Sunday, July 20, 2014

JE WAJUWA KUWA UKOO WAKO UNAWEZA KUWA UKOO TATA?
TAREHE: 20.07.2014
NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: UKOO TATA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima

MANENO YA MSINGI: Mwanzo 50:24, 1 Nyakati 4:9


Baraka au laana ya ukoo inatokana sana na shina la ukoo. Ulivyo ukoo wa mtu,ndivyo alivyo mtu kama hana Mungu. Kuna koo ambazo ni tata sana, hata zikitoa mambo, na mambo hayo nayo huwa ni tata.  Mara nyingi vyanzo vingi vya matatizo aliyo nayo mtu yana uhusiano wa karibu na ukoo alipotokea mtu huyo.
Mwanzo 50:24 “Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo alivyowabariki”. Tunaona jinsi ambavyo Unaweza kukuta ukoo Fulani kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho watoto wote ni tata. Hivyo kabla hujaoa wala kuolewa chunguza ukoo kama ni tata au sio tata. Watu wengine wakishafika mjini wanaanza kujisifu na wanasahau kama huko walikotoka  mfano shangazi hana hata viatu na bibi anapuliza kiko cha ugolo hadi sasa!
Kutokana na neon hili unaweza kuona Yakobo alikuwa na watoto 12, na kabila 12 zilitokana na watoto wale. Hivyo kila tabia ya mtu inatokana na msingi wa  ukoo wake. Hivyo yatupasa tuchimbe na tung’oe msingi ya koo tata. Kumbuka niliwahi kufundisha habari ya majeshi ya wafu, nikasema sio vizuri kabisa kuendekeza na kuwatolea sadaka.
Kitabu cha kwanaza cha maneno matakatifu kinaanza na majina ya ukoo. Mfano katika kitabu cha 1Nyakati 1. Kutokana na majina ya koo hizi, inatufindisha kuwa kila majina ya koo yalitengeneza majina ya sehemu hizo leo. Kila mtu ajue chochote utendacho leo unatengeneza ukoo wenye baraka au laana ya kizazi kijacho. Usifikirie kuwa unaposoma sana ndio kushinda katika maisha, lakini elimu inakupa tu mwanga wa kukuangazia utafute jinsi ya kujikwamua katika maisha yako, ukitumia kipawa alichokupa Mungu.
Unaweza kuona baadhi ya koo mabinti hawezi kuolewa, au kusoma mpaka chuo kikuu, au wanakufa katika umri mdogo. Kwa namna hii unaweza kuona kuwa matatizo hayo ndio chanzo na msingi wa ukoo huo. Hivyo rudia maneno haya “ katika jina la Yesu nayavunja mambo yote mabaya katika ukoo wangu “ Ukoo wa mtu unatabili maisha ya mtu anayoishi leo. Unaweza kukuta kila kinachotokea mfano kifo katika ukoo ni cha namna ileile. Mfano kule Bukoba unaweza kukuta nyumba ya Profesa Fulani , lakini maisha ya familia yake sio sawa na kiwango cha elimu walionayo. Jambo hilo limetokana na msingi wa ukoo wake. Sema maneno haya “ Kwa jina la yesu navunja mahusiano ya taabu yangu na familia yangu katika jina la Yesu
Leo uhame hapo ulipo kwenye ukoo wa laana na mikosi uingie kwenye ukoo wa kushinda kaita jina la Yesu. 1 Nyakati 4:9Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.”
Huyu mtu alizaliwa kwa huzuni na akaitwa jina lake ni huzuni, lakini baada hapo alimtafuta Mungu akaishia kuwa wa furaha na kuheshimiwa na ndugu zake. Walawi 25:47Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni”
 Na wewe ukiamua kumtii na kumtumikia Mungu ataona hata utakao wazaa hawataanzia wewe ulikoanzia bali ulikoishia wewe. Hivyo mtii Mungu na kumuheshimu Mungu utaheshimika na watu wote na viongozi wa nchi hii watokane na wewe katika jina la Yesu. Kama ukoo wako ni ukoo wa kushindwa utabaki kuwa wa kushindwa mpaka uhame katika jina la Yesu. Leo nahama kutoka katika ukoo wa laana, mkosi, kushindwa, kukataliwa, kuachwa, magonjwa, vifo vya mara kwa mara.
Zamani mtu alikuwa anaweza kujiuza kutoka kwenye familia ya umaskini na kuingia katika familia ya kitajiri na anakuwa mali ya familia au ukoo huo na sisi tumeamua kujiuza kwenye familia  ya mwana kondoo.
Mchungaji kiongozi katikati ya makutano

