ya kifo naiharibu kwa jina la Yesu na kila aliye ipanga namrudishia yeye kwa jina la Yesu”
Katika kitabu cha Mathayo mamajusi waliiona nyota ya Yesu hata kabla hajazaliwa na walikuwa ni wachawi na ile nyota ikawaashiria kwamba kunamtu Fulani amezaliwa mahali Fulani ni mfalme ndio maana alisema yuko wapi aliyezaliwa huyu mfalme wa wayahudi na inatupa ufahamu kwamba shetani na wachawi wanaweza kuona maisha yako miaka ijayo na wakaanza kushindana na wewe leo. Kwenye ulimwengu wa rohoni kuna kiashiria cha mafanikio ya mtu ya baadae kabla mtu hajafanikiwa na wachawi wanaona utakuwa mtu gani baadae na wewe unashangaa unachukiwa bila sababu ni kwasababu wanafahamu utakuwa nani baadae ndio maana watu wote wanaotumiwa na Mungu leo walipita kwenye matatizo kwanza kabla Mungu hajawatumia mfano: Musa alitakiwa auwawe lakini kwenye ulimwengu waroho shetani alikuwa anajua kwamba kuna mtu anakuja ambaye atawaokoa wana wa Israeli baadaye na hata wewe leo hii ndio maana wanafanya vita mbele yako wanajua utakuwa nani siku zijazo haitoshi Yesu alipozaliwa herode alitoa amri wauwawe watoto wakiume lakini alikuwa analengwa Yesu “huta kufa bali utaishi ili uyasimulie matendo  makuu ya Bwana” “japo ninapatwa na matatizo mengi sitakufa mpaka nimetimiza kusudi la Bwana”  wameona utakuwa nani baadae wametuma watu wanaoonekana ni binadamu lakini ni mashetani wametumwa kukuzuia usifikie kusudi lako wametumwa, mashetani majini, wachawi wanataka kukuzuia usiwe kama ulivyokusudiwa na Bwana lakini Biblia inasema hakuna atakaye zua vile ulivyopangiwa na Bwana. Wataangukia pua wanaofanya vita na wewe wachawi na wote wanaofanya watakuinamia “kwa jina la Yesu nitakuwa kama vile Mungu alivyo panga niwe katika jina la Yesu, siku ya ubaya iliyoandaliwa juu yangu naishinda kwa jina la Yesu ile siku ya mabaya ninaifuta kwa jina la Yesu” mabaya hayatakupata wewe wala tauni haitakariba hemani mwako kwa jina la Yesu.Mashetani duniani wako wa aina nne tu
1.       Majoka walioanguka toka mbinguni “Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;”  wanauwezo wa kuvaa maumbo yeyote yale lakini ni nyoka mashetani
2.       Majini, wanaoendana na mila za kiarabu lakini wanatenda mapenzi ya kishetani
3.       Mizimu wanaoendana na familia kuleta magonjwa ya kurithi, wanaweza kuelekezwa kwenye familia wakaelezwa familia hii isizae au isifanikiwe au izae inje ya ndoa mfano Ibrahimu na isaka na mtoto wake walipatwa na urithi wa kupatwa na shida ya kuza hii inatufundisha kuna mambo yanatokea kwenye ukoo ambayo ni ya kujirudia rudia, na kuna koo nyingine hata ukisoma namna gani hawawezi kupata kazi na shida zinaanzidi kumbe tatizo ni mizimu.
4.       Miungu ni mashetani yanayo abudiwa; mabudha na wengine kibao
“Hawa wote wanaitwa mapepo” nashindana na mashetani wanaoongoza familia yangu kwa jina la Yesu mashetani wa talaka, aibu, umaskini, kukataliwa walioandaliwa kwaajili ya siku ya uovu/mabaya nashindana nao kwa jina la Yesu.
Kwahiyo haya mashetani yanakuwa yameshatumwa karibu na wewe walishafika ili waharibu ndoa yako,kazi yako, bihashara yako na maisha yako. “kwaajina la Yesu ninaharibu siku ya ubaya iliyotengwa na wakala wa shetani kwaajili yangu,  aliyeiandaa ajali, kuharibu mahusiano yangu ninaamuru  impate Yeye aliye iandaa kwa jina la Yesu, kifo kimpate yeye aliyekiandaa kwa jina la Yesu,” ninafanya vita na kila aliye elekezwa kwangu kwaajili ya siku ya ubaya aliyetumwa siku yeyote ninashindana naye leo kwa jina la Yesu.
Kila silaha itakayo fanyika juu yangu haitafanikiwa kwa jina la Yesu kwa jina la Yesu”kwa damu ya mwanakondoo nina jitakasa kwaajili ya vita vya Bwana kuanzia leo saa yeyote niliyopangiwa tukio kwenye ulimwengu wa roho ninaifuta kwa jina la Yesu, siku ya uovu iliyopangwa kwajili ya taifa langu ninaifuta kwa jina la Yesu.

III.                MAOMBI.
Baba Mungu ninaomba unipe nguvu kwaajili ya vita ya kuteketeza siku ya uovu juu yangu kwa jina la Yesu. Ninaharibu mabaya yote yaliopangwa siku ya uovu kwa jina la Yesu, ninateketeza mashetani yote yaliopangwa kwaajili ya siku ya uovu kwa damu ya mwanakondoo, ninatengua kila mauti iliyopangwa juu ya familia yangu kwa jina la Yesu, ee mkuu wa bahari ninakukamata katika jina la Yesu na mawakala wako wote ninakushambaratisha kwa damu ya mwanakondo, katika jina la Yesu ninatengua matukio yaliopangwa juu yangu kwaajili ya siku ya uovu ninayasambaratisha kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu imeandikwa mabaya hayatanipata mimi wala tauni haita ingia hemani mwangu ninaharibu mabaya yaliopangwa kwenye bihashara yangu kwa damu ya mwana kondoo, ninaharibu na kuteketeza mashetani yote yalioandaliwa kwaajili yangu katika siku ya uovu kwa jina la Yesu, ninatengua kila ajali iliyoandaliwa na makuhani wa kishetani juu yangu na familia yangu kwa jina la Yesu, kwa mamlaka ya jina la Yesu ninafuta kila saa na mwaka wa siku ya uovu na mabaya juu yangu na familia na kwa jina la Yesu.

AMEN.

2 comments:

  1. Amen in might name of Jesus Christ

    ReplyDelete
  2. Dear might God your power excel the power of enemies any wickedness pursuing your servants let be consumed by holy ghost fire

    ReplyDelete