 2 Wakorintho 8:9
Inatwambia kumbe yesu alifanyika kuwa maskini ili tuwe matajiri. Na yesu ametukubali kwa umaskini wetu sisi tupate kuwa matajiri kwa njia ya imani. Na kwa namna hiyo tunapata kibali na kuweza kuendelea mbele. Ndo maana unaweza kuona unaweza kuwa na sifa nzuri za kupata visa, tenda, kazi lakini usipate. Hili kwa sababu ukoo wako umeandikiwa muwe wa kukosa. “Leo natangaza kwa jina la yesu lazima  uhame katika jina la yesu.”Unaweza kukuta familia zinatawaliwa na nguvu za giza? Kabla hatujamjua yesu, wazazi wetu walikuwa wanatumia ulinzi wa kimila. Kuna familia nyingine wewe kabla kuja mjini kuna kitu ulipewa uje nacho kama ulinzi kwako dhidi ya watu wabaya. Anaweza kuletwa na baba wa familia au bibi au babu wa ukoo, akiwa na nia njema ya kuwawekea ulinzi, lakini kumbe ndo chanzo cha nyinyi kuanza kulindwa na mashetani.
Wakati mwingine mambo hayo yanatengenezwa kama karatasi yenye maandishi ya kutoka kulia kwenda kushoto Fundo hili linaitwa talasim. Kimsingi kupitia zindiko hili familia inaanza kulindwa na masheteni. Kwa mfano pia unaweza kukuta mtua ana namba ya waziri mkuu, mkurugenzi au mtu mkubwa.Lakini pamoja na kuwajua watu hao haikukusaidia kwa kuwa kuna utata wa kishetani unaolinda familia yenu. Unahitaji kuhama ukoo huo wa utata.  kwa jina la yesu nakataa kabisa kung’ang’ania ukoo tata”
Wakati mwingine unaanza kujiuliza mbona nimejitahidi kusoma sana lakini bado mambo
2 Timetheo1:3
“Leo navunja kila laana, balaa namatatizo yaliopandwa ndani ya ukoo wangu katika jina la Yesu”
Maombolezo 3:30-32
Isaya 53:4
Tumeumba kwa neno hivyo unapaswa kutamka  kwa kinywa chako. Na utambue imeandikwa wewe u rungu langu na silaha za bwana za vita. Mtu yeyote kuanzia sasa naamuru achiwe katika jina la Yesu. Unaweza kujiuliza maswali ya kwamba mbona kaka  zangu wananafuu? Tambua kuwa balaa iliyo ndani ya famila au ndani ya ukoo inaweza kijidhihirisha kupitia mtu mmoja. Imeandikwa pi kuwa amelaaniwa mtu Yule amwagaye damu ya mtu asiye na hatia. Inaweza kutokea ajali inatokea anakufa mtu mmoja au unazaa mtoto anaulemavu wa ngozi. Lakini kwanini usijiulize kwanini itokee kwako?  Kimsingi lazima ujue kuwa kunakitu kinapelekea au kimepengwa kikupate kama ilivyofanyika katika ulimwengu waroho.
Mfano katika taifa la Marekani kila raisi aliyekuwa anaingia madarakani alikuwa anauwawa mpaka walipoamua kuingia ikulu na kuomba na kuvunja laana hiyo na haikutokea tena. Unaweza kukuta kunatabia Fulani inatawala kabila Fulani, lakini hakuna kabila bora kuliko nyingine sema tu inategemea kiwango cha kutawaliwa na mashetani hao. Jiulize pia wakati naomba kwa nini watu wanalipuka mapepo? Hii ni kwasababu mtu anayelipuka mapepo kimsingi ameshikiliwa na mashetani wasimamizi wa laani maana wamewekwa kusimamia laana hiyo na kuhakikisha unaangamia na kupotea kabisa. Lakini kwa wanao mwamini Yesu pia kuna damu ya mwanakondoo imewekwa ilikusimamia na kuvunja laana ya ukoo huo au inayokufatilia wewe.
watu wenye shida mbali mbali wakifunguliwa.
Watu wa hospitalini huwa wanasema tutaweza kuicontrol pressure yako au kisukari lakini sisi tumepewa mamlaka ya kung’oa kubomoa na kuharibu. “Lakini leo sema nakataa kusimamiwa na mashetani wa balaa, laana na mikosi na toroka na kuhama kutoka maeneo ya kishetani katika jina la Yesu.” Kuna namna mbili shetani anazoweza kutumia kukushambulia.
1.       Anaweza kuwa nje
2.       Anaweza kuwa ndani yako
Zakari3:1
Maelfu ya watu wakiwa ndani ya Bonde la kukata maneno
Kuna mtu analalamika anadegree 2, au 3, lakini hapati kazi.
Pamoja na kushindwa lakini unaweza kuanza tena, kushinda tena, kutengeneza tena. Tumejifunza kuomba wenyewe kwa mamlaka ya jina la Yesu.  Unatakiwa ujue kuwa hatumuombi Mungu atende bali twatumia mamlaka ya Yesu iliyoko ndani mwetu. Hivyo unatakiwa ujue kuomba mwenyewe. Kila mtu anayo  mamlaka shida tu huwezi kutumia usichokijua.  Uwezo  wako wa kuvunja, kushambulia na kuharibu katika ulimwngu wa roho, ndo uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu wa mwili. Utakuwa kama bwana anavyotaka uwe, wala hautakuwa kama watu wanasema nini juu yako. Mungu anajua kesho yako kabla haujaiona, na kesho ya maisha yako iko mikononi mwako. Wanakuita aliyeshindwa lakini mbinguni wanakujua kama shujaa.
Tanzania mpya inakuja, na wewe unayonafasi ya kustawi katika nchi mpya ijayo katika jina la Yesu. Mungu anawatafuta waliodharauliwa na watu, na anakufanya kuwa wa heshima na anaanza kukufanya hatua kwa hatua.” Nina kataa  balaa zilizopangwa kuharibu  kesho yangu, naiona kesho yangu  inang’aa  katika jina la Yesu.”
          Amen

No comments:

Post a Comment